Friday, October 28, 2011

WATANGAZAJI WA RADIO/TV NILIOKUWA NAWASIKILIZA AU KUWATAZAMA WAKATI BADO NASOMA...

Kwa kiasi kikubwa mimi nilikuwa mfatiliaji sana wa vipindi mbalimbali vya radio na tv toka nikiwa mdogo.Ukiacha watangazaji wale tuliokuwa tukiwasikia wakati wadogo kabisa kama Deborah Mwenda na mama na mwana.Kuna watangazaji ambao walinifanya nipende kusikiliza radio au kuangalia tv wakati nikiwa sekondari mpaka nilipokuja kuwa na mimi mtangazaji/mburudishaji.Nawakumbuka sana wafuatao....

Sebastiana Maganga...akiwa radio one na Dj show,weekend show na vingine nimevisahau mpaka wizara ya ladha akiwa clouds fm.

Misanya Bingi hahahahahah alikuwa ananifurahisha katika kipindi cha chemsha bongo na kikengele pale kati ukikosea jibu.Pia itv alikuwa ana kipindi cha mziki nimekisahau jina kama kuna anaekumbuka tukumbushane.

Nilikuwa namzimia Asha Mtwangi katika taarifa ya habari pale itv,akiwa na nywele zake za curl hivi

Betty Mkwasa alikuwa akisoma taarifa ya habari lakini pia alikuwa na kipindi chake cha ukimwi ni huu....she was amaizing kwa kweli.Flora Nducha katika taarifa ya habari itv

Sunday Shomari nilikuwa nikiangalia kipindi alichokuwa anafanya na dada anaitwa Monica Mfumie.Ilikuwa kupitia itv kipindi cha miziki miziki.

John Dilinga wakati yupo radio one alikuwa ana kipindi usiku cha mapenzi sikumbuki kama wakati ule kilikuwa kinaitwa chombweza kama ilivyo sasa.Kili kipindi kilikuwa talk of the town kwa kweli nakumbuka tulikuwa tukikutana shule ni kusimuliana vyote tulivyosikia kwenye kipindi hicho hasa hadith za mapenzi.

Taji Liundi nilimsikia clouds fm akifanya vipindi vingi nimevisahau

Sos B alikuwa magic fm ila nimesahau alikuwa anafanya kipindi gani.

Gadna G Habash hapa hapa clouds fm na top 20,Dr Beat,fataki...jahazi ilianza nikiwa tayari nipo clouds fm.


Amina Mollel alikuwa anafanya kipindi fulani hivi jioni ya jumamosipale radio one.Kilikuwa kipindi cha kuchagua miziki,pia kutafuta ndugu uliowapoteza siku nyingi.

Jimmy Kabwe kupitia clouds fm akiwa na Fina Mango katika power breakfast kwa lugha ya kiingereza.

Fina Mango nilianza kumfatilia wakati wanafanya kipindi cha asubuhi power breakfast wakati huo cha kiingereza akiwa na Jimmy Kabwe.Powerbreakfast ikaja kubadilika na kuwa kwa lugha ya kiswahili ndio akaungana na Madudi kipanya na Gerald Hando. Pia kipindi cha rafiki.

Kaka Bonda.....nilikuwa namsikia sana katika chuchuchu akiwa na marehemu Amina na Masudi Kipanya
Marehemu Amina Chifupa na Afrika Bambataa,chuchuchu akitumia a.ka. ya mama mdogo,leo tena,kwa raha zetu ndani ya radio ya watu alikuwa noma sana.

Masudi kipanya na Bambataa,chuchuchu,powerbreakfast hapa clouds fm yaaani balaaaaaa

Janet Mwenda Talawa kwenye taarifa ya habari Itv nilikuwa navutiwa nae

Abubakar Sadiq na Dj show ya radio one stereo

Rose Chitala na wakati wa maakuli,chombweza time ya radio one
Sebastian Ndege na njia panda ya clouds fm ilikuwa lazima usikilize mikasa mbali mbali ya maisha ya watu kila jumapili.


