Wednesday, April 27, 2011

WIKI ILIYOPITA ILIKUWA NA MAADHIMISHO YA KUZALIWA KWA WAFUATAO..

Wiki iliyopita ilikuwa na maadhimisho ya kuzaliwa Gea Habib na ilikuwa jumapili ya pasaka...kwa sababu ya purukushani za hapa na pale sikuweza kupata muda wa kumwish hapa kwenye blog yetu.
Hivyo naomba nichukue nafasi hii nimtakie la heri na zaidi aendelee kujituma katika kazi zake maana kiukweli katika watu ambao nimewahi kufanya nao kazi Gea anajituma sana tu na nampongeza sana kwa hilo.Ni mvumilivu sana,mcheshi sana,tukiwa kazini tunaweza kugombana sana tu lakini mwisho wa siku tunaelewana na kazi inaenda kama kawa.Mwenyezi mungu akuongoze na akutie nguvu uzidi kusonga mbele katika kazi na maisha yako na familia kwa ujumla...Happy belated birthday.

Pia ilikuwa birthday ya mtoto wa Gea anaitwa Khalfan ametimiza miaka mitatu,ni mtoto wa pili na mwisho wa Gea.Hii nilichelewa kupata picha...

Halfan na marafiki katika kulishana keki...
Happy belated birthday mtoto Khalfan Habib.

6 comments:

 1. Mama Mboni(Bibi Chief)April 27, 2011 at 5:24 AM

  happy birthday Geya. najua ulikuwa Dodoma siku ya pasaka ukiusaka mkwanja. Keep it up. Mwanamke kujituma na ndipo utaona mafanikio yako. mungu akulinde na akupe maisha marefu yenye furaha.Amina

  ReplyDelete
 2. Ashura from MbeyaApril 27, 2011 at 8:14 AM

  Happy birthday Gea wa Habibu, pia nakupa pole kwa kazi yako ya hekaheka maana mh unakutana na mengi, be strong ma sister. M/z mungu akujaalie maisha marefu na yenye baraka tele.

  ReplyDelete
 3. Kwanini useme wa pili na wa mwisho?kwani Gea kasema haongezi mtoto mwingine?

  ReplyDelete
 4. Pia mimi nimeadhimisha siku yangu ya kuzaliwa wiki iliyopita kwa hiyo najipongeza kwa kuwa hapa nilipo na TUPO PAMOJA.

  ReplyDelete
 5. Pia my lovely son amesherehekea siku yake ya kuzaliwa wiki iliyopita tarehe 20,namuomba Mola anikuzie mwanangu vema na kumpa maisha marefu pia. Hongera sana Gea na mwanao Mola awape maisha marefu.

  ReplyDelete
 6. Mtoto wa Geha mashalaah
  Mungu amtunzie handsome boy wake
  Dada Dina na wewe mtoto lini?
  Katakuwa kazuri
  Kama ka kike sikapatii jibu
  Maana baba na mama wote wazuri
  Birthday njema

  ReplyDelete