
DINA,NA WADAU WA BLOG MIMI NI SICHANA MWENYE UMRI 34 NI MTANZANIA KWA SASA NAAISHI UK KWA MUDA MREFU KIDOGO. KILICHO NIFANYA NIKUANDIKIE NI UPWEKE NILIYOKUWA NAO KWA MUDA MREFU KUTOKANA N KUWA NI MUATHIRIKA WA UKIMWI,TANGIA NIMEJIGUNDUA NI MIAKA 2 LAKINI NAKUMBUKA SIKUNILIYOPIMA NILIAMBIWA KM INAONEKANA KM NILIATHIRIKA MUDA MREFU COZ CD4 ZANGU ZILIKUWA CHINI SANA NAMSHUKURU MUNGU KWA KUNIPA UJASIRI WA KUIPOKEA HAYO MAJIBU...NAKUENDELEA NA MAISHA.
KIPINDI HICHO NILIKUWA NIMETOKA KUACHANA NA BOY FRIEND KM MIEZI 6 NIKAWA PEKE YANGU. TATIZO NINALOPATA NI USUMBUFU WA WANAUME COZ MI MREMBO TENA NINAAYEJIHESHIMU SANA NIMEKUWA NIKIWAKWEPA ZAIDI YA MIAKA 2 MPAKA NIMECHOKA.
WENGINE NAJARIBU KUWAAMBIA UKWELI KUWA MIMI NI MGONJWA LAKINI HAWANIELEWI. SONONEKO KUBWA NILILOKUWA NALO NIKWAMBA SINA MTOTO, SINA RAFIKI WA KIUME KUTOKANA NA TATIZO LANGU..JE NTAWEZA KWELI KUZAA NA MTOTO WANGU AKAWA SALAMA?NA JE NAWEZA KUMPATA BOY FRIEND MUATHIRIKA MENZANGU NA AKAWA NA MAPENZI YA KWELI .NA MWENYE UWEZO WA AKILI NA WAKUIKUBALI TATIZO NILILO NALO KM LAKE NA AWE MWENYE KUIPENDA FAMILIA YAKE? NAOMBENI MNISAIDIE MAJIBU KWAMOYO MZURI KAMA NILIYOKUWA NAYO MIMI. ASANTE NATEGEMEA MAJIBU MAZURI KUTOKA KOTE NA YENYE BUSARA.
Pole sana dada ni janga ambalo limekumba karibu kila familia hatuwezi kusema kwa nini umekuwa hivyo ila kama kweli unahitaji mtoto na mwanaume ambaye ni muathirika mwenzako kama unavyodai utampata endapo tu utakuwa wazi. wapo watu wamejiweka wazi kwa kujitangaza na wamepata wachumba na wameona kwa ndoa kabisa halali. Kuna jarida linaitwa Yaliyopita Sindwele = Femina HIP ukilipata linakueleza kila kitu
ReplyDeleteAsiwe mpweke kiasi hicho. Yeye aendelee kuwaambia wanaume ukweli, atakayekubaliana nae aendelee nae. Kuishi na mtu muathirika siyo kwamba utaathirika. Akipata mwanaume atumie nae njia zilizosahihi basi maisha yatakwenda, hata kama kuzaa mbona watu wanazaa na wameathirika lkn mtoto anakuwa mzima?
ReplyDeleteMy Lovely Sister uliyeandika ujumbe huu,nataka nikueleze kua Kuishi na Virusi Vya Ukimwi sio kwamba ni mwisho wa maisha na pia sio kweli kwamba huwezi kupata mtoto,pili nakupa hongera kwa kuikubali hali unayopitia,ningetamani sana kuwasiliana na wewe nje ya hapa ili tuweze kusaidiana na nikupe namna ya kufanya,tafadhali usiache kufanya hivyo..tumia john@ohc.co.tz Ahsante
ReplyDeleteIts possible and will happen if you give urself a chance to experience that kind of love.. na pia usisahau kuwa mume bora utoka kwa mungu muombe mungu sana atakupa yule unayemuhitaji no matter ur conditions. na pia its possible kupata mtoto asiye na maambukizi ukizingatia ushauri wa madaktari. never loose hope and courage to face this situation.. take good care of urself.
