Tuesday, November 16, 2010

DUNIA INA MAMBO NDUGU ZANGU!!!!!!

Huyu baba amekuja leo ofisini akajitambulisha kwa jina la Ramadhani akidai yeye ni mkazi wa hapa Dar es salaam na amekuja kutangaza kumtafuta mkewe.Amekuja akiwa ameongozana na watoto wake ambao wanaonekana hapo chini pichani.Ntakwambia kwa nini huyu baba amenishangaza mpaka niseme dunia ina mambo.
Huyu ni binti yake mdogo kama unavyomuona amepakwa masizi usoni,mikono yote miwili imefungwa hirizi kibao na mtoto ana chale kila sehemu mikononi...baba akiulizwa mbona hivyo anasema ni dawa...

Gea akiongea na huyo baba kuona kama kuna hekaheka...ila imekuwa ngumu kupata hekaheka maana haeleweki...
Watoto wanne miguuni wamefungwa vitambaa mfano wa irizi na wamechanjwa chanjwa chale kibao na usoni wamepakwa masizi..

Baba mwenyewe sasa mikono yake imejaa vyuma na hirizi na hata shingon na miguuuni ana sema hizo zote ni dawa.

Kilichonishangaza sasa,anasema yeye alisafiri kwenda Nigeria mwaka 1982 kwa ajili ya matibabu ya kienyeji na amerudi mwezi huu amekuta mke wake kakimbia kaacha watoto wao hao peke yao.Ukimuuliza baba mbona hawa watoto ni wadogo kama wakati unaenda Nigeria 1982 uliwaacha wangekuwa na umri huuu kweli???si wangekuwa na miaka 28 na ushee????baba anakuwa mkali kujibu maswali kitu ambacho tumeona inawezekana ni msanii tu au ana matatizo ya akili.

Yupo hapa ofisini anasema haondoki mpaka ampate mke wake!!!!!

26 comments:

 1. Hana lolote huyooo...dakika 2 mbele...nani kamuelekeza mjengonii???? Huyo anataka vijisenti vya msosi tuu mjazieni muone kama hajaondoka na iyo midawa yake ndo imemdatisha....kazi kwenu
  Ndo uzuri wa kuwa Radio ya Watu na Watu wenyewe ndo haoooo..

  ReplyDelete
 2. poleni kazi mnayo.....ugumu wa hekaheka upo hapo,haondoki mpaka apate mke wake.na labda mngeliwahoji watoto nao wanasemaje juu ya hilo.

  ReplyDelete
 3. Sikiliza Dina! mpelekeni mirembe Kuleee Dodoma akapimwe akili.Na watoto wapeleke ustawi wa jamii.......Kizito!!

  ReplyDelete
 4. Sasa si umchukue wewe akuoee, ili umsaidie kulea hao watoto

  ReplyDelete
 5. Hahahahahahahaha...kweli hicho kioja, Dina una haki ya kucheka.....maana hata mimi nimechoka, ye kaondoka 1982 na ana watoto hadi wa miaka mitatu...na hizo alizovaa ndo dawa alizopewa huko Nigeria...jamani kweli duniani kuna mambo na hiyo hekaheka ni kali natamani ningemuona LIVE....sasa haondoki mpaka ampate mke wake nyie ndo mliompoteza...?
  Haya kila la Kheri maana nyie ndo vioo vya jamii anaamini mkiongea mke wake atajitokeza hoep ampate jamani na huyo mwanamke kajua kabisa kuwa hao watoto so wa hao mwanaume ndo maana kakimbia...hahahahaha....jamani mi nimeshindwa kijuzuia kucheka, KHA!!!!

  ReplyDelete
 6. Nguvu za giza hizo. Ana akili zake timamu. Mbona ameweza kuwakusanya wanae na kuja nao hapo! Na bado anasema haondoki mpaka ampate mkewe.
  Ng'ombe wake wangekuwa hawajarudi zizini asingekataa kuondoka hapo.

  ReplyDelete
 7. Dina mydear obvious huyo mzee ana matatizo ya akili from the appearance, anyway tafuta mbinu ya kuweza kumtoa hapo ila hayuko sawa huyo kichwani

  ReplyDelete
 8. kweli Dunia ina mambo, ila dina inawezekana kweli wanawe we hujawahi ckia wachawi wanasafiri, utakuta alikuwa huko Nigeria lkn kila Ucku alikuwa anaonana na mkewe wanaduu na wamezaa km kawa, hiyo hipo mwaya,inaelekea hapo ofcn kulikuwa na vioja.ASIA ALAWI

  ReplyDelete
 9. hana lolote just mkwaraa tuu. hiyo mibangili kaja nayo ili awaogopeshe. achaneni naye

  ReplyDelete
 10. Pole dear,huyo ni mwanga mpelekeni kwa mama Rwakatale akaombewe huyo alikuwa anasafiri na midawa yake akanguka hapo ebu jaribuni kuwahoji watoto mwanga mkubwa huyo na mikorokoro aliyovaa ndio inazidi kumchanganya poleni washirikina

  ReplyDelete
 11. mmmm Dina pole sana wangu hicho ni kioja na kama ulivyosema dunia ina mambo hujakosea ukisikia magumu ambayo watu wanayapata maeneo ya kazi mengine ndo kama hayo kwa upande wako aka babu anatisha huyo bwana NAKUFUNIKA KWA DAMU YA YESU LOO!!!!!

