SOUP YA KUPUNGUZA MAFUTA MWILINI

6:59 AM by
Mahitaji:
Vitunguu vikubwa 6, Pilipili hoho 2, Nyanya 4 kubwa, Cabbage 1 kubwa, Leeks kubwa 4, Cube 2 za Knorr au Roiko (kwa ladha na si lazima). Hii inaweza kutosha kwa nusu siku mpaka siku nzima kutegemea uwezo wako wa kuila.
Boresha ladha kwa kuongeza chumvi, pilipili kawaida au manga, hot sauce au malimao/ndimu.

Namna ya kutengeneza:
Katakata mboga viwe vipande vidogodogo. Weka maji yajae kufunika mboga. Chemsha haraka kwa muda wa dakika kumi halafu punguza moto zitokote taratibu mpaka zilainike kabisa.
Baada ya hapo saga kwenye blender au utakavyoweza ili upate supu yenye rojorojo.
Kula hii supu kwa kadiri uwezavyo kwa kuwa haita ongeza calories kwenye mwili. Jinsi utakavyo kula hii supu ndivyo utakavyo pungua uzito.
Ni vema kuweka supu kwenye thermos asubuhi kama hautakuwepo nyumbani ili uendelee kula mahali popote utakapo kuwa.


TAFADHALI KUMBUKA: Mahali popote panapoandikwa supu, ni hii Basic Fat Burning soup hapo juu na siyo supu nyingine.
UKILA HII SUPU PEKE YAKE KWA MUDA MREFU SANA UNAWEZA KUPATA UTAPIAMLO (MALNUTRITION).
SIKU YA KWANZA

· Kula matunda aina yeyote isipokuwa ndizi.
· Matikiti maji yana calories chache kuliko matunda mengine kwa hiyo ni bora kula hayo.
· Siku hii kula supu peke yake na matunda.
· Kunywa chai isiyo na sukari pamoja na maji.

SIKU YA PILI

· Kula mboga aina yeyote ile.
· Kula mpaka ushibe mboga ambazo ni fresh kama vile saladi au mboga za majani zilizosindikwa kwenye kopo.
· Usile maharage yaliokaushwa, njegere au mahindi makavu.
· Kula hizo mboga pamoja na supu.
· Kwa chakula cha jioni siku hii unaweza kula kiazi kimoja kikubwa kilicho okwa na unaweza kupakaa siagi.
· Usile matunda ya aina yeyote nyingine.

SIKU YA TATU

· Kula supu, matunda na mboga za majani aina yeyote.
· Usile kiazi kilicho okwa.

Kama utakuwa umekula kama ilivyo onyeshwa hapo juu, na huja danganya, basi utakuwa umepoteza uzito wa mwili kwa wastani wa kilo 2 mpaka 3 baada ya siku hii ya tatu.

SIKU YA NNE

· Kula ndizi mbivu na maziwa yaliyopunguzwa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula ndizi mbivu tatu, maziwa glasi nyingi uwezavyo pamoja na supu.

SIKU YA TANO

· Kula nyama ya Ng’ombe na nyanya fresh.
· Kula nyama kiasi cha robo mpaka nusu kilo pamoja na nyanya fresh kadiri uwezavyo.
· Jaribu kunywa glasi 6 mpaka 8 za maji ili kupunguza uric acid kwenye mwili.
· Kula supu angalau mara moja siku hii.

SIKU YA SITA

· Kula kiasi chochote cha nyama ya Ng’ombe na mboga za majani. Ni bora kula saladi kwa wingi pamoja na nyama, lakini usile kabisa Viazi siku hii.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

SIKU YA SABA

· Kula wali, juice isiyo na sukari na mboga za majani. Kula kadiri utakavyoweza.
· Hakikisha unakula supu angalau mara moja.

Inategemewa kuwa baada ya siku ya saba utakuwa umepoteza kati ya kilo 4.5 mpaka 7.7 ya uzito wa mwili.
Kama umepoteza zaidi ya kilo 6.8 simama kwanza kwa siku mbili kabla hujaendelea na huu utaratibu wa mlo tena.
Utakapo anza tena, anzia siku ya kwanza na kuendelea mpaka siku ya saba tena.
Kwa kuwa miili ya binaadamu inatofautiana, diet hii italeta mabadiliko tofauti tofauti kutegemea mwili unavyo ipokea. Kawaida baada ya siku tatu mwili wako utajisikia nguvu zaidi kama hujadanganya.

