TAFUTA HAPA

Loading...

KAMA UNATAFUTA PAKWENDA SIKU YA WAPENDANAO BNN RESTAURANT &LOUNGE WAMEKUANDALIA MAMBO MAZURI.

MAHALI:BNN RESTAURANT & LOUNGE NI MPYA IPO QUALITY CENTRE NYERERE ROAD
BURUDANI KUTOKA KWA BAND YA SUPER STAR BENGA AFRICA ATOMY SIFA KUTOKA KENYA.
MCHEKESHAJI MAHIRI PILIPILI NDIO ATAONGOZA SHUGHULI NZIMA.
KIINGILIO 60,000 KWA MTU MMOJA
COUPLES 100,000 NA ZAWADI KIBAO KUTOLEWA PAMOJA NA CHAKULA CHA JIONI.
 
BOOK TICKET YAKO KWA KUPIGA NAMBA 0713 501049 NA 0682 602809

MISEMO YA KWENYE KANGA!

BASI SAWAAAA!!

MAPISHI:BBQ YA NYUMBANI(NYAMA CHOMA)

Mimi nyumbani kawaida hata kama kuna housegirl chakula napika mwenyewe.Hasa cha usiku na weekend pamoja na tumbo langu bado nimo.Sasa jumapili siku hizi siingii jikoni nina wanaume ndio wanahakikisha mchana tumekula na usiku tumekula kama kuna lolote ntasaidia ila kila kitu wanafanya wenyewe.Ndio tunafanya nyama choma at home.
Nyama ya mbuzi mbavu na inawekewa marination ya kawaida tu ili kuilainisha na kuipa ladha kabla ya kuichoma.
Tunatumia tangawizi,kitunguu saumu,ndimu au limao na chumvi.Nyama inapakwa hivyo vyote kisha inawekwa kwenye fridge kama lisaa hivi ndio inaanza kuchomwa.Inaweza kuwekwa hivyo vyote hata usiku ikalala kwenye fridge kesho yake ikachomwa.
Kuku nao huwekwa marination ila hii ni kitunguu saumu na limao na chumvi.Wakati mwingine tunaweza kufanya chicken tandoor kama tunataka ile ladha ya pilipili.Mikono ni ya my brother in law akishughulika.
Hii ni mbuzi ikiiva taratibu...mdogo wangu yupo vizuri kwenye kuchoma mbuzi na shemeji yangu yeye kwenye kuku.
 Mambo yako tayari kuliwa..
Mdogo wangu akitengeneza kachumbari.
LUNCH:Mbuzi choma,ugali,kachumbari na mboga ya majani ya maboga.
DINNER:Kuku choma,ndizi tamu za kukaaanga na kachumbari bila kusahau chachandu.
Jumapili ikawa imeishia hapo.Kama ipo ndani ya uwezo wako unaweza kujibajeti vizuri ukafanya nyumbani.Sio kwamba unanunua mbuzi mzima mbuzi kilo mbili hata moja inatosha kulingana na ukubwa wa familia yako.Kuku mmoja,wawili au watatu pia wanatosha.Sio mpaka tukale kuku au mbuzi bar hata nyumbani vinawezekana tu hasa baba akiwa ndio kashika usukani.

8020FASHIONS BLOG INAKULETEA...

HAYA HAYA WALE WAKIKENI KWA HESHIMA NA TAADHIMA NAOMBA NIWATANGAZIE KUWA ILE EVENT,/TUKIO LA MWAKA LA WANAWAKE LINALOENDA FANYIKA KWA MWAKA WATATU SASA  HAPA JIJINI TUKISHEREHEKEA SIKU YETU SISI KWA KUUMBWA WANAWAKE HIYOOOOOO LAJONGEA.
 
