Wednesday, October 26, 2011

UMEWAHI KUFANYA MAAMUZI MAGUMU?

Nimepokea msg za wadau kadhaa mkilalama sijaweka kitu haya ndio naweka sasa ila nikiwa nina swali.
Umewahi kufanya maamuzi magumu sana kwenye maisha yako?ilikuwa ni kuhusu nini?
haya funguka sasa!

90 comments:

 1. Dina mi nimewahi dada niliwahi kufanya maamuzi magumu katika maisha yangu yaliyopelekea kutengwa hata na familia lakini niliamini nilichofanya kilikuwa sahihi na baadaye walielewa kwanini nilifanya hivyo ujue ni vizuri mtu kuwa na msimamo na kitu unachokita pasipo kuangalia jamii inataka nini ni vigumu lakini inahitaji ujasili maamuzi yalikuwa ni lazima niondoke katika ndoa pamoja na kwamba sikuwa na kipato kizuri na nilikuwa na mtoto mdogo lakini ndoa ilikuwa ndoano lakini namshukuru mungu ameniwezesha ukiwa sahihi hata mungu anakupa baraka zake ni mimi Deliwe

  ReplyDelete
 2. mh ni kweli dd Dina nishawahi kufanya maamuzi makubwa na mpaka leo najuta, ni kwa mtu ambaye alikuwa very important to ma whole life the p who i love the most, kwa kuwa nilimkuta na mwanamke nikaamua kuaachana nae still nikiwa nampenda sana na tukiwa mbioni kufunga pingu za maisha, inaniumiza sana, dd dina maana mpaka leo i never compere to any man i saw to ma life.

  ReplyDelete
 3. nimewahi kumuacha mtu pekee ninayempenda kwa dhati ili niokoe maisha yake asife, bila yeye kujua, ni historia ndefu sana ila hadi leo hajui ninamaumivu gani moyoni mwangu,anadhani nimempata mwingine, bila kumuacha yeye asingekuwa hai leo hii angekufa kifo kibaya zaidi ya cha ajali....... he is the one and only in my life.i love him till now,but i cant do anything..i want him alive i always pray for him hope one day, if i will be die, he will knw the truth may be.........

  ReplyDelete
 4. Dada Dina upande wangu nilifanya maamuzi magumu pale nilipo pata mchumba na kulazimika kuachana na bwana niliyekuwa nae ambaye alikuwa ni mume wa mtu we jasho lilinitoka kwani yule bwana tulipendana na alikuwa akinijali mnoooo! lakini dah masharti ya mchumba ilikuwa ni lazima niachane na yule bwana nakumbuka alilia sana baada ya kumwambia nashukuru mungu alinipa baraka zote na tukaachana! upo hapo dear

  ReplyDelete
 5. yap! nimewahi kumtema BF ambaye kiukweli nilikuwa nampenda sana lkn kutokana na tabia zake za ku-undermine girls, nikaona baadaye itakuja kunicost, maana yeye kumpiga demu ni kitu cha kawaida sana, na pia hayuko straight foward, yaani alikuwa balaa but MUNGU mkubwa niliweza kuachana naye kwani ilikuwa ngumu kutokana na vitisho alivyokuwa akinitolea kwamba siku nikimwacha atahakikisha ananitoa uhai,. kweli kuna siku alitaka kunigonga na gari, but nikasave

  ReplyDelete
 6. siyo tunalalama mama ni haki yetu mpedwa kupata habari kutoka kwako. na hiyo ni dalili ya kupendwa na watu. sasa tena kama umekuja na hasira vile kututupia swali mama? mbona habari ni nyingi tu wewe tu sijui siku hizi ukoje? au ndiyo unataka kuwa kama zama tena? anaweka picha mwezi!

  ReplyDelete
 7. Mimi nilishawahi kufanya maamuzi magumu, Kuhusu kuachana na Mwanaume tuliedumu nae katika ndoa kwa miaka sita na tukajaliwa kupata watoto wawili,. lakini ilifika sehemu nikasema nimeshindwa kuvumilia nikasema inatosha. Baada ya hapo nilichukua maamuzi magumu ya kuachana.

  ReplyDelete
 8. mimi maamuzi magumu niliyowahi kufanya pale nilipoamua kufanya check up ya HIV ndani ya masaa mawili without cancelling kwasababu ni kitu ambacho nilikuwa naazimia kukitimiza halafu najiigiza mitini mwenyewe.lakini siku hy nikafanya maamuzi magumu mpaka kwa doctor i thank God im safe.

  ReplyDelete
 9. heri leo umekuja na swali kuchangamsha akili afta kama siku 3 bila post.
  Maamuzi magumu niliyowahi kuyafanya ni siku moja nilipotakiwa kuchagua kati ya ndugu"wa damu kabisa tumezaliwa tumbo moja" na best friend when i say best friend i mean it a friend ambaye mnajuana kila kitu damm i dont need to remember that day,,,,dah but mwisho wa siku unatumia kajiakil alichokutunuku Mungu....

  ReplyDelete
 10. Mimi dada dina maamuzi maguu niliyofanya nuikuachana na mwaume ambaye nulikuwa nampenda sana ila siku ya siku nikagundua kuwa ana mwanamke mwingine yaani niliachana naye lakini niliumia sana kwani alishanippotezea muda wangu mwingi sana kwa kuniahidi kuwa ananioa lakini mwisho wa siku maneno yake yalikuwa hayana ukweli ndani yake yaani niliumia sana yapo nilifanya maamuzi magumu

  ReplyDelete
 11. Japo umepost kwa hasira!Cku nilipofanya maamuzi magumu ni pale nilikaa na BF KWA 4yrs kwa dhiki sana thn alipofanikiwa akaja hm kujitambulisha ili kutoa mahari kumbe alifanya hivyo sehemu mbili tofauti na niligundua kuwa na wazazi wake walishiriki sehemu zote mbili isipokuwa kaka yake na mkewewe hawakushiriki ndio walionipa habari baada ya kumbana alikubali kufanya hivyo!nilimwambia tuachane hapo hapo onsport!alinibembeleza sana nikakataa,thn akaja kwa na wazazi wake kwa wazazi wangu nilipogundua wapo hm nikaenda zangu Zanzibar kulala huko huko!iliniuma sana ila ilibidi nifanye maamuzi magumu coz naamini nimeubwa ili niwe na furaha

  ReplyDelete
 12. Kwa kweli Dina mimi nimefanya maamuzi pale nilipofiwa na mume wangu kwa kuwa alikua ameshaanza kuniumia katika mahusiano yetu alivyokufa baada ya miezi mitatu tu nikakutana kimwili na mtu baadaye nikagundua nina mimba. Kwa kweli ilikuwa mbaya kwani hata taratibu za miradhi zilikuwa hazijaisha na niliishi na huyo mume wangu kwa miaka kumi bila mtoto. NIKAFANYA MAAMUZI MAGUMU YA KUTOKUTOA MIMBA. Leo hii yaliyopita yamepita na nna mtoto mzuri anaitwa FARAJA ANGEL. THANKS GOD.

