NI MTANGAZAJI GANI WA HAPA RADIO CLOUDS ANAKUVUTIA NA KWA NINI?

9:33 PM by
Anold Kayanda...anafanya top 20 ya clouds fm na Afande......
Efraim Kibonde ...Mzeee wa magazeti ndani ya Jahazi.......jamani maoni yako nimeyaomba nikimaanisha utendaji kazi katika kukuburudisha wewe na si mvuto wa sura wala umbo....NANI ANAKUVUTIA HA PA CLOUDS FM RADIO?

Kila mmoja anafanya kazi yake katika kukupa burudani ndani ya radio yako ya clouds fm,amekuvutia sana..utendaji wake wa kazi unakuvutia na kukupa burudani...unaweza kumpa credit hapa,na hata kama kuna mahali hajakufurahisha pia wewe sema tu maana ni katika kuhakikisha burudani inaendelea ndani ya mjengo


Dj Bulla,Sophia Kessy,Antonio Nugas na Dj Tooshot...Bambataaaaaa


Babra Hassan na Gerald Hando...wanasikika katika power breakfast


Dj Fetty...katika Bongo Fleva na XXL


Gadna,Adam mchomvu,Jackline Kombe,Ibrahim Masudi,B12,Reuben Ndege.

Loveness Love...ala za roho na Adam Mchomvu


Gadna katika Jahazi la clouds fm na mkewe Ldy Jaydee

138 comments:

 1. Babra na Hando ni number one akifuatiwa na Ephraim Kibonde japo hapa naona hujamuweka. Hawa wote watatu ukisikiliza vipindi vyao hata kama umekasirika utacheka tu. Halafu ujumbe ulioko kwenye vichekesho au matani yao unakuaga na mafundisho mazuri sana na yanachoma ku moyo kama wahusika wangekuwa wanawasikiliza kwa makini

  XXL INABORE NA SUZY NA GEA WAMEZIDI MAMBO YA USWAHILI. SOPHIA KESSY NA MADJ WAKE (BULLA NA TOOO SHOOOT NAWAPA BIG UP

  ReplyDelete
 2. hi Dinah,its mariam,

  Today u got me, kwakweli navutiwa sana na dina marios, gea,gadna ananibamba sana na jahazi akiwa na kibonde, please tafuta picha ya kibonde ni muone, love big

  ReplyDelete
 3. wengine wazinguaji hamna mvuto wala nini!hao wa asubuhi wakina gerald na bi hassan wako juu sana

  ReplyDelete
 4. Na mpiga Big up Gea, kwanza kwa ufasaha ktk kusumulia jambo na pia ana vi tune vyake fulani kwenye sauti ambapo anajua wapi pakuvichomeka na wekea mkazo issue husika. na kicheko chake cha ki ....., kwa wengine siwezi jua sana manake mie waga nasikiliza power breakfast nikiwa njiani ofcn ikifika saa nne naweka leo tena mpaka jioni tena nikwia njiani jahazi!!

  ReplyDelete
 5. Babra Hassan na Gerald Hando they always make me laugh they like to blast each other when I listen at them I remember my bodies at university they are really fun. Their questions and answers always jazzy me, followed by Gadna D H he is gud he is a gud presenter he poses while he is talking some time he brings nice jokes i really like to listen jahazi.
  All Clouds presenter you are really gud you know how to entertain people am dying to watch your TV.
  Clouds FM mko Juu hamna mpingaminzi

  ReplyDelete
 6. Dina, labda ungeweka wazi kuvutia kwa nini hasa.Yaani ufanyaji wake wa kazi au utanashati(uzuri wa mtu-urembo...)....au unataka tu kujua kwa ujumla yaani kila kitu nilivyoorodhesha hapo juu.?

  ReplyDelete
 7. Dina mbona hujamuweka yule anayesemag asalam aleykhum ktk kpind cha jahazi?kumbe babra ndo mnene hivyo,ckutegemea,Gea na suzy hawajatoka vizuri,ai buuuuuuuula!kumbe yupo simple co kam adam mchomvu blazamen,fety kapendeza sana huyu yupo simple.

  ReplyDelete
 8. nlikuwa cmjui babra kumbe ndo bonge hivyo,yn tofaut na saut yake,napenda ucheshi wao ktk power breakfast akiwa na Gerald,kiukweli mi kpind ninachokpenda ni leo tena,na mtangazaji anayenivutia na yule ambaye huwa na Gadna ktk jahazi nmemsahau jina,kiukweli huwa nacheka sana nkmckiliza,wengine nao nawapenda hmna ambaye hanivutii.ASIA ALAWI

  ReplyDelete
 9. Adam aache ublazamen!

  ReplyDelete
 10. jamani nampenda Gadna,anajheshim alafu katulia flan yn co mtu wa papara,mstaarabu,anamvuto kfp yuko pouwa.jide kapata

  ReplyDelete
 11. Nampenda Gerald ananifurahisha sana,kuna cku alikuwa anaongea na bonge,kpnd hicho bonge alitembelea kwa wanyamwezi huko,asa bonge akamuuliza Gerald et unajua mnyamwezi akitaka kummuulza mwenzie huu mtumbwi wa nani wanasemaje?gerald akamwambia cjui,bac bonge akamwambia huwa wanasema WATOMBWAGA?gerald akamwambia asa njoo uwaambie wazee wa pwani km hawajakukmbiza,jaman nlicheka sana,hadi ss nkikumbuka huwa nacheka,nampenda san gerald,alafu dina weka picha ya bonge.

  ReplyDelete
 12. Dina huyo loveness ndo nani?m cmjui

  ReplyDelete
 13. anayenifurahisha wa kwanza ni wewe mwenyewe Dina. kwakweli unakonga nyoyo za mashabiki wako. Big up Dina.But wengine pia wanafanya vizuri japo mnazidiana. from my side sijaona anayefanya vibaya katika kipindi chake

  ReplyDelete
 14. Dina kiukweli mtangazaji anaenifurahisha hapo clauds ni Kobonde hasa akisoma magazeti kwenye Jahazi

  Kadada ka cnza

  ReplyDelete
 15. Mhhhhhhh Jamani Dina hapo kazi ipo
  Kwani mimi binafsi hakuna mtangazaji nisiyempenda hapo Clouds fm, unajua kwa nini? kwa sababu vipindi vyenu vyote mimi navipenda sana na sio kuvipenda kwangu tu nivizuri sana kuanzia Power breackfast, Leo Tena, XXL, Jahazi, Night express na kile kipindi cha watoto cha j'mosi mm nakipenda.
  Kikubwa labda mzidi tu kuviboresha ili viwe vizuri zaidi kwa mwakani. ila kwa sababu umesema tutaje wanaotufurahisha, binafsi mimi kama mimi
  1. Dina Marios
  2. Gadna Ggggggggggggggggggggghabash
  3. Gerald Hando
  4. B12
  5. Zamaradi, Suzy na Gea hawa wanaenda pamoja kwa upande wangu, kiukweli Clouds wote
  Adam mchomvu,Loveness, Jackline Kombe,Babra Hassan, Ibrahim Masudi,DJ fety, Reuben Ndege.mpo Juuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu zaidi.
  Mama mario (tbt kisukuru)

  ReplyDelete
 16. nafurahishwa zaidi na kipindi cha leo tena, na mtangazaji anae nikosha ni wewe hapo dina, wakifuatiwa jopo lako lote la leotena yaani: Gea Habib, zamarad, Suzy, bila kumsahau GGGGHabash. Watajwa hapo juu wanavutia katika kazi yao.
  Ni mimi Ann, wa Makongo

  ReplyDelete
 17. I real like U guys bu mh!!!! Fetty I like u mo. Ki ukweli uko juuuuuuuuu kip t up darling'gal.
  Ts Mima hapa.