ReplyDeletepole sana kwa tatizo dada yangu ila elewa kuwa kupata mtoto inawezekana na mtoto akazaliwa akiwa hana maambukizi yoyote ila unachotakiwa ni kumtafuta mwenzako na mkikubaliana basi mnatakiwa muende mkamuone daktari na atawapa ushauri ni nini cha kufanya kabla ya kubeba ujauzito na jinsi ya kuishi na vyakula vya kula...
ReplyDeletepole dada!ni kwamba hongera kuikubali hali!kwanza kabisa elewa wewe ni binadam kama binadam wengine!na una mahitaji kama mtu mwingine yoyote!kwa miaka 2 utajiona mpweke!ushofu atatokea mtu wa maana ni mapema wala usijione umechelewa endelea kuikubali hali!!wala usisononeke kwa hilo na kama unataka mtu wa kukuliwaza ongea nae mtumie kinga!na kama unahitaji mtoto ni vema ukaenda kwenye vituo vya ushauri watakushauri vizuri kwa ajili ya kuzaa mtoto asie na maambukizi
ReplyDeletePole sana dada yangu,naomba kuchukua nafasi hii kukutia moyo katika janga kama hili.Dada yangu kuathirika sio kwamba ndo mwisho wa maisha yako,Mtumaini Mungu katika yote yeye ni faraja katika maisha yetu ya kila siku.Baba wa Yatima,na Mume wa wajane na kimbilio wa wote.
ReplyDeleteMimi kama mimi nachoona cha kufanya kwa sasa ni hiki;
Najua unatamani sana kuwa na familia kama wanawake wengine,sasa jaribu kuonana na madaktari wakupe ushauri kama inawezekana ukazaa na mtoto asiaotwe na maambukizi.lakini ukiangalia kwa upande wa wanaume wengi hawapo tayari katika hili,pia sitopenda dada yangu umtafute muathirika mwenzako then mtafute mtoto kwa pamoja kwani maisha ya mtoto wenu hayatakuwa ya furaha kama ya wengine,pia sitofurahi kama utatoka na wanaume bila wao kujua ikiwa lengo lako ni kupata ujauzito katu nakwambia utakuwa umejichumia dhambi ambazo zitakufikisha pabaya.
Suruhusho;Naomba umtumainie Mungu wetu kama Mume wako na faraja juu ya kupata mtoto,Muombe mungu kwa sana,natumai Mungu wetu ni mungu wa amani pia anasikia maombi yetu katika hili utakuja ishi maisha ya furaha sana kuliko binadamu wengine.
Pia katika swala la mtoto,dada yangu naomba ujaribu kutafuta kwenye vituo vya kulelea watoto yatima umtafute mtoto mzuri ambaye utakaye muona anafanana na matakwa yako then um adapt yani kama sijakosea umrithi kuwa mwanako,kwani swala hili ni la kawaida tena hata watu wengi may be wanaokosa watoto kwa namna moja au nyingine huwa ufanya kama hivyo.
Hayo ni maoni yangu,pia naomba kuchukua nafasi hii tena kusema kuwa usikate tamaa,yupo mtetezi weetu ambaye ni Yesu Mungu wetu.
Kind®ards
Mutalemwa baitani.
TTCL staff.
Pole sana dada yangu,naomba kuchukua nafasi hii kukutia moyo katika janga kama hili.Dada yangu kuathirika sio kwamba ndo mwisho wa maisha yako,Mtumaini Mungu katika yote yeye ni faraja katika maisha yetu ya kila siku.Baba wa Yatima,na Mume wa wajane na kimbilio wa wote.
ReplyDeleteMimi kama mimi nachoona cha kufanya kwa sasa ni hiki;
Najua unatamani sana kuwa na familia kama wanawake wengine,sasa jaribu kuonana na madaktari wakupe ushauri kama inawezekana ukazaa na mtoto asiaotwe na maambukizi.lakini ukiangalia kwa upande wa wanaume wengi hawapo tayari katika hili,pia sitopenda dada yangu umtafute muathirika mwenzako then mtafute mtoto kwa pamoja kwani maisha ya mtoto wenu hayatakuwa ya furaha kama ya wengine,pia sitofurahi kama utatoka na wanaume bila wao kujua ikiwa lengo lako ni kupata ujauzito katu nakwambia utakuwa umejichumia dhambi ambazo zitakufikisha pabaya.