  ReplyDelete
 13. uups!!kaz kweli kweli..sijui nianzie wapi lakini anonymous wa october 26 2011,11:17 PM naomba tuwasiliane............u wont regret!!if u care

  ReplyDelete
 14. habari Dina kiukweli nimewahi kufanya maamuzi magumu ambayo yalipelekea familia kunitenga baada ya kuishi na mwanaume mpaka kupata mtoto bila hata familia yake kwenda kwetu. Nashukuru Mungu maana yalipita na akaenda maisha yanaendelea japo matatizo mengi ila Mungu Mwema.
  Bea

  ReplyDelete
 15. habari dina, mimi ni mama wa mtoto 1 na nimeolewa na mume wangu ninayempenda sana, nilishawahi kufanya maamuzi mawili magumu katika maisha yangu, kwanza nilikuwa na boyfried muislam na mimi mkristo, kutokana na imani za wazazi wetu hilo lilikuwa gumu kuoana, nikamuacha, baadaye nikapata mtu kumbe alikuwa ni mume wa mtu alinidanganya, nilipogundua tu naye niliachana naye mara moja, sikupenda katika maisha yangu mapenzi yaje kunicost.

  ReplyDelete
 16. Mimi bwana uamuzi mgumu nilioufanya ulikuwa wa kimafia zaidi lakini ilinibidi niufanye, mume wangu alikuwa anatabia ya kurudi usiku huku akiwa mtungi halafu anakuwa mjeuri, nikasema nitamkomesha, siku hiyo karudi tungi nikasema leo ni leo, nikacheki pochi lake nikakuta anahela nyingi sana, sasa nikachomoa kiasi ili apate loss, nikalala, ila baadae nikasema kama nimebakiza pochi inamaana atajua tu hela zake zimepotea ndani, nilichokifanya ni uamuzi mgumu wa kuondoka na pochi lote likiwa na vitambulisho vyote muhimu na hela zake. Asubuhi weee akaanza kutafuta nikamwambia mimi sijaliona kwani jana ulikuwa wapi, nenda ukalicheki huko huko ulipokuwepo....akalitafuta wee mpaka, hakuliona. Mwisho akasema mke wangu kweli ulevi noma...toka siku hiyo ametulia kwakweli. Sasa kila nikifiria huwa nacheka lakini nasema ni uamuzi mgumu uliokuwa na manufaa though nilimwonea huruma alipoanza kutafuta vitambulisho vipya teeeeh...teeeeh..teehhh..uwiii.

  ReplyDelete
 17. MIMI NILIFANYA MAAMUZI MAGUMU PALE NILIPOKUWA NIKIINGIA KILA SIKU NAKUKUTA POST ILE ILE...NIKAAAMU KUANZIA LEO NISIINGIE KWENYE BLOG YAKO LAKIN NIMESHINDWA NA LEO NIMERUDI...HAYO NDO MAAMUZI MAGUMU NILITAKA KUYAFANYA ILA NIMESHINDWA...UBARIKIWE KWA KURUDI.

  ReplyDelete
 18. habari Dina, kiukweli mimi nilifanya maamuzi magumu ya kumsamehe mume wangu baada ya kumfumania na binamu yangu ingawa niliumia mno ila niliamua nimsamehe baada ya yeye kuomba radhi.

  ReplyDelete
 19. We mafia kweli dah!!...bora hata siku ya pili yake au hata baada ya wiki ungejidai kuna kijana amevileta hapa home na akadai alipwe 50,000...tena ungempigia simu akiwa job ukamwambia kuna kijana yuko hapa na vitambulisha vyako ila anadai nimpe 50,000...angetaka kuongea nae angejidai hataki kuongea nae....Kwahiyo ungejidai kutaka ushauri kwa mumeo umpe pesa, au umpeleke pollisi...kwa vile alikuwa job angesema mpe tu nk...KULIKO KUMUACHA MWENZIO AKAANZA KUHANGAIKA UPYAAAA DUH! ILA ADAB ULIMTIA WEWE NI JASIRI...ILA INABIDI UVICHOME MOTO HIVYO VYA ZAMANI.

  ReplyDelete
 20. Dina hii topic imenigusa sana sana sana.....ni story ndefu ila naifupisha.
  Mimi ni mama wa mtoto mmoja kwa sasa nilifanya maamuzi magumu sana na nilifanya siri hakuna mtu anayejua isipokuwa mimi na huyo mwanaume aliyenioa.
  Dina niliishi na mwanaume kwa miaka 3 kama boyfriend katika uhusiano huo nilipata mimba nikajifungua kwa matatizoikabidi huyo mwanaume aniongeze damu. miezi mi3 badae wakati tunajiandaa kwa harusi tukaenda kupima ukimwi akakutwa ameathirika na vvu na mimi sikuwa nimeathirika...mind you tulikuwa ktk harakati za harusi na mambo yalikuwa tayari kabisa. nilifanya maamuzi magumu nikaamua kuolewa naye na mpaka sasa ninaishi naye ila mimi bado hajaniambukiza HIV kwa sasa.
  Lakini cha kushangaza mwanaume huyu bado kaweza kunisaliti katika ndoa na nimempa second chance nikisikia bado anaendelea na tabia hiyo nitafanya maamuzi magumu tena ya kuachana naye najua nitaweza.

  ReplyDelete
 21. Dada dina mimi nilifanya maamuzi magumu ya kubadili dini na kuolewa na muislam through wazazi walipinga sana ila ndio nishaamua na tunaishi vizuri tu ni mwaka wa 5 sasa and am hapily married with 2 kids tofauti na walivyofikiria wazazi wangu.

  ReplyDelete
 22. mmm...!kuna comment moja imenigusa though tumetofautiana kidogo,mm ilibidi niachane na mwanaume nimpendae kwa dhati kwanza kuokoa maisha yake na pili ili kuweza kuwa karibu na mtoto wangu,na sasa nimekubali kuolewa na mtu ambae hayupo moyoni jst bcz nimezaa nae na nampenda mtoto wangu,na imebidi nivumilie maumivu kero na migongano ya kila cku.nafunga ndoa december this year.

  ReplyDelete
 23. Annonyonous wa October 27, 2011 2:19 AM...HAYO SI MAAMUZI MAGUMU BALI NI UJINGA.....UNATAKA MWANAO AJE AKULELEE NANI SIJUI.....MANA UNAONA HII NI HATARI BADO UNAKIMBILIA?....WEWE UMEGUNDUA JUZI KUWA ANAKUCHEAT ILA INAONEKANA ALIANZA SIKU NYINGI NA NDO HUKO ALIKOPATA HAYO MARADHI....LABDA KAMA NA WEWE UNATUFICHA LAKIN UMESHAATHIRIKA.

  ReplyDelete
 24. DYNA KAMA COMMENT HAIJAMTUSI MTU SIDHANI KAMA KUNA SABAB YA KUIBANIA?!!...USILAZIMISHE WATU WACOMMENT VILE UNAVYOTAKA....KAMA HAKUNA AMBAO WALIWAHI KUAMUA MAAMUZI MAGUMU NA WAMEZOEA KUCHANGIA NOD WAKAE KIMYA?.....KAMA UTAANZA HIYO TABIA YA KUFICHA COMMENT KWA MTAZAMO WAKO TU, TUTAKUCHOKA MUDA SI MREFU.