NI TAREHE 8 MARCH SIKU ILE ILEEE  MAALUM YA WANAWAKE WOTE DUNIANI AMBAYO ITAKUWA INASHEREHEKEWA DUNIA NZIMA NASI TUTAKUWA NAO SAMBAMBA
TUTALAKOENDA ANGAZIA SAFARI HII KATIKA SIKU YETU HIYO NI
‘KUONDOA AINA ZOTE ZA UKATILI NA UNYANYASAJI DHIDI YA WANAWAKE’
NA WAPO WATAKAOTUWEZESHA ….KAMA MNAVYOONA HAPO TUNAWEZA WATAKUWEPO KUFANIKISHA.
KIVAZI /DRESS CODE /KIVAZI CHA KUTINGA SHUGHULINI NI ILE ILE:: AFRICAN PRINT VAA KITENGE/ KANGA/BATIK MRADI TOUCH YA KIAFIRIKA IHUSIKE
MAHALI ::DIAMOND JUBILEE VIP HALL
MUDA ::SAA 5 ASUBUHI HADI 2 USIKU
SIKU ::JUMAMOSI
TAREHE ::8 MARCH
WATAKAOPENDA KUSHIRIKI SHOPPING BAAZAR ILI KUONESHA BIDHAA ZAO NA MAKAPUNI MBALIMBALI YANAKARIBISHWA KATIKA KUFANIKISHA SHUGHULI HII PENDWA NA PEKEE YA SIE WAKIKENI
WASILIANA NASI ::0784 418941/0713 551077
BARUA PEPE :: shamyomy@yahoo.com /vituvyakhadija@yahoo.com
SIKU YETU …..SHUGHULI YETU ….KWA RAHA ZETU
 
 
 
 
 

VIPINDI VYA TV NINAVYOTAZAMA WAKATI NIPO NYUMBANI.

Wakati huu ambao nipo nyumbani nautumia vizuri kuangalia vipindi vingi vya tv ikiwemo hivi hapa.
Kwa wale waliounganishwa na DSTV mtaweza kuona vipindi hivi.Body Mind and soul cha mchungaji TD Jakes ni kati ya vipindi ninavyovifatilia sana najifunza na pia napata ideas mpya.Hapo huzungumzwa mambo mengi yahusuyo maisha yetu ya kila siku kiroho,kimwili na kiakili.
Oprah Winfrey ni mwanamke ambae ameweza kuinspire millions of people especialy women hapa duniani nikiwemo mimi.
Nimekuwa namfatilia kwa miaka mingi sana na alinisukuma kitambo kuanzisha talk show lakini naona muda bado haujafika ukifika nitafanya hivyo.
Jumapili huwa naangalia vipindi vyake vingi tu super soul sunday,oprah next chapter na oprah behind the scene.
Kupitia Oprah behind the scene unaona ni jinsi gani ana team kubwa ya production nyuma yake.Ana maproducer ambao kwa miaka yote wamehakikisha akirusha kipindi lazima kiache historia.
Hii imenifanya niumize kichwa sana.Hatuwezi kuwa kama Oprah ila tunaweza kujifunza kupitia yeye.Vipindi vyetu tunavyofanya ukiwa wewe ndio mtangazaji basi vitu vingi utakuta unaviwaza wewe na wakati huohuo unazalisha wewe mwenyewe hakuna team ya producers nyuma yako.Hata vijana wanaosomea journalism wengi wanataka kuwa watangazaji hakuna mtu anataka kuwa behind the scenes kama mzalishaji.Lakini hii nayo ni ajira ila inataka uwe mbunifu na mwenye upeo wa hali ya juu wa kugundua madini yanayoweza kupelekwa hewani.Ujitume na uwe na upeo kumzidi hata mtangazaji husika,je wangapi wanataka kuwa wazalishaji?una vigezo?
Steve Harvey Show...Steve ananifurahisha sana na wageni wake,ucheshi wake na topics anazozileta kwenye show.Steve talk show yake amewalenga wanawake nimependa idea ya yeye kuwa mwanaume lakini anafanya show target yake ikiwa ni wanawake.Akiwa ni mwandishi wa kitabu kilichouzwa sana mwaka juzi THINK LIKE A MAN ACT LIKE A LADY.
Napenda kipindi hiki maana mie mwenyewe nafanya kipindi kinachomlenga mwanamke kwa hiyo najifunza zaidi japo mie nipo radio.Talk show inataka uwe live na wale waliopo kwenye show,wageni unaowahoji na bila kusahau anaekuangalia nyumbani kupitia luninga yake very challenging Steve yuko sawa kwa ucheshi wake lazima niangalie kipindi chake.
 
Haya kama nilivyosema nipo tu home nitakuwa naandika yale ninayoyaona katika mazingira yangu.