  ReplyDelete
 18. GEA napenda sana hekaheka zako ila my favourite presenter ni Zamaradi

  ReplyDelete
 19. Mchofomvu ni nomaaaaaaaa!

  ReplyDelete
 20. mimi nina vigezo kadhaa ninavyovitazama ninapojaribu kujibu kile unachokiuliza.
  1. sauti ya mtangazaji
  2. ubunifu, uniqueness na kila siku a presenter should comeout with new ideas
  so generally kwa vigezo hivyo hawa wafuatao wapo juu.
  1. Ephahim Kibonde & Gadna (Sio kwa kuwa wanatangaza kipindi kimoja bali kwa vigezo wamefanana)

  Aliko, Tukuyu

  2. Babra na Gerald

  3. Gea na Adam Mchofomvu

  4. Fetty, Suzy, Sofia, B12 na Loveness

  5. Waliobakia kina Jacqueline na wenzake wanamaliza portion iliyobaki.

  Dina mbona mbaguzi, mzee wa chabo yuko wapi? hatujaiona picha yake pamoja na Bonge

  ReplyDelete
 21. dah!kazi kweli kuchagua.Wote mnafanya vizuri.Ila mimi Top TWO yangu ni
  1.Gerald Hando
  2.Babra Hassan
  Nawapenda sana na kipindi chao cha power breakfast.Nice!keep it up guys

  ReplyDelete
 22. MIMI NAWAFAGILIA SANA GERALD NA BABRA KATIKA POWERBREAKFAST HAO WANANIVUTIA SANA HASA KATIKA ZILE MADA ZAO ZA UKWELI NA UWAZI, HAO HAWAOGOPI KITU BABU NA HIVI NDIVYO INAVYOTAKIWA KUMCHANA(KUMPA UKWELI), KITI, AU CHOMBO CHA SERIKALI LIVE BILA CHENGA

  ReplyDelete
 23. 1.ADAM MCHOMVU
  2.DINA MARIUS
  3.Ephraim Kibonde
  4.Gadna G
  5.RUBEN NDEGE

  ata ukimuuliza LARRY KING atakupa same list...

  ADAM ni mmoja kati ya watangazaji bora kabisa AFRICA...i sometimes think pengine amekosa watu wa kumshauri vizuri...uwezo alionao,ata akina Kabelo hawasogei.yuko natural,mbunifu na ni mwepesi kubadilika kulingana na mazingira...

  ReplyDelete
 24. jamani mi mzee Kibonde, babrah,Gerald,bonge na mzee wa chabo...jamani napenda jinsi wanvyotangaza na kuwaeka mambo serious na kuyazungumzia katika lugha yenye kutokumfanya mtu apasuke kwa hasira, bali kuelewa na kujaribu kautafuta muafaka wake... yani hata kama we ni fisadi ukasemwa na hawa watu9MAFISADI NA WALENGWA KATIKA TOPIC ZA VIPINDI VYAO) waeza ona aibu ilihali unacheka na huwa naamini watu wanaolengwa hubadilika huku wakitabasamu....

  napenda aproach yao... wakati mwingine sio lazima kuweka ndita usoni katika kurekebisha mambo ka polisi,but do it in a funny way,tell someone that you are wrong while smiling and that person will change for sure..

  Ahsante Guys, maana mi nimetumia aproach hiyo ofisini, nyumbani, na kokote its working.. i see the result every day...

  kwa kipindi cha dada Dina, kukweli sijabahatika kusikiliza kwa muda mrefu, si unajua sisi wafanyakazi kokoliko ofisini lala salama nyumbani,,, but it seems watu wankifurahia, i wish nipate walau wiki nzima ya kupumzika nami nisikilize... keep up the good work guys...

  ReplyDelete
 25. Namkumbuka sana Kibonde alivyokuwa anatangaza katika tv fulani (ctn) kipindi hicho akiwa anasimulia kipindi cha michezo unaweza ukajikuta unanyanyua mguu unapiga hewa ukidhani ni mpira. Halafu kwenye magazeti jioni akikusimulia visa mahakamani utavunjika mbavu halafu ni mbunifu wa kuiga sauti za watu yaani weeee acha tu Kibonde ni number one. Naombeni kwenye Clouds Tv asikosekane kwenye kipindi cha michezo

  Number mbili ni Babra na Hando kwa pamoja. Hawa bwana ukisikiliza PB asubuhi wewe ni kucheka. Yaani wana utani mpaka basi na wakati mwingine utafikiri wanatongozana

  Sofia Kessy ile africa bambataaa unanikosha vya kutosha ukishirikiana na dj bulla. Number tatu yenu

  Ila kama kuna kutaja wa kwanza kutoka mwisho ni huyo mdada wa xxxl fetty na yule wa ala za roho loveness. Sina hakika kama tatizo liko kwa hao watangazaji wenyewe au ni nature ya kipindi chenyewe. Ila ukisikiliza mfano kipindi kama hicho cha ala za roho kutoka katika radio nyingine yaani unajikuta unabembelezwa na nyimbo zenye hisia kali hadi unalala na kusahau kuzima redio

  ReplyDelete
 26. You people you are all gud you are very unique compare to other presenter you are very funny this is very hard am telling you.my favorate presenter are
  Babra Hassan and Gerald Hando, and Bonge
  Gadna G Habash and Kibonde
  Adam Mchovu
  Dina Mario
  DJ Fetty
  They all make my day love you all

  ReplyDelete
 27. ujamuweka detective inakuaje dada dina?

  kiukweli kaka kibonde is the best presenter kwa hapo ana vionjo flani ambavyo kila jioni waga lazma nimckilize na magazeti yake kwakweli..

  ubunifu mwingine wa dogo anorld kayanda..i like him kip it up broda

  dina kiukweli waga sisikilizi sana vipindi vyako bt naamini unarock ile mbaya maana mara nyingi wife waga anacheka mwenyewe ananiambia mmh kweli kina dina machizi,, kuna cku nadhani mlikua mwasema vitendawili au methali alicheka sana..

  kip it up mamii

  ReplyDelete
 28. JAMANI NAMPENDA SANA SUZY MBEYAAA LAKINI HUWA ANANIFURAHISHA SANA NA VIJIMANENO VYAKE WAKATI WA CHACHANDU LEO...DUU AMEJALIWA MANENO MDOMONI LOOO SIJUI KWAMUMEWE INAKUAJE...PIA NAMPENDA MAMA WA KITCHEN PARTY YAKO LEO...DINA NAKUFAGILIA SANA AFU WATU WENDI WANASEMA NIMEFANANA NA WEYE...GEA JIANDAE UWE MC WA KPARTY YA MDOGO WANGU

