HAHAHAHAHA NICHEKE NINENEPE JAPO SI YA KUCHEKESHA...WAOLEWA MPO??

10:32 PM by
Kila mtu huwa ana ndoto za aina ya harusi anayotaka,hasa wadada ndio huwa tuna ndoto kweli....gauni,vyakula,familia,mapambo yaani iwe ya kufa mtu.Kijana mmoja mkazi wa hapa Dar wiki chache zilizopita amefunga ndoa lakini si kwa mwanamke ambae alimtambulisha kwao,si yule ambae wamekaa vikao vya harusi ni mwingine tofauti kabisa...


Bibi harusi mtarajiwa alikuwa ashafanyiwa mpaka kitchen party jamani na vyombo kibao akavikusanya,na send off juu lakini harusi ameisikia kwenye bomba.


Kisa cha kuachwa kwenye mataa,inasemekana bidada alikuwa akiliponda gauni la harusi alilotafutiwa na mawifi zake na kugharamiwa na mumewe mtarajiwa na pia akawa anasememasema kuwa harusi ya kimasikini sio alivyotarajia...basi mawifi wakampa habari kaka yao juu ya jeuri za bibi harusi mtarajiwa,kaka ikamuuma akaghairi kumuoa yule dada ila akawaambia nduguze harusi ipo palepale.Kumbe kaka alikuwa anampenzi mwingine aliyekuwa amemuweka pending...patamu hapo hahahaha bidada akapigiwa simu na kuitwa kuelezwa kuwa anaolewa...


Jamani sikiliza heka heka leo saa tano na robo.

Hekaheka ya leo nakuomba usikose maana Gea Habibu kaitoa mbali sana jamani.

18 comments:

 1. sidhani kama bwana harusi alikuwa anampenda sana Mke mtarajiwa

  ReplyDelete
 2. Bwana harusi alikuwa ameshapata sababu.

  ReplyDelete
 3. Dina mawifi wambea hawana lolote nimesikiliza leo tena katika heka heka, inaonekana wifi mkubwa alikuwa hampendi toka mwanzo, hata huyo aliyeolewa watamtoa kasoro tuu sisi wanawake tutakuwa wa kwanza motoni siku ya kiyama!!! Bwana harusi nae msimamo, maamuzi, na uwezo wa kutatua matatizo uko finyuuu yaani kuduchuu.

  ReplyDelete
 4. hata mimi sidhani kamakulikua na mapenzi hapo... ila Dina wengine hatuko nyumbani(TZ) please tujulishe kile kinachoendelea kwenye leo tena.

  ReplyDelete
 5. Bwana harusi alikuwa anatafuta sababu tu labda ya kumuacha kwa sababu alikuwa na uhakika gani na maneno aliyoambiwa na dada zake kama kweli kasema, me nafikiri mpk mtu anaamua kuolewa ni kuwa anakuwa ameshaijua family background anakotaka kuolewa au kuoa hali yao kiuchumi na maisha yao kwa ujumla so i think hao mawifi walikuwa hawampendi huyo mdada wakaamua kupandikiza majungu kwa kaka yao. NI MTAZAMO WANGU TU.

  ReplyDelete
 6. mmh dunia iko na mengi sana, sio rahisi kubadiri maamuzi fasta kihivyo. Itakuwa huyu dada alikuwa na kero za siku nyingi na majigambo kama hayo ya siku nyingi. Sasa jamaa alikuwa anatafuta mahali pa kulipia kisasi chake, ndio akaamua kupiga pigo la Karne. Lakini wanawake mmezidi midomo aah. Pia sijasahau kumpa pole huyo dada na kumpongeza huyo kaka kwa kuwatia adabu woteee wenye vidomodomo.

  ReplyDelete
 7. huyo bwana harusi ana asili ya umalay tu hana lolote hakuwa muoaji wa ukweli hata huyo aliyemuoa atamuacha tu. na huyo aliyeolewa atakuwa lazma kaloga sana mwenzie asiolewe. na hao mawifi wakumbuke na wao pia ni wanawake yatawakuta tu ukute nyumba zao zimewashinda au la hawajaolewa.