SHUKRANI ZA DHATI KWA SAPOTI YAKO KWA MWAKA JANA 2013.

Kwenye maisha yangu sikuwaza kama ipo siku nitaweza kupewa tuzo ya heshima kwa kile ninachokifanya katika kazi zangu za kila siku.Msingi wa yote ni kipindi changu cha leo tena kufanya kipindi haitoshi wewe kama mtangazaji unajiongeza vipi katika taaluma yako?hapo ndio nikajikuta nafanya mambo mbali mbali yaliyoniwezesha kupewa heshima mwaka jana mwezi wa tatu.Ilikuwa tarehe 28 mwezi wa tatu nikapata tuzo ya WOMAN OF THE YEAR ya TANZANIA WOMEN OF ACHIVEMENT.Wakati jina langu linatajwa nilihisi kama naota hivi au nimesikia vibaya sikuamini maana nilikuwa nipo na mama zangu wengi waliofanya makubwa katika sekta mbalimbali nilipojihakikishia ni mimi kweli wala sioti ndoto ndio nikasimama kwenda kupokea tuzo yangu.Namshukuru Mungu sana sana kwa baraka hiyo katika mwaka 2013.
Mwaka jana 2013 pia nilipata nafasi ya kuteuliwa kuwa miongoni mwa mabalozi wa shirika la OXFAM.Shirika linalojihusisha na wanawake,chakula na kilimo.Tuliteuliwa mabalozi 7 na kukabidhiwa tuzo maalum ya mabalozi.Mwaka huu tukijaaliwa kuna wanawake watafanikiwa kushiriki nami katika mradi wangu kama balozi wa oxfam utakaohusu mambo ya chakula.
Kwa kushirikiana na UWF tulifanya tena tuzo ya mwanamakuka kwa mwaka wa pili.Tuzo kwa wanawake wajasiriamali wale ambao bado wana struggle na tuzo ilienda kwa Aziza Mbogolume mama mchora picha.Alijishindia tsh ml 6.
Mwaka jana nilianzisha mradi unaitwa dada dina cares.Kwa kutembelea vituo vya watoto yatima nimegundua watoto wanalelewa na watu wenye mapenzi ya kulea watoto lakini bado hawawezi kuwapa huduma mbalimbali muhimu kwa uhakika.Malazi,chakula,mavazi,vifaa vya shule bado wanahangaika.Ndio nikaanzisha hiki kitu ili kushirikiana na wadau mbalimbali tuweze kuvisapoti hivi vituo.
 Tulipata vituo vitatu tulivyoweza kuchanga pesa na kuwanunulia chakula,unga,mchele,sukari na maharage.
 Vifaa vya shule kuanzia madaftari,pen,pensil,vifutio,rula n.k
 Vitanda,mashuka,magodoro,mapazia,nyavu za madirisha,na vyandarua

 Nilipata chance ya kukaa na watoto,kuongea na kuconnect nao.
 Tulikula na kucheza nao
 
Toka nilipoanza Dada Dina Cares nimepokea simu nyingi sana za wadau,watu binafsi,vikundi,makampuni,mashirika mbalimbali yakiomba kuelekezwa namna ya kuvifikia hivi vituo ili kuvipa misaada mbalimbali.Na wao wananipa feedback kila wakati ya namna wanavyoendelea kupata misaada.Watu kujitolea kwa yatima wanaweza ila kuwa na taarifa sahihi ya wapi waende ndio wanakuwa hawajui.
Mwezi dec ilikuwa nifanye tena huu utaratibu lakini sikuwa kwenye hali nzuri ya kuhimili mikiki mikiki.
Pia nilianzisha vibubu viwili hapo ofisini ambavyo watu wamekuwa wakidumbukiza pesa humo,hata wale ambao wamekuwa wakituma nimekuwa nadumbukiza humo ili kukusanya hela zitakazoendelea kusaidia mahitaji ya vituo vya watoto yatima.Nina vibubu kama kumi hivi ukiwa intrested nicheki nikupe kimoja utakaa nacho mpaka mwezi wa saba tutakifungua na hela zitakazokuwemo tutazitumia kwa mchakato mwingine wa dada dina cares utakaofika mpaka vituo vya mikoa nje ya Dar es salaam.
Kwa mwaka wa tatu mimi na my patner Vida Nassari tumefanikiwa pia kuendeleza semina za wanawake za kitchen party gala.Tulianza mwaka 2011 na mwaka huu wa 2014 ni mwaka wetu wa nne.Kwa hilo tunamshukuru Mungu tunaendelea japo kumekuwepo na chagamoto nyingi sana.
 