VITU VISIVYO RUHUSIWA KABISA WAKATI WA DIET HII.

· Hairuhusiwi kutumia Mkate, Pombe aina yeyote, vinywaji vyenye gesi kama vile soda na vyakula vilivyo kaangwa na mafuta.
· Tumia maji, chai isiyo na sukari, kahawa isiyo na maziwa wala sukari, juice za matunda zisizo na sukari na maziwa yalio ondolewa mafuta (skimmed milk).
· Unaweza kula Kuku aliochemshwa au kuokwa badala ya Nyama, lakini uondoe ngozi yake. Unaweza vilevile kutumia Samaki aliyechemshwa katika siku moja inayohitaji Nyama badala ya Nyama lakini sio zaidi ya siku moja.
· Supu hii inaweza kutumika saa yeyote unapo hisi njaa. Kunywa uwezavyo. Kumbuka jinsi unavyo inywa kwa wingi ndivyo unavyo punguza uzito.
Supu hii haingiliani na dawa zozote utakazo andikiwa.
Endelea na utaratibu huu mpaka utakaporidhika kuona mabadiliko katika mtazamo na mwili wako.

[Diet hii imetumiwa na The Sacred Heart Memorial Hospital, Rochester, Mayo Clinic, Marekani. Inatumika kwa wagonjwa wa moyo, wenye uzito mkubwa ambao wanahijati kupunguza uzito wa mwili haraka kabla ya upasuaji wa moyo.Hata watu wengine wanaohitaji kupungua wanaweza kuitumia Imebadilishwa kidogo kutokana na vitu vinavyopatikana hapa kwetu bongo kirahisi.]

Katutumia Fiona kwa wale mtakao weza.

24 comments:

 1. hii itakuwa kazi kweli kweli mmmmh ila kama mtu utafuata masharti ina weza kusaidia sana nimeipenda mpenzinice one..

  ReplyDelete
 2. Dina na Gea .. hiyo ni ya kwenu .. nina imani baada ya muda hivi mtadrop kama kilo 5 hivi. Kwa upande wangu mfadhili wangu kaniambia jinsi nilivyo ndivyo anitakavyo kwa hiyo issue nzima ya soup nimeipoteza. Lkn nilipoliona neno soup hapo juu nidhani sabuni.

  ReplyDelete
 3. Mafuta gani mnaongelea kuhusu kupunguza mwilini? Muhimu sana kuwa makini na haya maelezo maana watu wanaweza pamia tu kama ilivyo kwa baadhi ya watu hasa wakina dada siku hizi wasivyokula chakula cha kutosha ati kuthibiti uzito.

  ReplyDelete
 4. Sio uandishi tu hata huu udakitari wa mwili unaujua. Ahsante sana

  ReplyDelete
 5. Hujambo hii Supu anayo Tira pia tena siku nyingi sana

  ReplyDelete
 6. dah thanx for that topic imenigusa sana, hivi niko kwenye zoezi la kupunguza mwili na uzito wake. isonge mbele safi sana.
  Gg

  ReplyDelete
 7. Asante dada Dina kwa kutuwekea njia ua dada ambayo ni nzuri kwa sisi tunaopenda kupungua,THATS HWY NAKUPENDA.

  ReplyDelete
 8. hi dina!
  thanx kwa diet soup! sasa nimetengeneza hii supu bt sijaweka hizo leeks maana sijazijua.
  nataka niifuatilie hasa nia ninayo sasa baada ya wiki nitatoa feedback! now nina kg 84

  ReplyDelete
 9. hi Dina nikuwa nauliza kuhusu chai mie ni mpenzi wa chai sana . umesema bila sukari je ukitumia spelendor au sweetener is ok?