  ReplyDelete
 29. JAKLIN NAPENDA UNAVOTANGA TAARIFA YA HABARI HUWA UNASOMA VIZURI SANA

  ReplyDelete
 30. JAMANI MI ANAENIVUTIA NI eFRAIM KIBONDE MZEE WA ASALAM ALEYKUM, WA PILI pJ MZEE WA KUDADIS INGAWA HAMJAMUWEKA NA MSOMAJI MZURI WA HABARI NI GEORGE NJOGOPA INGAWA NAE HAMJAMUWEKA MWISHO SAUTI YA GEA IMESHIBA WANAWAKE WENGINE IGENI.
  PENDEKEZO DINA PUNGUZA UBAGUZI WEKA PICHA ZA WATANGAZAJI WOTE HALAFU NAOMBA PJ ALIPO ARUDI NAMSUBIRI KWA HAMU AJE KUTUPERUZIA WENGINE MICHOSHO TU

  ReplyDelete
 31. Du! kiukweli mi sikufikiria hata ckumoja ka Babra Hassan ni mnene kiasi hicho huwa nadhani nibinti tu mwenye mwili wa kawaida bac sauti yakeinalipa sana kama ya mtoto mchanga ila kwaupande wanao nivutia ni 1. Babra,na kina gerald hando, paul james, na kwenye kipindi chenu cha leotena pamoja na Jahazi ya kina Gadna na Kibonde yani hasakibonde anaposoma habari za magazetini du anauwa ile mbaya na wengine walio bakia na wapenda wote jamani tuko pamoja kama one love ya Fiesta.

  ReplyDelete
 32. kiukweli mi i KIBONDE na GADNA nawapa namba 1,
  2. GERLAD NA BABRA
  3. SOPHIA KESSY
  4. GEA NA DINA
  5.ANTONIO
  WENGINE WANAFUATA

  ReplyDelete
 33. Kundi lote la Leo Tena, Dina, Gea, Zamaradi na Suzy! Yaani nikiwasikia tu mie Huku sina mbavu,hasa mama lao VIP, Gea,ananikuna mno!XXL ubrazamen mwingi asa Adam

  ReplyDelete
 34. feti- bomba (ila kipindi si mshabiki)
  Jackline- unasoma vizuri sana sana sana habari
  Bonge- unajituma kuliko
  Kibonde- uko juu
  Babla- napenda unavyolalamika lalamika

  tuambieni wale waanzilishi wa clouds enzi hizo Jyde akiwamtangazaji wako wp?
  kina Cyndy mwandanji, seven n.k. pia msiache kuwaalika ktk annivesary zenu as wao ndio founding presenters

  ReplyDelete
 35. Japokuwa wote mpo juu kwa namna mbalimbali, ila Clouds nzima hakuna mtangazaji km Ephraim Kibonde, mzee wa asalaaam alyaikum. Huyu jamaa ndiye anayekibeba sana kipindi cha jahazi, ni mbunifu, ni mchekeshaji ni muelimishaji na ni mchangamfu. Kwakuwa Clouds ndiyo radio namba moja Tanzania, hivyo basi Tanzania nzima hakuna presenter anayemfikia Kibonde.
  Ephraim Kibonde yupo juu saaaaaaaaaaana.

  aka Observer.

  ReplyDelete
 36. 1. Gerald Hando
  2. Gadna G. Habash
  3. Ephraim Kibonde
  4. Paul James

  I detest Loveness Love, she's is so fake in the industry!

  ReplyDelete
 37. yani on ma way to wrk lazima niwasikilize wakina barbra na gerald...nawazimia sana na bonge...katika upande wa kurasa za habari ni ephraim kibonde...habari kamili namzimia george njogopa...kwa habari za entertainment well ni timu ya XXl...kwa habari za jamii we mwenyewe da dina na namalizia kwa top 20 ya arnord kayanda namzimia jinsi anavyoweka nakshi...madj kama kawa bulla kwenye bambataa na steve b..sijajua sikuhizi venture anafanya nini?but namzimia pia

  ReplyDelete
 38. Eeehe hapa mwake jamani mimi hawa ndio wangu nawaona wananivutia kwa vigezo viwili Sauti, vichekesho, kuelimisha, na lugha fasaha
  1. Jamani Gerald Hando, Paul James, Babra Hassan
  2. Ephrahim Kibonde
  3. Dina Of course
  4. Gadna Habash
  5. Ditector wamefungana na BONGE

  Jamani kwa kweli nikiwasikiliza Gerald Hando, Paul James na Babra Hassan asubuhi huwa NASAHAU MADENI YOTE NINAYODAIWA wananifurahisha sana jamani wanastahili NO. 1 wooote . Dina TUNAOMBA UTUONYESHE Ditector wenu pamoja na Bonge.

  Hakuna kipindi kinaniudhi kama cha yule DJ Fetty sijui Feheee jamani kwanza nikiangalia dhana nzima ya chombo cha habari ni kuelimisha sasa huyu dada na wenzie wanaongea lugha za kupotosha KISWAHILI chetu kabisa. Wakati unajua kiswahili ndio kwanza kinaanza kupanda chati alafu unamsikia mtu anatambulisha mtu eti MWANADADA anamwita MWANADAFADA ndio nini jamani. Sidhani kama kuna kamusi ya kiswahili ina neno kama hili. Sawa sikatai ni kipindi cha vijana lakini tuangalie na IMPACT ya hayo maneno yanayotumika. Unamfundisha nini mtoto anayesikiliza, unamfundisha nini raia wa kigeni anayekuja kuekeza nchini kwetu na anahitaji kufahamu kiswahili? Are we doing the right thing? Sidhani kama chombo cha habari mtu anapaswa kuongea vitu kama hivi.

  Kusema kweli Mimi huwa nampenda Sana Dinna pamoja na Gadna, yaani akiwa anaongea na mwenzake au anamuhoji mtu alafu akaongea neno ambalo kidogo linaenda kunako sipo UTAWASIKIA wanapatwa kigugumizi kama vile wanaona aibu fulani hivi. Kwa kweli Dina na Gadna kwa jinsi wanavyoongea unajua kabisa huyu ni mtu wa aina gani. Wanaongea maneno ambayo una uwezo wa kusikiliza kipindi chao na mtu wa rika lolote lakini hao sijui kina ADAM MCHOMVU SIJUI FETYY NO PLEASE, WANATAKIWA WABADILIKE

  Nawasilisha - Violet

  ReplyDelete
 39. kati wa wote uliojitahidi kuwataja hapo juu sijaona kama DJ FETTY kuanzia tabia sura utanashati sauti na utangazaji pia. mnabishaaaaaaaaaaaaaaa keep it up baby gal

  ReplyDelete
 40. ...and the winner by split decision is Efrahim Kibondeeeeeeeee!

  ReplyDelete
 41. Dina Number 1 ni Kibonde wa pili ni wewe na kundi lako lote na wanaofuatia ni Gerald na kundi lake pia

  helen

  ReplyDelete
 42. jamani kama sijaweka picha ya mtu si kwamba nambania ni vile sina picha yake,lakini mimi ninachoomba taja tu jina lake na kwa nini,mnisamehe nikizipata nitawawekea.