Ninachosikitika mwaka jana sikuweza kufanya tuzo ya dada bora wa kazi za nyumbani.Ni tuzo tuliyoweza kuifanya kwa miaka miwili mfululizo tena kwa mafanikio.Tumeweza kuwafanya wasichana wa kazi za majumbani kuonekana na wao ni watu na wanapaswa kuheshimika kwani mchango wao katika malezi na ustawi wa familia ni mkubwa wasipuuzwe,kunyanyaswa na kubezwa na waajiri wao.Ilishindikana kufanyika kwa sababu za kiofisi ratiba ilikaa vibaya mwaka huu panapo majaaliwa tutafanikisha naamini.
 
Malengo ni mengi ndoto ni nyingi lakini huwezi kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja.Kila jambo na wakati wake tusichoke kuamini katika ndoto zetu na kuzifanyia kazi.Ukiwa na ndoto bila uwajibikaji katika kutimiza ndoto husika ni sawa na ndoto ya usiku ukiwa umelala umeokota mahela mengi na asubuhi kuamka na kukuta ilikuwa ni ndoto tu na sio kweli.Wakati mwingine ni ngumu kutimiza malengo flani lakini usichoke kujaribu.Jaribu tena na tena na tena ni bora ujaribu ushindwe kuliko kutokujaribu kabisa.Na uwe na imani kama huna imani ni kazi bure.Imani yako ndio itakufikisha kwa sababu unaamini katika hiyo ndoto husika.Hata akitokea mtu kukukatisha tamaa au kukubeza hawezi kufaulu kwasababu una imani na ndoto yako.
 
I wish u all the best katika mwaka huu mpya 2014!

WAPENZI WANGU HAPPY NEW YEAR 2014.


Happy new year wapenzi wangu woteee ni muda sijaongea nanyi hapa kwenye blog lakini wapo ambao naongea nao kwenye simu kila siku tukijuliana hali na kutakiana amani na upendo katika maisha haya tunayoishi.Mungu ni mwema tulifanikiwa kufunga mwaka 2013 na kuukaribisha 2014.Na bado tunaendelea kumuomba na kumshukuru aendelee kutusimamia na kutupigania kwani tunaweza mambo yote katika yeye atutiae nguvu.
Kiukweli mwaka 2013 kwangu ulikuwa wa baraka tele sina malalamiko yoyote zaidi ya kushukuru kwa hali zote nilizopitia.Kwa kazi ninayofanya nakutana na watu mbali mbali ambao pengine wamekata tamaa ya maisha kwa wingi wa changamoto zinazowakabili kimaisha na mimi kuona nimebarikiwa sana hata kama kuna jambo nalitamani kulipata sitalalamika kwa nini sina?bali ntaendelea kumuomba Mungu aendelee kunibariki.
 
Nimekaa muda kimyaa maswali yakawa mengi kuhusu mie kuwa mjamzito.Sikutaka kuzungumza hapa ili kukidhi kiu ya udaku kwa yule alokuwa akihoji tena wengine walikuwa wakituma comments na kashfa juu.Niliamua kukaa kimya nideal nalo mimi mwenyewe personal.Kama ulishawahi kusoma nilichowahi kuandika hapa http://dinamarios.blogspot.com/2013/05/maisha-bila-mama.html
nilielezea maisha yangu ya nyuma yalivyofanya niwe muoga wa kuwa mama au kuolewa kama hukusoma ingia hapo usome.
Kwa hiyo hili lilipotokea nilihitaji love and support ili kusimama na kuamini kila kitu kitakuwa sawa.
Nashukuru Mungu nimepata hivyo vyote kutoka kwa mhusika mkuu.Anaitwa Reuben Ndege sio meneja wa skylight band kama walivyandika wadaku na wadakuzi.Amenipa love and support kwa kila hali.Tumekuwa wapenzi kwa miaka mingi sana lakini kama ujuavyo mapenzi ya ujana off and on zisizoisha kuvurugana kila leo.Ila sasa tupo pazuri.
Familia yangu pia baba yangu Mzee Peter amekuwepo na mimi bega kwa bega maana ndio baba ndio mama kwangu.
 
