NILIKUWA NA VUMI LEO KATIKA LEO TENA!!

4:57 AM by
Vumi ni msanii wa muziki wa hapa bongo lakini katika mahadhi ya zouk.Nilianza kumjua Vumi kupitia wimbo unaitwa Nenda ambao ndio ulikuwa wimbo wake wa kwanza kabisa kumtoa,baadae akatoa Utanikumbuka,na mwaka jana akatoa Tatizo ni umasikini wimbo ambao umependwa sana.Vumi alianzia pale nyumba ya vipaji T.H.T akiwa na kina Mwasiti,Maunda Zoro,Buibui,Zuhura na Rogers wengine nimewasahau.Kwa sasa yupo na Band inaitwa Kemondo sound wana wa kibajaji chini ya Richard Mangustino.
Akizungumzia wimbo utanikumbuka,Vumi anasema aliutunga wimbo huo maalum kwa ajili ya dada yake ambae alikuwa ana matatizo katika ndoa yake na mumewe mpaka ikafika mahala dada yake akarudi nyumbani akiwa na mtoto mdogo sana.Dada yake kila wakati alikuwa akilalamika na kusema ipo siku huyo mumewe atamkumbuka tu kwani yeye alikuwa mke mwema na alimtendea mema lakini akamlipa kwa mabaya.Sasa Vumi akaamua kuandika huo wimbo kama umeshausikia una maneno mazuri sana.

Vumi anavutiwa sana na Mwanamuziki Pouline Zongo,anasema japo yupo kimya ila anamkubali sana hasa vile anavyoweza kumudu kuimba na kupiga gitaa kwa wakati mmoja.

Jina lake kamili ni Vumilia Abraham Mwaipopo ni mama wa mtoto mmoja anaitwa Mariam ana miaka 2 na nusu sasa,ukiangalia video ya wimbo wake wa Utanikumbuka kuna mahali amebeba mtoto amevaa miwani mikubwa ndio huyo mtoto wake.Na anamudu vizuri tu malezi ya mtoto wake na wakati huohuo akiwajibika na kazi yake ya kuimba katika band kwenye mahoteli.

Leo nimeutambulisha rasmi wimbo wake mpya unaitwa That day ambao utakuwa katika albam yake itakayotoka hivi karibuni ikiwa ina nyimbo zake zote zilizotangulia.Ni katika mambo leo ya leo tena kila wiki nakuwaga na msanii ndani ya studio.

21 comments:

 1. nyonyo umependeza mashallah! mi kiatu tu. asiyekusifia mjeuri.hanifa mati.

  ReplyDelete
 2. kiatu kizuri sana ila punguza unene unatisha sasa

  ReplyDelete
 3. umependeza lkn acha ubaguzi, nimekutumia email uipost lkn mashauzi hata kuipost umeringa,andika basi unataka post za namna gani au watu wa status gani maana naona yangu imekuwa ignored..si wewe tu mwenye blog wameposti wengine mama ila habari msg sent

  ReplyDelete
 4. Kiatu kizuri sana, umependeza lakini angalia usijeanguka kama lady gaga! Just joking!!

  ReplyDelete
 5. asante kwa wote hahahaha sitaanguka kama Lady Gagaa,kupungua kumekuwa shughuli mwenzenu.
  Kwa mdau uliyesema nimekubagua sijui ulituma email gani maana zinakuja nyingi tu na wengi nawajibu kwa uwezo wangu na kuzifanyia kazi,simbagui yoyote wala kujali stutus maana unaponiandikia sijui hata stutus yako.Kama umeona nina mashauzi asante kwa hilo ningependa nikusaidie lakini umesema ushasaidiwa na wengine wenye blogs yote heri tu.Ubarikiwe!!!

  ReplyDelete
 6. jamani mdogo wangu bado mavazi yanakupia chenga, jitahidi kupitia majarida na mavitu mengine uone wengine wanavyovaa umevaa vitu vizuri vya nguvu ila haviendani dear. jitahdi mdogo wangu

  ReplyDelete
 7. mambo dinna naomba kesho ukiingia ktk kipind naomba uwanze wimbo wa poline zongo napia wimbo wa vumiy nenda,napia finna mango mapenzi ,ilo ndochaguo langu me mdau waleo tena mama tariq

  ReplyDelete
 8. Hi Dina!!
  Umemuweza huyo alokwambia unajishaua. Hongera sana kwa kazi nzuri, unaimudu vizuri kazi yako pamoja na walimwengu.
  Hongera sana and I wish you good lucky!!!

