A 23 years old anaswa na madawa ya kulevya kwenye Rasta. Balaa, lazima atanyongwa! You can see hela inavyosumbuwa watoto wetu jamani. Kuvusha mzigo ulipwe only Tshs 3m! This is very absurd!!!
akikaguliwa na polisi
baada ya ukaguzi kukamilika madawa yanaonekana kwenye nywele zake
' wajifanya mjanja wewe tumekukamata dada,utajutaje'hapa nahisi walikuwa wakisema hivyo maofisa hao.
maskini njaaa hiii itatuua.......... Ni cocaine yenye thamani ya sh. Mil 235.3* Ni Nolubabalo (23) aliyeahidiwa kulipwa sh. Mil 3* Anaweza kuhukumiwa kifo.
NOBANDA NOLUBABALO (23) kutoka Afrika Kusini jana alikamatwa akijaribu kusafirisha madawa ya kulevya aina ya cocaine katika nywele zake za rasta (dreadlocks) katika ndege iliyokuwa inakwenda Bangkok, nchini Thailand.Nobanda alikamatwa nchini Thailand na wanausalama waliohisi kulikuwa na kitu cheupe kwenye rasta zake ambapo walipomfanyia upekuzi wakagundua madawa hayo.Uchunguzi uliofanyika baadaye uligundua kuwa dada huyo alipanda na madawa hayo kabla ya kupanda ndege iliyokuwa inatoka Brazil.Madawa hayo yanakadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 93,000 ambazo ni sawa na sh. Milioni 235.3 ambapo yeye aliahidiwa kupewa Paundi 1,200 ambazo ni sawa na sh. Milioni tatu.Kiasi cha kilo 1.5 kiligundulika kwenye rasta za dada huyo.Nolubabalo bado anashikiliwa na vyombo vya usalama baada ya kukamatwa uwanja wa ndege wa Suvarnabhumi alipotoka katika ndege ya Shirika la Qatar ambayo ilikuwa imetokea Sao Paolo, Brazil, kupitia Doha.Mwanamke huyo alisema kwamba alikubali kusafirisha madawa hayo baada ya kukubaliana na mfanyabiashara mmoja wa Thailand ambaye angempa Pauni 1,200.
Kukamatwa kwa raia huyo wa Afrika Kusini kunafuatia kunyongwa kwa raia mwingine wa nchi hiyo aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko China.Thailand hutoa adhabu kali dhidi ya wauza madawa ya kulevya ambapo ni pamoja na adhabu ya kifo.Janice Linden (38) ambaye ni raia wa Afrika Kusini pichani juu, aliuawa kwa kuchomwa sindano ya sumu jana baada ya kukamatwa katika jiji la Guangzhou, China, na kilo tatu za madawa kama hayo Novemba 2008.
STORY BY MOHAMED SHAWEJI
Hii ni habari ya mid December, ndo leo unaiona??
ReplyDeletemmmmh kwa kweli inasikitisha now adays hata vibinti vidogo vimeona dili biashara hiyo!!dunia inakoelekea siko maana hata taifa la kesho wamekumbwa.eee mungu wasaidie sana vijana tena kama mabinti wasishawishike aibu
ReplyDeleteJAMANI BADALA YA KUWA COLEGE ANAPIGA KITABU ILI KUJENGA FUTURE YAKE, ANAFANYA BIASHARA YA KUBOMOA FUTURE ZA WENGINE NA KUHARIBU AFYA ZAO.
ReplyDeleteHATA KAMA MTU UNA NJAA KIASI GANI HAIFIKII KUJIWEKA KATIKA RISK KIASI HICHO NA KUSAIDIA KUUWA WENGINE.
HII HABARI SI YA JANA NI TANGU DECEMBER KAMA SIKOSEI...
ReplyDeletehata ikiwa ya december muhimu amepata ujumbe ambao walikuwa hawajui maisha yenyewe haya.
ReplyDeleteKuna watu wengine akili zao kama ziko ndani ya shimo la choo. Hata kama ilitoka December inasumbuaje mwili wako. Asante sana Dina kwa mimi kuweza kuiona hii habari hapa kwako inasikitisha sana na vile vile tunajifuza.
ReplyDeleteLazima Dina Kama muandishi wa habari atoe habari sahihi na kamili. Kama kakosea arekebishwe, maana wengine tulioijua hiyo habari tulishtuka na kudhani ni mwingine tena karudia kosa. Na wasioijua lazima wajue exactly kinachoendelea! Mbona watanzania tunapenda ligi hivyo! Labda Dina mwenyewe hakujua ni ya lini, sasa kajua. We ndo mwenye akili zilizo ndani ya choo, hupendi kukosolewa na kujifunza, utabaki na ulimbukeni wako milelea! Na we Dina usiwe unaongeza wala kupunguza mambo kwenye habari, that's so unprofessional, maana nakumbuka ulishatuzinguaga na picha yako ya animal print top ukadai imepigwa miaka ya 80 wakati hiyo ndo miaka ulo zaliwa!Kama habari huijui vizuri fanya uchunguzi kwanza wa kutosha ndo uiweke hapa, otherwise u won't be taken serious in ur work/career!
ReplyDeleteakuna cha njaa wala nini maisha ndivyo yalivyo wewe mtangazaji mwingine mganga mwingine anauza mwili wke wengine mafisadi wengine wanaenda shule wangine mitahani waigizaji wanamuziki n.k kinachotakiwa pesa tu si kingine na dunia inaendelea
ReplyDeleteHabari inakua habari pale unapoipata! hata kama niya karne ya kwanza... kwako wewe uliyeiona last year hii si habari lakini kumbuka kuna wengine akina sie NDIO KWANZA TWAIONA mbona unataka kutukosea haki yetu ya msingi ya kupata habari jamani. Punguzeni maneno watoa comments.
ReplyDeleteDina ahsante kwa kutuletea habari hii whether ni ya mwezi uliopita au ni ya mwezi huu wa kwanza. Ukweli ni kwamba wauza madawa ya kulevya wametangaza vita dhidi ya vijana na jamii kwa jumla. Katika vita kuna mambo mawili: umuue adui yako au yeye akuue. Wauza mihadarati ni maadui zetu wakubwa. Wao wako tayari kutuulia vijana wetu kwa ajili ya pesa. Nazipongeza nchi zote zinazowaua washenzi wenye kuuza madawa ya kulevya. The war against drug should be merciless on f****** drug dealers. Tazameni walivyomuua Amina Chifupa kwa "arsenic poisoning". Dalili zote za "ugonjwa" wake zinaonyesha kuwa alikuwa anapewa sumu ya arsenic. Pia tuwaelimishe vijana wetu juu ya madhara ya mihadarati. Badala ya malumbano yasiyokuwa na kichwa wala miguu, viongozi wa dini zote wana wajibu wa kuwaelimisha watu kuhusu madhara ya heroin, cocaine, ulevi, ukahaba, n.k. Narudia tena, HAKUNA HURUMA KWA WAUZA MADAWA YA KULEVYA. Nawasilisha.
ReplyDeleteNakubaliana na Anonymous wa Jan 27, 2012 11:31 AM, hamna kuwaonea huruma wauza madawa ya kulevya. Wauza drugs ni wauaji wakubwa.
ReplyDeleteNakubaliana na Anonymous wa Jan 27, 2012 11:31 AM, hamna kuwaonea huruma wauza madawa ya kulevya. Wauza drugs ni wauaji wakubwa.
ReplyDeleteacheni ushamba asa unamtukana mwezio ndo nini kuweni wa staarabu na msirudie tena kutukana ama la nitawatia viboko
ReplyDelete