Tuesday, November 29, 2011

NILIPOSEMA SKU YA BDY YANGU NTAJIPA ZAWADI NILIMAANISHA..................

Katika maisha yangu mimi sikuwahi kudhani kama kuna siku ningekuja kunenepa.Nilikuwa mwembamba sana tena nahisi picha hii wakati inapigwa nilikuwa nimenenepa kidogo.Nilikuwa naomba kila siku angalau na mimi ninenepe jamani khaaa!kwani nimemkosea nini Mungu aninyime nyama za mwili.Shule walikuwa wananiita msomali,mnyarwanda,chikonda,tall basi taabu tupu! Lakini muda ulivyozidi kwenda nikaanza kunenepa.Basi nikafurahi kweli angalau na mimi sasa naanza kupata vinyama.Hizo soap dish nilikuwa sizipendi nilikuwa nataka ninenepe zipotee kabisa.
Mwili ukaendelea kuja tu mie sina wasiwasi kabisa tena nikiambiwa unanenepa nafurahiiiiiiiiiii mmmh acha tu!
Sina wasi wasi kabisa maana nilikuwa sijui mwili wangu unaweza kunenepa kwa kiwango gani!


Mashavu yakawa mashavu sasa ilipofika mwaka 2009 ilikuwa balaa.Ila mwaka 2009 sio katika hii picha..muda ulivyozidi kwenda nikaanza kupata stress za kupungua.Mwaka 2009 mpaka 2010 nilipata tabu sana mwili wangu nikawa siupendi tena.Nilijaribu kila aina ya kitu nilichoambiwa kinaweza kupunguza mwili lakini sikufanikiwa.


Ikafika wakati shingo hata haionekani hahahahahahahahh balaaa.Kila nguo ninayovaa hainipendezi wala haikai vizuri stress ndio usiseme kipindi hiki tayari nimeshakuwa na blog ukija huku kila mtu anasema la kwake kuhusu muonekano wa mwili wangu(unene).Wapo wanaokushauri kwa mapenzi upungue wapo wanaokuja kukutukana na kukukashifu kwa kukuita majina ya ajabu ajabu.Bado ndugu jamaa na marafiki hawajakwambia pungua wewee shauri yako.Kiukweli nikipindi ambacho nimepitia mengi sana ambayo siwezi kuyasema maana wakati mwingine nikifikiria naweza kulia kwa uchungu!

Nilichokuja kugundua ni kwamba ukitaka kufanya mabadiliko yoyote katika maisha yako kama upo kwenye stress HUWEZI.Jambo lolote lile ili ufanikishe lazima ulifanye kwa mapenzi na uwe umeamua kutoka moyoni mwako.Hivyo basi mwaka huu mwezi wa 8 niliamua tu siku moja kwamba nipo tayari sasa kupunguza mwili wangu.Siku hiyo nilikuwa nimeshika diary yangu ya mwaka 2009 nikaona mwezi wa 8 mwaka huo nilidhamiria kupunguza mwili lakini sikufanikiwa kwa nini isiwe sasa?Ndipo dhamira ikaniingia ya kufanya hivyo.Nilipima uzito nilikuwa na kg 96 balaaaa lakini sikuogopa maana najijua mwenyewe nikiamua kufanya jambo kwa nia inakuwaje.

Unajua ni sawa na mtu ambae anavuta sigara anaweza kujiambia kila siku kuwa ntaacha kuvuta lakini asiache.Ndugu,jamaa,marafiki wote mkamwambia aache kuvuta ina madhara kwa afya yake na asiache.Sio kwamba hawasikilizi bali hajaamua na inakuwa kama miluzi mingi hivi ambayo mwisho wa siku humpoteza mbwa.Lakini ipo siku tu anaweza kuamka asitake hata kusikia harufu ya sigara akaacha.Wapo watu walioacha kwa style hiyo na wana miaka sasa hawajagusa sigara.


Sasa basi nilichofanya mwezi huo wa 8 nilimtafutata dada mmoja anauza SHAKE OFF ni dawa ya kupunguza uzito ambayo unakunywa inakuwa kama chakula unakunywa mara 5 kwa siku ina virutubisho vyote unavyovitaka.Nikaitumia kwa mwezi mzima nikaja kupima nikawa na kg 92.

