KINA MAMA KAMA HUWEZI KUISHI NA MFANYAKAZI WA NDANI BORA UACHE...TUNAPOENDA WENGINE MTAFUNGWA JELA KWA UBAYA WA ROHO ZENU.

9:24 PM by

Kuna binti amelazwa pale hospitali ya mwananyamala ambapo bado tuna mfatilia,binti huyo alikuwa msichana wa kazi huko maeneo ya Mwananyamala hapa Dar es salaam alipokelewa siku 4 zilizopita pale hospital ya mwanayamala akiwa hoi taabani baada ya kubakwa,Manesi wanasema walimuhoji kabla ya kukata kauli juzi nini kulimsibu akasema yeye alikuwa mfanyakazi wa ndani kwa mama fulani(hapa manesi walituficha jina wakisema wao si wasemaji wa hospitalini hapo)...sasa siku ya tukio majira ya usiku huyu binti ambae ni mdogo alikuwa anapika mboga bahati mbaya akaunguza ndio huyo mama alipompiga usiku huo na kumfukuza nyumbani kwake.Baada ya kumfukuza huyu msichana asijue pa kwenda usiku ule akaishia kurandaranda ahatimae kuangukia mikononi mwa wahuni ambao waliishia kumbaka kwa zamu mpaka alipookotwa hajitambui asubuhi.


.Binti huyo ni mwenyeji wa mkoa wa Iringa Dar es salaam hamjui mtu hata mmoja zaidi ya mwajiri wake.Juzi ilishindikana kuongea nae maana alikuwa amekata kauli kabisa tena anakoroma mpaka manesi waksema tuombe apone maana lolote laweza kutokea......pia manesi walisema hawawezi kutupa habari nyingi mpaka tuongee na msemaji wa hospitali kuhusiana na hilo......Leo tena inalifatilia hilo.

Ila kina mama kuweni makini mtaishia kunyea ndoo jela,watoto wa watu kama hamuwezi kuishi nao wapeni nauli warudi makwao au usiwe na mfanyakazi wa ndani kabisa na si kuwafanya kama wanyama pls.

25 comments:

 1. Maskini imenckitisha kiukweli,cjui watu wengine wameumbwaje yan hawana hata chembe ya huruma,angalia mtoto wa watu matatizo yalomkuta,pengine kapata migonjwa ksa kuunguza mboga,thaman ya hiyo mboga inafkia vip na maradh atayopata au matibabu ya kumtibu huyo binti,watu wengine hawafkiri,mi nashauri huyo mama achukuliwe hatua za kisheria iwe fundisho kwa wengine mana c m1 wapo wengi wa namna hii,inatia uchungu sana.ASIA ALAWI

  ReplyDelete
 2. mxiii zake,wengine tunashida ya wadada wa kazi na tunakuwa watumwa kwao yeye anatesa watoto wa watu ,na yeye si anawatoto watafanyiwa mara mbili ya hivyo{yeye katika maisha yake hajawahi kuunguza nyama au kuvunja kikombe?} hao ndo walewale ukivunja kikombe utamsikia "ohooo unafikiri vinaokotwa,na kwa taarifa yako nakukata mshahara".....haihusu

  GOD IS GOOD ALL THE TIME,atamponya na asipona huyo mama ajue anadeni kubwa sana kwa MUNGU

  Ni mshenzi wa tabia sana,kama anaona kamshindwa kwanini asimrudishe kwa alimletea ili wamalizane vizuri,anajiona kafiiika eeh?

  ReplyDelete
 3. Dinah acha, acha
  kuna watu wanaroho mbaya katika dunia hii mpaka basi, ameshindwa kufikiria kama angekuwa ni mtoto wake wa kumzaa angemfanyia hivyo???
  kikubwa mfatilieni mkimjua na mkimpata huyo mama achukuliwe hatua hata kama huyo binti atakufa huyo mama nilazima ashitakiwe tu, lazima kwani ni muuaji. Nakutakia KAZI NJEMA mumy wangu.
  mama mario (tbt kisukuru)

  ReplyDelete
 4. Jamani huo ni unyama ulikithili,siku zote tuwe yunajiweka kwene miguu ya mtu kabla ya kutoa maamuzi.
  huo ni unyama.
  Dina inabidi tuanzishe club ya wana leo tena then tutakikaa pamija tutajua jinsi ya kushauliana na wamama na jamii kwa ujumla