  ReplyDelete
 10. mimi niliipata hiyo cabbage soup diet kwenye internet. nikaibrowse.niliifanya hiyo diet, kwa kweli ni nzuri, nilikuwa na 73 kgs, nikapungua mpaka 65kgs.baada ya wiki mbili, nikarudia tena, nikapungua 2kgs. ktk hii diet, siyo vyakula vyote unaweza kuvipata, maana vingine vimeandikwa kwa majina ya kizungu, kwa hiyo sio rahisi kuvielewa.ukiona kuna kitu hukielewi, usipende kufanya substitute maana utaharibu. Hapa fuata maagizo, usitumie sukari hata kidogo maana unaweza sema , ngoja nitumie small amount of it, utaharibu na haita -work, badala yake tumia asali..halafu, wakati wa diet, usipende kula late nyakati za usiku, kula mapema, na usilale promptly after taking your meals, spend sometimes ndipo ulale.jitahidi kunywa maji mengi kadri uwezavyo hasa siku ya 5 na 6,kabla ya breakfast, kunywa at least 2 ltrs.dont take any alkohol,ukiona umejisahau ukatumia hata glass moja ya wine, bora usitishe uanze upya.Then baada ya hiyo diet, jitahidi usipende kula heavy meals nyakati za usiku, jitahidi kula chakula cha usiku mapema, pia uwe na displine kwenye kula, sio unakula kula ovyo, unakuta mtu unakula wrong foods at the wrong time!!pia avoid starch intake, na vile vile angalia potion yako ya chakula, siyo unaji-over feed! ukweli, ukizingatia hayo utaona mabadiliko makubwa. mimi niliongezeka uzito kwa sababu nilikuwa nanyonyesha, sasa utakuta mwanamke hunyonyeshi, then unanenepeana mpaka unakosa size za nguo. nikuwa naona kero maana hata mr wangu alikuwa ananiambia kila wakat' mhhh huo unene!'nikawa najisikia vibaya maana mwingine hakawii kwenda nje ya ndoa maana alikupenda ukiwa slim, sasa maunene hayooo!! lol!!

  ReplyDelete
 11. aisee nimeanza hii diet jana loh kazi ipo maana unakuwa dhaifu huna nguvu! bt still nimekomaa nayo hahahhaaaa

  ReplyDelete
 12. thanks Fiona kwa diet uliyotutumia. kwa mdau aliyeuliza hapo juu kuhusu leeks ni jamii ya vitunguu ila sijui tutaviitaje ila ukienda sokoni utaviona nivitunguu chini ni vyeupe na havikatwi majani yake hivyo viko na majani yake. nadhani utakuwa unavijua ila nikutokana na lugha iliyotumika. ukienda kwenye google ukasearch maana ya leeks unapata wanakutolea na picha yake utaona ni kitu ambacho kinapatikana kwa urahisi.

  ReplyDelete
 13. mdau hapo juu asante kwa ufafanuzi. mliopo Dar Leeks zipo soko la Kisutu i think hata masoko mengine unawezapata. mie nimeianza hii diet j2 ikinisaidia ntaitumia once a month maana nna 90kgs!

  ReplyDelete
 14. nimeipenda hii supu maana nina kilo 78 najichukia jinsi nilivyo hivyo nitaianza kesho ili nionee matokeo yake. asanta sana

  ReplyDelete
 15. Jamani wapendwa naomba niwe shuhuda wa hii diet, mie nilikuwa na 98 kgs niliona diet hii hapa nika print then nikasema ngoja nijaribu cause diet nyingine naziona ngumu! believe me or not ndani ya siku 5 nilipunguza 4kgs mpaka naandika nimepunguza 7kgs kwa muda wa siku 12 na naendelea na hii diet mpaka nifike 70kgs, na naamini kwa muda mfupi nitapunguza. Kikubwa ni nidhamu tu na ushauri kabla hujaanza hii diet kaa na marafiki ambao ni close nawe, ndugu na boyfriend/Husband mwambie nataka kuanza diet please please support me! maana hao ndugu ni adui wa diet. Kuhusu Leeks Karikoo na Kisutu Sokoni zinapatikana. Kizunguzungu hauwezi sikia kama unakunywa supu mara usikiapo njaa. Please wenyewe weight kubwa kama yangu tumia hii utajuta, maana mie kila mtu ofisini wananiomba hii diet.

  ReplyDelete
 16. Mimi niko Zanzibar nitaipataje hiyo mboga ya leeks nimehangaika sana tu sikufanikiwa nakilo125

  ReplyDelete
 17. pole sana nuru

  ReplyDelete
 18. mh jamani hii supu haipo lovely kabisa ila ndo nimeanza leo ntajikaza hivyo hivyo then ntawapa feedback

  ReplyDelete
 19. Jaman hata mie nimeipenda xana hii diet

  ReplyDelete
 20. i had 98 kgs juz kati,nkaianza diet then baada ya cku tatu nkaikatza bcz nlikua na safari ya ghafla.nlipoenda hosptalin kuchukua kadi ya manjano nkaona nipime kilo.nlipo pima nkajkuta nina 94kgs.imagn after 3days!!!!sahv nmeianza tena n am looking forward to hav my sexy back...ndio inakatisha tamaa lakini wewe komaa tu

  ReplyDelete