  ReplyDelete
 25. HV HAKUNA ALIYE FANYA MAAMUZI MAGUMU YA KIMAENDELEO ZAIDI YA MAPENZI?????????????? kila mtu nilimuacha mchumba mara kaniacha.

  Kweli wa bongo kwa mapenzi ni noma, inaoneka ndio kitu pekee muhimu mnacho waza nakukipigania maishani mwenu, ndio maana tunashindwa kufanya vya muhimu kilicho baki BF wangu mara mchumba wangu.

  ReplyDelete
 26. anonymous wa october 26 2011,11:19 PM kwakweli nahisi story yako kama yakusikitisha sana kama hutojali unaweza kushare na sisi kutuelezea yaliyokusibu mpenzi. sio umbea jamani, ila pole kwa yote dear.

  ReplyDelete
 27. Dada dina! Maamuzi niliyotaka kufanya yalikuwa ya hatari ni pale mwaka 2004 nilipokuwa kidato cha pili nilipata wastani 50 kwa hiyo roho iliniuma nikaamua kunywa mafuta ya taa ili nijiue lakini niliokolewa na hapo ikawa mwisho wa kufanya maamuzi magumu bila kufikiria mbele

  ReplyDelete
 28. Jamani Dina mimi nimekasirishwa na huyo dada aliekubali kuolewa na muathirika na bado anajisifia kuwa ni maamuzi magumu anataka kufa yeye na bado mumewe si muaminifu,mbona watu wanapenda kucheza na maisha yao jamani unazani ungekuwa ni wewe unailo tatizo huyo mwanaume angekukubali,embu jaribu kufanya uamuzi mgumu ila uo ulioufanya sio kwakweli

  ReplyDelete
 29. Dada dina nilifanya maamuzi magumu pale nilipoamua kuachana na mpenz wangu kisa muisalm na kupata mkristo mwenzangu nashukuru ananipenda sana na mimi nampenda tuko mbio kufunga ndoa

  ReplyDelete
 30. Hivi maamuzi magumu yote ambayo watu wamefanya ni kwenye mahusiano ya kimapenzi tu?heri mdau aliesema yeye maamuzi magumu aliyofanya ni alivyoona hujapost akaamua kutokuingia kwenye blog lakini uzalendo ukamshinda akarudi kundini

  ReplyDelete
 31. dina mi nimefanya maamuzi magumu ya kutembea na mtu ambaye nimemzidi umri lakini twapendana kwa dhati

  ReplyDelete
 32. Dina umenigusa leo uwii... mimi ni muislam kuna kitu huwa nakijutia sana. Nilichumbiwa ramadhani ya 2008 na mwanaume huyu alikuja kwetu Mza kufanya hizo taratibu za kuposa,sasa alifikia hotel na mchana mmoja tukiwa na swaum tukajikuta tumefata kitu hotelini anapolala nia ikiwa kuchukuwa na kuondoka. Yani ibilisi wa ngono akatuvaa tukafanya mapenzi ijumaa ndani ya ramadhani tena tukafungua..baada ya hapo nikashika ujauzito kwa siku hiyo moja. Ilibidi nifanye uamuzi wa kuitoa kwani familia yote walikuwa wanajuwa huyo bwana alikuja wakati wa mfungo akakaa siku chache na kuondoka. Nikamsisitiza naitoa hii mimba hii aibu mimi siiwezi maana kusogeza harusi ilikuwa haiwezekani alikwenda nje ya nchi kitumbo kingeonekana na hata visa sijapata. Nipo nae UK ila najuta kutoa ujauzito ule huwa naomba Mungu anisamehe maana mhh nilihangaika kuja kushika mimba nyingine nimekuta kupaja mtoto mwaka jana. Ningeacha tu midomo ya watu ikasema ila ningekuwa na mtoto wangu huyo..najuta

  ReplyDelete
 33. nipo out of the topic lakini..nilikua nakuomba utuwekeee vipindi vingine vya hekaheka apo,ubadirishe ivyo vya zamani.asante kazi njema

  ReplyDelete
 34. Daaah! wewe anony wa saa 2:08am, umenipa akili, naenda vichoma leo leo.Thanks.

  ReplyDelete
 35. Dina mie nipo katika process ya kufanya maamuzi magumu, naomba Mungu anisaidie..... Nataka nivunje ndoa yangu niliyodumu kwa muda wa miaka 6, na watoto wawili. Kisa ni Mume hataki majukumu kabisa. Najikuta nahangaika mwenyewe kulea watoto, kujilea mie, wazazi wangu, na hata anataka niwatunze na wazazi wake. Huwezi kuamini ninapoondoka kwenda kazini asubuhi saa 1, huwa namwacha anakoroma, kalala. Haleti hata shilingi moja, na anadai anafanya kazi. Nalipa kila kitu, kuanzai kodi ada za watoto na chakula home natoa mie. Na nipo katika process ya kuanza kujenga nyumba, si atakuja kuing'ang'ania aseme ni ya familia wakati hajachangia hata maji ya kujengea? Na cha ajabu nimemwomba sasa mwaka wa 3, tuachane hataki. Nikaamua kumnyima tunda mwaka wa tatu sasa, lakini yupo tu, tena kawaida kama hakuna kitu kinaendela!Sasa hapo kuna ndoa kweli? Nafanya maamuzi magumu hivi karibuni

  ReplyDelete
 36. Mh anonymous wa oct 27,2011 2:19 mh huo ni ujasiri aisee ila kama hajatulia inabidi umuache huwezi jua mungu kakupangia nn katika maisha yako coz nina uhakika siku ulioenda kupima angekuta ww ndo umeathirika asingekuoa huyo fikiria upya na ujipange labda sio akili yako

  ReplyDelete
 37. Maboss jamani wananyanyasa sana wafanyakazi, nililazimika kuchukua Maamuzi magumu kwa kuacha kazi bila ya kuwa na uhakika wa kupata kazi kwingie baada ya manyanyaso kuzidi, kisa ni mtoto wangu kuugua na kutumia muda mwingi kuhangaika naye hivyo Boss kuona kwamba natega kazi na si ugonjwa wala nini, nililazimika kuacha kazi kuepuka manyanyaso hayo. Hata hivyo namshukuru Mungu kwani niliweza kupata kazi baada ya miezi mitatu na naendelea vema. Acheni Mungu aitwe Mungu. Baada ya muda kiwanga hicho kilifirisika!!!

  ReplyDelete
 38. Wewe unataka kujua maamuzi magumu tuliyofanya sisi, Je wewe kwanini usituambie yako?