  ReplyDelete
 43. Gerald Hando
  Gadna G. Habash
  Ephraim Kibonde
  Paul James

  These dudes are future Larry Kings or Jenerali Ulimwengu! They are really and very analytical. They can pass the message in any way be sarcastic, emotional, sympathizing. Yaani all weather. They are really into the industry!

  Of course I like their work and don't miss vipindi vyao

  ReplyDelete
 44. nawapenda wote na ningeomba wote muwe na vipindi ktk clouds tv..hasa dina na kaklin kombe ...anzisheni vipindi vyenu najua vitakua bomba sana ila jaklin endelea na taarifa ya habari upo juu sana...suzy mpeni kipindi cha mapishi ktk clouds tv

  ReplyDelete
 45. kwakweli wote mpo juu ila Ephrem K.Gerald Hando, Babra Hassan Lovenes Lov mko juu zaidi,Dina sauti yako mashalaah,Gea cheko lako aah mi hoi,ila nimestaajabu kuona Babra na Dinah mlivyo vibonge,nilijua ni viportable kama Dj Fetty!Duh asalam alykum.

  ReplyDelete
 46. Dina weka picha ya mzee wa njia panda pleeeeeeeaaaase

  ReplyDelete
 47. My favorite presenter ni Adam Mchovu. Power breakfast iko poa kwa Gerald na Paul James. Lakini Babra simpendi ana mashauzi sana na kujidai anajua sana wakati hajui. Gea pia uko juu.

  ReplyDelete
 48. kwa kwelui the first preasenter naye mpenda ni gadna the guy is so natural cool.....ila mpole tu baazzazi wa mwisho (ahahahahaahahha), but again gadner kama gadner hawezi simama peke yake kuna mtu anaitwa kibonde, yaani wanadepend to each other, huwezi kuwa na mtoto mpaka mimba itungwe yes, ndio uhusiano uliopo. gadner and kibonde are good, na ukitaka kuona kipindi kinaboa, awekwe garner na jamaa mwingine or kibonde na mwingine, yaani siku hiyo jaazi inakuwaga ovyo........

  mtu wa pili anayenivutia ni gerald, huyu ni mropokaji na yuko free sana na anavyojisikia kusema inasaidia sana, ila dada anamuharibia babrayuko artificial so ,much, pj is good in peruzi, na asipokuwepo unaona kudorora......ila bonge jamani big up you are doing good job

  wa tatu si wengine ni mashostito kaaaa umbea mnauweza, and you arebien, ila zamaradi kipiondi akimfahi amekaa kunata sister doooo....yeye anafaa zile yes....am,....am

  ReplyDelete
 49. vipindi vinavyonivutia kuvisikiliza tena kwa raha na tabasamu kubwaaa ni
  1. POWER BREAKFAST- WATANDAZAJI WAKE WOTE NAWAPENDA SANA AMBAO NI GERALD HANDO, BABRA HASSAN,PJ & BONGEEEEEEEEEEE

  2. JAHAZI- GADNA & EMPHRAIM KIBONDE

  WINNIE

  ReplyDelete
 50. mimi kwakweli wanaonikuna "in no particular order" Gerald Hando, Babra Hassan, PJ Mzee wa Chabo, Dinnah na Gea and last Kibonde na Gadna, kibonde ananifurahisha sana na habari za magazeti ya jioni yaani huwa sitaki kukosa. Ila Gadna kidogo huwa ananikwaza ambavyo yuko free kuongea maneno mengine kama vile anapenda sana neno kujamba au ushuzi kulitumia i dont think ni sahihi sana vile anasikilizwa na watu wengi ikiwamo ndugu na jamaa zake ana wakwe ana mtoto sijui huwa wanajisikiaje otherwise huwa nafurahia jahazi na asipokuwapo huwa sioni kama inanoga.

  ReplyDelete
 51. Number one kwa maoni yangu ni Gagna Habash na Number two ni Paul James kwasababu wametulia wanatangaza kwa ufasaha napenda sana utangazaji wao na sauti zao

  ReplyDelete
 52. ok me naona mtangazaji bora ni wewe dina,kibonde,gea,gadna,na anorld kayanda pia sauti ya reuben naipenda sana na george njogopa.
  sababu
  1.wabunifu
  2.sauti nzuri
  3.hints za kipindi
  kipindi cha laza roho atafutwe mtu mwingine anaweza kuandaa then loveness ndo aongee na kutuwekea miziki mizuri,apunguze maneno ya mapenzi

  ReplyDelete
 53. Kibonde is the best!
  Yuko natural, yuko all-weather,yuko well informed, ana sense of humour, yuko humble, mbunifu, na yuko flexible. Anajua afanye nini kwa wakati gani, anakuwa amejiandaa sana, mwepesi kubadili mwelekeo wa mawazo au mjadala kulingana na matakwa ya wasikilizaji. Kifupi ndie kiraka cha utangazaji Clouds!. Hakuna kipindi atakachotangaza akashindwa. Ndio maana huwekwa vipindi vingi kuweka uhai. Ana taarifa (data) nyingi katika nyanja mbalimbali duniani. Hata akipewa kipindi cha watoto, atawafurahisha sana. Mtumieni sana kwenye maandalizi ya TV Clouds, atasaidia sana kubuni mpangilio wa vipindi. Ana kipawa hicho. Kamanda nakupa 5.!

  ReplyDelete
 54. bahati mbaya ile live streaming website yenu niijuayo kwasasa haifanyi kazi tena, ila kwa kipindi nilichobahatika kuitumia na kusikiliza, nilivutiwa na Kibonde na GArdner.
  asante

  ReplyDelete
 55. kiukweli dina na wenzako mnanipa raha sana kina gea,suzy,zamaradi na wengine ni gadna.mz wa aslym alykm.samahani dina vp kazi ya kua mc unafanya jamani mana nataka unifanyie mana unafaa sana haswa wa kitchen party au dada gea tafadhali naomba jibu ili 2wacliane!

  ReplyDelete
 56. Gerald anatisha... ni mbunifu wa mada as a result ni starring wa Power breakfast.

  ReplyDelete
 57. Clouds fm iko juu,watangazaji wanaonivutia ni Gadna,Adam Mchomvu,Dina na E. Kibonde.

  ReplyDelete
 58. Kuna huyu mtangazaji anaitwa suzy kwa kweli anaboa na maneno yake ya kijiweni mara utamsikia Gea nimekumbuka kukuchamba, mara we anord umechokonoa chokonoa hapa njoo urekebisha. Dina umshauri mwenzio awe anachuja maneno ya kuongea mnasikilizwa na mamia ya watz wakubwa kwa wadogo, anashusha credibility ya kipindi mnaonekana kama mnapiga gumzo tu muda uende. namfagilia sana Gea mama wa hekaheka yuko juu

  ReplyDelete
 59. kibonde ananifanya chizi nikiwa naendesha gari kwani huwa nacheka sana naomba umfikishie aslam aleykhum yangu please. Rey

  ReplyDelete
 60. Nionavyo mimi.
  Babra H. Gerady H. wako juu sana. wakifuatiwa na Dina M. Gea H. Kapten G. Ephraim K. ki ukweli watangazaji wote wako juu sana Big up.