Suruhusho;Naomba umtumainie Mungu wetu kama Mume wako na faraja juu ya kupata mtoto,Muombe mungu kwa sana,natumai Mungu wetu ni mungu wa amani pia anasikia maombi yetu katika hili utakuja ishi maisha ya furaha sana kuliko binadamu wengine.
Pia katika swala la mtoto,dada yangu naomba ujaribu kutafuta kwenye vituo vya kulelea watoto yatima umtafute mtoto mzuri ambaye utakaye muona anafanana na matakwa yako then um adapt yani kama sijakosea umrithi kuwa mwanako,kwani swala hili ni la kawaida tena hata watu wengi may be wanaokosa watoto kwa namna moja au nyingine huwa ufanya kama hivyo.
Hayo ni maoni yangu,pia naomba kuchukua nafasi hii tena kusema kuwa usikate tamaa,yupo mtetezi weetu ambaye ni Yesu Mungu wetu.
Kind®ards
Mutalemwa baitani.
TTCL staff.
jamani dada yangu amini usiamini kwamba unaweza ukapata mume au boy friend mweny hali kama yako naamanisha ambaye ni muathiika kama wewe na ukaweza kuzaa naye na kudate naye bila hofu yoyote lakini wataalamu wanashauri kutumia kinga pindi unapokuwa kwenye hali kama hiyo ili kuepuka maambukizi mapya na kama utakuwa tayari umeshapata mpenzi au mume see a doctor atakushauri vizuri jinsi ya kupata mimba ukiwa na hali hiyo na jinsi ya kuzuia maambukizi kwa mtoto aliye tumboni all in all never give up
ReplyDeleteunaonekana muongo muongo sana na hii stori si ya kwako wewe.
ReplyDeletepole sana,nina uhakika utakuwa unashauriwa na wataalamu,na nina uhakika kutakuwa na clinic ambazo watakupa ushauri.kuhusu kuzaa salama,mbona hilo linajulikana?utazaa salama kabisa.nchi za wenzetu nina amini dawa zao ni nzuri.kuhusu suala la kupata mtu,zipo website jaribu ku google,ambazo watu wanatafuta wapenzi ambao wameathirika kwani na wao ni waathirika.maana maisha ya ulaya kidogo ni ya upweke
ReplyDeleteyes inawezekana kuzaa mtoto yeye asiasilika mimi nina mdogo wangu kaasilika ila yeye kaolewa anamtoto wa 6 month ila inabidi uwajulishe madaktari kuna dawa wanatoa ambayo inasaidia mtoto tumboni asiasilike kuhusu boyfriend hapo ni kuomba mungu utapata usikate tamaa
ReplyDeleteDINA ZAIDI YA KUMPA POLE NA KUMUOMBEA MUNGU AZIDI KUMTIA NGUVU SINA LA ZAIDI SASA NAJIULIZA SI CHAIN HIYO JAMANI NA YULE ALIYEMWACHA ANAJIJUA? JE? KAWAAMBUKIZA WANGAPI MPAKA SASA? EHH MUNGU TUSAIDIE
ReplyDeleteREADING UK
Hello dada,kwanza pole.Naomba kukujibu kupitia experience yangu binafsi.Mie ambae pia naishi UK nimeishi na tatizo kama lako kwa zaidi ya miaka mitano.Mwanzoni ilikuwa vigumu sana lakini baada ya kupata ushauri nasaha imenisaidia mno.Nijibu maswali yako.Kwanza,maendeleo ya kisayansi kwenye kudhibiti athari za ukimwi yanaufanya ugonjwa huo kuwa kama magonjwa mengine yasiyotibika.Zamani ukimwi ulikuwa ni kifo mojakwa moja,lakini kwasasa magonjwa kama kansa,nk ni tishio zaidi (mwenye kansa anaweza kuambiwa kabisa kuwa ana miezi kadhaa tu ya kuishi,lakini kwa ukimwi kama ukizingatia masharti unaweza kuishi muda mrefu hata zaidi ya asiye na ugonjwa huo).
