Mwanamuziki kutoka Uingereza kwa wapenzi wa muziki mnakumbuka nyimbo zake alizotoa mwaka 2000.Nyimbo kama 7 days na walking away zilipendwa sana hapa Tanzania.
Style zake za nywele vijana wengi walitengeneza vile vibutu na kuvaa hicho kikofia balaa. Unyoaji wa ndevu ile chanel O iliwasumbua sana vijana.Kama hauna ndevu nyingi za mzunguko basi utahakikisha saloon wamekusiriba super black angalau vimistari vionekane.
Kwa sasa amekuwa na kubadilika sana akiwa na umri wa miaka 31.Mwaka jana alichaguliwa kuwa balozi wa kujitolea wa mapambano dhidi ya kifua kikuu(TB)
Katika pitapita zangu nikakutana na picha zake nikagundua ni kitambo sasa sijamsikia.Ila nikapata taarifa kuwa anatarajia kutoa albam mwaka huu mpya 2012.Lakini kubwa ni style yake ya kufanya mazoezi yaani huyu kwenye suala la mazoezi hataki utani.
Kwenye picha hapo juu ni yeye alipokuwa mdogo.Akiwa mdogo alikuwa aina ya wale watoto wenye obesity wanene kula ndio usiseme ilikuwa ikimtesa sana sababu ya kutaniwa (bullied).Alipokuwa mkubwa na kujitambua ndio akaanza kufanya mazoezi sana na kuangalia anachokula.
Kwa sasa anakula kawaida maana ana uhakika kuwa anafanya mazoezi.Anasema akijiachia tu kuna 'mtu' yupo ndani yake akitoka huyo hatutoweza kumtambua ni nouma huo unene.Haya wakaka kwa wadada wale wenzangu na mie japo kuna shortcut nyingi lakini jibu kubwa ni mazoezi.Nasukuru Mungu sasa nimezoea sioni kazi kama zamani nimejaribu na nimeweza.Usiogope,uskate tamaa,weka nia na imani kila kitu kinawezekana.Mie kuanzia wiki ijayo naingia mchangani baharini kukimbia sitaki utani kabisa.Lazima azma yangu ya tumbo flat itimie..Pata burudani motomoto mpenzi mtazamaji na huyo ni kijana machachari sana Craig David anakwambia walking away lol!

all the best dina mimi nilianza mazoezi tarehe 1 mwezi 8 2011 nilijipangia mpaka january 1 2012 malengo yangu ya kupungua yatimie. nashukuru mungu nimepungua nilikuwa na pound 175 sasa nini 145 pound nimekimbia huko park na kuruka kamba mpaka siamini namshukuru mungu kwa kunipa nguvu. utaweza tu dina all the best. mdau wa houston
ReplyDeleteJamani mbona uhandsome umeisha ndio utu uzima Dina? yaani siamini kama Craig David huyu roho imeniuma eti utafikiri ananijua
ReplyDeleteAISEE MY DEAR HADI HAPO ULIPOFIKIA UMEPUNGUA SANA MBONA TENA SANA JAMANI PILI HUO KAKA KABADILIKA SANA MWEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEH!
ReplyDeleteniliwahi kusoma mahali kua huyu jamaa kawa shoga tangu hapo niliacha kumfuatilia wala kusikilizaa nyombo zake na nikatupa cd zake zote jalalani,kaacha hiyo mambo?
ReplyDeleteNimechekaje...Dina ni kweli mazoezi yanasaidia tena sana tu. mi nilianza diet ya chakula mwaka jana mwezi wa 9 tarehe 2.Nilikuwa na kg 75.5 lakini sasa nina 69. Bado naendelea nayo ila gym siendi na kwanza i cant afford. The only alternative i have ni kupunguza kula msosi.Kama kweli mtu upo determined unapungua vizuri tu.
ReplyDeleteDada Dii umenikosha na aidia yako ya kutaka tumbo lako liwe flat.Mh! naamini penye nia pana njia utafanikiwa tu.Craig David napenda sana nyimbo yake ya 7 days.
ReplyDeletedina tuwekee na thienry kwa sasa nae kabadilika na kaachia misharubu lol
ReplyDeletewe jamaa wa huu hapo so uingie net mwenyewe utafute huyo thienry wako tena nyingi utaziona
ReplyDelete