Hii ni listi niliyoikumbuka kwa haraka haraka kama una wa kwako aliyekuwa akikuvutia unaweza kumtupia hapa.Hawa hapa kwa kiasi kikubwa wameweza kuinspire na wengine kuingia katika kazi hii ya utangazaji.Wapo ambao bado ni watangazaji na wengine wanafanya kazi tofauti na utangazaji.

78 comments:

 1. kwakweli dada dina leo umenigusa nilikuwaga napenda sana kipindi cha njia panda ya kila jumapili nilikuwa siachi kusikiliza sijui kama mpaka leo bado ipo maana sasa hivi sikai nchi niko nje ya nchi naomba sana dada dina kama bado inaendeleaga hicho kipindi cha njia panda naomba unielekeze namna ya kuipata huku ubarikiwe sana na kazi yako nzuri

  ReplyDelete
 2. umemsahau julius nyaisanga jamani na joyce mhavile kulikoooni

  ReplyDelete
 3. Asante niliye tokea kuwapenda sana kati ya watangazaji wote ni Betty Mkwasa na Flora Nducha, ingawa siwajui sijawai kukutana nao

  ReplyDelete
 4. RUKIA MTINGWA,
  CHARLES HILLARY
  KAKA BONDA KIPINDI FULANI CHA WATOTO


  CUTHB

  ReplyDelete
 5. Da! umenikumbusha mbali kichizi, ila hiyo picha uliyosema ya Misanya Bingi ni yeye kweli? Asha Mtwangi, yuko wapi jamani? nimemmisi sana na mitindo yake ya kiafrika. Saafi sana Dina

  ReplyDelete
 6. Dina umeziba pengo la Amina Chifupa hilo halina mpinzani ila hawa wafuatao mapengo yao hayawezi zibika juu mpk sasa jujudi hazijaonekana.

  CHARLES HILARY alinifanya nipende charanga jamani huyu mzee alikuwa soo sooo deep kwenye ule mziki
  MOSES JUSTIN kipindi ni mtaa wa mangoma
  JOHN DILINGA kipindi dedication
  BLANDINA MONGEZI kipindi cha kusoma salamu
  kipusa kilikuwa kikipigwa vema kabisa na ABDALAH MAJURA alikinogesha hasa
  JULIUS NYAISANGA taarifa ya habari
  RAINFRED MASAKO na sauti ya pekee ktk matukio ya wiki
  MIKE MHAGAMA na dj show sauti murua kbs
  SUSAN MUNGI taarifa ya habari
  MIKIDADI MAHAMOUD na sunday special

  ReplyDelete
 7. Dina ckujui ila nakukubali kupitia leo tena na utakuwa miongoni mwa watu watakao zungumziwa sn sn badae kwa utangazaji wao mzuri. My point is siku hizi hakuna watangazajiiii ilikuwa zamani na si sasa wengi wanaigana sauti,majivuno,umaarufu,mara luga gongana afu broken,vichekovicheko visivo na msingi studio,sometym wengine wanaboa kbs.

  ReplyDelete
 8. Nawe pia tutakukumbuka sn siku ukiacha hii kazi.Kipindi chako kinasikilizwa na wengi mno ila type flani ya watu ndo wengi na wewe utakumbukwa kwakuwa unajua kuwalenga hao watu huchanganyi luga,hapo ndo uliposhinda,unauvaa uswahili kbs na vijimaneno flani yani mtaani kule kati ukimiss unajisikia vibaya.
  Sasa mwingine kipindi km icho eti anachanganya luga yani WANAKERA sn watangazaji wengine hii fani imeingiliwa sn kwa sasa zamani ilitendewa haki ila kwa sasa NO.
  Article nzuri sn hii

  ReplyDelete
 9. umenisuuza sana na hii listi. mie naongeza Julius Nyaisanga, Malima Nderema, Abdallah Mlawa, Halima Mchuka wote RTD, Rukia Mtingwa ITV, Edda Sanga RTD, Godwin Gondwe na Juma Ahmed Baragaza RFA, Samadu Hassan KBC Nairobi...Listi ni ndefu sana dada.