ReplyDeleteUnaweza kuzaa,na mwanao anaweza asipate maambukizo.Chamuhimu kabla ya kuchukua uamuzi huo inabidi upate ushauri wa kitaalamu.Kuhusu kupata mwenza mwenye hali kama yako,hilo pia linawezekana.Kuna tovuti mbalimbali za watu wenye maambukizi ya ukimwi (kwa mfano pozpersonals.com,nk).Pia taasisi kama Terrence Higgins Trust (THT) zinatoa sapoti kwa wanaohitaji dating.Labda cha muhimu (na hii naongea kwa uzoefu wangu) kama online dating ya watu wasio na hiv ilivyo na drama zake,huko kwenye hiv dating site is no different.Na huko inaweza kuwa even worse kwa sababu baadhi wanaenda huko kuondoa frustration,confusions zao.Tatizo kubwa zaidi ni mazingira ya kufahamiana na mtu unayetaka kuwa nae.Kwa mfano ukitaka kuwa na Mtanzania mwenzio inakuwa vigumu kwa kuhofia labda atakutangaza.Lakini mtu mwenye akili timamu hapaswi kumtangaza mwenzie mwenye tatizo kama lake.Ni risk lakini wakati mwingine people have to take some risks to get what they want.Ukihitaji ushauri zaidi unaweza kuniandikia willy264john@gmail.com (kama utaona inafaa kufanya hivyo).
mh pole sana dd yote ni mitihani ya mwenywezi mungu kwa kuvumilia umevumilia vya kutosha miaka miwili bila kufanya mapenzi as a human being ngumu, sijui tatizo ni moja kwamba umpate eti mwanaume ambae nae kaathirika kama itakukost utajuaje inamaana utakuwa kila unaempata unamuuliza ngumu sana dd ila unaweza kubeba ujauzito na ukazaa mtoto salama kabisa kwa kufata ushauri wa dr pole mwaya may God bless u
ReplyDeleteUKIWA NA IMANI HII INAWEZEKANA DADA
ReplyDeletemimi napenda kukushauri hivi, mana hata mimi nilipima mwaka jana nikagundulika ilikuwa jan 2011 ila nikaamua kuokoka kwa imani kwamba ntapona, sasa hivi ni MZIMA,sasa napenda nikupe baadhi ya mistari ambayo itakutia moyo na kukupeleka katika muujiza wako, Marko 11:24, Mathayo 11:28-30, Isaya 1:18-30 Isaya 43:18-19, Isaya 43:25, Maombolezo 3:31-33, 1Kor 10:12-13, 1Petro 5:6-7, Zaburi 103:3, 1petro 2:24 na Joel 3:21. pia pendelea kusikiliza mahubiri mbalimbali ya dini, na leo Jumanne saa mbili kamili usiku kuna kipindi PPR jitahidi usikilize. barikiwa sana dada na wala usihofu amini yote yawezekana kwake aaminie. Mungu azidi kukutia nguvu.
Dada, naomba nikupe hongea kwa ujasiri wako na kuendelea kujitunza. Mimi naomba nigusie swala la wewe kua na mtoto. Karne yetu hii there is more than one way to become a mother, biologically najua utataka upate mimba uzae mtoto, lakini hili litakuzorotesha wewe afya yako kwa kiasi fulani, kiasi kwamba hutokua na nguvu za kumuenjoy mwanao kivile kwa nyakati za mwanzoni. Hivyo basi ushauri wangu ni huu, kama kweli unataka mtoto wako mwenyewe wa kumzaa basi beba mimba, njia ziko nyingi sana kama (artificial insemination) sio lazima mwanaume.
ReplyDeleteIla kama shida yako ni mtoto wa kwako mwenyewe basi adopt, either huku nyumbani au huko UK lakini popote utakapopenda adopt mtoto mchanga. Nikwambie dada, mtoto ni mtoto tu as long as ni wa kwako mwenyewe, utakua na nguvu za kumuenjoy mwanao from the beginning, mungu akusaidie dada.
POLE SANA DADA, JITANGAZE KUWA UNATAFUTA MUME MWENYE HALI KAMA YAKO, NENDENI KWA MA DR. MTAELEKEZWA JINSI YA KUPATA MTOTO ASIYE NA MAAMBUKIZI. MDAU DSM
ReplyDeleteyou are so courageous to let the public know this mi nakushauri nenda clinic sijui huko ulaya kama zipo huko utakutana na watu wengi wenye hali kama yako kisha mtaanza mahusiano au waweza kuongea na madaktari wa hizo clinic nini cha kufanya na hata kukusahidia kukuunganisha na waathirika wengine kisha atakayekuvutia mtakaa na kupanga mambo yenu mkishauliwa na huyo dactari wenu
ReplyDeletehi dada nakupa imani wala usijali Mungu yupo pamoja nawe mtumaini yeye tu nawe utakuwa na amani na furaha tu ya maisha mana ukimwi ni kama magonjwa mengine tu. naomba utumie mail hii nikushauri vizuri zaidi.
