KUNA VITU VINGI SANA NAPENDA,KIMOJA WAPO NI KUPAMBA NYUMBA...
Leo nimeamua kushare na wewe kitu ninachokipenda kufanya...kiukweli napenda sana kupamba nyumba na kuiweka katika mpangilio mzuri.Nyumbani kitu kikiwa hakija kaa sawa najisikia vibaya...
Hata nikiwa katika matembezi ya kawaida njiani lazima nitataka kununua kitu cha nyumbani kwangu iwe cha kuirembesha au kwa manufaa tu ya nyumbani...kubwa zaidi napenda sana picha za ukutani..
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Dina nakukubali,yaani i wish nifike kwako!yaani unaonekana wewe ni smart sana!napenda watu wa namna hii!big up!
ReplyDeletesio mbaya mwanamke nyumba pia ukipamba nyumba na usafi tayari mwanamke mimi hupendelea sana kupamba nyumba
ReplyDeletehongera nyumba nzuri na kweli mwanamke nyuma ila dina naomba tumjue hubby wako pls
ReplyDeletehongera Dina, nyumba yako imependeza sana.
ReplyDeletesamahani dina ni nyumba yako au umepanga????????? km yako dada nakupa hongera sn sn sn na km si yako komaa unaonekana si muoga wa maisha na unamalengo Mungu atakupa tu
ReplyDeleteHongera Dina. Umenitamanisha sana kuja kukutembelea ili nione mapambo yako mazuri nyumbani mwako.Naamini muonekano wako nje unafanana na muonekano wako wa nyumbani mwako hadi kitandani kwako ingawa huko hujatuonyesha.
ReplyDeleteTena nasema hongera maana nami nina hoby sawia nawe.
I like pia kudecorate da house dahh and nipo katika mipango ya kwenda kusomea even if hata sina mpango wa kuja kiifanyia kazi kabisa but itakuwa special for ma self, ma family and for the people I love Most,,Its No Name
ReplyDeletetunashukuru kwa upendo wako always wewe si mchoyo ndo mana nakupenda. hata mimi napenda nyumba ikiwa nadhifu huwezi acha rudi mapema nyumbani.unanifunza vitu vingi sana uishi milele na mungu akubariki sana.
ReplyDeleteDina nimekupenda bure kwa hili la kupenda mapambo ya nyumbani na mengine menzi kuhusu wewe, lkn hebu nisaidie mwenye nyumba wangu hataki kuona msumari uktani je kuna namna naweza weka mapambo yangu bila kutoboa kweli? hebu nisaidie.
ReplyDeleteThx ma FM - Arusha
Dina mimi sichangii kitu hapa kwani sijui hata Randi nzuri za mapazia ni zipi nisije nikaharibu bure!Nikupongeze tu.........Kizito!!
ReplyDeleteNashukuru sana kwa kutushirikisha kitu unachopenda. Mimi pia napenda sana nyumba ilopambika vizuri kisasa. Naamini nyumba ikiwa inavutia inakutamanisha kuwahi kurudi nyumbani na unakuwa unapa-miss home ukiwa mbali.
ReplyDeleteHongera Dinah kwako kuko simple!
ReplyDeletehongera dina wewe msafi sana...nyumba inaelezea na wewe mwenyewe Mzuri
ReplyDeleteMimi tuliwahi kukutana duka la vipodozi Makumbusho kwa kweli wewe ni msafi na mzuri
Be Blessed
kwa kweli ni pazuri, yani pamekaa kizunguzungu , nahisi ata ukiwa na stress, the minute you walk into ur house stress zote zinaisha, i admire you, you have achieved a lot at a very young age.
ReplyDeleteIvi Dina unaishi wapi? na je ni nyumba yako au umepanga?Kwenu mpo wangapi na wewe wangapi?mbn unatubania kuhusu mpz? tuambie tu km unae wala usitutajie jina. Napenda sn maisha yako ingawa sikujui na hata sijui ntakuona lini mi naishi nje ya nchi ila nafatilia sn kipindi chako thru hii blog yako,napenda sauti yako na hapa kwenye swala la nyumba yani ndo umenimaliza kbs yani nazidi kukuadmire hongera sn na Mungu akuzidishie
ReplyDeleteanonym ulieuliza kama ni nyumba yake ua ya kupanga?
