Thursday, February 16, 2012

NINAPOAMUA KUTANGAZA MAHABA YANGU YA DHATI KWA "MENDE"



TAMKO HILI LINAWEZA KUNIHUSISHA KWA KARIBU NA "UGONJWA WA AKILI" KWANI KATIKA HALI YA KAWAIDA, NI JAMBO LA KUSTAAJABISHA PINDI AMBAPO, BINADAMU ANATAMKA BILA UOGA KWAMBA ANAMPENDA MENDE, UKITILIA MANAANI KWAMBA, KIDESTURI WADUDU HAWA WANAHUSISHWA NA UCHAFU.
LAKINI KAMA WASEMAVYO WASWAHILI, A.KA. WAHENGA "HAKUNA UJINGA ULIOUJINGA MTUPU' TENA KAMA TUNGELIJUA KUTHUBUTU KUIGA MAISHA YA MENDE NI KUTHUBUTU KUCHUKUA MAARIFA AMBAYO YANAWEZA KUTUSAIDIA KATIKA MAISHA YA KILA SIKU,

KWA MFANO:

A] MENDE ANAUWEZO WA KUISHI KATIKA MAZINGIRA YEYOTE, IWE BARIDI KAAAALIIII AU JOTO LILILOKITHIRI, YEYE HUJIWEKA TAYARI KUTOKANA NA MAZINGIRA, KWANINI NA SISI TUSIJIANDAE KWA MIKIKI YA KIMAISHA? IL HALI MAISHA YETU YANAWEZA KUBADILIKA WAKATI WOWOTE? .

B] MENDE ANAWEZA KUISHI BILA KULA KWA MWEZI MZIMA, ANAWEZA PIA KUISHI BILA KUNYWA MAJI KWA WIKI NZIMA, KAMA VILE HAITOSHI HATA UKIMKATA KICHWA ANADUNDA HAI KWA SIKU 7....HAYO KWA BINADAMU HAYAWEZEKANI LAKINI KWA MIFANO HIYO CHA KUANGALIA HAPO NI KIWANGO CHA UVUMILIVU NA USHUPAVU WA MENDE, KWA KUIGA USHUPAVU NA UVUMILIVU WAKATI TUNATAFUTA NJIA YA KUTIMIZA NDOTO ZETU, KUTATUSAIDIA SAANA KWANI TUTALAZIMIKA KUFANYA MAAMUZI MAGUMU NA KUBADILISHA MFUMO WETU WA KIMAISHA, NA JAPOKUWA ILE HALI ITUTUPA MATESO LAKINI, FARAJA YA MIPANGO YETU NA UVUMILIVU WETU, ITAZAA MATUNDA, WAINGEREZA WANASEMA WAZI WAZI NAMI SIBISHI "HARD WORK PAYS".


C] MACHO YA MENDE YANA LENSI KAMA 4000 HIVI, HIVYO KUMFANYA AWEZE KUONA PANDE ZOOOTE WAKATI MMOJA, ANTENNA ZAKE (ZIKO KAMA ZILE ANTENNA ZA TV ZILIZOPEWA JINA LA CHADEMA) INAWEZA KUWASAKA MENDE WENZAKE KWA URAHISI HATA KAMA WAMEJIFICHA FUTI SITA CHINI YA ARDHI, KWA MFUMO HUO TUNAWEZA KUJIFUNZA NAMNA YA KUTUMIA TEKNOLOJIA TULIOKUWA NAYO KWA MINAJILI YA KUTUPA TIJA ZAIDI KATIKA MAISHA YETU BINAFSI NA KIKAZI.

MWISHO KABISA NI KWAMBA MENDE ANA PAIR MBILI ZA MENO, YALE YA MDOMONI NA TUMBONI...SOMO KWETU HAPO NI LA MUHIMU SAANA , LAZIMA TUWE NA MPANGO WA AWALI NA MPANGO SAIDIZI IWAPO MPANGO WA AWALI UTAFELI TUTACHAGUA KUTMIA MPANGO SAIDIZI...KWA MIFANO HII NADHANI UTAJUINGA NAMI KATIKA KUELEKEZA MAHABA YA DHATI KWA MDUDU "MENDE"

(NYONGEZA NI KWAMBA MENDE NI KITOWEO SAAAFI KATIKA NCHI NYINGINE
)


Imetoka kwa...
Sebastian Maganga programs manager clouds fm!