  ReplyDelete
 61. Ephraim Kibonde.. Assalaam alayykum... The one and only Kibonde..Wengine wanamfuatia kwa mbali mnooo..niskize mimi..

  ReplyDelete
 62. kiukweli tz nzima hii hakuna team ya radio station kama cloudz,ni radio ambayo huchoki kuisikia mwaya,kuanzia subuhi mpk kuchwe,likianzaaga hilo power,leo tena xxl,jijahazi,libambataa,nimalize na hiyo ala za rohoni,mh kazi wanayo wapinzani,mwenzenu hoi kwa loveness diva/dina jamani wapo juuuu,ingawaje wote mnafunika,Mussa Mgaya hapa

  ReplyDelete
 63. mimi binafsi yangu nampenda sana Ephraim Kibonde ebwana asikwambie mtu huyu mshikaji anajua kumfanya mtu aliyenuna acheke yaani nikipanda kwenye basi muda wa kutoka kazini never miss kusikiliza Jahazi wakati wa magazeti yaani unachekka mpaka basi.wengine ni we Dina,Gadna pamoja na Dj Fetty.

  ReplyDelete
 64. Mimi nawafagilia saaaana Babra Hassan, Gerald hando na Ephraim Kibonde. Mpo juu kiukweli mnatukosha.

  ReplyDelete
 65. Gerald Hando nakupendaa uko wazi sana na ni muelewa
  Gadna G. Habash umetulia sana halafu uko fast thinking capacity yako naikubali thats why una balance na Ephraim.
  Ephraim Kibonde ur so creative and talented.

  Paul James unajitahidi sana unapochambua magazeti mi huwa lazima niwasikize kila siku.

  Vipindi vingine huwa nakuwa mzigoni so sipati muda wa kuvisikiliza.So no Comment ninachojua Clouds wote mko juu.

  ReplyDelete
 66. gerard na babra ndo mi naona ni watangazaji wazuri,lakini sauti ya huyu dada loveness love...huwaga ni sooo!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 67. mzee wa salam aleykum, nomaaaaa

  ReplyDelete
 68. Always EPHRAHIM KIBONDE his smart.

  ReplyDelete
 69. KWELI MMETUFIKISHA KUNAKO,,
  BABRA HASSAN NAMPENDA KUPITA MAELEZO HANA MAPOZZ ALIKUJA ARUSHA ALICHEZA MZIKI NA WATU NA BILA MARINGO HUYO ANACHUKUA NAMBA MOJA,,PAUL JAMES ,,GERALD HANDO ,,GEA MIE KICHEKO CHAKE TU KWA KWELI HATA KAMA NILIKUWA NA HASIRA NIKIMSIKIA TU KACHEKA NA MIMI NAFARIJIKA SANA,,, DINAH WE UNA MAPOZZ SANA UNA KUJISIKIA FULANI HIVI PUNGUZA KIDOGO,,EPHRAIM KIBONDE UKO JUU SHEMEJI GADNER NDO USISEME KWA UJUMLA CLOUDS MKO JUU ILA WACHACHE NDO MNA MARINGO YA HOVYO HOVYO.

  ReplyDelete
 70. nampendag huyu diva,yuko poa sana,wengine wote pia big up

  ReplyDelete
 71. kwa kweli me nimetaja kati ya wale nnao wasikiaga. nasikilizaga PB asubh nikienda kazini na Jahazi on the way back hm vipindi vya mida ya kati sina time inaweza ikapita hat miezi 6 sijasikiliza, hivyo ambao sijawataja msihofu, sijawasikia. I hope wote mko juu kama mkungu wa ndizi

  ReplyDelete
 72. Binafsi sitaki kumtaja ni mtangazaji yupi wa hapo clouds anafanya vizuri zaidi,kiproffesion mm ni mtangazaji pia na ili niwe poa zaidi huwa nachukuwa muda mwng nnapokuwa free kusikiliza redio zingne ikiwemo clouds,naona mko poa serious na mnapiga kazi kwelikweli.
  Ila sasa kuna huyu wa sasa anaitwa Loveness Love,duh kiukweli huyu mtangazaji nashindwa kumuelewa kuanzia kwny blog yake mpk lifestile ya maisha yake japo sina hakika anaishi vp,naomba leo nizungumzie kikazi zaidi.Loveness anafanya kipindi cha Ala za Roho saiv lakini hakuna kpnd kinachoboa clouds katika miaka kumi toka ianzishwe kama kipindi hiki cha Ala za Roho.
  Nomba nitoe sababu,nahisi Loveness si mtangazaji,au si mtu aliyekuwa na ndoto za utangazaji tangu alipokuwa mdogo,nahisi zaidi ndoto zake zilikuwa ni ustaa na isingejalisha ni ustaa wa namna gani coz zaidi anachokifanya katika Ala za Roho ni personal interest za kwaker mwnyw,ndio mtangazaji pia ni binadamu na ni kawaida kuwa na vitu unavyovipenda but personal interest zisiingilie kazi unless otherwiz utakuwa unaboronga,tunajua Loveness anampenda sana Beyonce,sawa hatumkatazi lakini isiintafie Ala za Roho,Loveness hajui kuchagua muziki wa kucheza,yeye anacheza nyimbo azipendazo yeye zaidi,mara zote tumezoea kusikiiza muziki wa taratibu slowjams n.k katika vipindi vya mida kama ya Ala za Roho lakini imekuwa tofauti sana kwa Loveness,kwa Loveness samtimes tumekuwa tukichezewa r&b hasa zile zny tempo ya juu(dancables).
  Kitu kingine nahisi Loveness huwa haandai kipindi b4 hajaingia studio coz amekuwa na topics ambazo zinakuwa raised katikati ya show,nahisi kama anapokuwaga kwenye show ndo anapata wazo na kuli-present palepale kitu ambacho nafahamu ni out of proffesion,vilevile amekuwa ha-conclude topics ambazo zimekuwa zikichangiwa na wasikilizaji,yaani topics zimekuwa mara nyingi zikiishia hewanihewani tu,pia amekuwa akitumia kipindi samtymz kuzungumzia mambo yake binafsi na kujisahau kuwa yuko redioni na anasikilizwa na mamilioni ya watu.
  Hayo ni kwa uchache tu kati ya mengi mapungufu nnayoyaona katika kipindi hcho ambayo naamini yakirekebishwa Loveness atakuwa ni very good presenter coz ana sauti nzuri ya kuvutia na amabyo inafit sana kwenye kipindi kama hicho au asikilize vipindi vya zamani vya muda huo alivyokuwa anafanya Tarrence au Sophia Kessy.
  Thanx Dina!!!!!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 73. I love all you guys, keep it up!! Hivi iyo clouds TV itaonekana mpaka mikoani? me nipo A-town kama itafika it will be awesome.
  Keep it up guys, cheeeeeeeeeers

  ReplyDelete
 74. HEBU DINA TUANDIKIE HIYO BLOG YA HUYO LOVENESS TUCHUNGULIE KUNANI

  ReplyDelete
 75. DINA WEKA BAC HIYO WEB SITE YA HUYO LOVENESS MUMY.