Mwezi wa tisa nikaanza mazoezi pale THT na wale dancers kila siku jioni naenda pale nafanya aerobics na kucheza kwa muda wa lisaa limoja mpaka lisaa limoja na nusu.Mwezi ulipoisha nikapima nikakuta nina kilo 90 kamili.Sio mazoezi tu najitahidi kuangalia ninachokula niliacha kunywa soda zamani sana japo kuna wakati naweza kunywa kwa hamu.Nakunywa maji sana,chips niliacha kula japo kuna siku naweza kula ile ya hamu,ugali nina miezi minne sijaula.Mimi ni mwendo wa kuku choma au kuchemsha na samaki choma au kuchemsha...mbogamboga,matunda ndio mpango mzima nikienda ofisini nabeba.

Nina miezi miwili sijapima uzito kujua kwa sasa nina kgs ngapi ila nimepungua sana tu.Wakati mwingine naweza kupiga picha nikaiweka hapa ukahisi sijapungua ila inakuwa ni picha tu ukiniona ana kwa ana ndio utabaini.Kubwa ambalo bado ni tumbo na mikono ila maeneo mengine yanapungua.Sina haraka ya kutaka kujua nina kgs ngapi kwa sasa.Ikifika mwisho wa mwezi wa 12 Mungu akijaalia ndio nitapima tena.

Hivyo basi niliposema ninajipa mwenyewe zawadi itakapo fika siku yangu ya kuzaliwa nilimaanisha hili.Zamani nilikuwa naenda gym leo kesho najiangalia kwenye kioo najiona sijapungua na mazoezi naacha maana nataka matokeo hapo kwa hapo.Leo hii ninapoandika hapa nina miezi miwili naenda kufanya mazoezi nisipoenda naona kuna kitu kinakosekana.Nimeweka malengo ifikapo mwezi wa pili mwakani nitakuwa na tumbo flat kabisa nina amini hilo kwani hakuna linaloshindikana palipo nia.Sasa najua mwili wangu ni wa unene hivyo nimejifunza nini cha kufanya na ndio ninachofanya sasa.Wala sijutii chochote bali ni mambo ya kawaida tu kwenye maisha haya pengine imenisaidia kuwajua watu kwa rangi zao halisi.
MUHIMU

Mwili wa mwanadamu unaweza kubadilika muda wowote kuwa vyovyote.Kashfa na maneno mabaya kuyatoa kwa muonekano wa mwenzako sio vizuri wala Mungu hapendi.Pengine mimi nimenenepa tu na uwezo wa kupungua upo je wewe unajua kesho mwili wako utabadilika na kuwaje?utakuwa na uwezo wa kubadili chochote?Unapomtolea mwenzako maneno mabaya yeye atasema na moyo wake kwa sababu umemkwaza lakini wewe unaiweka nafsi yako katika nafasi gani?Angalia baadae usije kutafuta mchawi kumbe mchawi ni wewe na maneno yako pengine utakuwa umesahau ni wapi uliyatoa.


One love!

78 comments:

 1. GOOD DINA NDIO MAANA NAKUFEEL MDOGO WANGU

  ReplyDelete
 2. kweli hujafa hujaumbika

  ReplyDelete
 3. awesome Dina!THATS how life goes..waliosema what goes around comes around hawajakosea, BIG UP kachuna ketu!!!we love ya ooohoo.here from NIGER

  ReplyDelete
 4. Hongera Dina, mara nying watu wakiwa na matatizo yao wanatafuta pakuondolea stress zao ndio maana kucha kuchwa hawakosi kutoa maneno machafu na ya kashfa,wanajifurahisha tu na roho zao.. Mungu atakusaidia tu penye nia pana njia....mimi nilikua na 82kgs sasa hivi nina 64 kgs ukiamua kufanya jambo kwa nia hushindwi. God bless you.

  ReplyDelete
 5. MMMH KWELI DADA UPO SAHIHI KUSEMA SEMA MTU SIYO VIZURI CYO KAZI YETU JAMANI MUNGU NDO KAPENDA AWE HIVYO ALIVYO,PILI HATA MIMI NILIKUWA MWEMBAMBA HADI KERO JAMANI ILA SASAHIVI NIMENENEPA NENEPA SI HABA ILA NAJIZUIA KUWA BONGE LA MTU NA HUU UREFU NILIONAO NAWEZA KUWA JIMAMA SOON OR LATER ILA NASHUKURU NIMESTUKA MAPEMA KABLA YA MAMBO HAYAJAKUWA MABAYA.ALL N ALL USHAPUNGUA MBONA ILA ENDELEA TENA KUPUNGUA KILA KITU KINAWEZEKANA.ALL THE BEST MY DEAR.

