STAND YA MABASI MOSHI

3:10 AM by
Mji wa Moshi kiukweli ni msafi mpaka basi nilifika stand kuu ya mabasi mpaka nikaogopa...pasafi mpaka raha.


Yaani wakazi wenyewe wa mji huu wapo makini na suala la usafi maana kuna mtu tulikuwa nae akanunua vocha alipokwangua akatupa chini kile kikaratasi cha vocha watu waliokuwepo pale wakaanza kumpigia kelele aokote uchafu wake.

7 comments:

 1. huu kwa kweli ni mfano wa kuigwa dina.tukiamua inawezekana

  ReplyDelete
 2. hehehe yaani nimecheka sana ulivostuka kushuka stendi kuiona safiiii , ni ajabu sana kuona stendi safi hata mimi ningeogopa , lakini mimi huwa najiuliza kwanini moshi waweze na dar pashindikane ?? utakuta mtu mwenye akili zake timamu yuko barabarani anaendesha gari anatupa chupa za maji barabarani pwaaaaa !! huyo anaongeza spidi ya gari anaondoka , hebu niambie tutafika kweli ? yaani natamani nikaishi moshi basi tu sitoweza kazi zangu ziko huku dar ..
  any way vizuri umetupa habari ,naomba katika vipindi vyako hamasisha usafi wa miji hasa dar uwe unaongelea kidogo kidogo ujumbe ufike .. asante

  ReplyDelete
 3. dina ubarikiwe sana tunakushukuru kwa picha za arusha sisi wengine tulioko nje ya nchi umetukumbusha nyumbani hasa tuliotokea arusha endelea kutuhabarisha

  ReplyDelete
 4. La la laa aisee hii ni tam mno,usafi namna hii inapendeza sana.Hii inawezekana jaman.Cha msingi tupate WAPIGA KELELE kama hao wa Moshi, naamini baada ya muda watu wataona umuhimu wake.Usafi mambo yote jaman asikwambie mtu...kazi njema mdada

  ReplyDelete
 5. Jamani Dina umenikumbusha mbali kunionyesha iyo stand ya moshi kwetu huko jamani wenyewe twapaita stand kubwa mosh ni kusafi mno ukicompare na DSM jaman ungetembea kidogo na moshi pia utuonyeshe picha

  ReplyDelete
 6. nilipanda madaladala mawili tofauti la coastal la ubungo posta kwa siku yake na dcm moja la tabata kimanga -posta kwa wakati wake nilifurahi kuona kuna vidust bin vimefungwa pembeni ya carrie karibu na kwa dereva ,sasa kama uhamasishaji ungeendelea wa namna hii mji ungekua mchafu na nikimuona mtu anatupa chupa ya maji nje ya gari namgombeza mpaka anaona
  aibu kabisa-jamani da ni kuchafu

  nilipiga picha yale madustbini ila bahati mbaya scrren ya simu yangu imeharibika nikirekebisha ntazirusha hata kwa michuzi ili tujifunze

  ReplyDelete
 7. jaman dina,inaelekea mlienjoy cna,embu hamasisha mambo ya usafi ktk vipind vyako plz

  ReplyDelete