ReplyDeletesidhani kama hilo ni mada hapa, dina hutushirikisha vitu vyake vingi hivyo siku akitaka aseme kuhusu kupanga au kujenga atasema kwa wakati ulio muafaka. mada hapa ni hobby yake ya upambaji, hongera sana dinna kwa kipaji ulichonacho, keep it up siku moja waweza kuja kuwa mpambaji maarufu
Alphoncene Gerald(Mama Aisha wa magomeni)
ReplyDeleteDina wewe kiboko nyumba safi mpaka nimeitamani.
Mwanamke usafi babu siyo wengine usoni tuu kwake mmmh........
Mengi mafanikio
Uko kiutamaduni zaidi
umenikuna sana dina hata mimi huo ndio ugonjwa wangu kupamba nyumba napenda sanaaaaaaaaa! hongera sana huo ndio uanamke hata kama umepanga ndio uwe mchafu! Lol
ReplyDeleteDina kwako ni patamu. Hongera sana. I hope marafiki zako hawajuti kuwa na ww. unaonekana una roho nzuri sana. Mungu akubariki.
ReplyDeleteyap nyumba nzuri safi na simple km za kinaijeria vile napend@nyumba ikiwa simple c kupamba saaaaana km ukumbi wa haruc naona inakuwa too much kuna nyumba nyingine jamani cjui km ndo inavyotakiwa midoli imejaa kochi zota mito + vitambaa tena vingine vina na ujumbe juu god bless my house or whatever,maua sasa kila kona adi nyuma ya mlango kwenye ctuli muzani kwenye stend ya tv dinning table ukija picha za wazungu zimejaa kutani bado picha za memba wa family jamani naomba mswaada dina ni sawa au me ndo mshamba jamani,najua blog hii tunatembelea wengi wanawake japo na wanaume wapo dina ebu tusaidiane au km kila mtu ambae yupo interested atume picha bac japo ya kitchen or living room bedroom toilet whetever tuelimishane dina fanyia kazi ilo.asante
ReplyDeleteYa house is so nice but naomba nikushauri kidogo mpnz picha za hapo kwenye coridor kama mlangoni hiviii umezijaza sana bila arrangeement zimerundikana sana plz zipange tena vizuri so far its nice.
ReplyDeleteKiumri sio mkubwa sana Dina lkn una mawazo mazuri na yenye busara sana, km mtu hajawahi kukuona anaweza kusema huyu anayeongea au anayefanya hv vitu ni wale watu wazima wa zamani wenye busara zao na adabu. Km baba yako alivyosema sema namnukuu "WEWE NI MBUNIFU KAMA MAMA YAKO" hakukosea
ReplyDeleteHongera Dina!
ReplyDeleteila nahisi kama kupamba nyumba kunahitaji pia pesa. mana mtu kama unaishi katika nyumba ya kupanga sakafu imebomoka bomoka, ukuta rangi chafu, huna pesa ya kurepair, huna pesa ya kununua carpet? lazima utaonekana mchafu, kumbe pesa huna.
Hongera dada!
anzisha shindano la kupambanisha wamama wenye nyumba chafu au zina ufa au ukuta mchafu etc, ili uombe sponser na kampuni ya rangi, au home shopping center mkafanye ukarabati, kama anavyofanya Ice cube kukarabati magari. umenipata?
Mama Beto, DSM
best!
jamani Dina! katika watu ninaowapenda na kuwatamani ni watu wanaojipenda natamani nije nikuone kwako, hasa chumbani unaonekana ni mtanashati kama ulivyo nje, mimi nakaa jumba bovubovu toka 2003 niko na familia yangu ya mme na watoto 2 lakini kila mtu akija kwangu ananipenda na anasema hivi ungepata nyumba ya maana ingekuaje? dina mungu atakupa kama hiyo nyumba si yako ni ya kupanga inshallah mungu atakupa na pia utakua mfano kwa wanawake wote wa Tanzania wapenda usafi
ReplyDeletegday
Dina nimezidi kukupenda,leo nimeangalia blog yako paka saiv sa saba usiku sijalala. Hongera sana
ReplyDeleteDina, Big up sana, mwanamke urembo na maendeleo pia. Nimependa hobby yako.
ReplyDelete