  ReplyDelete
 6. Maneno yako mazuri n kwel m2 ukiamua kubadilika inawezekana pindi utakapoamua ss nataka kubadilika, jamani n vzr tunapomkosoa m2 tumkosoe kwa ustaarab km alivosema dina sio kumchamba kwa maneno mabaya, alaf dina me naomba ss hv anza kusuka yan kushonea maweaving km inawezekana lkn!!! me napenda ukishonea naona km unapendeza zaid tena style km ya hapo juu ulipovaa shirt white yenye mistar ya gold, pia endelea na gym na diet utapungua tu ila ucwe km zamani uwe mnene lkn c sn ikiwezekana ubaki km hapo ulipokuwa kwnye hyo shirt white.

  Joh...

  ReplyDelete
 7. hahahahah, yan dina hii kiboko, umetoka mbali aisee, jitahidi mwaya utapungua 2 ila usiwe km hyo picha ya kwanza, big up my dear!

  ReplyDelete
 8. kaza buti Dina, umepungua kweli umependeza. Nasubiri huo mwezi wa pili mwakani panapo uzima.

  ReplyDelete
 9. KWELI MAMY UMEPUNGUA HONGERA SN PIA MIMI NILIKUWA NA KL 92 NIKATUMIA SHAKE OFF POWER SLIMMING NIKAPUNGUA KL 5 NIKAWA NA KL 87,WATU WANASEMA NIMEPUNGUA ILA BADO MIKONO NA TUMBO NDIO ISSUE, NIMEJIWEKEA TIME TABLE YNG ASBH NAKUNYWA CHAI MCHANA LUNCH ILA USK CLI NAKUNYWA MAJI MOTO NALALA.

  ReplyDelete
 10. umeongea dina,kweli kuna watu huwa wanaongea maneno makali kweli hawajui wanamkwaza mtu kiasi gani.

  ReplyDelete
 11. dina usipungue sana bana cheza kweny 65-70 wembamba sana nao sio mzuri ndio ulee ulioukataa.

  ReplyDelete
 12. yap ma dia sister umepungua naona ata shingo sasa hivi inaonekana!ongeza mzaoezi zaidi unene mbaya sana.

  ReplyDelete
 13. I admire u..............

  ReplyDelete
 14. well done dina pungua mpka utakapoona hapa basi ndo uache jiangalie mwenyewe , nunu a mizani weka kaibu na bafu lako uwe unajipima mara kwa mara kumaintain ile standard unayotaka, inayobaki ni kuwa mwangalifu kwa kila kitu unachokula ili usirudi ulipotoka , nimejifunza jambo dina ,all the best

  ReplyDelete
 15. Safi saaaana ndugu yangu ila sasa upungue koooote lkn sio kalio hilo!! uzuri wa nyumba ni choo ndugu yangu, punguza tu kwingine lkn makalio jitahidi uyaongeze na package pia iwe bombaaaa ili uvutie zaidi kama JLO!!!!

  ReplyDelete
 16. Hongera sana...twajifunza toka kwako ILA kwenye msosi, unavyokula...tutaweza kweli na laki mbili kwa mwezi kama kipato? All in all, all the best sister.

  ReplyDelete
 17. MWAYA MI PIA MKONO NA TUMBO SHOGA VINANIUIZA KWELI MANA NAJITAIDI ILA KILA NIKITZAMAMA MKONO NA TUMBO NAKASIRIKA YANI SIPENDI TENA KUVAA KATA MIKONO NAONA KM SIPENDEZI.  SEHEMU NYINGINE ZOTE ZA MWILI ZIKO POA ZIMEPUNGUA VILE NINAVOTAKA MPK RAHA ILA MANEO HAYO NLOTAJA MWANAWANE KAZI NINAYO

  ReplyDelete
 18. Kila la heri,kaza buti

  ReplyDelete
 19. maneno yako yamenigusa.mimi zamani nilikuwa mwembambaaaaa,nikaitwa vya kuitwa.na comment za watu zinakufanya ujisike vibaya,ingawa utajifanya unacheka,lakini moyoni unaumia.hayo mashimo ya kwenye shingo,yalikuwa makubwa hayo,mpaka nikawa sina hata raha.kwa sasa nimekuwa mnene sana,nataka nirudi kama vile lakini wapi.nimegundua kila ninachovaa sipendezi kabisa,nabaki kuangalia picha zangu tu,nilivyokuwa mwembamba.ila nitajaribu hizo diet kwani kwa sasa kila ninaekutana na watu,hee umekuwa mnene hivyo.naamini saa nyengine,binaadamu ndio tunarudishana nyuma.ila ukiona mwenzio anavaa nguo inamkaa vizuri,lakini ukijiangalia wewe unakaa kichekesho.na mimi nitaanza mazoezi rasmi,kwani sio mlaji wa hivyo

  ReplyDelete
 20. Dinah mambo?yaah umepungua my dear na unajua wewe ni mzuri sana,sory naomba unielekeze ni wapi naweza kupata iyo shake off plz nijibu mumie mana nami nahitaji nitumie,plz naomba uniambie na bei ili siku nikienda niende moja kwa moja.love youu my sisy.

