BIBI HARUSI MTARAJIWA ANA TATIZO LA NGOZI YENYE MAFUTA HASA YA USONI,TUNAMSAIDIAJE....

6:37 AM by
Dina mambo vp shost, pole na kazi dada, Mimi kwa jina naitwa Loveness ni msichana Mungu akipenda natarajia kufunga ndoa mwezi ujao,tatizo ndugu reception mbovu yani nimeharibika uso Dina we acha tu sasa nilikuwa naomba unishauri nipake nini niwe soft kama wewe jamani ila mimi ni mweusi uso wangu ni wa mafuta sana hata nisipopaka kitu nameremeta mafuta nisaidie dada yangu mpenzi.

Loveness mpenzi yaani mimi huwa ni muoga sana katika kumshauri mtu nini atumie usoni ili awe mrembo.Naogopa kwa sababu mimi situmii chochote special usoni kwangu ila naweza sema namshukuru mungu sina ngozi mbaya.Mimi wakati mwingine naweza kuja ofisini sijapaka hata mafuta usoni wala lotion labda poda tu.Na kuna wakati natokewa na chunusi lakini sipaki chochote usoni kuzitoa zinapotea zenyewe au ngozi kuwa rough inanitokea but sipaki kitu maana hata mimi ni muoga kupakapaka vitu usoni kwa hiyo linapokuja suala la kumwambia mtu nini afanye kuhusu ngozi yake hasa yenye mafuta naogopa maana sijaexpirience hilo ila kama kuna mtu anasoma hapa na anajua anauwezo wa kukusaidia basi najua ataacha ujumbe wake na maoni yake hapa.Na pia mie si mtaalamu sana wa masuala ya urembo hasa ngozi.Kiukweli mimi nimeshatumia sabuni,mafuta,lotion tofautitofauti ila sijui kwa wenye ngozi ya mafuta wanatumia nini maana ngozi yangu mimi kavu.
Pia tembelea http://www.bongourembo.blogspot.com/ unawezajifunza mengi huko kuhusu urembo.

16 comments:

 1. sijui bongo kama unaweza kupata facial wipes.instead yakuosha uso na maji na sabuni jaribu for a week kutumia wipes tu.make sure una wipe everytime before you go to bed too.kama yawezekana hacha kupaka na makeup for the same week.ebu jaribu dada.it works for certain people

  ReplyDelete
 2. jaribu pia no marks criam ni nzuri sana sio mkorogo wala inatoa taka taka zote usoni, zipo aina tatu ya ngozi ya mafuta na ngozi ya kawaida na, na kavu na zote zimeandikwa, utaangalia aina ya ngozi yako, nenda pale chemistry oppisity na hindu mandal hospital.japo ni ghali kidogo.

  ReplyDelete
 3. Mimi nakushauri utumie Vitu asilia chukua nazi yako kuna na ujisugue na lile chich ala nmazi hata kama ni nusu saa halafu osha uso wako kwa maji ya uvuguvugu na sabuni yeyote ya kuuwa bacteria km vile Protex

  ReplyDelete
 4. MH! mimi sio doctor wa ngozi, but naweza advice kidogo nikijuacho, mimi ni mweupe, na ngozi yangu ni mafuta sana, yani kila saa nameremeta kama vile nimejimwagia mawese usoni, yote tisa, kumi nilitokewa na michunusi nikubwa shost, ambayo kiukweli ilininyima confidence kabisa, yani kama majipu, uso wote, but niligundua kwanini imekuwa hivyo, ni kwasababu nilisimamia harusi ya rafiki yangu, basi nikapakwa makorokoro kibao, since there, ndio hali ilipobadilika, sasa hebu imagine, nilivyo mweupe, na michunusi, lo! kama chui yani, hadi nilijichukia,
  NILICHOFANYA
  nilikwenda regence hospital
  nilimuona dr, specialist wa ngozi anaitwa Dr, Mgonda, anapatikana pale juma mosi na jumanne, ni gharama kidogo, but kama unataka upone lazima ugharamie, na nakuhakikishia utapona tu,
  nilielekezwa kwake nikaenda, akanipatia dawa ya kunywa, na cream kavu ya kupaka usoni, na shampoo ya uso na sabuni moja hivi inaitwa Peiary, its a gud soap, coz imenisaidia sana, ukiniona utaninijuwa? utasema katoto, mlaini hadi najipenda, na im still in use, so kama upo dar kamuone atakusaidia,
  but pia kwakuwa ngozi yako ina mafuta kama yangu, waweza tumia hivi, lakini inaleta mabadiliko kwa taratibu sana, nenda duka la dawa, nunua cream inaitwa adelaide cream, na hiyo sabuni inaitwa peare, anza navyo kwanza, then u'll see some changes, but ni nzuri zaidi kama utamuona specialist wa ngozi, nakwambia usikate tamaa, utapona na utajiona mnono kweli
  MAMA TRACY

  ReplyDelete
 5. mambo,
  pole dada kwa tatizo lako, ila me nakushauri unaweza pia kwenda kwa doctor maana pengine ni ugonjwa kama ni nyingi sana hizo chunusi, be harus inabidi usipendeze tu harusini pendeza hata ukiingia ndani kwako mume afurah mpz.

  harusi njema dadaaaa

  aisha

  ReplyDelete
 6. jaribu kumuona daktari kwa msaada zaidi

  ReplyDelete
 7. Huyo bibi harusi mwambie atumie unga wa dengu utamsaidia kama hajui afanyeje Diva mweleze

  ReplyDelete
 8. Dada mi nakushauri tumia dengu kama mdau hapo juu changanya na ndimu pamoja na manjano.

  hivyo ni vitu asilia.

  ila kama unatisha muone daktari kwanza, jitahidi uwe unakunywa maji ya kutosha.