  ReplyDelete
 10. Fauzia T Aboud, Suzan Mungi pale I.T.V,, Hao nawakubali mpaka kesho,,walipotea aliporudi Suzan Mungi nikawa happy noma..then nikawa nawafagilia MArehemu Amina Chifupa"R.I.P" we always gonna remember you.Fina MAngo I wish siku arudi on Radio,Jack Jackline Kombe"dada rudi tunakukubali sana now days unasikika kidogo sana hewani..No Name

  ReplyDelete
 11. ACHA USHAMBA WEWE..Watangazaji hapo ni wanne tu waliobaki ni maDJ...HAKUNA hata mmja mwenye sauti ya kuvutia...

  ReplyDelete
 12. aaaah umetisha,ila ctomsahau jamaa aitwae MIKE PESAMBILI MHAGAMA na jamaa flan msomaj wa taarifa za hbr kipind kile jina la mwanzo ni JOHN

  ReplyDelete
 13. MASOUD KIPANYA + FINA MANGO =BAD NYUUZ....

  ReplyDelete
 14. HHAHAHAH DINA UMENIKUMBUSHA MBALI KIPINDI CHA MISANYA BINGI JAMANI ALAFU NA SANDE SHOMARI HAPP KATI SADIKI HAHAH ENZI HIZO NA HICHO KIPINDI CHA MALOVEDUVE CHA SOS B NA JOHN DILINGA MATLOW HAHAHAH JAMANI NILIKUWA NAIZIMIA SAUTI YA JOHN DILING ANYIE ACHENI TU JAMANI!

  KW AUPANDE WA WANAWAKE AAH SIKUNA NA MVUTO NA MTU YOYOTE HHAHAHHAHA NATANIA JAMANI

  ReplyDelete
 15. HIYO LISTI MIMI ONGEZA SUSAN MONGI TAARIFA YA HABARI ITV LOL MDADA ALIKUWA ANANIVUTIA SANA

  ITIKA

  ReplyDelete
 16. jamani dina usinambie kama kwenu mlikua mnakamata radio one,magic fm na itv basi radio zingine hakuna hakuna watangazaji jamani umemsahau fred dwaa kweli mamii unakumbuka radio Tanzania kipindi hicho we mtoto embu kumbuka vizuri

  ReplyDelete
 17. hivi wewe dinah una umri gani ? maana hao watangazi wote ni wa juzi juzi tu na wewe ndo ulikuwa unasoma , umezaliwa 1991 nini ?
  na kama kweli basi una mwili mbaya , unaonekana mzee...

  ni maoni yangu tu hayo natumai hujachukia

  ReplyDelete
 18. dina hyo picha ya misanya bingi ni yeye kabadilika sana

  ReplyDelete
 19. ki2 cha flora nducha,misanya bingi na mama teri,amina mollel,rose chitala,janeth,dilunga walikuwa noma.siyo siku hizi wengi wanaboa,wachache wanapatia na hii yote its due to kuvamia fan-lucy

  ReplyDelete
 20. KAKA BONDA,MAREHEMU DA AMINA CHIFUPA NA MASOUD KIPANYA DA COMBINATION WAS AMAZING SANA WAKITANGAZA NA PIA FINA,MASOUD NA GERALD HANDO IN POWER BREAKFAST

  ReplyDelete
 21. Yan dina umenkumbusha mbali sana me chemsha bongo ilikua ndo favourite session kwa kweli.

  ReplyDelete
 22. dinna kuna mdada alikua anaitwa asia mohammed alikua kwenye kile kipind cha kusoma card mida flan hiv ya mchana mchana na misanya bingi pale radio one.......nlikua napenda sana utani wao radioni. yani somtym hadi nazubaa kwa kuwaskiliza jaman...sjui yuko wap yule dada alikua na sauti nzuriiii then ya upoleeeeee!

  ReplyDelete
 23. BLANDINA MONGEZI CJUI YUKO WAPI CKU HIZI?
  NEMHINA

  ReplyDelete
 24. John Ngayoma ktk taarifa ya habari

  ReplyDelete
 25. raido one/itv yaonesha njia nyie mwafata...umemsahau fauziat aboud,suzan mongi,masoud masoud,charles hiraly,chris lugoe,marehemu kiza kahama...ongezea

  ReplyDelete
 26. Dina mie kati ya wote hawa Amina Mollel ni miongoni mwa watangazaji walionivutia sana kuingia katika kazi hii. Nakumbuka mwanzoni kabisa mwa 2000 alikuwa akifanya kipindi cha Salaam Club na Misanya Bingi hakika nilikuwa sikosi kipindi hiki. Baadae nikawa navutiwa sana na Nani Zaidi yeye na Abubakar Sadiki. Nikaendelea kumfuatilia katika kipindi cha Chombeza we sauti yake hakika dada huyu kajaaliwa. Amefanya sana pia Wakati wa Maakuli na kipindi cha Miwani ya Maisha kweli alikuwa anaelimisha jamii.