  ReplyDelete
 21. DINA HIYO PICHA JUU ULIYOKAA UKIWA UMEVAA SURUALI YA JEANS NA BODY SUIT NYEUSI NA WEKUNDU YAANI ULIKUWA NA UMBO ZURI SANA. HIVYO JITAHIDI UWE KAMA ULIVYOKUWA KATIKA HIYO PICHA. ULIKUWA BOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOMBA ILE MBAYA.

  ReplyDelete
 22. YES U CAN!I ONCE HAD 68KG AND NOW I HAVE 48KG.KiLa kitu malengo dadaangu...GOOOO

  ReplyDelete
 23. Dina wewe ni mzuri sina cha zaidi
  James

  ReplyDelete
 24. me penda iyo pic ya kwanza kabsa mna ulikuwa kma dada angu nae anaomba kuongezeka leo kesho sema wapi ila ipo siku tu kma ulivyosema....ila kweli kila kitu malendo tu mamy,pia nachukizwa sana na tabia za watu kukashifu wenzao ila ndo wanadamu hao wamezaliwa kusema thn siku ya siku wanabaki midomo wazi...yani dada ebu sema iyo SHAKE OFF yapatikana wapi na bei gn mna hapa wengne vitumbo na mikono balaha...big up dada kaza buti maneno ya watu wala yasikuumize kichwa cos hawajui walitendalo

  ReplyDelete
 25. dina dear nimefurahi kusikia umeamua kupungua huwa naingia kwenye blog yako bila kucomments lakini leo nimeona nicomment mimi nina watoto wawili 4 na 2 kama unavyojua ukizaa mwili unaongezeke sana nilianza mazoezi mwezi wa 8 tarehe 1 nimepungua sana nashukuru mungu kuhusu tumbo na mikono fanya situps nyingi kila siku hata ukuwa nyumbani ila usiwe umekula nzuri ni asubuhi ukiweza kwa nusu saa.na ruka kamba kwa dk 15 au zaidi.mikono inabidi uwe unabeba vyuma ambavyo vina kilo 15 au 20 kila upande vinakata nyama na kutone mikono ukiweza kuwa navyo nyumbani pia ni poa vitakusaidia sana pia kama unaweza kukimbia mala 3 kwa week saa moja kwa kila utakapokimbia ni nzuri utapungua haraka zaidi.nakutakia kila heri mungu atakusaidia tu.ila nakushauri upunguze kula nyama esp nyama ya ngombe kama unataka kupungua tumbo uwe unakunywa soup yake tu bila nyama zenyewe.mdau wa houston

  ReplyDelete
 26. love the second pic, you were so beautiful dia..! yawezekana ukapungua kikubwa nia tu, kitu ambacho kinanivutia sana kwako ni rangi, una rangi nzuri sana p'se usije kuiharibu

  ReplyDelete
 27. Love the second pic u're so beautiful Dina..utapungua kikubwa ni nia tu. Napenda sana rangi yako p'se usije ukaiharibu

  ReplyDelete
 28. Nimependa ushauri wako na nimesoma mwanzo mpaka mwisho. Sitaki kukukatisha tamaa Dina, ila mimi nilikuwa miss mpaka nilipoolewa ndo nikaanza kunenepa. Nilipojifungua mwili huo. Sasa hivi nina two kids nimeanza zoezi la kujipunguza. Kwa kuwa wewe bado hujawa na watoto, bado una safari ndefu, unaweza nenepa tena baada ya kuzaa.

  Mimi kwa sasa kwa kuwa nshamaliza kuzaa najua ntaweza ku maintain uzito niutakao.

  Kweli hupaswi kuwa na stress. Mimi nilinunua mzani kabisa; lakini nikaja gundua ndio ulikuwa unanidescourage kabisaaa. Kila nkipima kilo ziko pale pale.

  Utafanikiwa kama ukifanya nazoezi kwa funny. Again ni vizuri umeacha kunywa soda. Hata mimi sasa hivi ni mwendo wa maji glass nane kwa siku. Maji yanasaidia kupunguza njaa hivyo mtu unakuwa unakula kidogo.

