Leo katika kipindi ulipiga wimbo wa kukamata mwizi nikawa natikisa kichwa kukubaliana na yale yanayoimbwa kwenye wimbo... Mpige tofali, mchome moto.....!
Jana nilienda kanisani Kristu Mfalme Tabata kuhudhuria ibada ya Mazishi. Nikaengesha gari kwenye maegesho ya Kanisa kwa imani kuwa ni eneo salama. Kulikuwa na mkoba wangu (Hand bag) ambayo niliitoa kwenye gari na kuifungia mwenye buti ili nisiingie kanisani ni mkoba. Cha kustusha nilipoka kanisani nilikua kioo cha gari yangu kimevunjwa, buti imefunguliwa na mkoba kutoweka. I was very shocked Dina, kwa sababu nilipoteza vitu vvyangu vingi. Kulikuwa na pesa Taslimu, nyingi tu nilibeba kwa ajili ya kulipa ada ya mdogo wangu, kulikuwa na Simu aina ya Blackberry, Driving License, Work ID, Cards za Bank na vikorokoro kibao, unajua tena mabegi yetu hayakosi vitu vya aina tofauti tofauti.
Juzi nilikuta kibaka/mwizi anapigwa nikamwonea huruma na kuwasihi wale walokuwa wanampiga wamwache, ila tangu nimeibiwa, I hate vibaka, na siku nikikuta kibaka anaipigwa, I swear nami nitaongezea kipigo changu, tena cha hali ya juu.
Niko kwenye masikitiko makubwa sana Dina rafiki yangu! Poa, Kazi njema.
Nakutumia picha uone gari yangu ilivyopasuliwa kioo.
dah, pole sana dada yng, hawa vibaka hawana mana hta kidogo na hyo kibaka naamin alikuwa maeneo hayo akaona unavyoweka huo mkoba kwenye buti, pole sana dada.
ReplyDeleteSasa hapo mkono ulipita vipi mpaka ukafungua buti jamani?maana hicho kioo kilichovunjwa kinaonekana ni cha nyuma au mi naangalia kunyumenyume
ReplyDeleteehh we mtu hapo alifungua mlango kwanza ndo buti likafungulia wee mtu maswali mengine bwana
ReplyDeleteKioo kilivunjwa ili kuwezesha mkono kupita na ku-unlock mlango. Kwa hiyo kibaka aliingilia mlangonui ndo akafungua buti mdau.
ReplyDeleteHUWA WANATEMBEA NA KICHUPA CHENYE DAWA FLANI HIVI,WAKIIPAKA KWENYE KIOO KINAKUWA LAINI KAMA KINAYEYUKA SO KINAVUNJIKA KIRAHISI THEN,WANATOA LOCK YA HUO MLANGO WA NYUMA NDO ANAINGIA KWENYE GARI NSDHANI UTAKUWA UMEELEWA MDAU WA 2.MUHIMU USIACHE KITU HASWA MKOBA KWENYE GARI
ReplyDeletePOLE SANA DADA YAWEZEKANA WAKATIUNAWEKA MKOBA KWENYE BUTI VIBAKA AU KIBAKA ALIKUWA ANAKUANGALIA KILA HATUA KWA HATUA .
ReplyDeleteMAMA P
pole sana dada vibaka wanaturudisha sana nyuma jamani.
ReplyDeletenazani hapo kristo mfalme tabata ndo kawaida yao wazazi wangu waliibiwa mwaka jana power window na simu zao siku ya jumapili na hata walipotoa taarifa kwa uongozi wa kanisa hamna kilichotendeka zaidi ya pole so watu mnaosali tabata kristo mfalme kuweni makini na magari yenu. Pole lakini
ReplyDeleteJamani, mie niliibiwa mkoba tena nilikuwa nimeuweka chini ya kiti cha gari. Ulikuwa na vitu mbalimbali na pesa taslimu za chama cha wanawake kwani ilikuwa jioni yake tunakuta kwa kikao. Angalau kadi za bima ya afya na kadi ya sanduku la posta vilitupwa posta ambayo anwani yangu ilionyesha ktk kadi lakini bank crds hawakurudisha. Vibaka bwana sio watu hata kidogo walibeba hadi bible, sijawaelewa mpaka leo. Tangu siku hiyo sina huruma na mwizi yeyote hata awe ameiba kijiko, nikimkuta anapewa kichapo, nami nashiriki hata kwa kuongeza hamasa ya maneno tu ili wanaompa kichapo waendelee.
