Sunday, February 19, 2012

KIDS PLAY TIME...ILINIKUTANISHA NA KINA MAMA NA WATOTO WAO

Jumamosi nilipata nafasi ya kujumuika na akina mama kadhaa na watoto wao.Dada Yvone aliandaa kitu kinaitwa Kids play time ambapo watoto walikuwa wakija na wazazi wao kwa ajili ya kucheza na wenzao.Wenye kuogelea,kucheza mpira,n.k
Agness na baby wake

Saraha na mwanae Malick

story za akina mama hapo ni........

1.Product mbalimbali za watoto kama vile pampers,wiper,maziwa,sabuni,mafuta n.k

2.Chakula na muda wa kunyonyesha

3.Tabia mbalimbali za watoto kama kutopenda kula,kukataa kunyonya kabla ya muda,ukorofi,ucheshi,kuto kulala,kulala n.k

4.Magonjwa yanayo wapata watoto kama vile allergy,vipele vya joto,homa,UTI,malaria..n.k
5.Urembo wa watoto kusuka,kutoboa masikio na tohara ya watoto wa kiume.

6.Nguo na mahali wanaponunua nguo na viatu vya watoto wao

7.Idadi ya watoto wanaotaka kupata na muda wa kupata wanaojipa.

8.Msaada wanaoupata au kutoupata kutoka kwa waume zao katika malezi.

9.Hawaachi kuwamwagia watoto wao sifa kedekede na maneno wanayotamka.
Ni mengi haya ni kwa ufupi tu.

Dee alitusumbua sana kumtoa kwenye hicho kigari.

Mashostito wamekutana

Shosti mwenye nyeupe:shoga mama yako wewe amekubali kukusuka?

shosti mwenye pink:ndio mama angu utamuweza basi ananifanyaga mie kama mdoli wake.

shost mwenye nyeupe:Mie baba kamkataza mama asinisuke
shost mwenye pink:kwa nini?

shost mwenye nyeupe:kasema mpaka nikianza darasa la kwanza.
shost mwenye pink:sasa wewe unasemaje kuhusu hilo?

shost mwenye nyeupe:ntasubiri mwaya ndio kwanza nina mwaka na miezi kadhaa kazi ipo.

shosti mwenye pink:vumilia tu mwaya mie mwenyewe nakoma usinione hivi.Siku nyingine sijisikii nachoka lakini wapi nasukwa hata usingizini dada.

shosti mwenye nyeupe:Haya twende shosti kabla hawajaanza kututafuta.



Erica na mwanae Michelle

Yvone na mwanae Chantel

Kaka Dee,mtoto wa rafiki yangu.

Kiukweli nilienjoy na pia kukutana na watu wapya,marafiki wapya.

Jioni tukarudi makwetu tumechoka kwa kucheza tumelala.

20 comments:

  1. RAHA SANA KUCHEZA NA WATOTO MI NAPENDA SANA, HONGERENI WATOTO WALI-ENJOY SANA MPAKA WAMECHOKA.

    NOTE:

    DINA NAOMBA UNITANGAZIE BLOG YANGU HAINA MUDA MREFU INAHUSU MAMBO YA KIJAMII KATIKA FAMILIA HASA MASWALA YA NDOA NA CHANGAMOTO ZAKE NA JINSI YA KUKABILIANA NAZO NA PIA HABARI ZA BURUDANI NA MATUKIO YA HAPA NA PALE.INAITWA MAJOY BLOG.http://majoyy.blogspot.com

    ReplyDelete
  2. Da Dina umependeza hapo chini picha ya mwisho na huyo mtoto, I like kids.

    ReplyDelete
  3. Dina , may the loving God bless you. Nakufuatilia saana uyafanyayo na naomba nikiri, uko tofauti kwa kiasi kikubwa na niyaonayo mengine katika nyanja-nyenza kama hizi.
    Mie pia nina binti mduuchu basi nimehisi kama alikuwapo hapo.
    Mungu awabariki maana hayo mnayoyafanya, hayafutiki kirahisi fikrani mwa hawa binadamu wadogo.
    Mungu awabarikini!

    KIPAPLI

    ReplyDelete
  4. ila hapo kumsuka mtoto mdogo ni kumnyima raha inatakiwa vitu vingine mtoto ajiamulie mwenyewe,hata hii kumtahiri mtoto akiwa mdogo nayo ni kumtesa

    ReplyDelete
  5. PICHA YA MWISHO IMETULIA SN

    ReplyDelete
  6. Dina,ujue mtu mwenye akili timamu akifuatilia mambo yako anagundua kua u mis somthing in ua life now and that should be ua mission to accomplish u know what is that?Mtoto,ebu ongea na shemeji yetu atupie vitu upate wakwako otherwise utakua mtu wa kuzungumzia watoto kila siku

    ReplyDelete
  7. Yaani nimekufa mbavu kwa hayo maongezi ya mashostito hao wenye nyeupe na pink

    ReplyDelete
  8. You look nice with kids. You should pray for one of your own. Nakuombea upate wa kwako fasta. Remain blessed.

    ReplyDelete
  9. dinnah hayo maongezi ya hao watoto mie hoi
    imetulia
    fetty...

    ReplyDelete
  10. picha ya mwisho hayo macho mhhhh umekula kungu nini?

    ReplyDelete
  11. Hahahahaha thanks Dina, it was nice meeting uuuu...nimewamiss salamz kwa mama D!!!

    Lol nimechekaa apo kwa Michelle na Louise duh
    cheers,
    mama Louixxx

    ReplyDelete
  12. Dina hii ilifanyika wapi na lini? mbona hamtangazi mnatuonyesha picha tu jamani? na mimi natamani kweli niwepo kwenye jambo unaloli host wewe i real admire you.

    ReplyDelete
  13. Dina lini ww mungu atakujalia nawe kupata mtoto wako?

    ReplyDelete
  14. huyo ni YVONE mbona amechoka jamani au ndo kulea, nimekumiss toka enzi zetu za Cabrige

    ReplyDelete
  15. Dina huwa nakukubali sana, Hope one day i will broke my silence and face u! its me Hans from brewery company.

    ReplyDelete
  16. Thats why i love this blog, i cant go a day without havng my eyes on it. keep it up ur almost there

    ReplyDelete
  17. Hans ongea tu Kiswahili kitupu utapendeza achana na mambo ya...I will broke my silence...yaani hicho si kiingereza I think it's a language close to english bro.
    Mlavumbi Orijino

    ReplyDelete
  18. jamani mbona hukuiweka wazi ili nasisi tuhuzurie inapendeza sana kucheza na watoto.ikiwepo tena naomba utufahamishe.

    ReplyDelete
  19. hahaha, Dina conversation hiyo mie sina mbavu! u really have made my day......

    ReplyDelete
  20. jaman i love kids na hao mashostito wawili hapo mbavu sina yani ukiwaskiliza unaeza ujikute unacheka tuu en u forget ol ur worries...nice pics

    ReplyDelete