  Yani nina juice ya box kweny friji kila nikisema ninywe, sijisikii kwani sina kiu sababu ya maji. Maji ni mazuri ukiweza kunywa ya vugu vugu kwani yanasaidia kuchoma mafuta.

  ReplyDelete
 29. Bora ulivyostuka ukapungua kilo 96 una bahati sana mimi nilifika 84 nikaanza kuburuza mguu wa kulia na kwi kwi kila wakti kumbe moyo ulianza kuleta shida, nilipoenda hospital kupigwa x ray kumbe uzito ute wa mfupa na mfupa umekauka kwa hiyo nikitembea mfupa kwa mfupa unasuguana, nilipigwa diety mpka nilikoma, jitahidi utazoea japo mimi nashindwa ugali huwa nautamani sana sana na mara moja moja nakula ila nimejitahidi mno mno na nimepungua sana sana sana, hongera usijihurumie tu na kushinda tamaa ya kula kula ovyo basi umeshinda, Hivi nikitaka kukuona nafanyeje shonga nina shida na wewe dada yangu

  ReplyDelete
 30. umeongea point kabisaaa,dada yangu kaza buti najua utafika unapo pataka, we mzuri na hiyo sura ya kinyalwanda sipati picha ufikia mwezi wa pili uko,utapendezaje? na ukiweka blazilian hair uwiii utakuwa kama msombe flani yaani utapendeza sana.mungu atakusaidia utakamilisha mabo yako.

  ReplyDelete
 31. Dina aerobics haiwezi kukufanya upungue! Hayo sio mazoezi ni anasa! Ili mtu apungue anahitaji aupe shida, karaha, dhahama kubwa mwili wake. Huwezi kusema utapungua kwa eti kucheza cheza muziki, hiyo ni starehe! Ukitaka kuthibitisha kwamba hujapungua angalia ile picha aliyokukumbatia Gerlad Hando. Angalia mkono wake ulivyoshindwa kukizunguka kiuno chako!

  Halafu hakuna dawa ya kumfanya mtu apungue! Watakutapeli kwa kukuuzia madawa feki. Ushauri wangu kwako ni kufanya mazoezi ya nguvu. Uwe unakimbia asubuhi (kwa kuanzia) si chini ya kilometa tano. Ukija kuwa fiti baadae unaongeza taratibu hadi kufikia kilometa kumi na zaidi. Ukifanya hivyo kwa muda wa wiki moja tu utakuwa umepungua sana! Amini nakwambia! Lakini ukisema ucheze muziki kama unavyofanya sasa, utacheza milele na kamwe hautapungua.

  ReplyDelete
 32. KUTOKA KUWA MWEMBAMBA HALAFU UKAWA MNENE WATU WANAKUELEWA NA WENGI HASA MARAFIKI ZAKO WATAKUWA WANAKUAMBIA MOJA KWA MOJA BILA MAFUMBO KWAMBA UMENENEPA. TAABU INAKUJA PALE UNAPOKUWA MNENE UNAONA UNAANZA KUWA MWEMBAMBA HATA WALE WA MWANZO WALIOKUWA WANAKUSIFIA SASA HIVI WATAKUWA WANASEMEA PEMBENI KWAMBA NI NGOMA NINI????? DINA HONGERA KWA HILO ZOEZI NI VIZURI UMELIWEKA WAZI KWAMBA UNAPUNGUA KUTOKANA NA JITIHADA ZAKO NA WALA SIYO KWA SABABU YA AFYA MGOGORO. MWISHO NAOMBA UJIBU MASWALI YETU TULIYOULIZA

  ReplyDelete
 33. Hongera Dina una busara sana MUNGU na akuzidishie zaidi na zaidi

  ReplyDelete
 34. Hongera sana my dear, mimi ni mnene mpaka boyfriend anachukia ananisema yaani nimejaribu sana kupungua ila sipungui, natamani kupata hiyo dawa, kama unaweza kuweka contacts za huyo mtu anayeuza nitashukuru kwakweli sina raha Dina
  Kila la kheri

  ReplyDelete
 35. Hongera mpenz me c mnene kivile ila nina 2mbo na mikono minene itabidi nikutafute unisaidie kwa hlo.

  ReplyDelete
 36. Nice ila zoezi likizidi noma mi napenda mwili kiac piga zoezi mdogo mdogo wangu na kilo c unene mifupa hata mwembamba kama mifupa mizito sana 2.But vip cjakuckia ya pili wk inakata cjickii whr u csta.