ReplyDeleteMungu akubariki
furaha1984@yahoo.com
Napata wasiwas juu ya hili! Ushauri wote uliopewa na watu hapo juu ni wa kawaida huku kwetu bongo ambako habari kama hizo haziwafikii watu wengi hasa vijijini ambako miundo mbinu sio mizuri, lakini kwa level yako na nchi uliyopo sidhani kama hujui kuwa kuishii na virus sio mwisho wa maisha, naamini unajua kuwa unaweza kupata mume na mtoto na ukaishi maisha ya furaha kabisa pamoja na hilo unalosema kuwa ni tatizo.
ReplyDeleteLabda kama umetoa kama changamoto kwa sie tuliye huku dunia ya tatu?
Kwa UK you can google all challenges you have explained above and get the suggested solution.
dada pole sana,lakini huko UK kweli?maana kama mdau hapo juu alivyosema UK wapo advance sana kwenye maswala haya thou wagonjwa si wengi lakini ukigoogle utakuta kuna vyama vingi vya kuwasaidia walioathilika.
ReplyDeleteHONGERA SANA DADA NA SI POLE kwa ujasieri wako na kuwa mwaminifu kwa mwili wako, ushauri wangu ni kuwa unaweza kupata mtoto asiye na VVU endapo utaendelea kuwa muwazi kuanzia kwa mume utakaekuwa nae na madaktari utakaokuwa karibu nao. Muhimu ni kuwa kabla hujaamua kupata ujauzito jaribu kukutana na wataalam wakupe njia za kumkinga mwanao tangu tumboni tena usihofu utaweza kujifungua kwa njia ya kawaida na mwanao asipate maambukizi.Endela kuwa muwazi kwa wanaume ili atakaekubali kuishi nawe akupende kwa hali uliyonayo.
ReplyDeleteNIna mengi sana ya kuongea nawewe ila niko internet kafee laptop imekufa naomba nitafute dada kwa mail hii kadinari4@yahoo.co.uk naishi uk Hackney nitaongea na wewe kwa kirefu sana usiogope mimi ni dada na yesu anakupenda sana
ReplyDeletelovely dada,mimi ninaweza kukulead kwenye suluhisho la tatizo lako,plz mpendwa can i get ur contact?
ReplyDeleteHi Dina, naomba niweke hii mada tofaufi kidogo, ila uipe uzito mkubwa kwa Blog yako wadau waweze kuijadili. Ni kuhusiana na haya mambo ya DNA na ofisi ya Mkemia Mkuu. Kutokana na hekaheka yenu ya wili iliyopita, mbona inaonekana kutatiza, maana mimi nilifikiri DNA ni ufumbuzi mkubwa kwa wanawake kutokana na kudhalilishwa na kunyanywaswa na wanaume kwa kuwakataa watoto wao. Inawezekana kuna wanawake ambao si waaminifu, lakini linapo kuja suala la kupeana mimba, naamini ni wanawake wachache ambao wanakosa kutambua nani ni baba wa mtoto. Na mpaka mama anakuwa tayari kufanya DNA, ni wazi kuwa ana uhakika na baba mtoto. Sasa tatizo linakuja huko kwa Mkemia Mkuu, nina mashaka napo sana, nahisi kuna mianya ya rushwa, iweje mimi mama nina uhakika na baba mtoto halafu majibu yaje tofauti! Wahusika lazima wapamulike Ofisini kwa Mkemia Mkuu, na kama ni tatizo la mashine, wahusika watoe ufafanuzi. Wanawake tunanyanyasika jamani....................
ReplyDeletemnh pole sana sister wangu,yaani nakuonea huruma sana but ndo mitihani mungu aliyokwisha kuandikia so ulikua huna budi jinc ya kuiyepuka,pili nakupa hongera sana kwa msimamo wako uliokua nao zidi ya wanume,khs kupata mtoto unaweza na athiasirike,cha muhimu ukipata ujauzito tu wahi clinic na uwaeleze dr.hali halisi uliyokua nayo.