  ReplyDelete
 9. yaani mm mwenzenu ndo balaa. kwanza ni mweupe sana! usoni nn mifuta utasema kiti moto! mwilini ni mkavu kaa jiwe! yaani mpaka najichukia,nifanyeje? Mwilini napaka cocoa butter white rose!miaka karibu 6 sasa, but ngozi haina mabadiliko. usoni fair & white,nimepaka kwa miaka 2 but now naona imenichoka maana nimetoka machunusi mno! so tangu jan napaka vya kiafrica tu, yaani mpaka ointmeal nnayo, ss hizo asali, dengu, manjano,liwa,curd, alovera.n.k ndo usiseme!HAKUNA MABADILIKO. NIFANYAJE?

  ReplyDelete
 10. KUNA MTU ALITUMA MAONI HAYA KWENYE EMAIL YANGU
  ;Mimi binafsi sipaki chochote
  ktk face yangu, zaidi ya kunawa na maji baridi tu, & ktk week siku moja tu huwa naosha uso
  wangu kwa maji asili ya tango kisha napaka mchanganyiko wa yai la kienyeji, asali, nyanya na ndimu.
  Na hata wakati mwingine sina muda wa kupaka hivyo vitu,nikiamka nafuta kwa maji ya tango basi nakuwa bomba.
  Napenda kupaka poda bt nikipaka siku ya pili lazima nitoke vipele,so namshukuru Mungu mwili pamoja
  na ngozi yangu havihitaji gharama. Kwani mwili wangu haukubali lotion wala mgando, hapa ni baby oil tu
  na futa la nazi asilia, na hata ukinitazama nina mvuto na mnato wa asili. So asijaribu kutumia cream wala lotion ya
  aina yeyote, ajitahidi kila wakati kuusafisha kwa maji baridi ama hata ndimu kwani haina madhaa yeyote ama achukue
  tango kisha akate smallpcs na kubandika usoni kwa muda wa dakika 15 ili kuweka uso mkavu wakati wote. Ujue kuna
  wakati uso unakuwa na mushkeli na mara nyingine unaseto vizuri mpaka unajishtukia kabla mtu hajakuuliza unatumia nini?
  ni mabadiliko tu ya skin asijali hali hiyo itapotea,namsisitiza asishawishike na walimwengu na kuanza kuchanganya creams
  ajalibu kutumia vitu asilia kwani havina madhara. NB: Ajitahidi kunywa maji mengi kwa siku angalau lita moja,karoti, matango, mboga mboga navyo vinasaidia, hata mimi at my office i hv cocumber,carrot na maji ya kutosha, ni vizuri kujizoesha vitu kama hivi kila wakati vinasaidia ngozi ishine.

  ReplyDelete
 11. Tatizo la Loveness ameshajifananisha na mtu sasa hapo tutakusaidiaje? Anasema awe kama wewe(Dina) kwani wewe ni Soft? yaani kafananisha na nani mwingine ndo kakupata wewe kuwa Soft? Sijui labda kama kajifananisha na yeye mwenyewe! vinginevyo usoft wa mtu unategemea na chakula pia. na miongoni mwa chakula kinachoweza kukufanya uwe Soft ni Parachichi na Maziwa Fresh. Acha kula Chips kuu kila kukicha huwezi kuwa Soft. Kizito

  ReplyDelete
 12. yote yaweza kuwa stress, try to relax, fanya mazoezi utoke jasho jingi japo kuruka mara 100 kabla ya kwenda kuoga kila siku, na kunywa maji mengi japo lita kama dada alivosema, lala japo 8hours kwa siku, na chagua moja usifanye vyoote ulivoshauriwa utaharibu ngozi yako, pia isikupe presha sana mume ushampata, na kakupenda ivo ivo ulivo dear.. harusi njema shost..

  ReplyDelete
 13. inawezekana vyakula unavyokula vinakusababisha hivyo jaribu kuchunguza,ama mimi nikila vyakula vya aina ya karanga,mayai,tunafish,cheez,choklete basi uso wangu huwa na chunusi nyingi kama majipu

  ReplyDelete
 14. SHUKRANDINA, NIMEPITA BONGO UREMBO KUNA MAMBO ILA LUGHA TATIZO

  SHUSHU

  ReplyDelete
 15. TUMIA VIPODOZI VYA ORIFLAME KUTOKA SWEEDEN VINATENGENEZWA KWA VITU ASILIA, TAYARI VIKO TZ KWA WAUZAJI WA REJAREJA. KATIKA HIVI VIPODOZI KUNA VYA WATU WENYE NGOZI KAMA YAKO NA MACHUNUSI- HIVI VIPODOZI NI ASILIA NA HAVINA MADAWA (chemical. Kuna cleanser ya kusafishia uso pamoja na cream ya kupaka. tuwasiliane kwa namba 0713 252031.

  ReplyDelete
 16. Mi nakubaliana na dada wa Regency ni bora uende ukamuone specialist ujue hasa tatizo ni nini.Hii habari ya kujaribu jaribu bila ya kujua tatizo nilijuta,usoni nilitokewa na bonge za michunusi mpaka nikiinama nahisi zinavuta na maumivu juu.Hawa watu wapo kwa ajili yetu bora kuwatumia na wala haitakuchukua muda kupona.
  Frank

  ReplyDelete