  Baadae nikamsikia na kumuona TBC akifanya kipindi cha Shajara, nakumbuka kipindi cha yule dada wa Makete mpaka Rais akatoa msaada wa BAJAJ na alimwambia pia amtafute, Je Amina Ulishamuona Rais KIkwete? Sasa hivi namuona pia akisoma habari na sauti yake kamwe haijabadilika hongera sana dadangu kwani wewe ni miongoni mwa watu waliochangia mie kuingia katika hii fani. Nakupenda sana na mungu akupe maisha marefu.
  Dina asante sana jua hata wewe wapo unaowavutia. Msalimie sana Amina Mollel, nampenda sana.

  ReplyDelete
 27. nilisahau mtangazaji wa ITV taarifa ya habari aliitwa Laura George jamani alikuwa ananivutia enzi hizo niko Secondary

  Itika

  ReplyDelete
 28. Mimi nilikuwa nampenda sana Susan Mungi.

  ReplyDelete
 29. Blandina Mughezi yupo Barick Gold Mine ni Community R'ship manager, baada ya kutoka British Council.
  Hakuna anayemfikia kwa sauti ijapokuwa si maarufu sana Mohamed Kisengo wa Redio One.
  Mliokula chunvi kidogo, mwamkumbuka MALIMA NDELEMA na HALIMA MCHUKA enzi za Radio Tanzania
  ?

  ReplyDelete
 30. Kuna mtangazaji mmoja alikua ananikosha sana ingawa hakukaa kwa muda mrefu kwenye utangazaji. nakumbuka jina lake la kwanza alikua anaitwa Terence sijui yuko wapi siku hizi.

  ReplyDelete
 31. asante sana dada dina,nilimpenda sana misanya bingi saaaaaana itv enzi hizo kipindi chake kikifika cha muziki itv tunakaa chini sebuleni watoto hadi wa majirani tunaanza kuangalia.umetisha sanaaaaaaaaaa

  ReplyDelete
 32. UMEMSAHAU LADY JAY DEE NAE ALIKUWA ANATANGAZA MID MORNING JAM NADHANI HAPO CLOUDS FM KABLA HAKIJABADILIKA JINA KUWA LEO TENA.

  RADIO ONE NILIMPENDA SANA AUNT NDINA, BLANDINA MUNGEZI.

  RUKIA MTINGWA ALIEKO VODACOM SASA HIVI NAKUMBUKA NI ZAO LA ITV & RADIO ONE LILE.

  DOSCA.

  ReplyDelete
 33. Ijapokuwa miaka minne imepita tangu Amina Chifupa atutoke, kila nikimkumbuka nasikitika sana. God will punish those drug dealers who poisoned (arsenic poisoning???) her. RIP Amina.

  ReplyDelete
 34. Dina nimekukubali. Naomba uongeze list ambayo wasomaji wameiongeza na pia ukizingatia zaidi list ya watangazaji wale wa RTD enzi hizo ambayo ndiyo ilikuwa radio pekee nchini na kila mtu ilikuwa ni lazima uisikilize hiyo kuanzia taarifa ya habari na zile ngoma za mzeee moris nyunyusa, kile kipindi cha misakato kila jumamosi, chechei shangazi etc. Pia naomba kila mwisho wa kila mtangazaji utuambie kwamba yuko wapi kwa sasa