  ReplyDelete
 9. Nimegundua why umetuma full pic.thnx!

  ReplyDelete
 10. Mdau hapo juu, sidhani kama unene/kuongezeka ni tatizo.Kuna wazuri wangapi na bado ni wanene.Ni kujipatia tu na kuendelea kutesa na jinsi ulivyo. Sidhani kama kila mtu anaweza akawa mwembamba dunia hii(kwasababu hatufanani binadamu wote). Bythe way kila mtu ana taste zake........

  ReplyDelete
 11. Mambo Dina,yaani umependeza mno jamani,na asante kwa kipindi chako kizuri kwani ni lazima nikisikilize kila siku.Jamani hicho kisamvu hata mimi nimekitamani sana,ila mi mvivu sana wa kutwanga nikipata kama hicho du ntafurahi sana,tunasubiri utuwekee contact za huyo dada. siku njema

  ReplyDelete
 12. MMH! Looking good mamie, i like your shoes, nice one. Mimi mama Blanca am just reminding you my song, '' END OF LOVE'' am waiting for it.

  Have a gd day!

  ReplyDelete
 13. Dina, miguu ina nini? Umejichuna au?
  Please explain coz they look un usual.

  ReplyDelete
 14. Dinna eeeeh!! Nakupenda sana ila cna jinsi. Naomba contacts zako plz

  ReplyDelete
 15. Abdulrahman Ismail JahniJuly 1, 2010 at 1:40 AM

  pole kwa mafua Dada mzuri usiye na kasoro hata Chembe, na hongera kwa kipindi chako keep it Up mama

  ReplyDelete
 16. dear umependeza lakini mavazi uliyovaa ni ya kutanulia kuleee kitaani siyo ofisini yaani kwa kifupi hayaendani na sehemu uliyopo rekebisha hilo.

  ReplyDelete
 17. JAMANI MBONA MNAMCHAGULIA MAVAZI BIBIE DINA? HAYO MAVAZI YANAENDANA NA KAZI YAKE COZ SIYO TV PRESENTER NI RADIO PRESENTER SO HAKUNA ANACHOONYESHA REDIONI MWACHENI AVAE ATAKAVYO ILI MRADI WAKUU WAKE WA KAZI WAMEMWONA NA HAWAJAMKATAZA NA WALA HAJAKAA UCHI, TATIZO LENU NINI? KILA KAZI NA MAVAZI YAKE BWANA, MWACHENI AJIACHIE. MTANGAZAJI WA REDIO HAWEZI VAA SAWA NA WA TV AU SAWA NA MFANYAKAZI WA BENKI. ACHENI UZUSHI

  ReplyDelete
 18. Jamani watu mnapenda kuongea/kukosoa zaidi kuliko kutoa compliment.... kwani huo unene wake unawahusu nini? na wewe uliyesema mavazi siyo mahali pake kwani wapi kumeandikwa dress code na isitoshe yeye ni mtangazaji tu kazi yake siyo kutoa huduma kwa wateja. Acheni maneno yasiyo ya lazima jamani coz siyolazima mtu ucomment kila kitu. Dina keep it up my dear!

  ReplyDelete
 19. Tunampenda Dina sana ndo mana tunamsifia na tunamkosoa pia..Hata kama hatoi huduma kwa wateja but the top and the shoes are too much kwenda navyo kazini. Yes, sio lazima avae suti but anaweza vaa casual but decent ones,like jeans na shati, trouser na top, vigaun gauni flani, sketi na shati au top eeee... vitu kama hivyo. Sio kama alivyo vaa hapo juu as if anaenda Bills bwana.

  ReplyDelete
 20. MMHHHHHHhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh umeyataka mwenyewe mamie!!!!!!!!!!!!!!!! Ila kipaji chako ni bomba hasa.We waache wacheue tu siku zitapita wataacha na kurukia mengine.

  ReplyDelete