  ReplyDelete
 5. mimi naona vyombo vya selikali viingilie kati hii inamfanya watu kukosa human right. watu wengi wamekuwa wakinyanyasa sana wafanyakazi wa ndani. kuna mama mwingine anakaa mabibo mfanyakazi wake mumewe na mwananae wa kiume walikuwa wanamtaka.Mwanae wa kiume alipogundua kwamba baba yake naye anafukuzia akamwambia mama yake kwamba yule baba anatembea na huyo mfanyakazi. kilichotokea yule mama na binti zake na mwanae wa kiume walimpiga huyo msichana na kumchoma na pasi. kesho yake wakampa nauli arudi kwao kijijini. kwa kweli inasikitisha sana ukisikia mikasa mingi inayowatokea wafanyakazi wa ndani.

  ReplyDelete
 6. wamama wa namna hii wapo wengi sana tena wenye elimu zao na vyeo juu!!
  kuna mmoja yeye house girl akiumwa hampeleki hosp. anamshindilia madawa ila watt wake wakiumwa house girl halali mpk mtt apone.
  kuna siku dada alidondoka huyo mama akapigiwa cm akaambiwa watu wamechukua taxi wanamkimbiza hospitali basi mama akafoka eti nani atalipa hiyo taxi (anafikiria alfu 3 za taxi na si maisha ya huyo mtt)
  kumbe wakati huo anapelekwa hosp yule mtt wa watu alikuwa tayari ameshafariki.

  ReplyDelete
 7. mmh dina inahuszunisha sana,umfukuze mtoto wa watu usiku, aende wapi?akamatwe dinah huyo mama,dinah mm nina kisa kimoja kilichonitokea mm na housegirl wangu, huwa nina tabia moja ya kuwatreat kama wadogo zangu, ila akijua huna maneno hufoki wala nini basi wanafanya wajuavyo wao,na mara nyingi huwa naajiri mke na mume wanakaa bycoter,mume anatakecare ya ulinzi na mkewe kunisaidia pale ninaposhindwa,basi housegirl 1 alinizoea sana, sijui alipandaje ngazi mpaka kwenye room yangu akakuta wallet ya mume wangu akatoa 2000 Eur,na mume wangu alikuwa yupo chumba cha gym mimi nilikuwa town, sasa nikakumbuka huku mjini natakiwa nichenji 3000eur ndio kujipapasa na kurudi home, roho yangu yote kwenye wallet nikakuta euro 2000 hazipo, nikaa kimya nikijua labda nilichukua na kuziangusha,nikapatwa na wasi kuwa h.g amezikomba,baada ya kujiakikisha, basi nikamwambia mdogo wangu, nenda kwa mlinzi na mkewe hakikiha hawatoi miguu pia waambie kam dada kapoteza pesa kam wanazo nipigie cm nisije na polisi, kawabembeleza gii, c nikaingia na afande akasachiwa h.g kakutwa na pesa zaidi ya zile nilizokusudia, alikuwa na dollar 700,nikajiuliza dolar amenikomba saa ngapi.polisi akamtia vibao 2, mimi kesho yake ubungo na mumewe kwenye basi kwao,mumewe acha alie maskini aseme dada mimi cjui kaibaje wala hajaniwakilisha, so hawa mahous girl dina some time nao ni wanyama sio ss tu tunaowajiri ndi wabaya,nikajifunza km ni boss act like a boss,ila isipite kikome kama huyo mwanamke mwenzetu.

  ReplyDelete
 8. Dinah mimi mwenyewe tokea Augost nimeletea mtoto,stori yake ni alikuja hapa dar na shangazi wa kufikia, basi kalipata mateso mengi kakaamua kakimbie, sasa ndugu yangu wa huko wazo ndie alimpoke na yy hana uwezo wa kuishi nae, sasa akaja kwangu nikambambia mlete, kwao ni dodoma,basi kanajituma si mchezo, kakatuzoea nikampa mama aende nako kwake akamsaidie mm, nilikauli kma kanataka nauli karudi dom, akasema maisha kwao mangu, sasa ndio dina nafikiria katoto ni kadogo niwe nakapa mshahara elf 25per month, na mama yy hanamfanyakazi wake wa tokea, nimefikiria may be kaishi tu kama mtoto wa family then nikaendeleze kwa ufundi charahani, mana kameishia la 4 au vyovyote, nakaonea huruma