  ReplyDelete
 37. wadau naomba maelekezo ya jinsi ya kupunguza tumbo na mikono jamani.nimeipenda picha ulipiga na jinsi hapo juu ulikuwa mrembo.

  ReplyDelete
 38. Kweli wewe ni kioo cha jamii mastar wote wa Bongo wangekua kama wewe wangefika mbali sana....All the best Dina!!

  ReplyDelete
 39. yaani dina kwa maneno ya busara tu ndio ninachokupendea

  ReplyDelete
 40. Umependeza sana D, mi nakupenda tu haijalishi umbo liko vp, ila ni kweli ukuwa relaxed ni rahisi kufanya mabadiliko yoyote.

  Love ya...

  Mama FM - Arusha

  ReplyDelete
 41. Congratulations Dina!!!! You are so beautifull. I like you. take care

  ReplyDelete
 42. hi da dina...
  pole sana kwa kuomba unene,ila nahic watu walikuwa na wivu na wewe or something.. cos coni wembamba wako muonekano wako wa sasa hivi ndiyo worse m sorry.. ulikuwa unachukia soap dish why..? unajua kunawatu wanene na bado wanasoap dish? mimi mwembamba ila sina soap dish nivile ulivyoumbwa yani ulikuwa perfect i swear.., m 24yo ila ukiniona niko kama 15yo wananiita little girl.. napenda kunenepa nina 45kg ila i want to be 50kg only cos najua nikizaa nitaongezeka.
  pia dina jitahidi upungue kabla hujaturn 35yo cos metabolism wakati huo itakuwa slow.. so itakuwa vigumu sana wewe kupungua nikimaanisha kila utakachokuwa unakula wewe kitakuwa kunasagwa polepole sana so utakuwa unanenepa tuu tuu...
  dont stress it much cos mwili wako unaonekana ni mkubwa hata ulipokuwa skul..
  good luck..

  ReplyDelete
 43. waoh! picha ya pili kutoka juu ulikuwa msomali/mnyarwanda wa ukweli, so cute mumy, achana na binadamu ndivyo walivyo HATA KWETU WAPO..............
  LOVE UUUUUU

  ReplyDelete
 44. ulipokuwa mwembamba ulikuwa unapendeza sn

  ReplyDelete
 45. Pole bonge mwenzangu, hata mimi nimeshayapitia hayo yanayokukuta lakini usijali kwa yoyote yule alie kukwaza kwa maneno negative kuhusu mwili wako mshukuru kwa kuwa amekusaidia kwa kukwambia ukweli na ndo maana umeanza kufanyia kazi...so take it as an advise and keep working on it..as you can see umeshaanza kuona changes!

  ReplyDelete
 46. binadamu mnatabu mara umenenepa,maramwembamba hii yote tabu

  ReplyDelete
 47. whatever has been said to you take it as a challenge, ndio maana umekerwa na maneno hayo ukaamua kufanya ulivyofanya sometimes haters hutupa msukumo fulani kufikia malengo fulani, hivyo hata tunaowaita haters wanaposema jambo tujaribu kusikiliza na kuona je tunaweza kufanyia kazi iwe ni kashfa au matusi waliyoyasema??? maana lisemwalo lipo ingawa wakakti mwingine mtu anakuwa hana sababu kwa hilo tutaliacha lipite lkn kama lako la kupungua naona hayo manaeno ndio yaliyopelekea wewe kuchukua uamuzi huo kwani hata shuleni huwa tunachpwa ili tuelewe. ukizingatia wewe ni mdogo sana na mwili ni maradhi especially siku hizi kuna canser kibao nyingine eti zinasababishwa na chakula!!!! see sasa aliyekutukana kakusadia, Natamani unione halafu nikuulize umri wangu kweli utashangaa.

  ReplyDelete
 48. mi sioni km kuna tatizo, ukawa mnene kwa raha zako halafu ukajali kwa kuwa watu wanakusema. ah bwana mrelax tu.

  ReplyDelete
 49. Dina umenitisha na umenifundisha jambo kuhusu mambo ya mwili, mimi pia nilikuwa mwembamba sana mpaka nikawa najichukia maana nilikuwa naona sina mvuto wala sipendezi hata nikavaa nguo na watu nao kusema we nae mwembamba basi ikawa inanikera. Mwaka huu sasa mwanzoni ghafla mwili umeanza kuja ninavyofurahia hizo hips na tako, na watu wanavyonisifia mie bichwa ndo linazidi najiona mimi ndo mimi, ila kwa historia yako kwa kweli umeniogopesha, maana juzi kuna mdada kaniambia we toto anza diet unakoelekea siko na kweli hata me nimeshaanza kuona ninakoenda siko inabidi nianze kujilimit

  ReplyDelete
 50. kwa la tumbo na mikono kupungua weka email yako nitakupatia mbadala utakusaidia.

