Wednesday, January 25, 2012

WAHESHIMIWA WABUNGE WANAWAKE LEO MJENGONI KATIKA KUHAMASISHA KUICHANGIA TWIGA STARS

Baadhi ya wabunge wanawake leo walikuja hapa clouds fm kwenye PB na baadae kwenye leo tena kupigia debe wadau mbalimbali kuichangia timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars.Kubwa ni kuiwezesha timu hiyo na pia kuhamasisha watu kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yetu ya taifa jumapili ya tarehe 29 pale uwanja wa taifa wakati ikicheza mechi ya marudiano na Namibia.
Wabunge pia kesho wana mechi ya kuchangisha pesa kwa ajili ya timu hiyo.Mechi itachezwa kati ya Twiga stars na wabunge katika uwanja uhuru kuanzia saa kumi.Watu wote mnakaribishwa.

Mbunge wa viti maalum Vicky kamata akisistiza watu kujitokeza kwa wingi kuishangilia Twiga stars jumapili hii.

Mbunge wa viti maalum ccm Zainab Kawawa akizungumza

Mbunge wa viti maalum ccm,Mh Zainab Matitu Vulu akisisitiza

Picha ya pamoja na waheshimiwa

Wabunge wakizungumza na mkurugenzi wa clouds media group bwana Joseph Kusaga.

Kikosi cha timu ya taifa ya wanawake Twiga Stars ambacho ndio timu ya nane kwa ubora Afrika kwa wanawake kama ulikuwa haujui.Timu yetu ilishacheza na timu ya Namibia nakuwafunga huko nchini kwao mechi ya jumapili hii ni ya marudiano kuwania kufuzu Fainali za Afrika kwa wanawake(AWC).

Viingilio kwa siku hiyo ni 2000 kwa jukwaa la blue,3000,jukwaa la orange,5000 kwa VIP C na B,10000 kwa VIP A.

Kwa wale mtakaoguswa kuiwezesha timu hii wasiliana na TFF.Twendeni jumapili hii tukaishangilie Twiga stars.

9 comments:

  1. Good job waheshimiwa!

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza sana Twiga Stars! Nawaombea kwa Mwenyezi Mungu waweze kushinda mechi hiyo.

    ReplyDelete
  3. ndo maana wanasiasa wa kibongo wananikera,walikua wapi cku zote mpaka wameona mafanikio ndio wanakuja kudandia treni kwa mbele ili kesho wapate mtaji wa kura,fuck u politicians

    ReplyDelete
  4. Ingekuwa amri yangu ningeivunja TFF,ivi kile kitengo cha masoko chini ya Jimy Kabwe kinafanya kazi gani?simba na yanga zinaingiza mamia ya mamilioni,makato yenu ni makubwa,mnazifanyia nini mpaka leo hii wabunge waje kuhamasisha?
    Kuna mgomo wa wadaktari na wauguzi nchi nzima,ebu tujaribu kutumia MUDA kwa mambo ya msingi na yenye kuleta tija kwenye jamii,kila mmoja wetu awajibike pale alipokuwa assigned.

    ReplyDelete
    Replies
    1. kabisaa wamekosa kazi ya kufanya wazungu wanasema kushoo off

      Delete
  5. Ingekuwa amri yangu ningeivunja TFF,ivi kile kitengo cha masoko chini ya Jimy Kabwe kinafanya kazi gani?simba na yanga zinaingiza mamia ya mamilioni,makato yenu ni makubwa,mnazifanyia nini mpaka leo hii wabunge waje kuhamasisha?
    Kuna mgomo wa wadaktari na wauguzi nchi nzima,ebu tujaribu kutumia MUDA kwa mambo ya msingi na yenye kuleta tija kwenye jamii,kila mmoja wetu awajibike pale alipokuwa assigned.

    ReplyDelete
  6. Heko Twiga Watanzania tuko pamoja nanyi na mungu atatenda mema tu.

    ReplyDelete