  ReplyDelete
 39. Diana nasi twaomba utuambie maamuzi magumu ambayo ulishawahi kufanya

  ReplyDelete
 40. Yaani Dina acha mimi familia yangu ni islam tipical kwa umaskini wetu nikaamua kubadili dini ili nipate nafasi ya kuendelea na masomo, we walivyosikia waliwenifungia ndani nikawa siendi kokote Mungu wa ajabu binamu yangu alikuwa na vijipesa akasema ngoja nimkomeshe akanilipia ada ya A level kwenye shule ya kiislam nikawekewa vikwazo hakuna hata kurudi likizo home, nashukuru sasa nina kadegree kangu na Muomba Mungu anisamehe kwani kusudio langu lilikuwa elimu

  ReplyDelete
 41. kweli hii mada ya leo nimeipenda sana ahsante dada dina kwakuleta hii mada ubarikiwe sana imechangamsha kijiwe mimi maamuzi magumu niliyowahi kufanya nikuacha familia yangu na kwenda nchi za nje kutafuta maisha japo sijutii ila nawamiss sana familia yangu haswa watoto wangu

  ReplyDelete
 42. jamani jamani sasa mbona kila mtu mapenziiii, mapenziiii, hakuna hata mambo ya kifamilia, kielimu au topic nyingine.....

  ReplyDelete
 43. Dina, binafsi sijawahi fanya maamuzi magumu ila natarajia kufanya hivi karibuni baada ya kuona huyu demu uliyembandika kwenye hii post. Nimeishi na demu wangu karibia mwaka sasa ila ananiboa namtaka huyu demu uliyembandika. Je, ni mbongo na anaitwa nani? Please help!

  ReplyDelete
 44. Teteteh maamuzi magumu ya dina ni kutokuonyesha nwana wake

  ReplyDelete
 45. Dammmmmm Watz noma noma noma noma,,Dina ungebadili kichwa cha habari ukaandika maamuzi magumu katika mahusiano...kudadadeki hatuwezi kuendelea kwa hivi wote maamuzi magumu ni kumuacha mpenzi,sijui BF,sijui mume....dah kiukweli kimtazamo wangu imenisikitisha sana.to be honest inaonyesha jinsi gani watu wameweka mbele mapenzi coz woteeeeee ni kuachwa,kuacha etc etc..guys hayo si maamuzi magumu ni kawaida tu na katika wote waliogusia mapenzi aliyefanya maamuzi magumu ni aliyekubali kuolewa na mwanaume mwenye V.V.U wengine wote huo ni .........poleni sana akili zenu ndo zimeishia hapo kufikiria.

  ReplyDelete
 46. Nilifanya uwamuzi ambao mpka leo ninajuta sana sana sana nilikuwa na boyfriend nikashika mimba alinisisitiza usiitoe nilimwambia mimi naitoa akakataa nikalazimisha nilitoa mimba aliniambia kwa sababu hukutaka kunisikiliza mimi na wewe basi nimeolewa na mtu mwingine ninamiaka 38 sasa sina mtoto huwa ninajuta sana.

  ReplyDelete
 47. mimi Dina nilifanya maamuzi magumu pale nilipotoroka nyumbani kwetu upanga nikiwa bado mwanafunzi wa form II na kuhamia gheto kwa mwanaume maeneo ya fire bila wao kujua nakunitafuta mji mzima, walipopata fununu walikuja na polisi na kunichukua mimi na mwanaume wangu wakamuweka ndani namimi nikawakana wazazi wangu kuwa siwajui sina undugu nao kwa wakati huo, matokeo yake bwana alininyanyasa nakunizalisha mtoto akawa ananipiga nikarudi kwetu baba yangu kipindi hiko alikuwa mwanajeshi mstaafu akanifukuza hataki kuniona nikaamua kumtelekeza mwanangu nje ya geti lanyumbani kwetu, nikakimbilia arusha nikasota maisha kwangu yakawa mabaya nikazeeka hadi nikawa cjipendi tena hapo nilikuwa na niaka 19, badae nikapata bwana mkenya nikaenda nae kwao kenya akawa ananitesa nikaamua kukimbilia mombasa huku nikaanza uchangudoa nikapata bwana mzungu nikaenda nae Ujerumani nikakaa nae miaka mi3 akafariki dunia ndipo nikaamua kurudi Tz nakwaangukia wazazi wangu ambapo babaangu nilimkuta mgonjwa wa sukari nikakaa nyumbani miezi4 baba akafariki nikabaki na mama na mwanangu na ndugu zangu walikuwa na maisha yao wana magari mimi ndio nimebaki na mama mpaka leo na mwanangu yuko formII jangwani, babaake ni teja huko kinondoni saa nyingine anakuja home kufanya fujo hatulali, na mwanangu akiambiwa ni baba yake analia hataki kusikia baba yake sio teja. MERCY

  ReplyDelete
 48. Hi Dina. Mimi nilifanya maamuzi magumu pale nilipomuacha mtoto wangu wa mwaka mmoja na house girl na babayake nilaenda chuoni kusoma degree ya pili. Siku niliyoenda ripoti chuoni, ndo siku niliyomuachisha kunyonya. Iliniuma sana lakini sikuwa na jinsi.

  ReplyDelete
 49. Maamuzi magumu ni kuachana na wanaume jamani?? Ila nimecheka sana humu kina daDA MNA MAMBO KWELI KAZI YENU KUACHANA NA WANAUME NA NDIO KUAMUA MAAMUZI MAGUMU??

  hAHAHAHAHAAAAAAAAAA AMA KWELI POLENI SANA JAMANI.KUMBE HIYO NI SOCIAL PROBLEM SANA MAANA WATU WAMETAPIKA HUMU JUU YA KUACHA WANAUME WALA SIPIMI DU!!

  ReplyDelete
 50. WW ULIE MWENYE FIKIRA PANA MBONA HUJAANDIJA HAPO CHINI UMEKALIA KUPONDA, KWANI HUJUI KUWA MAPENZI NI ASILIMIA 99 KATKA MAISHA?

  ReplyDelete
 51. MIMI NIMEFANYA MAAMUZI MAGUMU SANA IMAGINE NDOA YANGU ILIKUWA HAIJATIMIZA MWAKA MMOJA LAKINI KITENDO ALICHONIFANYIA MUME WANGU NILIONDOKA NA NGUO ZA KULALA BILA VIATU MTOTO MGONGONI NA MSICHANA WA KAZI NA MPAKA NINAPOANDIKA MSG HII SIJAWAHI KURUDI HATA KWENDA KUCHUKUA LAPA NIMEANZA MAISHA MAPYA. NA U CANT BELIEVE NIMEMPELEKA MAHAKAMANI NA KESI NDIO INANGURUMA

  ReplyDelete
 52. Nyie anony mnaojidai cjui mnataka maamuzi magumu yawe kuchoma moto gorofa ni wapuuzi sana..hv hamjui maisha ni mapenzi au mnajitoa akili? Hovyooo
  Unafikiri hatuna maendeleo kwa akili zenu? maendeleo ni vile unavyo yadifine wewe...sasa tumefanya maamuzi ya kuachana nao na bado tunamaendeleo na misha yanaendelea....Haya toeni maamuzi yenu magumu tuyatasmini kama na nyie sio kutoka na nyumba ndogo ahahahahahaha

  ReplyDelete
 53. mimi nafanya maamuzi magumu leo natangaza ndoa kwa huyo binti kwenye picha hapo juu dina nipe contact haraka

  ReplyDelete
 54. sito sahau siku niliyo toroka kwetu na kwenda kwa mjomba wangu kisa kipigo cha mama kwakuwa nili mwacha mdogo wangu kitandani kalala mimi nikaenda kucheza halipo hamka kalia weeee mpaka majirani wakaja kuhuliza kulikoni? ndipo wakagunda kuwa hakuna mtu nyumbani nimi ndonilihachiwa nyumba siku hiyo mama halipo rudi hakazipata taharifa ndo kuhanza kiunipa kipigo ndipo nikatoroka kwenda kwa mjomba wangu Arusha nami wakati huo nilikuwa nikihishi moshi na wazazi wangu japo Arusha nilikuwa sipajui lakini niljipa moyo kuwa nitafikatu Mungu nimwema nilifika kwakuhuliziazia na hapo ndiyo pakawa mwanzo wa mafanikio yangu kwani mjomba hali nitafutia shule nanika hanza masomo yangu kwani mada huo nilikuwa na elimu ya msingi tu.