ReplyDeletePole sana mdau, I can imagine how you feel, itachukua muda but you will heal as time goes on.
Mdau mwanza.
duuu polesana,lakini mbona gari hii imepigwa picha ofisi za bantu knondoni?
ReplyDeletemdau.
-
JAMANI POLE SANA DEAR. UNANIKUMBUSHA YALIYONIKUTA SIKU YA BOXING DAY NILIKUA NATOKA TABATA KUELEKEA KINONDONI ASUBUHI SAA 12.30 NILIPOFIKA KWENYE MATAA YA PALE BIBI TITI TAA NYEKUNDU ZILIWAKA IKABIDI NISIMAME. ILE KUSIMAMA TU WALITOKEA VIBAKA WAWILI MMOJA AKACHUKUA SIDE MIRROW YA KULIA NA MWINGINE YA KUSHOTO NA KUTOWEKA NAZO. YAANI SIKUWA NA LA KUFANYA ILA KUNUNUA NYINGINE. YAANI I HATE VIBAKA. YAANI SIKU HIYO NINGEKUA NA PISTO NINGEWASHOOT. WANATURUDISHA SANA NYUMA. WALAANIWE!!!
ReplyDeleteRAHMA
HIVI WADAU, NIMESOMA MAONI... WENGINE HASIRA, WENGINE HAMUELEWI, WENGINE MNASUBIRI MKIKUTA MWIZI MTAPIGA ILE MBAYA.. MBONA HAMUMPIGI LIJAMBAZI LENYEWE LINALOITWA 'SERIKALI' JAMBAZI NDILO LA KUUWAWA, HUYU MWIZI KAGANDAMIZWA NA HILO JAMBAZI, HIVYO TULIUWE HILI LIJANGILI, HAKUTA KUWA NA VIBAKA
ReplyDeletesiku nyingine usiweke vitu vya thamani katika gari, mbona ndo mchezo wa siku hizi, mimi niliacha begi la madaftari wakadhani ni kompyuta walivunja kama walivyokufanyia wewe nikaingia hasara ya kubadilisha kioo, na wao wakaishia kupata madaftari ya kozi zisizowahusu na hata kuuza hawaweza labda begi ambalo watauza kwa 5000 tu. Pole mwaya.
ReplyDeletepasi nikihangalia kwa idadi ya watu waliohibiwa hapo naona list ni kubwa sna na kuna wengine bdo wameibiwa na hawajasema na mimi kaka yangu alinipigia cm akilalamika kuwa apo kanisa alipaki gari kuingia kanisani alipotoka akakutu kihoo kimevunjwa wamemuibia cm pesa jins zke 2 mpaya na nguo za mtoto wtu kwas ushauri tu ni bora ujumbe uwafikishia viongozi wa kanisa alafu wao waweke walizi ata 2 pesa za sadaka zina tosha kuwalipa walizi 2
ReplyDeleteJamani Pole sana! Niliwahi kuibiwa hand bag na ilinichukua zaidi ya mwaka ku-recover... unajua hand bag za wadada tena zinavyobeba so mpaka leo nikisikia mtu kaibiwa hand bag inaniuma maana "I have been there" sijui nchi inakwenda wapi?? maana hata mie nina mtindo wa kuweka vitu ktk buti ya gari nowdays baada ya kuna vioo vinavunjwa duh! sasa sijui itakuwaje kama na ktk buti nako wanaingia.
ReplyDeletePole sana mdau, ina maana pale kanisani hakuna walinzi au na wao wanakula njama na vibaka? halafu hao lazima walikuona unavyoweka begi nyuma..... pole sn.
ReplyDelete