  ReplyDelete
 76. wadau wa loveness aka sauti ya kutoa nyoka pangoni salam zenu hizo hapo.
  www.diva255.blogspot.com
  Dina usinanie hii kitu bana sie ndo wadau wenyewe!
  Alafu nikija kwenye pwent...
  Me ntakuwa na top 3 tuu basi.
  1.Arnold kayanda
  2.ephraim Kibonde
  3.Loveness Love
  kwanini?nimeangalia creativity,tone of voice,exposure of whats goin on outside the world.

  ReplyDelete
 77. Yani asante kwa kuuliza hili swali, kiukweli hakuna kama Gadner na Kibonde ni nomaaa....ubunifu wao haupimikiii,.. Gerald, Kayandaaa na crew zimaa la XXL mkoo juuu....

  ReplyDelete
 78. EFRAHIM KIBONDE, WATANGAZAJI WA KIPINDI CHA POWER BREKFAST. hao ndio watangazaji ambao wanatangaza vizuri pia wanafurahisha,wanaelimisha,wanaeleweka katika vipindi vyao. Sio kwamba vipindi vingine ni vibaya la hasha ila hao na hivyo ndivyo vinaavyo nipendeza.

  ReplyDelete
 79. DINA!...Pls tuitie kibonde atupigie salaaaaaaaaaaaaam alaikum ktk uwanja wetu huu....japo kwa maandishi....almost kila alie comment kamtaja aisee...NEXT YEAR ntakupigia debe uwe msimamiz mkuu wa uchaguz pia,u seem to be the best referee.

  ReplyDelete
 80. Nampenda Zamaradi coz she is CNN/BBC material...nilipomsikia siku ya kwanza nilishtuka nikaulizia ...huyu dada ni nani? kwa kweli nilivutiwa sana na sauti yake...kaza buti zama iko siku utakuja kuniambia...tuombe uzima...
  Mwingine ni Kibonde...kaka amebarikiwa na kipaji kwa mola...anauwezo mkubwa wa kutangaza iwe habari, matukio, kuiga sauti au lafudhi za makabila, watu etc...keep it up bro...god bless

  ReplyDelete
 81. Napenda pia sauti ya Babra...she is good...

  ReplyDelete
 82. CLOUDS KAMA KUNA KIPINDI KINABOA NI KILE CHA ALA ZA ROHO SIJUI MTANGAZAJI LOVNESS LOVE, MIMI USHAURI HUYO BINTI AWE COACH TENA AMA KIPINDI KITOLEWE, AM SURE YOU ARE CAPABL TO DO IT BETTER.

  ReplyDelete
 83. Angela tbt kisiwani said
  Kiukweli clouds napenda kuisikiliza maana huniondolea upweke wakati ninapokuwa mwenyewe! Yaani utaelimika sana na kuburudika mno. Ila mimi ni mnazi wa PB,Leo Tena,Njia Panda,Habari na Jahazi la Captain vingine kiukweli siyo mshabiki sijui shida nini nahisi wale wenzangu na mie wanapata tabu pia hususan ala za Roho!
  Vigezo ntavyotumia hapa ni kama vifuatavyo:uelewa wa mambo kwa kina,uwezo wa kuwasiliana na hadhira vema,maandalizi kabla ya kipindi na kukiendesha kipindi kitaalamu na mwisho kabisa ni sauti nzuri whether nzito au nyepesi. Na wafuatao ndiyo wanaonivutia Clouds FM;
  1. Ephahim Kibonde
  2.Gerald Hando&Paul James
  3.Gadner Habash
  4.Njoroge
  5.Dinna Marious
  Wengine siyo kwamba hawafai la hasha wanjitahidi lakini katika tano bora yangu hawapo maana hawanishawishi.
  Ahsante DM maana kwa hili mtajua washabiki wenu ni wepi na wanawa-rank vipi!

  ReplyDelete
 84. Wanao vutia Clous FM 88.4 DSM.
  1.Garder Habash
  2.Efrahim kibonde
  3.Dina Marious
  4.Shankupe Geha Habib

  Chipukizi:Antonio Nugas.Ushauri apige shule ya kutosha atakuja kuwa momba mbaya.

  ReplyDelete
 85. Kiukweli siyo msikilizaji wa vipindi vyote vya clouds..... lakini ninasikiliza sana Powerbreakfast na Leo tena. PB wote wapo juu coz kila mmoja wao anaburudani yake, including Bonge. Then Leo tena Dina ni muhimu sana, Gea na Suzy wananiburudisha sana hata kama wana maneno ya kiswahili sana lakini hayo ndo maisha halisi ya baadhi ya watanzania wenzetu na ni burudani pia.

  Hongereni sana wote kwa sababu mnafanya kazi kwa moyo na upendo wa dhati kwa radio yenu. God bless you all!

  ReplyDelete
 86. MAONI YANGU NI KWAMBA, PAUL JAMES, ANTONIO NUGAZ,EPHRAIM KIBONDE NA ANORD KAYANDA NDIO THE BEST HAPO CLOUDS, NIMECONSIDER ZAIDI UELEWA KATIKA VIPNDI WANAVYOENDESHA.

  ReplyDelete
 87. Maoni yangu ni kwamba, tukianza na ubunifu ni wafuatao;
  1 Gelard Hando & Barbara,-baraha
  2Kibonde-Aslaahm
  3Adam-mpango mzima
  4.PJ-mbuzi karamba reli
  5Gea-Mama Lao.

  Kujenga hoja;
  1 Hando- kaa chonjo,nk
  2Gea-Hekaheka
  3Said Bonge
  4Dina

  Kibonde ananikela papara sana.....tulia unapojadili mada kama watu wa PB, Dj Fetty,Reuben,B12, Mashauzi sana hasa ukija hapo mjengo kama sio super star wanakuangalia tu hata salaam upewi. All in all PB is my best show followed by XXL because of Adam,Jahazi Kibonde, Leo Tena I feel relaxed during Chachandu la leo.

  ReplyDelete
 88. dah! ili ni bonge la puzzle. kiukweli clous wafanyakazi wote mpo juu, mi nawapenda kupita maelezo hasa da dina,Gerlad,Babra na Gadna. kiukweli ningependa cku moja pata dinner nanyi coz lov u much. All da best guys!