  ReplyDelete
 55. dina vipi nangojea contact ya hyuyo mrembo hapo juu nataka ndoa chap chap aanze kupika na kupakua kitu cha nguvu hicho yaani we acha tu

  ReplyDelete
 56. mmmmmmm kwa kweli ni social problem maana kila mtu maamuzi magumu yanahusu mapenzi hakuna maamuzi magumu yoyote zaidi ya hayo jamani???????? kweli ubongo umetawaliwa na hili jambo usipime haya poleni kwa maamuzi magumu ya kuachwa, kuachwa, kufumaniwa yaani ili mradi tu balaa la mapenzi

  ReplyDelete
 57. niliacha kazi wakati sijapata kibarua kingine,kisa ilikuwa na mshahara mdogo pamoja na nilikuwa si gain kitu in term of experience,for the whole month i was free except 5 days end of the month,so i decide to quite coz was bored and not gain anything in term of experience. mpaka now natafta kazi not yet get hope to get it soon, but want challenging post

  ReplyDelete
 58. ahsante dina kwa kupost hii mada,yaani ujumbe wa mercy unafundisha sana.

  ReplyDelete
 59. Dina nimependa hii topic. Nimepitia pia comment zooote, unao mashabiki wengi sana. Napenda kusoma mawazo ya wengine na mikasa iliyowakuta kwani kujifunza si lazima yakukute wewe bali twaweza kujifunza kutoka kwa yale yanayowakumba wenzetu...

  Pia naona waliosema kuwa watu wanawaza mapenzi tuuu. Ukweli ni huo mchangiaji; mapenzi yanaRUN dunia! Kila binadamu anapenda attention, twatumia muda mwingi kuwaza wale wanaotupa hizo attention/ wanaotupenda. Mara nyingi huwa ni wanafamilia au mwenzi. Lakini inapotokea huyo anayekupa attention anakusaliti, dunia hugeuka na kuwa mpya. Utatafakari jinsi ya kupata ulichokuwa unakipata kwa huyo aliyekugeuka(mliyegeukana) na ndipo wengi wamesema hapa kuwa walichukua maamuzi magumu.

  Binafsi jambo gumu nililowahi kuamua nikiwa mkubwa ni kuachana na boyfriend wangu wa miaka 5. Huyu tulikuwa naye akiwa anaanza maisha mapaka akafanikiwa, nilikuja kugundua kuwa alikuwa na mahusiano na binti wengine nami nikaamua kuachia ngazi. Hapo palikuwa pagumu maana imepita miaka sasa lakini mimi sijamsahau kwani nampenda sana. Sina raha miaka inaenda lakini yeye alipata uhuru wa kuendelea na yale mahusiano na hadi watoto kashazaa. Mpaka leo najutia maamuzi yale kwani sikutoa nafasi yake kujieleza lakini ndio hivyo tena mambo yamebadilika. Maamuzi magumu tunafanya yanasumbua akili na mawazo yetu huko mbeleni. No matter how tough the decision you made was; just believe in the future. It's never possible to forget but atleast we can believe in greater things........
  Christine

  ReplyDelete
 60. jamani mdau wa 1:10,mbona kiswahili kibovu hivyo.samahani lakini,hata kwa aliemaliza darasa la 7 haandiki hivyo.naomba jifunze

  ReplyDelete
 61. nilifanya maamuzi magumu pale nilipoamua kwenda kupanga chumba baada ya kufukuzwa kwa ndugu niliyekua naishi nae siku akacharuka usiku mzima kasema ilipofika asubuhi nikaona bora niondoke nikaingia mtaani nikamtafuta dalali akanitafutia chumba nikaanza maisha ya kulala chini.namshukuru mungu naendelea vema kabisa na namwomba aniepushe na kila baya anijalie afya njema

  ReplyDelete
 62. maamuzi magumu ambayo nilishafanya,nilikuwa na soma day school alevel,nilikuwa naishi na walezi sio wazazi,nikaomba niondoke nyumbani nikae kwenye nyumba zilikuwa karibu na shule.Bahati mbaya nikakuta vyumba vimesha wahiwa vimeisha na kurudi nyumbani siwezi kwa sababu nyumbani nilikuwa sipati muda wa kusoma kutokana na kazi zilizokuwepo.kukawa kuna nyumba ya udongo ipo hapo imebaki na chumba kimoja,ikabidi tukichukue mimi na rafiki yangu,tulikuwa tunachekwa sana na wanafunzi wenzetu kuwa tunakaa nyumba ya makumbusho hatukujali kwakuwa tulijua nini kilitupeleka pale.tukawa tunaishi hapo na kusomea hapo.kutokana na uchakavu wa hiyo nyumba,ilianza kutaka kuanguka ikabidi mwenye nyumba atuambie tuhame.Alafu ilikuwa ni kipindi nakaribia kufanya mtihani wa form six,ilibidi tuondoke sasa kila mmoja akatafuta nafasi kwingine.mimi niliwaomb marafiki zangu nikaishi kwao kwaajili ya kampani ya kusoma ingawa wao walikuwa waarabu,mkristo nilikuwa mimi tu.walinikubalia,nilienda kukaa huko huku tukiwa tunaenda shule na kurudi na kusoma bila kuwajulisha nyumbani.Na nyumbani wakawa wanajua naishi kwenye zile nyumba zakaribu na shule.Nilisoma kwa bidii sana mungu alinisaidia nikafanya mtihani wa form six nikafaulu vizuri sana nikaenda chuo kikuu.sasa ivi ni mwajiriwa kwenye benk moja hapa tz.

  ReplyDelete
 63. maamuzi magumu si katika mapenzi 2, ila most of tanzanian girls wanathink mapenzi ndo kipimo cha ujasiri wao,but its not,binfsi siwalaumu coz due to little exposure they deserve to think that way,gals tufunguke tutafute maarifa zaidi,2tafute opportunities nyingi maishani,zipo a lot,tuache kuthink inside the box,says lucy,by the way hi dina how are things going on in your daily life, have gday shost.