  ReplyDelete
 8. mwaume kaonesha mfano; naiwe fundisho kwa wanawake wenye dharau na kujishauha;
  namwamke aliyeolewa akaze buti asichezee bahati hiyo; MUNGU ASAIDIE DUA ZAKE ZIMEFIKA.
  BORAKUPATA KULIKO KUKOSA

  ReplyDelete
 9. NIMESIKITISHWA SANA NA HUYO BWANA HARUSI. YAONEKANA DHAHIRI KUWA HANA MSIMAMO KWANI DADA ZAKE WAMEMPUMBAZA. ANGEFUATA SHERIA ZA KIMAADILI KULINDA HESHIMA YAKENA YA MWANAMKE ALIYEMWACHA NDOA HAITADUMU KABISA KWANI HAINA BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU

  ReplyDelete
 10. jmani mm naungana na wenzangu kwamba huyo mwanaume hakuwa na mapenzi ya kweli kwanini asikae kuongea namhusika mpaka hanaamua kuchukua huamuzi wake mwenyewe alishapata nyumba ndogo toka zamani hapo halikuwa hanasubili sababu tuuuuu napia mawifi sio watu wakuwaambia kila kitu kwani wao ndio wachonganishi kaka yao hangejuaje kama sio wao? UMBEA TUUUUUUUUU

  ReplyDelete
 11. Hapana kina dada msimlaumu sana kijana huyu mi nadhani sio rahisi yeye kusikiliza dada zake pekee,lazima huyo mdada alikuwa ameshalalamika kwake na hii ya kwa dada zakeh ilimuuma sana akachukua uamuzi huo.

  ReplyDelete
 12. Huyo mwanaume kajidharaulisha tu katika jamii ya wastaarabu kajionyesha kuwa yeye ana "AKILI ZA KUCHANGIWA", Dume zima ukasikilize maneno maneno ya kiwifi wifi, toka lini madada wakamseme wifi yao vizuri? wapooo, lakini mmoja ktk mia! Inaonyesha kama ni kweli pengine gauni wamemnulia baya pesa wamechikichia, kwani yameshawahi kutendeka si ajabu.
  kuna madada walikula hela za kaka yao wakaleta gauni lishavaliwa si mara moja na wala halijakaa kiharusi harusi,la mmoja wa madada ambaye yuko uarabuni ili biarusi avae na viatu vya mama mkwe vishavaliwa na vikubwa sana (41) kwa biarusi, Wakati biharusi anavaa 36/37.

  ReplyDelete
 13. harafu huyu aloingia kwenye nyumba hii ajue na yeye iko siku atatoka kwa sababu bwana harusi hana msimamo hata kidogo
  nampenda mme wangu namshukuru kwa sababu alinipenda sana pamoja na vikwazo vya kila namna

  ReplyDelete
 14. Jamani, Hiyo hekaheka ya leo iwekeni wazi kwa mtandao jamani maaana hapo juu naona comments za sema mara bwana harusi ana dalili za umalaya, hana msimamo mara mawifi ndio wabaya ivyo twashindwa elewa kamili ni nani anamakosaaa, kumbuka hapo mwanzo kabisa kumesemwa kuwa bibi harusi anadaiwa kusema vimaneno mara harusi gani ya kimaskini, shera sijui ikoje.kweli me nashindwa toa comments kwa mkanganyiko huo wengine wako nje ya nchi na wengine twaweza sikilizia maofisini na wengine tuko maofisini ila kama ikiwezekana iwekwe yote kwa mtandao au la sivyo Clouds waanzishe online Radio tuwe twaipata kwa kutumia internet please Dina do something for us.

  ReplyDelete
 15. jamani mie sipendi mawifi wenye roho za kwa nini,sijui wanataka kuolewa na kaka zao..
  gauni la harusi raha yake uchague mwenyewe,hata kama watakusindikiza una haki ya kuchagua ki2 unachokipenda wangempa budget yake kama ye ana pesa angejiongezea mwenyewe ili mradi uvae ki2 roho inapenda
  mie nakwambia hao mawifi ndio wamemkaangia mbuyu mwenzao. huyo bi harusi mtarajiwa ashukuru Mungu mana angeenda kupata shida 2 huko ndoani, inshallah Mungu atakupa mwengine and you will have a wedding of your dreams

  ReplyDelete
 16. Sasa Dina kinachokuchekesha ni nini? hivo vitu vya kawaida mi mwenyewe siwezi kuvaa nguo ya bei rahisi kwenye harusi yangu.

  ReplyDelete
 17. inaelekea wachangiaji wengi hawako kwenye ndoa na hawajui vitimbi vya wanawake,wewe umeshamuona mke unayetaka kumuona anajali sana ufahari kuliko ndoa,cha msingi ni ndio sio gauni la haarusi kama sina hela nijilazimishe kufanya harusi ya gharama halafu tulale njaa kwa kuwa mke kataka gauni la fahari lazima uwe na mke ambaye umemchunguza vya kutosha,na kukubali kuishi kwa khali yoyote ile huyo aliyeachwa ni haki yake na ni fundisho kwa wengine ishi kutokana na mazigira yaliyopo ili siku ukikosa unajua ni kawaida,angekusumbua huyo bora ulivyo mtema,mwenye hoja za msingi anijibu

  ReplyDelete
 18. hakuwa na mapenzi ya kweli kabisa alikuwa anatafuta sababu

  ReplyDelete