  Thanks. Jana nilikuona ukiwa DJ Dimond kwa MWASHA. Big up sana

  ReplyDelete
 35. kwa upande wa lugha na utangazaji hilo kwako halina mjadala uko juu ya zaidi. napenda timu yenu nzima wote mna control nzuri ya lugha ni aghalabu sana kwenye kipinidi chenu ikatokea mmechanganya lugha I mean swanglish. kazi nzuri. nikisema control ya lugha pale mnapoweza kuwa na matamshi sahihi ya kiswahili pasipo kuchanganya R na L. Dina kuna watangazaji wa baadhi ya vipindi vyenu kweli inasikitisha watu kama hawa wanapita vp kwenye usaili wa utangazaji wakati lugha hawaijui.Baba yangu aliwahi kuwa katika nyanja ya utangazaji lkn ni zamani sana wakati wa RDT na kina Suleiman Hega, Issa Mkamba ni 70s aliwahi kuniambia ukiwa na Kithe (th - S) au ukishindwa kutamka R na L basi hata kama ni mzuri vp kazi hupati lkn kwa sasa inasikitsiha badala ya kukuza naona ndio kwanza tunaharibu. katika list yote uliiweka naikubali kutokana na hayo yote niliyosema hapo juu. watoe walikuwa na sauti kujiamini na ufahamu wa lugha mpaka kweli mtu unavutika kusikiliza either ni habari au hata matukio tu.

  ReplyDelete
 36. Misanya Bingi kipindi chake kilikuwa kinaitwa Kwanja time kila alhamisi.. mzee wa kuslash yani enzi hizi kuna nyimbo yani zilikuwa neva miss kama Aaliyah ~Are you that somebody, Ginuwine ~ Same ol G, Donnel Jones ~ Shorty got her eyes on Me.. jamani i miss those days mimi nilikuwa nikitoka shule najua kabisa list nzima ya nyimbo zitakazopigwa.. Amina Mollel alikuwa pia kwenye Miwani ya Maisha kila jumamosi saa 4 kamili hadi 5 asubuhi..Jamoni mmemsahau Eddy Sultan, Tumaini Meshack, Fauziat Abood, Marion Elias alikuwa mamaa wa ratiba ITV na wengine wengiiii we appreciate your good work and miss you saanaa

  ReplyDelete
 37. Dina mwanzo mwisho umwnikumbusha nilipokuwa napenda kusikiliza power breakfast (Masud + Fina + hando) ilikuwa burudani sana maana wote wnajua siasa mambo ya kitaa nilikuwa nnawapenda sana

  ReplyDelete
 38. Ahaaaaaaaa Dina, kuna mtu alikuwa anaitwa Maiko Katembo (RIP) kipindi cha "Ngoma Zetu" Radio Tanzania utake usitake utapenda kusikiliza kwanza nahisi alikuwa studio yuko bwi utacheka ajabu

  ReplyDelete
  Replies
  1. nakumbuka nilikuwa bado mdogo sana hicho kipindi cha ngoma zetu na Maiko Katembo nilikuwa nakicklza sana kama sanne hv asb..lol kumbe alishafariki jaman RIP....
   akianza ku play wimbo anasema haya njoon sasa aaaaahhh rudirudirudi msiwe na haraka bac me nikawa najua n live lol nilivyokuwa ndo nikajua n recorded nyimbo

   Delete
 39. FINA MANGO AND MASOUD KIPANYA jamani kama kuna uwezekano wa hao ndugu kurudi kwa radio moyo wangu utasuuzika. DINA NAKUKUBALI HILO HALINA MJADALA

  ReplyDelete
 40. Mie sio msemaji wa dina ila nachukizwa na watu wanaopenda kumkosoa kwa sababu zao binafsi... Yeyey katoa listi yake kama wewe unaona haifai then suite ur self. Si lazima kukubaliana na mawazo yake...

  Na wewe uliyesema dina anaonekana mzee, huna haya then chini unaandika samahani kama nimekuudhi, tuwe tunaangalia jinsi ya kupresent comment zenu, yeye ni binadamu hamaanishi haumii ila ni kuvumia ili aweze kudeal na despicable creature like nyie mlio na negative view..

  Back to the point, I like the list coz hata mimi kipindi hicho nilikuwa nasoma.. Gud one dina.