  ReplyDelete
 64. mimi nililazimika kumuacha mpenzi ninayempenda pale nilipogundua ana mtoto na mke. nikiwa nampenda mnoo na mda wote huo alikua akinificha but bado nampenda sana

  ReplyDelete
 65. kuachana na mwanaume wangu wa kwanza ambae nilikaa nae 8yrs....1

  ReplyDelete
 66. HELLOW!!
  Maishani mwangu nimewahi kufanya maamuzi magumu mawili.
  1) Mimi ni bint wa miaka 29 nilipata mimba nikiwa shuleni, mimba nilipewa na mwanafunzi mwenzangu, hapo ilikuwa 2005, Kwa kweli iliniuma sana sana, ukizingatia mm nilikuwa na akili sana darasani kiasi kwamba nilikuwa ninasomeshwa na America Ambassador, kuanzia darasa la kwanza mpaka form six nilikuwa nafasi ya kwanza darasni,Baba yangu alikuwa mkali sana sana na alikuwa ananipenda sana, yule aliyenipa mimba alisema yeye hawazi kulea mimba hana uwezo na wazazi wake watamfukuza hata shuleni tutafukuzwa wote,kwa hiyo niitoe ile mimba.Tulikusanya vijipocket money ikatimia elfu thalasin, kweli tukamtafuta doctor, Dr. akanipa dawa halafu akaniambia amshatoboa kifuko kwa hiyo itatoka taratibu. Nikasubiri mwezi wakwanza wa pil, watatu oooh tumbo likaanza kukua huku shule inaendelea hakuna anaejua, nikalificha mpaka nikajifungua bila nyumbani kujua, kwani ule mwezi wa kujifungua niliaga niaenda kujisomea kwa rafiki yangu, nilijifungua salama mtoto nilimficha kwani mama wa rafiki yangu alijitolea kunisaidia, niliporudi nyumbani walinishangaa kwani nilikua nimekonda sana, niliwajibu shule ngumu. nikafanya mtihani vizuri na majibu yalipotoka nilipata div 1. Sasa kazi ilikuwa kumpele mtoto nyumbani, Siku ya kwanza nilimpeleka akiwa na miezi sita. Niliwadanganya ni mdogo wa rafiki yangu, nyumbani walimpenda sana hata baba, maisha yaliendelea nikaenda chuoni mpaka nikamaliza, nilipokuwa chuo nilipata hostel nikatafuta dada wa kazi nikawa na mwanangu, Wazazi na Ndugu wote wamegundua kama yule ni mtoto wangu akiwa na miaka mitano! Sasa anamiaka saba na ni dume languvu Mungu anikuzie kwani ninampenda sana Jr.

  ReplyDelete
 67. Mambo DINA!
  Mimi nilikutana na mwanaume, tukakubaliana kuwa na uhusiano wa kimapenzi, mm sikujua kama ni mume wa m2,kwa kipindi chote tulikuwa wote,eeh bwana kumbe anamke na watoto.
  hapo niligundua baada ya kuanza kupata matusi kutoka kwa mke mwenzangu, mimi pia tulifunga ndoa tena ya kikristo kabisa, kumbe mkewe walifungu ndoa ya kimila, Matusi yalipozid nilimbana akakubali na kuniomba msamaha.
  Maamuzi niliyoyafanya bila mume wangu kujua nilimtafuta yule mkewe, nikamweka chini na kumwambia mm ndiye aliyekuwa ananituka, yataka moyo nilikuwa ninaogopa ila ndio nilisha amua, alilia sana sana. nikamwambia haya bibi yamesha mwajika. Leah

  ReplyDelete
 68. mimi nilichukua maamuzi magumu kwa kumsamehe mke wangu baada ya kumfuma live akiongea na simu na awara yake,akimwambia nakupenda sana mume wangu ...akataja jina,akaendelea kusema unajua leo nilikuwa nimepania nikaku...penzi lote ila ndo hivyo baba ...kasema niende saluni ya karibu na nyumbani,niliumia sana ukizingatia ni mke wa ndoa,ila nimemsamehe ila roho bado inaniuuma

  ReplyDelete
 69. jamani wote mna maamuzi magumu lakini langu kubwa kuliko kama mnakumbuka kipindi kile wakati wa ujambazi wa mabasi watu wanaekwa na kubakwa jamani yamenitokea nilikuwa safarini majambazi yakatuvamia nilikuwa mimi na mume wangu wakamwambia kati yangu na mume wangu nani aanze kubakwa kwanza mume wangu akaanza kubabaika nikawajibu mimi mume wangu akapagawa wakamwambia tukuanze wewe akazimia nikabakwa na mtu 5 nikaachwa hoi tulibakwa wengi wakubwa kwa watoto.walivyomaliza aja zao wakatuacha hapo chini tukaja okolewa na polisi.mume wangu kuamka anauliza ushabakwa nikamjibu ndio akalia ila mpaka leo tupo pamoja tunasongesha life.Sitasahau.

  ReplyDelete
 70. Mimi nilifanya maamuzi magumu kwa kumpenda sana DINA MARIOS bila kumfikia mahali alipo ili nimpe hoja zangu, nilioona muda unazidi kwenda na siwezi kufika nchi aliyopo Dina basi nikaamua kutafuta mdada mwingine, huku roho ikiniuma sana kwa kutompata Dina.basi sina jinsi maamuzi magumu ni kuachia ngazi na kuparamia nyingine.

  Poleni wote aambao maamuzi magumu yamewasibu kwenye mapenzi.namsifu mmoja tu humu aliyefanya maamuzi magumu ya kuolewa na mwenye HV.Huyo kweli ndo mwenye maamuzi magumu sana.Sisi wengine wote ni ujeuri wa akili ya machoni na tamaa ya mapenzi tu na ile haraka ya kupenda na kutaka sifa ya na yeye kawa na fulani.

  Na kina dada mmekuwa wadhaifu katika suala la mapenzi linawaendesha mbio kama vile maisha yenu yanaisha leo na wanaume wanawatesa udhani mlikopa pesa kwako au kama ndo waliwazaa.

  ReplyDelete
 71. mmejiona mlivyo wafinyu wa akili na mawazo?so do you think sikuweka jina coz ni kuogopa ama what?au wewe unahisi nikiweka jina linasaidia nini?hata kama mapenzi yanachukua hizo asilimia 99"sijui kwa research ipi uliyofanya na wala sidhani kama una uwezo wa kufanya hiyo research kwa akili zako fupi ulizokuwa nazo,,,tatizo ndo mnafikiria mapenzi ni big ishu na kipimo chenu cha ujasiri kama mdau alivyosema hapo juu,ila kweli ukosefu wa exposure mna haki kufikiri mnachofikiri,dammm hii mada imezidi kufumbua watu akili na kujua watz tunasimamia wapi,,dina mama badili kichwa cha habari wawekee maamuzi magumu katika MAPENZI utawakuna wengi,,eti mapenzi asilimia 99 mbona hujifungii ndni tu sijui na bwana wako ama bibi yako mkala na kuvaa hayo mapenzi yenu,,shame on you anonymous wa October 27,2011 11:11PM