  ReplyDelete
 51. Nimependa saana picha ya 2..kisura wetu..unarangi nzuri saana..wewe ni mrembo dina

  ReplyDelete
 52. DINA .. NIMEKUKASIRIKIA NA KUANZIA LEO NAANZA MGOMO BARIDI DHIDI YA BLOG YAKO.

  UNAJUA KWANINI???

  ReplyDelete
 53. My dear friend Dina, hongera kwa kuanza kupungua... ongeza bidii utafika, utapungua pale unapotaka kufika, May Almight God be with you all the way.

  ReplyDelete
 54. Hi Dina, nakupongeza sana kwa hatua hiyo. Mimi ni mnene sana na nimeshakata tamaa ya kupungua, ila pia nakubaliana na wewe kuwa ili uweze kupungua inabidi wewe mwenyewe uamue kuwa sasa nataka nifanye nipungue, kelele za watu hazisaidii kama wewe mhusika huna determination. Mimi nadhani nakosa determination.
  Juzi nimepewa contact ya jamaa mmoja ambae anafanya consultancy, nasikia anasaidia sana watu kupungua kwa muda mfupi. Anakupa list ya special diet na mazoezi, ukiweza nasikia kwa mwezi unapungua kuanzia kilo 10 hadi 14. Kama uko interested wasiliana nami kwa msg namba 0713-268809 ili nikupe namba yake. Ukimpigia yeye anakufata ulipo,

  ReplyDelete
 55. Sikia Dina, achana na pombe na sisitizia sana diet yako huku ukipiga bangi kwa wiiiiiingi kama fleva artists. Utarudia tu kama zamani. This will take you at least two months kurudia kama awali.

  ReplyDelete
 56. Tatizo lako unapenda kula kula. We unapambana na unene sasa kuku unakula wa nini? Kuku ni ndege mwenye mafuta mengi haijalishi amekaangwa au amechomwa! Halafu unasema chips unakula kwa hamu! Hamu ya nini sasa? Sioni sababu ya kuwa na hamu ya chips wakati uko kwenye mapambano.

  Mi nafikiri ungejikita kwenye ulaji wa mbogamboga na matunda. Vitu hivyo vingekusaidia sana. Ukiongeza na mazoezi, ungepungua kwa muda mfupi sana.

  Wote wanaokupa ushauri wanaonesha ni jinsi gani wanakupenda. Don't lose hopes.

  ReplyDelete
 57. Nashukuru sana kwa maoni na changamoto...soon nitaanza kukimbia.Mimi sijawahi kuwa mtu wa mazoezi hivyo nilianza kwanza na mazoezi mepesi ili mwili uzoee na kupata pumzi nilipofika naweza kuanza kukimbia.
  Kwa unaetaka kuwasiliana na mimi kuhusu kupunguza mikono na tumbo email yangu ni dina_marios@yahoo.com

  ReplyDelete
  Replies
  1. naomba nielekeze pa kupata hiyo dawa.shake off

   Delete
 58. Dina hongera kwa uamuzi ambao umeamua kuuchukua.
  Google 7 days cabbage soup wanasema inasaidia sana kupungua ila ni strict kwa siku saba. Unaweza kutengeneza mwenyewe

  ReplyDelete
 59. Achana nayo mpnz hayo ni maneno ya mkosaji, hakuna kitu kinacho shindikana katika dunia, utarudi tu enzi za mwalimu dada ISHAALLAH.

  ReplyDelete
 60. hongera dina,umependeza....usichoke Mungu akutie nguvu.

  ReplyDelete
 61. Hongera kwa uamuzi, kitu chochote waweza kufanya ukidhamilia. mimi nilichukia unene, ila sikufikia uzito wako! nilifanya diet naweza kusema nyingi, napungua tena naongezeka. mwisho niliamua kutokula usiku, nitakula chakula chochote kila, ila mwisho ni saa 12 jioni, usiku nikizidiwa nakunya chai ya rangi(si mpenzi wa chai). nilifanya hivyo karibu miezi 12. toka wakati huo uzito wangu ni 58-62kg., ujauzito wa kwanza nilifikisha kg 70, lakini nilirudi pale pale, ya pili nilifikisha 80kg, navyo andika nina 61kg, na mtoto ana miezi 20. sijafanya diet yoyote. ila nimekuwa si mpenzi wa chips,mayai, vyakula vya mafuta. hata chakula mara nyingi nakula kiasi kidogo. all the best Dina, naamini Utaweza. unapendeza ukiwa na mwili wa wastani.