  ReplyDelete
 9. Mdau wa kisa cha kuibiwa EURO 2000..ULILOFANYA LILIKUWA LA MSINGI,kwamba baada ya kuona kakuibia na ukaprove kweli kaiba ukamsafirisha na mumewe kwao safi japo walikosea kabisa tena ungeweze kuwashitaki.Mimi ugomvi wangu ni pale unapomfanya mtoto wa watu kama mbwa mwizi,mmeshindwana mrudishe kwao,kwao ni kwao tu hata kama maporini...

  ReplyDelete
 10. Dada Dina hata huku marekani watu wanaleta mahousegirl na wana wa treat kama mbwa. Kwa kweli inatia huruma sana, kibaya zaidi huku unakuta hao wadada hawana ndugu na kupiga simu nyumbani hawaruhusiwi basi unakuta wanaishi kama watumwa tu. wadada wa watu unakuta wamekondeana , hawana raha wala amani. Tanzania nako mbali sio sehemu utayosema watambea na mguu warudi na kibaya zaidi wengine hata mishahara hawalipwi, wakiulizwa wanajibiwa si nimekuleta marekani kwa pesa yangu? watu wengine wanaroho kama za ibilisi kwa kweli.

  ReplyDelete
 11. some tymes mahouse girl wanakera sana! hata uwahudumie vipi, mimi nilikuwa na msichana mmoja, Dina nilimpenda kama mdogo wangu, na nilikuwa nampenda sana ili nae awapende watoto wangu wa miaka mitatu, coz kama nikimchukia basi hasira zake zitaishia kwa waototo, kumbe nilikuwa najidanganya,
  sikumoja kaka mmoja jirani yangu yeye ni mlinzi (mmasai) akaniita, akaniambia watoto wako wanateseka sna, asubuhi huwa hawapewi chai, wanakula chakula saa kumi, vikitoka shule (ni mapacha) saa saba vinaambiwa vilale, vinafungiwa ndani hadi saa tisa, ndio vinapewa chakula, tena some tymes vinapewa kiporo toka kwenye friji hakipashwi wala nini, nilisikia tumbo kukata sana, nililia sana siku hiyo, huwezi amini sikumuuliza, niliamua kufanya uchunguzi wangu mwenyewe taratibu, sikumfokea, Siku moja, niko kazini yule masai akanipigia simu, akaniambia sikia wanao wanavyolia, martha kaondoka na kawafungia mlango kwa ndani, wanataka kujisaidia, mimi niko hapa na hakuna hata funguo, Dina,hapo hapo nikampigia dada simu, nikamuuliza uko wapi???? akanidanganya niko nyumbani, nikamwambia nipe niongee na watoto,akasema wamelala (wakati mimi nawasikia wanavyolia) (roho iliniuma sana nikamwambia waamshe nipe niongee nao, yule msichana akakata simu, aisee nilichanganyikiwa sana, basi nikaotka kazini. nilipotoka niko njiani yule masai akaniambia, mama wawili,nataka uamini kwa kuona, ukija fikia huku nyuma kwanza ili asikuone, na yatakayotendeka wala usikurupuke wewe tulia tu! ujikaze. nilipofika nikapita kwa nyuma, nikawa nimesimama namchungulia alipokaa yeye na watoto muda huo ndio wanakula, basi kachukuwa kiporo cha wali, bila mboga akawapa watoto wale, yeye alikuwa amenunua chipsi, samaki, na pepsi anakunywa huku wanangu wakimtazama, mwanangu wa kike akamwambia dada namimi chipsi, mtoto alirambwa kibao huku nikishuhudia, Dina nilishindwa kujikaza, nikajitokeza huku nalia, nikamwambia Martha, kwanini unawatesa wanangu hivi??? kwanini hujapika mchana?je sikuachii hela ya kutosha? akawa hana la kujibu, dina niliingia ndani nililia sana, nikatoka nikawachukuwa wanangu nikawaogesha maana walikuwa wamepauka kama chokoraa yani, nikamwmabia nipe hela iliyobaki nipike mwenyewe, akanipa 15oo/= namuuliza ingine iko wapi maana nilimwachia 4000/= akasema nilinunulia chipsi, (NASHUKURU MUNGU SINA MKONO WA KUPIGA) nikamwambia, sasa hicho ulichokula ndio hadi kesho, na ujiandae kesho tu! safari, sikutaki.
  USIKU NIKO SITTING ROOM. Akanifata huku analia, dada naomba unisamehe, sitarudia tena, maisha ya kwetu ni magumu dada, nimeshazowea huku, nakuomba nipe nafasi ingine dada, alilia sana, nikamkatalia, akaondoka usiku huo akaenda kwa mama mmoja wametoka kijiji kimoja, akaja nae kumuombea msamaha,nikaamua kumsamehe, huku nikiendelea kumfatilia, baada ya kama wiki tatu akarudia upuuzi wake, siku moja narudi kama Mungu yani, nikapitiliza chumbani, yeye dada alikuwa uwani na watoto, hakujua kama nimerudi,nikamchungulia dirishani, (DINA MACHO YANGU HAYAKUAMNI NILICHOKIONA) unajua yale mabrash ya kusafishia chooni???? basi yale ndio alikuwa anawasugulia watoto akiwa anawaogesha,
  mtoto wa kiume alikuwa analia kweli, huku akiwasugilia lile brashi tunalotumia chooni, nilitoka speed hadi nje, nikashindwa la kufanya zaidi ya kuongea huku nalia, kesho yake nikampakia kwenye gari kumpeleka kwao,
  WASICHANA HAWABEBEKI DINA, UKIWA MKALI SHIDA, UKIWA MPOLE ZOBA, hapa nafikiria kuwapeleka Boding wakakae huko sitaki tena mschana wa kazi, maana naona wote akili moja
  Mama wawili