  ReplyDelete
 72. jamani ndau anayesme kiswahili gani hicho mbona hata redio zetu zinachangia kuua kiswahili mfano ule wimbo wa hakunaga nimeupiga narufuku nyumbani kwangu ndani ya gari yangu na katika tv yangu nikimuona mtu anauintatein siku hiyo namgadafi tu kiswahili gani kile

  ReplyDelete
 73. mimi nililazimika kuacha kazi

  ReplyDelete
 74. mimi nilitoa maamuzi magumu 2 , la kwanza kuacha chuo kikuu na kuolewa na mzungu sikutaka kuoelewa ila kutokana na kutokujaliwa na wazazi na hali ngumu ya maisha kipindi hicho inabidi tukae mwaka mzima kusubili majibu nilikuwa sina sehemu ya kuishi nilikuwa na rafiki mzungu aliniimbia anataka kunioa nikakubali nikaondoka nchini, ndoa yetu ilidumu kwa miaka 5 tukaachana .niliamua kuamua nchi nyingine ya ulaya kujiendeleza kielimu nikakutana na kijana mwingine wa kizungu akasema ananipenda , nikamwambia sina mda nimekuja kusoma tu akaniambia he is looking for long term relationship leading to marriage. basi nikamkubari baada ya mwezi mmoja nikapata ujauzito ndugu zangu wakaniambie nitoe kutokana na shule mimi nilikataa baba wa mtoto alikubali mtoto tatizo likawa hataki kutafuta kazi na hataki tukae pamoja .na mimi siwezi kufanya kazi kipinde kile na sikuwa na ela ya kodi ndugu na marafiki walinifukuza kwenye nyumba zao . Ilinibidi niache shule nirudi nchi niliyokuwa nakaa zamani . nashukuru mungu serikali ya hii nchi ilinisaidia kila kitu .baba wa mtoto hapigi simu wala hataki kumuona mtoto ananilaumu kwa uamuzi wangu wa kuondoka nchini kwao. anyway, mtoto ananiletea blessing nashukuru mungu ,nimepata kazi nzuri, mtoto shule bure , nyumba bure,na nyumba nimenunua tz .my life is much better than i was before.

  ReplyDelete
 75. Dina, big up sana yani hapa nasoma hizi comments na full kicheko! aisee..wewe ni mbunifu sana. imenichekesha ya wallet sipati kusema na kuna mdau mmoja naye eti onh! ungemwambia wallet imepatikana kijana mmoja ameleta hapa ila anataka alfu 5o! kwikwikwikwi! uwiiiiii! dawa ya moto ni moto naapa! well back to the topic..binafsi nilifanya maamuzi magumu ya kuacha kazi pale nilipotofautiana na manager wangu! na muda huo ilikuw nikipindi kigum sana kwani marehemu babangu alikuwa ni mgonjwa sana, pamoja na kusema kuwa wazazi wangu walikuwa hawahitaji msaada wangu kihivyo lakini my small contribution could had made a difference! lakini nilikuwa stressed up na manager mdwanzi mwingereza mmoja.. kwa wale waliobahatika kufanya kazi na waingereza watakubaliana nami kwamba most of them ni difficulty people..mbaya zaidi mimi huyu wangu alikuwa ni mwanamke mwenzangu, so she was mean to me.Unajua kazi ili ufanye vema unahitaji kuwa na akili iliyotulia, ili uweze kuwa makini na kazi yako. nilikuwa kama admin & finance manager, na issue malipo yote ya kampuni, including kumlipa yeye mshahara ama perdiems/night allowances kama anasafiri..halafu na ripoti directly kwake...sasa akataka kuleta mabadiliko gafla tena kwa personnel wa field..nilisimamia kupinga kwa nguvu zote kwani field officers ndo wanaofanya mashirika hayo (mushorooming DONOR FUNDED ORGS) yaweze kuandaa ripoti kuhusiana na hali halisi ya mradi..sasa yeye anakaa ofisini..hajui adha wanazokutana nazo hao field guys, (kuna sehemu miundo mbinu ni tabu, watu wanapaki gari wanatembea mwendo mrefu kuwafikia watu tena katika hali ya shida) then mtu anakukata kiji nite allowance chako kwa kisingizio ambacho ni very cheap! so, nikanunua mtanange, nikawatetea..Director aka rule in my favour (field officers favour, mana nilijipa u advocate) basi kuanzia siku hiyo mwingereza yule alikuwa ananitafutia sababu ili ani harras...nikawa sina raha ikatokea siku nikateleza kidogo...weeeeeeeeeee! alihakikisha naona ofisi chungu...ikafikia mahali hata salam ikawa shida..unajua kuna position flan mtu flani lazima aanze kusalimia..mfano umeingia mahali wewe ndo unatakiwa uanze salam..sio uanzwe..basi ikiwa ni hivyo yeye hasalimii..imagine!!!..nikaona duh! huyu amefanya ofic isiwe tena mahali ambapo nafurahia kufanya kazi..sijui wapi ntapata kazi, ntaishije, hasira zilikuwa zinanipanda hata natamani nimtukane ikitokea jambo kidogo ndivyo sivyo( alikuwa anani provoke kwa nguvu zote) ..nikaona lol..maskini mie but jeuri..nikawasilisha barua yangu ya kujiuzulu...(upinzani ukawa mkubwa, director hataki, wafanyakazi wenzangu hawataki...(director yeye hayuko nchini, hukaa UK, TZ hutembelea tu na alikuwa anajua how hard working I am.) lakini nilimeza pride na kusema no! either mimi niondoke au yeye manager (wakati katoka kwao dhiki tupu na somehow wana undugu na director...ni kitu kisingewezekana, so nikaacha kazi) KWA KWELI NI UAMUZI MGUM SANA...LAKINI KWA KUWA NILIKUWA SINA MAKOSA, MUNGU ALINISIMAMIA, NIKAPATA KAZI IN 3 MONTHS SINCE MY RESIGNATION!!
  DOREEN, MIKOCHENI.

  ReplyDelete
 76. Dina maamuzi magumu niliofanya ni masomo haya ninayofanya kwa sasa.Nimeolewa kwa sasa niko Abroad kwa masomo nimemwacha Mume nyumbani TZ na sasa ndio nimeanza mwaka wa mwisho wa masomo yangu if God wish nataraji kumaliza shule mwakani mwezi wa nane. Ni Maamuzi magumu sana. Marafiki zangu wooote hawakuamini nilipowaambia naondoka wafanyakazi wenzangu nao mpaka leo wananiona mimi kama chizi flani hivi ila Nachomshukuru Mungu Mumewangu ni muelewa sana na Muomba Mungu anipe ujasiri nimalizie mwaka wangu wamwisho nirudi nyumbani kujenga familia yangu na Taifa langu.
  Ni maamuzi magumu saaaana na linaumiza Mno! ila nikwa muda huu tuu then after ni kheri. Inshallah M'Mungu atanisaidia nitamaliza salama.