  NAIMA HASSAN WA MWANZA

  ReplyDelete
 89. DUUUUU!!!! YAANI NAOGOPA KUPATA LAZI YA MOYO WANGU PINDI NITAKAPO KUFA,BILA YA KUSEMA KIPINDI CHA LEO TENA KILIVYO BOMBA KUANZIA SWEET WANGU DINA,GEA HABIBU NA DADA MTATA SUZZII. NAWAPENDA SANA

  HUSSEIN NGAHUNGULA (chuo cha ukonga magereza -dsm )

  ReplyDelete
 90. Jamani huyu Jackline Kombe anaolewa lini? au yule mchumba wake wa Uingereza kamtelekeza?, kama mna habari tafadhali zidadafueni tujue

  ReplyDelete
 91. mapresenter nnaowakubali ni;-
  1.Babra na Gerald
  2.kibonde
  3.Nchakali
  wengine wanafuatia

  nnayemchukia ni m1 tu anayejiita lovenes(anaichafua Redio)

  ReplyDelete
 92. MBONA PICHA ZA GEA NA SUZY HAZIPO? MIMI NAPENDA SANA UTANGAZAJI WA GEA SANASANA SAUTI YAKE

  ReplyDelete
 93. Ephraimu
  Gerard
  Dina Marios
  Gadner G

  ReplyDelete
 94. Mhh yote yameshasemwa kiukweli lovenes love anaboa sana, Kipindi chake ni kizuri ila ila mtangazaji ndo hakuna. na Zamaradi bado hajapata kipindi yani haendani kabisa na kipindi chako Dina. Zama atangaze habari hapo najua tutainjoy sana mana mana usistaduu wake na kipindi chako ni tofauti ila anasauti tamu kuisikiliza dat is y napendekeza atangaze habari najua tutaenjoy zaidi hapo. Yani ukimtoa huyo diva Clouds ni bomba na vipindi bomba watangazaji bomba. kiasi wengine hua tunahisi kupungukiwa kama hujasikiliza clouds. Asubuhi bwana ndo utajua utamu wa clouds, umeamka umeota mindoto yakutisha ukiwasha radio tu wale viumbe wanakusahaulisha kila kitu.. yani hata foleni barabarani haichoshi kama umefungulia clouds, usiombe sasa siku eaphone za cm zimehabirika halafu unakutana na bonge la foleni hapo ndo utajua jinsi gani power breakfast walivyo na umuhimu. Nihayo tu kwa leo

  It's Me. Mam Shekhani

  ReplyDelete
 95. Kweli, Clouds nawakubali, Dr, Mataso, reach me so I could contribute to your progs, mkirway@yahoo.com

  ReplyDelete
 96. helloooow dinna naitwa emma kaaya,ni mpenz sana wa clouds fm...especially power breakfast na jahaz...ivi vipindi viwili vina nijenga sana katika nyanja tofaut...nawakibali first:kibonde,,2nd:gerald hando,,3rd:paul james(pj) and finally jirani gadner!!!!

  ReplyDelete
 97. mimi babu ni namba moja na timu nzima ya pawer break fast nawafagilia sana maana siku ikipita bila kuwasikia uwa nakosa amani sana moyoni mwangu siku nzima

  ReplyDelete
 98. aaaaaaaaaaaaaaaaaahhhh? ndio maana mjawapa air tyme kwenye TV kwasababu watangazaji wenyewe wazee lakini mmefanya vizuri kuwapa kidogo wenye mvuto kwenye TV kama unajijua mmbaya usichonge kwenye kipindi chako umenisikia

  ReplyDelete
 99. zamaradi acha njaa umetukimbia c2c umekuja uko alafu una act kama umeishi mtoni miaka kazaa iliyopita sasa umeenda CCM japo umekuwa CHALIIIIII? Pole usikimbie hapo mjengoni usiwe kama MPENDO ZOEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

  ReplyDelete
 100. MIMI NI MPENZI MZIMA WA SOCIAL FRESH. YANI NAMPA SHAVU SANA MTU MZIMA REABEN NDEGE KWANI NI MKALI ILE MBAYA.NAPIA ANVYO WA HULIKA WATU HUWA NAPENDA SANA HICHO KIPINDI NA KUJI EPRESS NA TIGO.CHAAAAO MZAZI

  ReplyDelete
 101. MIMI NI MPENZI MZIMA WA SOCIAL FRESH CHA KILA JUMAMOSI. YANI NAMPA SHAVU SANA MTU MZIMA REABEN NDEGE KWANI NI MKALI ILE MBAYA.NAPIA ANVYO WA HULIKA WATU HUWA NAPENDA SANA HICHO KIPINDI NA KUJI EPRESS NA TIGO.CHAAAAO MZAZI

  ReplyDelete
 102. dah unajua nilikuwa simjui babra sasa nimemuona japo kwenye net mana mi lile cheko lake kwenye power break fast na wale jamaa kila gerad wanamchekesha sn...ila dah emphraim kibonde yupo juu siku zote.... keep it up kaka.

  ReplyDelete
 103. nilikuwa sijawahi muona Babra na Hando, ila japo ni kwenye net yatosha. ki-ukweli jamaa wa power-breakfast mko juu kinoma hadi mmenifanya ninunue kiredio kidogo nalala nacho na ikifika saa 12 asubuhi niko nanyi hadi tatu. big up! your critical analysis of issues shows how serious you are, I think you deserve to be there. By Magani Udsm.

  ReplyDelete
 104. Babra na Hando nawapa kura ya kwanza ki ukweli they realy do power my breakfast wanakufanya uchangamke na ufurahi hata ukitoka usingizini
  My second vote goes to Adam mchomvu na Nchakali hawa wanamautundu flani ambayo yako so funny wanajua kile nini msikilizaji anataka hasa kwenye crazy furahi day Adam hua anakua crazy kiukwelii
  With B12 alikua mzuri kinoma by then ila siku hizi amekua akija na swaga flani ambazo zinamfanya asikue real, he should try to remember the real him and be it
  Fetty is good she will always be good and the thing that makes her be good is because she is herself and never pretend life it seems alivyo ndani na nje ya kipindi ndo real life yake, keep on beeing real dear sis....
  Otherwise wote mko poa, thats it

  ReplyDelete
 105. nakupenda dina na naipenda sauti yako

  ReplyDelete
 106. GEORGE NJOGOPA............nashangaa mmemsahau,kulikoni????huyu bwana mi kwangu ndio namba 1,anyefuatia ni GERLAD HANDO... HASA KWENYE ILE KAAAAAAAAA CHONJO!!!!HOLAAAA

  ReplyDelete
 107. NYOTE MNAFAKAZI VIZURI KUTOKAKANA NA STYLE YA RADIO YENU MNAJITAHIDI KUVUTA WASIKILIZAJI KWANI VILE MNAVYOTANGAZA NA AINA YA UTANGAZA WENU NDIYO JINSI MNAVYOPATA AINA YA WASILIKIZAJI MNAFANYA VIZURI LAKINI MWAMBIE,SHAFIII DAUDA,IBRAHIMU MASOUD,PJ NA HISI WANACHAMBUA ZAIDI SPORT KULIKO KUTUPATIA TAARRIFA MPYA LABDA NA KOSEA AU HUWA HAWAKAI KAMA WAANDISHI WA HABARI WANAKUWA KAMA WATARAAMU WA SOKA LAKINI WANAFANYA VIZURI KUTOKANA NA STYLE YAO HONGELENI MUNGU AWABARIKI MWAMBIE KIBONDE ASAALAAMALEYKHUM.LISUNGU DAVID KAMBONA

  ReplyDelete
 108. George kanuti njogopa nakupenda sana, you present news very well haswa kwenye news feature ya satoo, kwanzia 7.30 to 9 napenda sana, i wish nije nikuone one day unifundishe news presentation styles like tonations, rythms, microphones positions and soforth, like you.Its Amina J

  ReplyDelete
 109. hi! i lik diva loveness love, i like the show ala za roho, 4sure she present wel, try to sorve problem/conflict it`s all about relationship, chich it happen in real life,so keep it up.