  ReplyDelete
 12. anony wa juu hapo, kweli umenena, tusikurupuke tu kuwalaumu wamama hamjui kisa cha yeye mpka kumfukuza na hamjui hiyo mboga aliunguza kwa mazingira gani. tusikae kulalamikia side moja tu, wote ni binadamu, utakuta huyo mtoto kwa bahati mbaya alimjibu vibaya huyo mama na huyo mama akashidwa kuvumilia, anagalia pande zote mbili usilaumu tu waajiri.

  ReplyDelete
 13. Pole sana mama wawili kwa matatizo yaliyokupata, kwa kweli inaumiza sana. Hayo ni maumivu makubwa sana kwa mzazi, maana bora kuhadithiwa lakini ulishuhudia yote. Pia poleni sana na wote mliopata kadhaa za hawa wadada.

  ReplyDelete
 14. DUUH KIUKWELI HATUJUI KAMA HUYU DADA MZIMA AU KAFA.MAANA JANA GEA ALIENDA HOSPITALI YA MWANAYAMALA NA KUKUTA KITANDA ALICHOLAZWA YULE DADA KITUPU...NA MANESI HAWAKUTOA JIBU LA KUELEWEKA...SO KAMA AMESHAFARIKI MWENYEZI MUNGU AMPUMZISHE KWA AMANI KAMA NI MZIMA PIA NAMUOMBEA APONE AWEZE KUPAMBANA NA MAISHA YAKE...

  ReplyDelete
 15. asante Anonymous 3:55
  japo wanangu walipata shida sana, kumbe vilikuwa vikinyemwa chai asubh, vikiumwa njaa vinazunguka kwa majirani, aisseee inauma sana, mimi sitamthamini tena mschan wa kazi, ntapeleka kiaskar askar tu,
  yawezekana tatizo lilikuwa kwangu, kwa kuwa nilimpenda kupitiliza, coz kila weekend nampeleka salon, nampa nguo, yani nilimpenda kupitiliza, sassa nimekoma kumbe hawafadhiliriki hawa, ninae mwingine nimempata anamiezi miwili sasa, nae kaja na stail yake, siku nikishinda nyumbani labda week end, basi yeye ni kuumwa tu! hafanyi chochote ukimwamsha anasema naumwa sana, ukimwambia twende hsptl anasema ntapona, wakat nikiwa sipo radio saut hadi mwisho, Cd zitaangaliwa hadi basi, nikirudi tu! analala,
  mwenzenu kazi ninayo
  so niwashauri na wamama wengine, mwenzenu yamenikuta, tusiwe wapole kupitiliza, sometymes tuwe wakali napo pia tusipitilize, japo kwakwlei mateso ya wanangu kila nikikumubuka huwa naumia sana,
  ningekuwa na uwezo, nisingekaa na mschana natamani hata niache kazi nikae nilee wanangu, i wish ningempata msicha alietulia, na imani asingechoka kukaa namimi.
  wasichana wa kazi akili zao zinafanana kabisa yani. huyu mama hadi kufikia huko usikute amefanyiwe mengi sana hadi kumfukuza japo alichoafanya sio sahihi, naamini hivyo, tusikimbilie tu kuwatetea hawa, wanakera jamani ah!