  ReplyDelete
 41. ki2 suzan mungi ni noma,kuna tmy alaizna kutangaza kipindi cha ua letu tbc ,akatuletea wamama waukweli kama kina dr.asha -rose migiro , prof.anna tibaijuka, then akapotea tena,love her sana

  ReplyDelete
 42. Enzi zetu nilikuwa nawafahamu watangazaji wote wa RTD kwa majina na kipindi wanachotangaza lakini kwa sasa hata siwezi kufahamu maana sasa zimekuja tv na radio binafsi kibao hivyo inabidi uwe too selective kupata tu kile unachopenda. So kwa sasa mimi vipindi vyangu ni Power breakfast, taarifa za habari na za michezo, kutoka magazetini, zilipendwa/enzi hizo ya Radio One IJUMAA na RFA ALhamis usiku. Nasikitika Dina kipindi chako cha Leo tena siyo miongoni mwa ninavyovipenda na sababu kubwa ni kwamba muda ambao kinakuwa hewani mimi kwa nature ya kazi yangu siwezi kukifuatilia. Najua wengi wana tatizo kama langu. Kuna mdau hapo juu ameomba uandike waliko hao watangazaji kwa sasa tafadhali na mimi naomba uzingatie hilo ni muhimu sana. Na picha za Diamond jana tunazisubiri. Nilipewa story zake jana mlitisha

  ReplyDelete
 43. dah umenikumbusha mbali na hao watangazaji wa zamani na wengine wakiwemo bado ktk gemu wengine hawapo ila wapo wengi sana ila mi nakumbuka nilikuwa nikivutiwa na Joyce Mhaville na kile kipindi cha KULIKONIII,amina chifupa ktk Leo Tena wapo wengi sana ila good list.

  ReplyDelete
 44. ahmed jongo akitangaza mpira wa simba na yanga hakuna mwingine hapo

  ReplyDelete
 45. Masoud Masoud na marehemu Moses Justin na ka kipindi chake cha MTAA WA MANGOMA

  ReplyDelete
 46. Wasoma Taarifa habari;Ahmed Kipozi,David Wakati, Florian Kazia, Jacob Tesha na Godwin Gondwe(wababa). Eda sanga,Christine Chokunogela, Suzan Mungi, Faudhia(Wamama). watangaza mpira; Ahmed Jongo, Omary Jongo, Charles Hilary, Sekioni Kitojo,CHILAMBO DOMINICK alikuwa anatangaza kipande cha CCM Kirumba wakati huo Pamba aka "TUPWISA LINDANDA KAWEKAMO" ya Mwanza inatisha, Utamsikia Geooorge masatu, Geoooorge Masatu anapiga pale kwa Daviiid Mwakalebela..Duuuh ilikuwa tamu hiyo!! Mdada Halima Mchuka anawakilisha wamama watangaza mpira.Vipindi vya burudani kuna MAIKO KATEMBO-ngoma za asili,MOSES JUSTINE(Papaa Mo), JULIUS NYWAISANGA(Club Raha Leo Show).......Mwingine ni Regina Molekwa dada huyu nampenda sana maana yeye anatumia sauti yake ya asili siyo kubana pua. List yangu ni ndefu saaaana ila naomba niishie hapa.

  Cheers,
  Elmmy

  ReplyDelete
 47. nimeangalia vizuri sana hiyo listi yako ya Watangazaji kiukweli nimeipenda na inaonyesha Itv/redio one wapo juu kiukweli kwasababu asilimia kubwa wametoka huko hata ukiangalia asilimia kubwa ya watangazaji wa bbc wametokea huko,Dina nyie Cloud's hakuna watangazaji kuna madj na ma mc tu,hadi sasa redio one na Itv bado wanawatu wazuri,kwamfano Maulid Kitenge,Abdallah Mwaipaya na wengi tu ambao bado hata majina siwahui nafikiri ni wageni ila wanakuja vizur

  ReplyDelete
 48. jamani Dina tuwekee picha ya Marehemu Amina Mongi

  ReplyDelete
 49. List iliyobamba ni ya Anonymous October 31, 2011 7:54 AM - Bila kumsahau BEN KIKO na Mikidadi Mahomud

  ReplyDelete
 50. how about abdul ngalawa, s.s mkamba, mzee wa kijaruba abdala mlawa, abisay steven, ahmed and sango kipozi, salim mbonde, tido mhando, swedi mwinyi, shaban kissu, evelyne mpasha, halima kihemba, just to mention a few. wote wa RTD

  ReplyDelete
 51. hivi mnamkumbuka mama katunzi wa radio tumaini? wapi regina nazael, sebastian maganga, rose msoka, martin kuhanga, father franswaa wa Radio Tumaini? ama kweli tumetoka mbali.