  ReplyDelete
 110. aah kibonde na ncha kali noma, b12 alikuwa zamani siku hizi kawa tozi na kapoteza maana

  ReplyDelete
 111. MI NAMKUBALI SANA EFRAIM KIBONDE NA GADNER G HABASH KTK KIPINDI CHAO CHA JIONI,HUWA WANACHANGAMSHA WATU SANA WARUDIPO MAJUMBANI WAKITOKEA KAZINI,ILA DINA MDOGO WAKO LOVENESS LOVE KUMBE NI MTU MZIMA MI NILISHANGAA KUCHEKI WEBSITE YAKE ETI AMEWEKA PICHA YA STAR MMOJA MWANAMUZIKI WA KIMAREKANI ANASUBUTU KUUTANGAZIA ULIMWENGU KUWA HUYO NDIE MWANAUME WA MAISHA YAKE!! NILISHANGAA KWA MTU KUJISIFIA UONGO AMBAO HAUNA HATA CHEMBE YA UKWELI,NAJUA YUPO KTK MAHUSIANO NA MBONGO YEYOTE HAPO ILA AKAAMUA KUMKANA NA BADALA YAKE AKAJISIFIA UONGO KWAMBA YUPO KTK MAHUSIANO NA STAR HUYO WA KIMAREKANI,HAILIPI WALA HAINA MAANA KUJISIFIA UONGO ESPECIALLY INAPOKUWA NI MTU AMBAE KILA UKIPITA MITAANI KATI YA WATU KUMI NANE WANAKUJUA!MWAMBIE NI AFADHALI ANYAMAZE KULIKO AONGEE KWANI AMEJIVUA UTUPU MBELE ZA WATU,ok kwa ushauri zaidi mwambie anichek jimlak34@yahoo.com

  ReplyDelete
 112. I like you guys you normally make my morning napenda sana sauti zenu given that I would like to praise your creativity I would like you to start a talk show. I will be very much willing to assist with planning and implementation.

  Jibril

  ReplyDelete
 113. Dina Marios noma,

  ReplyDelete
 114. Aaaaaaaah! nani mwingine zaidi ya DINA MARIOUS

  ReplyDelete
 115. jamani simpendiiiiiiiiiiiiiiii lovenesslove sijui anajiita diva, kwanza mbayaaaaaaaaaaa misifa kibaoooooooo, nampenda, dina, gerard, na kibonde.

  ReplyDelete
 116. Kwangu mimi list ni kama ifuatayo?
  1.Gadna Habashi(ingawa kaondaka laikini mchango unaonekana)
  2.Gerard Hando-yuko wazi sana
  3.Babra Hasani
  4.Dina Marios-Creative
  5.Milard Ayo(mpya,namtabilia kuwa the best presenter kwenye Cloud radio kijana atafika mbali anafanya utafiti wa mambo)
  6.Efrahim Kibonde
  7.Gea Habibu(Hekaheka zinafahamisha na kufundisha jamii pia anapresente ipasavyo)
  8.Regina Mwalekwa(mpya-anakipaji)
  9.B12-mbunifu
  10.Adam mchomu-vituko
  11.PJ-Chabo
  12.Bonge-tafakari
  13.Zamaradi - Movie
  14.Fetty-Huyo mdada ni mzuri lakin yuko simple mpaka anatia raha.
  15.Reuben Ndege Eglish imetulia
  16.Anardo Kayanda
  17.Jelly Minja na Country Music.

  Vipindi,
  1.Power Breakfast
  2.Leo tena
  3.Amprifire
  4.Jahazi
  5.Easly Sunday
  6.XXL
  7.Nyimbo za dini
  8.

  ReplyDelete
 117. Kwakweli watangazaji wote wa cloudz mpojuu sana mnatangaza vizuri vipindi vyenu ndiyo maana radio yenu ipo juu sana lakini naomba nitoe mtazamo wangu.
  1.Ephahim Kibonde
  2.Babra na Gerald
  3.GEA NA DINA
  4.Gadna Habash
  5.Adam mchomu na bonge
  hawa wote nawapenda kwa utangazaji wao katika vipindi vyao tena wanavionjo ambavyo uwa wanavitumia kwenye vipindi vyao ambavyo uwavutia watu wanafutilia vipindi vyao.big up cloudz.

  ReplyDelete
 118. DINA mimi nawezasema umenibania naomba unitafutie picha mzuri ya gea habibu ili nimuone manaake sipati picha jinsi alivyo na anavyoendesha hekaheka mtaani mdada ametishaaa..................its me FADHIL NAJOCHE from MTWARA-MASASI

  ReplyDelete
 119. Kiukwel alipoondoka Gadna niliahidi kutoisikiliza tena clouds lakin kuna kifaa kimoja 2 ambacho mpaka sasa niwe clozd na radio Dinna wa Ukwel,2ache unazi ki ukweli anatisha Its me Ericky...................mtoto wa Kimara.

  ReplyDelete
 120. dina mbona ujaweka picha ya gea? manake anafanya kazi kwenye mazingira magumu sana.heka heka si mchezo.

  ReplyDelete
 121. all of you a hote!!!!!!!!!!!

  ReplyDelete
 122. dj fe eee wa ukweeee namfeel

  ReplyDelete
 123. Hi all i luv all power breakfast presenters they are all awesome guyz keep it up.my dear Babra Hassan mumy plz do some exercise u are looking too fat bunguza chips na burger that is my advice to u.

  ReplyDelete
 124. GEA power breakfast Gerard Hando 1
  XXL Mchomvu na B12 2
  kibonde japo anazingua na u ccm 3

  ReplyDelete
 125. MBONA SIJAONA AMPLIFAYA YA MILLAD NADHANI NDO INA KIMBIZA MBAYA

  ReplyDelete
 126. napenda sauti ya anold na millard ila sauti zao na muonekano wao tofauti

  ReplyDelete
 127. diva acha kulegeza sauti kama unakipaji siyo mpaka utangazea kwa kulegeza sauti

  ReplyDelete
 128. anold unasauti nzuri ila mwonekano wako wakawaida

  ReplyDelete
 129. ww mwenyew na lovenes mnankonga roho yangu

  ReplyDelete
 130. HI nawapenda wote watangazaji lakini wa powerbreafast ndo huwa nawapenda zaidi gerald,babra,pj na bonge wananifanya hata nisilize radio hadi class.mpo juu sana

  ReplyDelete
 131. Bhaaaaasiiiiii XxxxL

  ReplyDelete
 132. yaani mm nawapenda, Gerald Hando, Babra Hassani pamoja naEfraim Kibonde. are my best and favourate presenters.

  ReplyDelete
 133. Kibonde anajifanya mwanasiasa, daktari, mkemia,Engineer, mjiolojia , fundi umeme, yaan yeye anajua kila kitu!!!si kweli!!! anapotosha sana jamii kwa kuzungumzi issues zingine zinazomzidi kwanza akili, pili hekima tatu umri.

  Ajirekebishe nadhan atakuwa the best presenter after that, kwa sasa!!! PB is cute

  ReplyDelete
 134. Gerard Hando na Babra Hassani mnatisha hambabahatishi hongereni sana, ni mimi fun wenu Boniface Misana wa Dodoma.

  ReplyDelete
 135. Gerald Hando ni noma miaka 600

  ReplyDelete
 136. Gerald Hando ni noma miaka 600!

  ReplyDelete