  ReplyDelete
 77. Maamuzi magumu niluyoyafanyaa maishani mwangu ni kuacha kazi za watu binafsi na kwenda kijijini kufanya kazi za serikali na wakati naacha kazi nilikuwa sina pa kuanzia wala pakushikia ila niliacha na nikaenda mbeya na nikawa afisa elimu. namshukuru Mungu ni uwamuzi mgumu niliuchukuwa lkn sasa una faida na mimi . chaooooo

  ReplyDelete
 78. Dada d & wadau mm ni msichana mwenye umri wa miaka 20, naishi Mwanza na dada angu, nina ugonjwa wa uvimbe wa tezi ama goita nina clinic Bugando na end of the day nitafanyiwa opareshemi tatizo uwezo wangu ni mdogo na oparesheni ni gharama naomba msaada wenu iwe kwa hali au ushauri kwani sina wazazi wote wawili wameshafariki tegemeo langu pekee ni dada yangu ambae yeye pia ni muolewaji tuu. Ndoto yangu pekee ni kutibiwa huu ugonjwa kwani unanitesa sana sifanyi kazi nzito, siishi kuugua mara kwa mara siwezi, silali kwa raha, hali ya hewa ikiwa ya mawingu hunitesa sana. Nahisi nikitibiwa nitaweza kumudu maisha yangu na nitayaendesha mwenyewe. Natanguli shukrani zangu kwa yeyote atakaenisaidia kwa namna yoyote ile Mungu awabariki Naitwa Agnes Joseph.

  ReplyDelete
 79. mwanaume kunizalisha wakati sikuwa tayari na kutoa siwezi niliumia sana coz alinivurugia kila kitu bt bahati mbaya mwanangu alikufa bahati mbaya.

  ReplyDelete
 80. hey Agness Joseph,,pole ila kuna habari nimeisikia juu juu kuna madaktari from india wapo hapa Dar fuatilia unaweza kubahatika kupata huduma yao mi nilisikia kidogo kupitia clouds tv dondooo za habari mana si mtazamaji wa habari kihivyo

  ReplyDelete
 81. dada dinah,nawe tuambie maamuzi uliokwisha kufanya katika maisha yako

  ReplyDelete
 82. dada dinah nawe tuambie maamuzi gani ulishayafanya katika maisha yako

  ReplyDelete
 83. we doreen waonyesha una mneno mengi kuliko utendaji,summarize bana sa kila person akiwrite ka wewe humu ndani kutaeleweka kweli? c itakuwa chaos ?

  ReplyDelete
 84. mimi nina miaka 31, mwaka 2010 nilifanya maamuzi ambayo kwa mara ya kwanza niliona magumu ila mpaka sasa sijajuta, miaka mitano nyuma niliachana na mwnaume nilofunga nae ndoa, ndani ya miaka mitatu nilikuwa na mahusiano na mwanaume mmoja, naye ameniumiza Dina sipati kukwambia, nilikuta anataka kumolest mwanangu wa kiume, nikaamua kuchana na wanaume kabisaaaaa, niliweka moyo wangu pending nikagoma kupenda, mpaka leo hii sijawahi kuona mwanaume nikampenda ingawa wanakuja sana, Nimeabstain, sijawahi ona tatizo lolote kwenye hilo..yani nafsi yangu haisumbuki kabisa, nafurahia maisha yangu isivyo.Na ninamshukuru mungu kwa kuniwezesha so far..kama watawa wanaweza nami nitaweza zaidi...

  ReplyDelete
 85. anonymous wa oct.31, 2011,3.55AM..WEWE ni mmoja WA kati ya waliosoma hilo gazeti langu tetetetetetet...karibu sana ..mbona hujashea maamuzi magum uliyoshawahi kufanya....wasoma ya wenzio tu na kukosoa..uchoyo tu...mwone kwanza! tunajifunza kwa kubadlishan uzoefu! DOREEN!

  ReplyDelete
 86. Dada dina ebu weka vitufe vya kulike coz kuna comment huku ni nzuri sana.

  ReplyDelete
 87. Loh! inaelekea wengi wanafanya maamuzi magumu juu ya wao na wawapendao... story yangu ni tofauti, mie nilifanya maamuzi magumu pale nilipomaliza form six hapo zanaki girls... sikuchaguliwa kwenda mlimani ila nikapata IDM wakati huo hakiitwi chuo kikuu!!! nikakataa kwenda baba alikua ameisha andaa driver kunipeleka na mama kafanya shoping ya vitu vyote, sitasahau hiyo siku niliamua siendi coz I want to go to the university kupata degree and not so called equivallent to a degree. Basi bwana kila nilipokua naona scholarship nikawa na apply ndani ya miezi 3 nilipata scholarship nikaenda nje ya nchi, hapa nilipo nina MA in mass comm; Mpaka leo wazazi wangu wanaamini kuwa niligoma kwenda IDM kwa kua nilikua na hiyo scholarship lakini lah hasha nilifanya tu maamuzi magumu sana bila kujua mbele itakuaje, ila namshukuru sana Mungu imelipa sio siri.

  ReplyDelete
 88. hello Dina...dah am sory nimeion ahiimada too late kiasi fulani...mimi ni kijana mwenye miaka 30..nilijigundua mwaka huu kuwa naishi na virusi vya ukimwi..nimwajiri mwenye kipato cha wastani..nilikua na mpenzi wangu tuliedumu nae kwa takribani miaka 4..kuanzia mwaka jana niligundua nyendo zake hazikua salama sana..na tulikua tun autaratibu wa kupima kila baada ya miezi 6 nikaenda kupima nikajikut an ahali iyo..nilichoka sana il anashukuru Mungu nimepata courage na maisha yanaendelea kama kawaida..huyo msichana sikumueleza chochote maana kwanza tulishaanza kuwa na migogoro na kulumbana mar anyingi ..mwaka jana mwishoni nilikutana na binti ambaye kiukweli nilimpenda sana...na yeye pia alinipenda sana..ni wife material kuliko hata huyu niliekua nae kabla..nilimuaproach na akakubali kuwa na mimi.ila baada ya mimi kuijua afya yangu mwaka huu nilipunguza mawasiliano nae gafla...sikutak ajapo kulala nae for sex..nilihofia maisha yake nicje kuyaweka hatarini...maana hata kondom siziamini tena coz ndiyo zilinipasukua mar akadhaa hadi nikapat aivyo virusi...so niliamua kuachana nae ingawa tunawasiliana...nimempromiss ipo siku ataujua ukweli...na ninaamimi ivyo...huo ndio uamuzi mgumu..kwa sasa nimekua mpweke sana..nahitaji nipate mwanamke ambaye atanikubali na hali yangu japo nizae nae mtoto mmoja..au ikiwezekana tuishi pamoja kwa matumaini..naamini inawezekana...

  ReplyDelete
 89. Nillifanya maamuzi magumu pale nilipofanya ngono na baba yangu mdogo ili anillipie ada ya shule. Nililia mwaka mzima ila ckuwa na jinsi na mpaka sasa naumia kwa kumsaliti mama yangu mdogo

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kwa kweli mimi nimefanya maamuzi ambayo najiona mjinga mpaka leo ambayo ni kuchezea shule ila namuomba mungu niweze kupata chuo kingine na kuendelea masomo

   Delete