ReplyDeletePole sister kupatan ukimwi sio mwisho wa maisha yako. Na wala usiwe mnyonge kiasi hicho . Kuhusu kupata mume jaribu kwenda kwenye vitengo nya ukimwi ukawaeleze nao wanaweza kukusaidi kwa njia moja au nyingine na mume utampata na suala la mtoto halina tatizo kwa hilo atatoka akiwa mzima bila maambukizi ila muhimu kuwa karibu na watabibu (madaktari).
ReplyDeletePole sana kunakitu nataka nikushauri naomba uwasiline na mimi kwa email yangu ni tembast@gmail.com.
ReplyDeletehi, ts me deo from, ucc dar. dunia kwa kweli imebadilika, tena sana tu c kujali wenzetu tu, bali hata kujijali sisi wenyewe ni ishu tena sana tu. hiv/aids si ugonjwa bali ni hali ambayo inaweza kumtokea mtu yeyote yule, only what we fear about is when we hear that, finaly of it is death, n ni kifo chenye majonzi makubwa.
ReplyDeletebut huku kuuzoea huu ugonjwa now people tumepitiliza mpaka watu kujitoa muhanga, that dead with it its normal. madhala yake c kufa kwa mtu, but ni nguvu kazi tunayoipoteza after that death.
another thing is kwamba watu hatuaminiani pia, that even if you tell somebody that i am hiv positive, cant believe it easly. and that is a problem, seriously problem
mdada hongera for ur decision you take for seeking for the advice from other people especial through this site, n i hope you gonna get something. then i would like to say that, science and technology now dayz is increased n its continuosly increasing so things are easy. thereis no much need of looking only for the infected person, but hata mtu ambaye hajaathilrika pia anaweza kuwa wako if only ukimpenda and akakupenda and you realized that to each other. there are many means of protection which can make everyone safe in your relation, only if mkizingatia ushauri wa daktari. thanks
pole MUNGU NI MWEMA,, ATAKUSAIDIA .naona walioshauri humu wengi wameshauri vizuri, chagua unaofaa ufanyie kazi.
ReplyDeleteKwanza, pole sana dada yetu. Pili, naomba kukujulisha kuwa kuna watu wengi ambao ni HIV+ ambao wameoa au wameolewa na watu ambao pia ni HIV+ kama wao. Tatu, nimewahi kusoma mahali kuwa, kwa watu wanaotumia ARVs, uwezekano wa kuzaa mtoto ambaye hajaathirika (percentage probability)unaongezeka. La muhimu kuliko yote, mtegemee Mwenyezi Mungu mwenye uwezo juu ya kila kitu. Usiwe mpweke, nenda kwenye mitandao/mikusanyiko ya waathirika ili upate mwenzako ambaye mtaelewana naye na pata ushauri wa madaktari na washauri nasaha/counsellors. Hemedi.
ReplyDeletePOLW SANA MY SISTER,NATAKA NIKUPE HONGERA KWA KUPIMA NA KUKUBAKLI MAJIBU YAKO,MSHUKURU MUNGU KWA YOTE NA KIKIBWA NI KUNYWA DAWA NA KUFUATA USHAURI NASAHA,MBONA WENGI TUNAISHI NA MAGONJWA MAKUBWA KM KISUKARI NA BP NA TUNATUMIA DAWA KILA SIKU?KIKUBWA NI KUPIGANIA UHAI WAKO UENDELEE KUWA NA AFYA NJEMA KWA SIKU MUNGU ATAKAZOKUJALIA HAPA DUNIANI,UPAT MUME UOLEWE NA UZAE WANAO WENGI..PIA KUNA WATU WENGI WANASEMA WAMETUMIA DAWA ZA UKIMWI NA WAMEPONA,SO DONT GIVE UP,UKIPATA UTHIBITISHO WA TU ALIYETUMIA DAWA ZA KIENYEJI NA KUPANA GO AND LOOK FOR IT
ReplyDeleteKILA LA HERI
hongera sana kwa kupima afya dada hapo ulipo ndio unanafasi nzuri zaidi ya kufanya maisha yako kuliko sisi ambao hatuja pima bado .uwezo wa kuwa na mtoto ambaye hatapata maambukizi upo kabisa swala wa kuzaa nae mwachie mungu sali kwa moyo na imani utampata wako peke yako .nakupenda na hongera sana.
ReplyDeletepole.sana dada tupo wengi .toa emal yako tukusaidie .please.nipo sweden
ReplyDelete