  ReplyDelete
 52. anon 8:27 amenena ukwel,itv/radio one na tbc/rtd ndo wanawatangazaji tena wa ukwel(proffessionals),clouds na kwingineko 99.9% ni mamc na mdj,nendeni skul bana ili mpate madil ya mbele ka wenzenu,check flora nducha, charles hillary,suzan mungi na wengine kibao

  ReplyDelete
 53. Nimeipenda sana hii Dina. Binafsi nilikuwa nafurahishwa sana na Marion Elias na Laura George plse ikiwezekana weka picha zao na walipo sasa. Walikuwa warembo na wali imudu vizuri kazi yao.

  Bila kusahau enzi za Fina, Masoud na Gerald. Power Breakfast ilikuwa tamu sana enzi hio. Vijana wali jua Siasa vizuri,mambo ya dunia mpaka ya mitaani. I wish history ijirudie one day.

  ReplyDelete
 54. Mimi katika wasoma Habariwa kike wa ITV ukiwatoa magwiji Suzane Mungi,Laura George,Betty Mkwasa nilikuwa nampenda sana Janet Mwenda Talawa,alikuwa akisoma Habari siondoki hadi amalize. Siku hizi yuko wapi?hebu nitafutie Dina maana alikuwa ananikosha sana na mbwembwe zake

  ReplyDelete
 55. mbona dina umesahau sued mwinyi? huyu bwana ni kiboko kwa matangazo ya mpira, salum mbonde vipi,na pia yule kijana tangu enzi za R.F.A isaac muyenjwa gamba hadi sasa ITV REDIO ONE. ILA KWASASA NAVUTIWA SANA NA UPCOMING REDIO PRESENTERS RADIO ONE KAMA VILE FARIHIA MIDDLE, NASIKIA KATOKEA HUKO arusha, kwa kweli anasoama habari vizuri saa huyu bibie. alafu kwa taarifa FLORA NDUCHA HAKUWAHI KUTANGAZAI KATIKA itv, ila alisoma habari redio one, hapo umechemka bibie kuwa makini usikuprupuke.

  ReplyDelete
 56. yani me toka Masud kipanya na Fina Mango waondoke Clouds sijasikiliza tena power-breakfast hata nikisema nisikilize ile radha siipati tena, kwa kweli i wish i culd turn back the time ili niwasikie tena fina na kipanya. Nakumbuka hata kile kipindi cha watoto cha kaka bonda, Masoud na Amina, aisee nilikuwa sikosi jumamosi. Hata jahazi nalo halininogei tena kama ilivyokuwa kipindi cha G. Habashi, yani ilikuwa ikifika saa 10 me headphone za simu masikioni kumsikiliza kibonde na Kapten ila sikuhizi labda niwe nyumbani hivi hivi wala hamu ya kusikiliza sina. Masoud Kipanya, Fina Mango na Kaptain G. Habashi ni unreplaceble. Cjui kwanini vitu vizuri huwa havidumu popote pale. Atleast wewe na Gea mmeweza kum replace Amina Chifupa (R.I.P)

  ReplyDelete
 57. Katika list nawakubali Bujaga Izengo Kadago, Emma Chris na Masoud Masoud.

  ReplyDelete
 58. Nawalililia Fina, Masoud na Gerald. I loved u guys...

  ReplyDelete
 59. Hiyo picha ya Misana Bingi nadhani umekosea sie kabisaaaaaaaa!!!!!!

  ReplyDelete
 60. Kiukwel hata mimi nina mashaka na iyo picha ya Misanya,haiwezekane achoke ivo mana jamaa ni mtu wakujipenda pia ni msomi kwa sasa.hv uongozi wa CLOUDS una mpango wowote wa kuwarudisha watu kama Masoud,Fina??kiukwel walituteka kinoma tofaut na sasa

  ReplyDelete
 61. yaani natamani sana kina masoud na fina mango warudi jamani dah...... dina umemsahau Misanya bingi.