  ReplyDelete
 16. mama wawili pole sana

  umenikumbusha rafiki yangu yeye alikuwa na mtt wa kiume wa miaka 3 na hili joto la dar basi mtt kila wakati anakunywa maji dada akaona mmhh huyu kutwa kukojoa na maji yamekatika akaona isiwe tabu akamfunga kamba mtt kwenye kidudu chake ili hasikojoe.
  hamadi siku hiyo mama mtu aliwahi kurudi ss mtt akamkimbilia mama yake chumbani akawa hawezi kuongea anatoka jasho, machozi na kashikilia kaptula mama mtu akabaki anashngaa ndo kumuangalia mwanae nusu adondoke. kidude cha mtt kimevimbaa kimekuwa chekundu kama kinataka kupasuka
  yaani mtt alikuwa anakojoa huku anahemaa! mama hakuwa na la kuongea zaidi ya kumdaka dada na kumtembezea kichapo cha kufa mtu maana hakuweza kuongea! na kumuondoa usiku huo huo maana mumewe angeua kabisa kwani wakifikiria wamezaa uzeeni alafu mtu anataka kuwauliwa mtt!

  Liz

  ReplyDelete
 17. napenda sana kipindi chako dina big pia hiyo kwa kweli imeniuma sana mtu hunamyanyasa msichana wa kazi unategemea nini na wakati yeye akiamua kuwaangamiza ni dakika tu jamani tuwe na huruma na mabinti zetu kwani mtoto wa mwenzio no wako tu

  ReplyDelete
 18. ni kweli kuna saa wanatutesea watoto wetu kama hatupo majumbani lakini katika kumlea tunawalea kwa kila stahili kwenye hukali unatakiwa uwajibike kwenye upole uwepo pia na katika mazugumzo kama mtu na dada yake uwepo pia sio kuwa simba muda wote aipendedzi watakuwa wakituona tu wanajifanya kuumwa tuwe makin

  ReplyDelete
 19. Dina
  mimi nina swali, nikweli kitendo alichokifanya huyu mama hakikuwa cha ubinadamu, badala ya kumfukuza, angesubiri asubuhi amsafirishe kwao, lakini mimi nina maswali, ambayo ntafurahi kama utanijibu,
  1. huyo mschana ameishi na huyo mama kwa muda gani????

  2. mlipata nafasi ya kuongea na huyo muajiri nae mumsikilize????

  3. mmeamini vipi kwamba kosa ni kuunguza mboga tu!