  Beatrice

  ReplyDelete
 12. Gea, huyo baba na watoto wake sijui watoto wakufiki woooooote wendawazimu,wasiwashuhulishe

  ReplyDelete
 13. hako ka kikie jamani kaangalieni copy ya baba yake

  ReplyDelete
 14. MBONA KAMA MAKIRI KIRI HUYO DINA?? MI NAONA MAKIRIKIRI NA FAMILIA YAKE HAPO. UKITAKA KUHAKIKI HAPO WAWEKEE WIMBO WA "DUMELA" UTAONA WATAKAVYO ANZA KUPIGA MIGUU CHINI. KWI KWI KWIIIII

  ReplyDelete
 15. Ana njaa tu huyo, anajua akija hapo atapata hela za kujikimu maana huwa anasikia wengine mnawasaidia, hebu wachunguzeni hao watoto usikute kawafundisha maneno ya kuongea, mkiwabana mtaujua ukweli wote.

  Hamna cha hirizi wala tunguli, hana lolote njaa zake tu huyo, kama akili anazo timamu angekuwa hana akili asingekuwa mkali mnapombana kwa maswali, natamani niwe karibu nimtandike hadi ajue ulimwengu huu ulivyo.

  Au mwambieni mnampeleka kituo cha polisi ili akajieleze ndo atampata mkewe muone kama hajatoka mita.

  Mdau

  ReplyDelete
 16. Ha ha ha ha ha ha, nimecheka hadi basi, inaelekea huko mjengoni kuna mke wake kwanini anang'ang'ania kukaa hapo hadi ampate hahaha, hebu angalia hao watoto wamefanana na nani huko mjengoni kwenu, mi na wasiwasi na GEA hahahahahaha

  ReplyDelete
 17. Kitanda hakizai haramu ndugu zangu, Lakini pia itabidi wafanyakazi wa clouds fm na TV(WANAWAKE) mjiangalie upya isijekuwa kuna mkewe kaelekezwa!Mi naunda kamati ya kuchunguza Mkiti Shafi Dauda, wajumbe ma DJ wote wakiume wa clouds toka mikoani na mwenyeji wao Kibonde. Lakini kama sivyo chapa bakola atanyosha maelezo.

  ReplyDelete
 18. Clouds Fm...Radio ya watuuuu na watu wenyewe ndio hao,hapo lipo neno.

  ReplyDelete
 19. Gea kumbe una miguu ya chupa ya bia leo nimeiona na kifua cha bata leo nimekiona vizuri.

  ReplyDelete
 20. ASHINDWE NA ALEGEE KWA JINA LA YESU

  ReplyDelete
 21. Dina listen huyo mtu ni mgonjwa wa akili ila tujiulize anaishi wapi na watoto woote haoo anawapa nini watoto woote haoo huyu ni chizi ila anaakili zakuishi watoto watakua yale yale ya yule mama Tena Dina hujatu-update issue ya yule mama wa Ocean Road imefika wapi! well huyu ni yale yaleee watoto watakua wanatumwa hawa kuomba kama wale omba omba wengine wa fire na mahala pengine!

  ReplyDelete
 22. Bangiiiiii hiyooooooooo jamaniiii watoto sasaaaaMungu wa Rehema duuu Tanzania tutafika kweli hiviiii!!!nguvu kazi ndio hiyooo vijana wetu ndio hawa kweli Kikwete unakazi kweli kweli.

  ReplyDelete
 23. Mungu atusaidie, huyu kaka atakuwa ni mgonjwa wa akili masikini watoto wanateseka bure, kama kawachanja chanja hivyo si anaweza ata akashika na panga jamani?? Mungu awalinde watoto hao amen. Je ilikuwaje mpenzi aliondoka? au mpaka leo yupo hadi kieleweke?? pole kwa kazi.

  We MOJA ONE Dina ulimwona wapi? ulikuwa karibu na mjendo unatega?? Hukujua huyo ni MHAYA lol!

  Kokusima

  ReplyDelete
 24. Kokusima.. Nashukuru sana kwa comment yako, nimeipata live lakini mie sikusema ni Dina bali Gea na nimemuona kwenye picha ya tatu ya habari hii.

  ReplyDelete
 25. i luv u dina mwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaahhhhhhhhh

  ReplyDelete