16 comments:

  1. Dah nmepata somo Dina, yn ckujua km mende anavitu vyote hivyo. yatupasa tuwe km mende. Asia Alawi

    ReplyDelete
  2. Mende yeye ameumbwa hivyo. Hakupenda awe awe anakula uchafu, achukiwe na binadamu au kuwa kitoweo cha wanyama au ndege. alijikuta automatically yuko hivyo. binadamu nasi tumeumbwa kama tulivyo. hatuwezi kuwa kama mende, mende ni mende na binadamu ni binadamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mdau nimekukubali Dina na Seba wote vichwa maji,Mungu kaumba vitu kwa kila kitu na uwezo wako so unapotaka kuwa kama mende inakuwa haiingii akil kabisa,,,haya we DIna kuanzia leo nakuita MENDE

      Delete
  3. Dina .. 1+1=2 ni sawa kabisa hamna wa kubisha lkn 1+1=3 pia ni sawa ila jawabu ni wrong, tafuten mifano mizuri inayokubalika nukta

    ReplyDelete
  4. nimekupata swahiba, ckuyajua haya hapo mwanzo

    ReplyDelete
  5. Hivi hizo ndoto unazosemaga utatimiza zitatimia lini dada yangu?Ndoto nzuri zinaendana na objectives,strategies,skills,na vyote hivi hujengwa katika misingi imara ambayo ni elimu,kujituma na ubunifu,ambavyo yote haya wewe hauna.Tatizo lenu watanzania na hasa wauza sura runingani na redioni huwa mnajidanganya eti "nina kipaji", lakini hatuoni hivyo vipaji vinaleta tija kwa kiasi gani.Na hili ni tatizo kubwa kwa watangazaji wa clouds,ku-force umaarufu,shule imewashinda!Ndio majuzi nlimsikia mmojawenu akimhoji mtu runingani,anajisemea,"mimi sijasoma lakini ninafanya mambo makubwa",mambo makubwa gani mnayofanya zaidi ya kupotosha wadogo zetu kuwa maisha bila elimu yanawezekana!
    Ushauri wangu,rudini shule,au muwe wamama wa nyumbani(mtafute waume wa kuwaoa kabla hamjazeeka) maana wengi wenu huwa mnaishia tu kuchakachuliwa au kuzaa nje ya ndoa,mkishajiona mnazeeka mnaanza kudanganya umri,ili mradi tu kuhalalisha kazi unayofanya ambayo definately haindani na umri wako.Msione mkurugenzi wenu amefanikiwa bila elimu na nyie mkadanganyika kuwa maisha ni marahisi kiasi hicho,hao ni one out of hundreds!
    Ni hayo tu kwa leo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi,shule ni nini?,ni cheti,diploma,degree,masters au Ph.D.Hivi kuelimika ni lazima ukae darasani?.Hivi inawezekana kila mtu akaenda shule?.Maisha ni makubwa zaidi ya ulichojifunza darasani,tuache ulimbukeni.

      Tuwe fair,jamaa amemtumia mende kuwasilisha mawazo yake,na kamwe ajawataka watu wabadilike na kuwa mende.

      Ukweli ukisemwa,Clouds media Group ni kati ya watu wabunifu sana.

      Delete
  6. Hongera kwa Bw.Sebastian Maganga kwa utafiti aloufanya. Asante nawe kwa kutujuza wadau wako.

    ReplyDelete
  7. usiache kupost comment yangu...usipopost basi kuna ukweli

    cox

    ReplyDelete
  8. MERRY MLAY

    Sister unatisha kwa udadisi hadi mende kwali upo juu.

    ReplyDelete
  9. DINA, huyo mtoto kama babake ana uwezo, waende Nairobi kupima hiyo DNA, vipimo vya tanzania vingi feki, kutokana na Serikali kupenda kununua vitu kwa kuangalia mtu kubaki na chenji. Vipimo vingi vya kwetu havina ubora kabisa. Please!!! msaidieni huyo Mama, simamieni mpaka huyo baba akubali kwenda kupima hapo Nairobi

    ReplyDelete
  10. Mmmmmmmmmmmmmmmmh siwapende mende kabisa,sita ingia kwenye blog hii mpaka huyo mende atoke!

    ReplyDelete
  11. Dada vipi mbona kimya hakuna vitu vipya?

    ReplyDelete
  12. sawa,seba alivyokupostia ukaona na wewe utuwekee /hujui zuri na baya....?kazi kwelikweli

    ReplyDelete
  13. please tungeambiwa na dawa ya kumuuwa maana kwa kweli mimi simpendi tena wale jamii ya mende wadogooooo jamani kwangu ni balaa ikifika usiku ukazima taa unapowasha unaweza kukimbia nisaidieni wazo la dawa....

    ReplyDelete
  14. nadhn kuna watu wnapnda kukus0wa watu zaid kuliko kuelewa mtu huyo wnaemkosoa ame0ngea nini na lipi kusudio lake ktk ma0ngezi yke, hkuna bnadam asiejua kuwa hawez kufanana na mende kmaumble, ila alichkusudia hpa ni tabia za mende jinsi anavy0wza kupambna na maish yke ameamuwa kutumia mfan0 wa mende ili kutufikshia ujumbe sisi,sasa si0n sababu ya kuc0mment na kusema ni ufinju wa akili binaadam kufananshwa na mende. Musiwe na tabia ya kuropka ropka tu manen0

    ReplyDelete