  baada ya kujibiwa, naweza kushauri zaidi,
  naungana na wewe kwamba kama ukimchoka bora umrudishe kwao na sio kumfukuza kama alivyofanya mwenzetu, ila nafsi yangu haitaki kuamini kwamba issue ilikuwa ni kuunguza mboga tu!. nahis sio kweli, lazima hako kasichana katakuwa kameficha mengine, wasichana wa kazi jamani wanajua kubadilisha maneno, wanajua kudhalilisha, asikwambie mtu, simtetei huyo mama, ni kweli alichofanya sio cha uungwana, (na pia mngefatilia usikute wala hakufukuzwa, labda alimfokea tu kawaida kama kumuonya, akaamua kutoroka mwenyewe, mngesikiliza na upande wa huyo mama) wanajua kuigiza USIPIME. anaweza kukuzushia jambo ukajuta kuzaliwa duniani hapa. ah! mie sijui kwanini mahouse girl siwaamini kabisa, mimi huwa sipendi kufoka, ila vikizidi namuita , swali la kwanza umechoka kukaa na mimi???? akisema ndio, basi namwomba avumilie nitafute mwingine ili yeye aondoke, simfokei, ntambembeleza hadi mwisho
  na kama akisema bado sijachoka basi namwambia mapemaaaaaaa, ADABU IFATE MKONDO WAKE, akiendelea sana namuondoa,
  Dina una mschana wewe???? natamani uwe nae, utayaamini nisemayo, wako wasichana wanaojua nini cha kufanya, nini kimeleta, na adabu tele, ila wengi wao, we!!!! moto wa kuotea mbali, siku ya mwanzo akija anakuja mdogooo kama piritoni, uso umemshuka kama kuku mwenye MDONDO. ngoja amalize mwezi, ajue kuvaa suruali, ajue kubinua kiuno, aanze kutongozwa, mh! haitajulikana nani bosi, nani housegirl
  wanatusaidia sana, ila mH!!! YAHITAJI MOYO MAANA HATUNA JINSI, LAZIMA TUISHI NAO TU!. mimi msichana wangu si aliwahi kutuma sms ya kumtongoza mume wangu???? tena mapenzi kabisa, mume wangu akanifata na kunionyesha ile messej, siku ingine anampigia simu kwa namba ingine anaomba wakakutane gest, mume wangu akirudi ananiambia wife , kuna mtu tena nimemsave jini, huwa anaaomba kukutana na mimi gest, kuja kugundua kumbe ni yule house girl, MWANAWANE NILIMSHUSHIKA KIPIGO. kikali sana tena nilimuita na mama yake, mama yake akamsema sana, kumbe ndio tabia yake, nilimshushia kichapo cha kufa mtu, nikamtimua,
  Juzi juzi nimekutana na anti yake akaniambia alifumaniwa huko kijijini kwao na mume wamtu, acha apawe kichapo na wanachi
  hawafai hawa wasichana dina
  wanaofaa wachache sana
  mama frank, kizuini

  ReplyDelete
 20. Dina
  mada hii imenigusa sana kwa upande wangu,
  but jibu maswali ya mama Frank nami naamini nitakuwa na nafasi ya kutoa ushuri hapo maana tunajifunza kupitia blog yako mpenzi wangu.

  Kikubwa nataka kusema kwamba, Dina wasichana wa kazi hawa, mh! tukaenao tu! kisa cha mama frank cha mschana kumtongoza baba mwenyenyumba, kiliwahi kunitokea hata mimi, mimi sikumpiga nilichofanya nilimsafilisha kesho yake. sikutaka tabu

  DINA WASICHANA WA KAZI nao wanatakiwa kuwa na roho ya kibinadamu, hata kama bos akikuudhi wawe wanakaa wanafikiria, HII ILITOKEA TABORA, miaka mingi iliyopita, bosi kacheleweshewa mshahara kazini, hivyo nae kachelewa kumlipa housegirl, ila alimwambia kabisa nitakupa siku nikipata tu!, walikubaliana na huyo binti kwamba asipewe mshahara, awe anahesabiwa tu! ili siku anayotaka kuondoka ikifika apewe zote akafanye biashara. sasa hyo mtoto akawa amebadirika, katikati ya mwezi kaanza kudai hela tena kwa jeuri, na ukali, basi yule mama akamwambia subiri mwisho wa mwezi nikupe baada ya kupokea mshahara kipindi hiccho ilikuwa mshahara 15,000 na amekaa mwaka mmoja tu, yule mama alikuwa hajazaa, umri umeenda sana, baadae ameshakata tamaa ndio akapata mtoto wa uzeeni basi akiwa mjamzito ndio akatafuta msicha wa kazi ili akijifungua amfundishe kazi na jinsi ya kukaa na mwanae wa pekee. siku hiyo kaondoka kwenda kazini basi yule msicha alichukuwa kuni, akafunga geti, akaenda uwani, akakoka moto wa nguvu, akachukuwa sufulia kubwa la kuchemshia maji akabandika, akatia mafuta akakachukuwa katoto akakalisha matambala mdomoni akakatumbukiza uchi wa mnyama, akafunikia, kisha kachukuwa mfuniko, kafunikia na Moto juu. kisha kaandika barua, mama nimefanya hivi kwakuwa unanizungusha kunipa pesa zangu, SAMAHANI.
  akaondoka zake, JIONI mama karudi anasikia harufu, kaita hasikii majibu, kuzunguka hadi uwani kakuta sufuria, ile kufungua kakuta mwanae kaiva kabisa, alianguka na kupoteza fahamu, DINA NI TRUE STORY SIO HADITHI, IMETOKEA.
  haya niambie, ni wakumlea huyu??? kwanini asengeenda polis kushtaki??? au hata kwa wajumbe, au kwaninin asiondoke na mtoto akamfiche mahali hadi apewe hela zake?? ndio amrudishe, kwanini alifanya vile. basi toka nione hivyo. sina hamu mwenzenu, bora niwapelekwa wanangu kwa mama yangu wakalelewe huko, maana siku tunakaaga haka kale katoto kalikuwa kanaitwa Daudi, kalikuwa kamekauka sana kam mti yani, hakuna ambae hakulia dina
  MSIWATEE HAWA. MKUBALI KUNA MABOSI WAKOROFI, NA PIA KUNA WASICHANA MAKATILI KUPITA KIASI
  mdau Orginal

