Tuesday, January 24, 2012

LEO TULIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JUU YA KITCHEN PARTY GALA

Mchana wa leo mimi na Vida tulikutana na waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu Kitchen party gala.Tukio ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Danken house mikocheni ambao ndio ukumbi rasmi wa shughuli hii jumamosi ya tarehe 28 january.
Watoa mada ni watu wenye uwezo katika swala zima la uelimishaji
Aunt sadaka;Ni mwana saikolojia aliyebobea katika maswala ya wanawake na watoto.Ana uwezo katika Nyanja hii ambao umetokana kielimi na uzoefu wa kukutana na kesi mbalimbali amabazo zinazo mguza mwanamke hivyo kuweza kuwa funzo kwa wengine.
Bi Chau ni mwanamke ambae mbali na kuwa katika fani ya sanaa kwa muda mrefu wamekua wakito amafunzokwa wanawake tokea muda mrefu.Mafunzo ya mahusiano,ndoa na familia kwa ujumla.
Mama Victor;Ni mtumishi wa Mungu katika dini ya kikristo ambae anaelimisha wanawake kwa mafunzo ya kidini.Anafundisha mwanamke kujitambua vile mungu amempa uwezo wa kuitumikia jamii yake kama mlezi na kiongozi.
Kwa ufupi hawa ndio wakufunzi katika tukio letu hili la women in Balance jumamosi hii katika msimu wa pili.
Burudani itatolewa na Nyota Waziri.
Huu ni mkakati wa mwaka mzima huu 2012 na tutakutana kila mwezi mpaka mwezi march ambapo ratipa itabadilika na wanaume kuhusishwa.
Tulionyesha DVD ya kitchen party gala iliyopita ambazo tutazitengeneza kwa wingi na zitaanza kupatikana kuanzia mwezi ujao.Kila mwezi tutakuwa tunarecord kwa wale watakaotaka kununua labda alipitwa zitakuwa zikipatikana.
Unapokutana na jopo la waandishi wa habari maswali lazima...........
swali:kwa nini kitchen party gala?
Vida:Wazo hili limekuja mara baada ya kuona kwamba ule muda wanawake wanaopata kuongea mambo haya kwenye kitchen party ni mchache na hautoshi kumfahamisha mwanamke mambo yote muhimu.Mambo ambayo ni lazima ayajue au hata kama anayajua kutokana na pilika pilika za maisha anajisahau.Wasichana na wanawake wengi kwa sasa wanakabiliwa na changamoto nyingi sana ambazo zinapelekea kushindwa kusimama katika mahusiano yao.Teknolojia,mwamko wa elimu,wanawake kumiliki biashara binafsi,kazi,wazazi hawahusishwi ,kila mtu mjuaji ,kujisahau n.k
Matokeo yake talaka nyingi na mahusiano kuvunjika sasa tunataka kumkumbusha mwanamke wajibu wake na nafasi yake katika mahusiano.Ajitambue.

swali:hii ilivyokaa ni kama mmewalenga wale wanawake wa standard ya juu vipi hawa wa chini mna mpango gani nao?
Vida:Mpango huu kwa sababu ndio tumeanza na umeonyesha kupokelewa baadae tutawafikia wanawake wa kila eneo.Kwa sasa tumejaribu kuomba wadau mbalimbali kushirikiana nasi kwa kutuwezesha tunasubiria tuone itakuwaje.Hilo likifanikiwa tutakuwa hatuweki hata kiingilio kabisa.Kwa sasa kuna kulipa ukumbi,wataalam,chakula n.k

Ikitokea mtu wa kutuwezesha haitakuwa tabu sisi kufika kokote kule.
swali:kwa nini ni wanawake tupu?
Vida:
kwa sasa tunataka msichana/mwanamke aone wapi anapata changamoto kulingana na mafunzo anayopewa.Mfano iliyopita wengi walitamani waje na wenzi wao maana mengi yanawagusa wote wawili.Kwa hiyo basi somo likikolea tutampa kazi ya kumshawishi mwenzi wake kuja.Ni lini tutawaambia muda ukifika.Lakini kwanza ni mwanamke maana tunaamini yeye akijitambua basi jamii nzima itaelimika.

swali:Ticket zinapatikana wapi
jibu:Shea Illusion mliman city
8020 fashions sinza
maduka yote ya cassandra
born to shine mwenge


Mwisho tukawashukuru wadhamini ambao wamekubali kushiriki nasi siku hiyo ambao ni kinywaji cha baileys,MGen insuarance,cocacola,cooparate image na clouds fm.

Kinadada/mama karibuni sana wahini ticket mapema maana sio nyingi.Mlioko mjini pale cassandra zinapatikana au piga namba 0716485666.Tukutane saa nane mchana kuwahi muhimu msikae sana kwenye kioo.