  ReplyDelete
 62. Yani dada uwe mnene uwe mwembaba ila una uso mzuri sijapata ona, yani una kababy face! Hongera mumy!

  ReplyDelete
 63. Kila la kheri utafika tu utakako uzuri pamoja na unene badovuto upo. Hata mm mikono bado unasmbiwa nyanyua vyuma ndo nimeanza juzi unyanyaji wa vyuma.

  ReplyDelete
 64. dina ongera nina tatizo kama lako tangia nimejifungua stazamiki nimetumia vitu vingi hadi hiyo shake off na spliner lakini naona bila labda nianze mazoezi ongera sanaaaa rey

  ReplyDelete
 65. Hongera sana mrembo. Huo anaeuza SHAKE OFF unaweza kutupatia namba yake Pleeeeeeeeeeeese

  ReplyDelete
 66. Hongera sana Dina kwa juhudi za kurudia mwili wako wa zamani,usiumie moyo kwaajili ya sisi binadamu kila mmoja huwa ana roho yake tofauti kuna wengine wameumbiwa makwazo kwa wenzao kwa hiyo wachukulie poa hukumu yao ni wao na Mungu na ukiwachunguza sana huwa wana roho za wivu achana nao angalia wale wanaokusupport unasonga nao mbele upo juu sana.Usiuachie tena mwili wako hapo ulipo inatosha wala usipungue sana mpendwa.Big up

  ReplyDelete
 67. Jamani kitu muhimu kujua kwenye uongezekaji wa mwili ni kujua wewe ni mmeng'enyaji wa chakula wa haraka,wa kati au wa taratibu, na kila mmojawapo ana vyakula anavyotakiwa kula, atakayehitaji kujua hilo nitamsaidia na jinsi ya kujitest, mimi imenisaidia sana unaweza ukadhani hutakiwi kula mafuta sana kumbe wewe ni aina inayotakiwa ule mafuta kwa wingi

  ReplyDelete
 68. anonymous wa december 5 nahitaji kuwasiliana na wewe, please toa namba yako au email addres

  ReplyDelete
 69. toa hiyo mada ya vyakula basi humu umpostie dina ili iweze kusaidia wengi..kila mtu akikuuliza anatakiwa kula nini aache nn itakuwa kazi sana...pleasssss

  ReplyDelete
 70. Kwakeli umejitaidi sana nami napenda kupungua n nitaiga mfano wako. Hongera mama.

  ReplyDelete
 71. wel sister umenitia moyo sana coz hata mimi nakutana na mitihaniu kutokana na mwili wangu mi ni mnene mpaka sasa nina kilo 92 sijui naweza kupata wapi hiyo SHAKEOFF?

  ReplyDelete
 72. dina naomba contact za hapo tht dancers, nami nianze kwenda

  ReplyDelete
 73. Hongera sana Dina kwa kufanya uamuzi huo, mie mwenzie pia nilikuwa ni mwembamba na nilikuwa napenda mwili wangu sana na sikuwa napenda unene hata kidogo, tatizo lilianza pale nilipoolewa sa hiv nina watoto wawili na mdogo ana 3 month, nina kilo 98, suala la uji na mtori nimeweka kando kabisa sitaki hata kuvisikia labda siku moja moja tu nakunywa white supu, natamani sana kupungua pls ukifanikiwa nasi tujuzane, mie shake off niliambiwa kwa kuwa nanyonyesha haitafaa kwani mtoto pia atapungua uzito.

  kwa unayefahamu namna ya kuounguza tumbo na mikono naomba utujuze wote kupitia hapa ili angalau nasi tufaidike, na kuhusu suala la mmeng'enyo pia tunaomba msaada wako pia wa kutuelewesha.

  Big up sana Dina kwa hatua hiyo, usjali ukiwa na imani kila kitu kitafanikiwa.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hongera sana dina kwa uamuzi uliochukua na mimi ninatatizo hilo plz nielekeze ntaipata wapi hiyo dawa ya kupunguza uzito shake off

   Delete
 74. sa dina unaendelea vp na hii issue yako ushapungua tayari?

  ReplyDelete
 75. jaman nitapata wapihiyo shake off.dina nijuze pls

  ReplyDelete