Thursday, July 16, 2009

"JIKAZE WANAUME HUWA HAWALII"HUU NI USEMI UPO MIAKA MINGI SANA..


Kulia ni kitu ambacho unaweza usiweze kujizuia hasa hicho kinachokuliza kinapokuwa kweli kimekuuma,kimekuuzunisha n.k,watu hulia pindi wanapokuwa wanaumwa,wamefiwa,hata wakati wa furaha,wameshindwa katika maisha/masomo/siasa/au jambo lolote,kiukweli ni mengi humfanya mtu alie hasa pindi anaposhindwa kujizuia. Mwanaume kuonekana analia kama hapo kwenye picha wengine huona jambo la ajabu,lakini kiukweli mtu unapolia ndio unajitibu... tena unaambiwa ukiona mtu analia muache alie wee mpaka atakapo amua yeye mwenyewe kunyamaza maana hawezi kulia mwezi mzima..kulia kunafanya ajisikie vizuri hapo baadae,kulia hawakuumbiwa wanawake peke yao.Kwani mwanaume ukilia unabadilika kuwa mwanamke?lia tu jamani ni hisia ambazo zimeumbwa...

7 comments:

Sarp said...

mwanaume akilia kuna jambo jamani Dina!i lov3 yo blog...Keep it Tite mumie

Bwaya said...

Machozi kihisia yanafanana kwa mwanamke na mwanaume. Hili si suala la kimaumbile ni namna tulivyokuzwa tu, na si vinginevyo.

don said...

huyu ni udhaifu

don said...

huu ni udhaifu

lucas said...

Lakini Dina kuomboleza kupo kwa jinsia zote, ila wanaume wengine wanatia aibu, maana hulia hata wakitoswa na wapenzi wao hali hiyo mi naichukia.

Anonymous said...

Kulia si lazima uwe na huzuni, hata furaha inaweza kufanya ulie mf: kukutana na yule uliyepotezana naye miaka kadhaa, hapo inakufanya ulie kilio cha furaha.

Andrew sanga said...

mwanaume akilia ujue kuna jambo,so fikiria zaidi kwa nini analia ,usimchukulie poa.

Post a Comment