  ReplyDelete
 21. mimi nashukuru nina mfanyakazi wangu wa ndani huu mwaka wa 6,anafanya kazi zake vizuri na anawalea watoto wangu vizuri. Ukitaka kujua mfanyakazi kama analea watoto wako vizuri,hata ukiwepo mwenyewe wale watoto unawaona wako karibu na msichana wa kazi. alipata mimba nje sikumfukuza aliempa mimba alimkataa,dunia ikamfunza nipo nae na mtoto wake,nikiwanunulia watoto wangu nguo na mtot wake namnunulia,kwa kweli namtreat kama mwanangu.Ndani huoni tofauti ya mtoto wake na watoto wangu.

  ReplyDelete
 22. sister dina kweli wanaochangaia hizi mada ni kweli yanatokea wasichana wakazi hata uwape nini hawalidhiki kabisa kwakifupi hata uwabebe na mbeleko gani hawabebeki kinachotakiwa ni kuishi nao katika mazingira ya kiubishi mfano sisi tunaondoka hasubui kwenda makazin bila kudamka na kumsaidia huyo msichana angalau japo kuandaa chakula cha mtoto angalau unakuwa unampunguzia bahadhi ya kazi sio kila kitu msichana ndipo hapo unajikuta mtooto wako anapewa chakula cha asubui mpaka amalize kazi zote ulizomuachia unaemtesa hapo no mtoto na wala sio yule bint kwa kumlimbikizia kazi bila msaada woowte wewe unajifanya kwakuwa ulishakuwa na msichana kila kitu yeye sio vizuri japo sio watu lakina saa nyingine msaada wa kumpunguzia kazi unaitajika la sivyo kila siku utabalisha wasichana kama pipi kwa swala la kila kitu msichana

  ReplyDelete
 23. Nakubaliana na Anony huyo wa 5:48am, inabidi tuwasaidie kazi kidogo sio kila kitu wafanye wenyewe. Tanzania kwa kweli watu tunachukulia vitu for granted, mimi nimeishi ulaya kwa kweli nimejifunza mengi. Sikuwa na housegirl kwa hiyo kila kitu ni mimi na mume wangu, kuanzia kutunza nyumba, kupika,kusafisha, watoto na hapohapo wote tulikuwa tunafanya kazi na pia tunasoma shule full-time. Lakini tuliweza yote hayo bila housegirl, tumerudi bongo wala housegirl hatumtaki maana tumeshazoea hayo maisha ya kujitegemea wenyewe, zaidi ya mlinzi na mtu wa kuja kusafisha nyumba mara 4 kwa wiki thats it. Kuweka housegirl naona nitaweza kuua mtu bure, maana akimnyanyasa mwanangu kichwa chake halali yangu. Because hakuna mtu anaweza kukutunzia mwanao vizuri kama wewe mzazi mwenyewe utakavyo mtunza.

  ReplyDelete
 24. mmh hiyo story ya mtoto kuchemshwa imenitisha haki ya mungu,lakini huwa najiuliza swali moja nipo huku UK for mda mrefu,sijawahi kuona wazungu hata weusi na wafanyakazi wa ndani na both couple wanafanya kazi full time,kwanini wanawake tanzania wasiige mfano esp nyumbani kuna msaada wa ndugu?unakuta mtu ana wafanya kazi wawili au watatu hao wote wanini?

  ReplyDelete
 25. Da dinna mi sitaki hata kuonga mahousegirl wanayanyasika sana

  ReplyDelete