14 comments:

  1. i just love you Dina and everything you are doing,sio limbukeni km hawa wanaoijiita watoto wa mujini wanaoshindana kuchuna wazungu...go gal,mim ni mdogo kwako nipo nje kimasomo now,i wanna be you nikitoka out of sch life...keep shining

    ReplyDelete
  2. ni kitu kizuri sana i lik it but how about tuliokuwa mbali na jiji kwa nin msitoe hizo dvd mkazisambasa ili tufaidike wote? its me witness moyo from moro 0766888858

    ReplyDelete
  3. mambo D tusaidien na sisi wa nje japo dvd tuu tuwe tunaona na kujifunza pls ni wazo tuu kwan tunapitwa sana wadau wako na hiyo namba hapo ya simu mbona haipatikanagi ok love you

    ReplyDelete
  4. Najiuliza tu, kwanini ikaitwa `Kitchen party'?

    ReplyDelete
  5. Dada Dina hii nimeipenda sana kutukumbusha wanawake wajibu wetu asante sana msitusahau wa mikoani.

    ReplyDelete
  6. dada Dina na Vida nawapa big up kwa jamabo hili mnalolifanya! twahitaji kujua mtakapoanza kusambaza hizo dvd, zitakuwa zapatikana wapi ila nasi wa mikoani tuweze zipata tufaidike na vilivyojiri pia.
    ni mimi Meg, Morogoro.

    ReplyDelete
  7. Hi Dina!!! its a gud thng kwa kweli tunakumbushana vitu mbalimbali mwenzangu tuepuke talaka lakini!!!!!!!!!!!!!!! vipi sisi wa mikoani jamani sambazeni basi hata hzo dvd tuzipate na siye huku mi nipo Arusha.
    cheers.

    ReplyDelete
  8. hi Dina,
    this is very gud thing hasa kwa kipindi hichi ambapo most of marriage zina fall apart in a very short time. Lakini please consider na wanawake ambao wako out of Dar es Salaam coz they also need this. Sijui umeshawahi kuwa na thought kama hiyo , women who are out of Dar es salaam?

    ReplyDelete
  9. Dina nimependa hilo coat ulivyoshonewa, if u dont mind naomba namba ya fundi plsssss

    ReplyDelete
  10. WOW! U LOOK SO GOOD, YAN UMEPENDEZAJE! HZO WEAVING FUP2 ZNAKUPENDEZA SN DINA USIACHE PIA HYO B2A UMEKUTOA VBY SN HAD NATAMAN KWENDA KUSHONA.

    ReplyDelete
  11. You just rock my Dina,kwanza umependeza saanaaa saanaaa!!pilia the things you do makes lots of senses kweli cant wait for saturday for sure!!love you!

    ReplyDelete
  12. mie nipo tofauti kidogo na wadau wengi walotangulia,sidhani kama mafundisho ya siku 1,yanaweza kumbadilisha mtu tabia yake,mtazamo wangu mngekumbushana jinsi ya kulea watoto wa kike kuanzia umri mdogo na nadhani akiona jinsi mnavyoishi home ndo ataelewa zaidi,kwani nijuavyo mie ndoa haina formula,ila ni mawasiliano zaidi ndo yatafanya ndoa yenu idumu,haya mambo ya kitchen party sio kivile labda mseme matafuta mjumuiko wa jumla zaidi na kubadilishana mawazo tu lakini si mafunzo!na mivunjiko ya ndoa siku hizi ni matokeo ya utandawazi na vile watz tunapenda kuiga magharibi zaidi,kwani wenzetu hawana mila na desturi,tofauti na sie,na watu wanapenda sana kuishi maisha ambayo sio yao,mtajichanganya sana kwani kuna issues za usawa kati ya mwanaume na mwanamke kitu ambacho hakiwezekani,na hilo ndo kubwa linalovunja nyumba nyingi!! anyways niwachoche lakini fikirini sana>

    ReplyDelete
  13. Ni real wana practise hayo mafundisho waliyopata au imekuwa kama fashion kwa vile flani na flani watakwepo basi nasi tunashiriki halafu at the end of the day unaendelea na madudu yako.
    Natarajia hawa influential women wawe walimu wa jamii yote na haswa jamii ya chini maanake maisha ya mtanzania yanazidi kubomoka kimaadil.

    ReplyDelete
  14. DADA DINA TUNASUBIRI URUSHE KWENYE MTANDAO KILICHOJILI KWA SIE TULIO MBALI NA DAR KAMA WAKATTI ULE NINA HAMU YA KUJUA MATUNDU 7 YA MAMA VICTROR

    MFUATILIAJI WA BLOG YAKO KUTOKA SHINYANGA

    ReplyDelete