Pichani mimi,my brother in law Shady,mama mkwe,shadee,na mdogo wangu Ibra.
 
Namshukuru Mungu nimezungukwa na upendo na amani hilo ndio kubwa nililokuwa nahitaji.Kuna mliokuwa mnasema sijiu najificha,naona aibu,sijui sijiamini.Sasa ina maana siendi kazini?siendi hospital/clinic?siendi bank?shopping nipo tu nimejificha?
Kila mtu ana namna yake ya kudeal na vitu kwanza hata picha napiga basi sizipendi,sipendi simu wala computer naona vinanivuruga.
Kuna marafiki zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu kwa hali yoyote sio ile ambayo ipo confortable kwao.Maana kuna marafiki watakuwa karibu na wewe wakati ule unaweza kwenda club huku na kule ukiwa katika hali nyinginge hawakutafuti na hawana mpango na wewe.Utakesha wewe ukiwatafuta ukihisi ni wenzako kumbe siku nyingi walishakudelete.Nawashukuru sana
Fide Mwakitalima,Asma Makau,Queen Geofrey,Sophy,Vida Nassari,Zamaradi,Gea Habib yaani naongea nao kila siku since day 1 wakinishauri hili na lile hata iwe usiku mwingi wapo kwa ajili yangu.
Kupitia leo tena hapa kwenye blog nina mama zangu,dada zangu,aunt zangu na kaka zangu ambao wamekuwa sehemu ya maisha yangu hata bila ya mimi kuwafahamu.Kila siku asubuhi mpaka usiku naongea nao kwa simu mpaka nahisi kama nawafahamu.Wamekuwa sehemu ya maisha yangu ni wengi siwezi kuwataja hapa.Ni upendo wa pekee kwa kweli mpaka wakati mwingine naogopa.
Mwaka huu mpya mie kwa sasa nimeuanza nikiwa nyumbani nimeanza likizo sipo kwenye leo tena.Sasa hata vya kublog sivioni,nikijaaliwa ntakuwa naandika vile ninavyoviona katika mazingira niliyopo sio ya ofisini.
 
Haya wapenzi kama kuna malengo hatukutimiza mwaka jana tuongeze juhudi zaidi kuyafikia mwaka huu....amani kwenu wote!

SIKUKUU NDIO HIZI ZAJA,TUPEANE IDEA ZA VYAKULA VYA KUPIKA MSIMU HUU.

Msimu wa sikuu ya christmass ukifika watu wengi hufikiria nguo,mapambo ya nyumbani,vinywaji na chakula.Chakula ndio kiunganishi kikubwa cha familia kwani hutulazimu kukaa pamoja wakati huo wakula.
Shopping ya chakula hufanyika mapema kabisa hasa mama ukishajua utapika nini kwa familia yako.Na msimu huu kama ni familia basi mpo wote maana na shule zimefunga hivyo watoto wapo nyumbani.Ni kipindi ambacho ndugu jamaa na marafiki hufunga safari kuja kwako kujumuika na wewe inategemea na mlivyokubaliana.
Nilikuwa nimekaa nafikiria nipike nini siku hiyo maana nategemea wageni siku hiyo.
 
Sikukuu tumeshazoea kupika pilau yaani bila pilau sio sikukuu.Pilau la nyama ya ng'ombe,mbuzi,kuku,samaki,firigisi n.k.Kingine kinachoongezeka labda ndizi au balada la pilau kukapikwa biriani.
 
Tupeane mawazo ya vile tunavyoweza kuvipika siku hiyo.

HAPPY BIRTHDAY BARBARA HASSAN WA PB YA CLOUDS FM

Hongera kwa kuadhimisha miaka kadhaa ya kuzaliwa leo hii.Mungu aendelee kukupa hekma,nguvu na afya uwalee wanao Tonny na Ashley na kuendelea kupambana na maisha ya kila siku yaliyojaa kila aina ya changamoto.Nakutakia furaha na amani ya moyo wako.
Happy birthday mama Ashley!
 

MAISHA

MIMI NA WEWE