  ReplyDelete
 62. umemsahau kutoka MARA NI Emmanuel Chacha wa ITV

  ReplyDelete
 63. LAZIMA TUKUMBUKE ENZI YA RTD AKINA ALOYCE NGOSWE,HERRY MBOTO NA JACOB TESHA HUYU TESHA AKUSOMEE HABARI TENA YA KIZUNGU NA SAUTI YAKE NZITO ENZI YA EXTENAL SERVICE HAO NDIO WALIKUWA VIOO VYA WATANGAZAJI BONGO HIYO CO LEO WENGI MASHAUZI TU - Mdau wa bongo

  ReplyDelete
 64. jamani mi umemsahau IRENE MALONGA alikuwa akisoma taarifa ya habari ITV,yuko wapi now days?

  ReplyDelete
 65. Mie Susan Mungy na Fauziat Aboud habari ITV, ila katika vitu clouds mlivinisikitisha ni kuwatoa Fina na Masoud ktk power breakfast... the program is no longer the same!! yaani Masoud amejaaliwa utangazaji hata wakati wa chuchu yeye + Amina "R.I.P"+ kaka Bonda yaani na utu uzima muda ukifika wa chuchu nilikua nogombania redio na watoto.

  ReplyDelete
 66. amesahaulika Abdahla Majura

  ReplyDelete
 67. Sasa Nyie wote mmemsahau mama debora mwenda na hadithi zake za mama na mwanaMnamkumbuka binti Chuuura pia mnakumbuka Mama Mpenzi wa Nyangumi?

  ReplyDelete
 68. yani umenikumbusha mi nadhani nlikuwa nawpenda watangazaji wote jamani kuna suzan mungi,amina mongi R.I.P julius nyaisanga,othmani njaid,john ngahyoma,masoud masoud,ahmedi kipozi, abuu bakari liongo,salim kikeke,joyce muhavile, wow hadi raha they use to be my fav and i can,t forget them. i wish nijue walipo na wanafanya nini ambao sijui habari zao lol.

  ReplyDelete
 69. Jamani mimi namkumbuka Asma Basafar wa kipindi cha Afya ya Jamii.

  ReplyDelete
 70. dina chemshabongo ilikuwa majura bwana, amina mollel alikuwa akifanya kipindi cha chaguo la msikilizaji jumapili mchana, salamu na unasemaje pamoja na misanya, rose chitala salamu pamoja na master voice mbona umemsahau weye aka dulla au abdallah hussein, janeth sosthenes mwenda talawa habari, kwa kweli sauti yake inakosha sana na ilikuwa ya kubembeleza

  ReplyDelete
 71. frola nducha akuwai kutangaza itv bali alikuwa akitangaza redio one..............usiseme kwa kuwa ni kitu kimoja...... hupo hapo............

  ReplyDelete
 72. yani dina umenikumbusha mbali nilivyokuwa nakimbia kutoka kanisani ili niwahi kipindi cha mama na mwana

  ReplyDelete
 73. sister girl u surely did ur homework because remembering that list its good as for john delinga in 104.4 he rocked as well as when he came with his tapes of latest tracks hapo ndo balaaaa kuliko kukabwa na mwiba wa samaki also as for misanya bingi alikuwa inategemea ila j4 kipindi cha miziki ya kufokafoka kinaitwa rap em na alhamis kipindi cha miziki flava kibao kwanja tym ila umenipa raha kamanimeambiwa nimeshindaaa kwenda kuwa na mahojiano na steve spielberg kazi njema

  ReplyDelete
 74. Nakumbuka sana kuhusu Fina Mango.Natamani hata leo arudi Clouds.Naomba umualike kwenye kipindi chako cha Leo Tena,nimsikie,natamani kujua mengi kuhusu yeye,anafanya nini kwa sasa na vingine vingi.Please dada Dina.

  ReplyDelete
 75. This is amazing Dina, imagine one day this will be a good history, na thru hawa watangazaji ndio tunapata Wakuwa Wilaya, and who knows one day Dina nitakukuta ukiwa juuuu!!!. Lakini itakuwaje Leo Tena bila Dina? ???. Keep it up sister!.

  ReplyDelete
 76. mimi nauliza misanya bingi kwa sasa yuko station gani

  ReplyDelete