Friday, March 23, 2012

HAPPNESS MILLEN MAGESE ALIKUWA MJENGONI LEO

Alishakuwa miss Tanzania mwaka 2001.Akaenda Afrika kusini kimasomo na akapata deal ya modeling akafanya kwa miaka 6 baada ya hapo akahamia Marekani na ndio yupo huko kwa miaka 2 sasa.
Leo alikuja hapa mjengoni ofisi za clouds fm.
Akizungumza na Dj Venture na Boniluv Kilosa.
Akiwa na Ruge Mutahaba.
Baadae tulizungumza nae kwa kirefu katika leo tena.Kubwa lililomleta ni kwamba,kupitia kampuni yake amekuja kutafuta mamodel wawili wakitanzania ambao anataka kuwatafutia soko la kimataifa.
Kwanza watashiriki katika onyesho la mavazi litakalofanyika Afrika kusini linalotambulika kama South Africa fashion week tarehe 1st April.Tukio hilo kufanyika Serena hotel jumapili ya tarehe 25 kuanzia saa nane mchana mpaka saa kumi na moja jioni.Ni kwa wale wenye miaka 18 mpaka 24.
Anasema mpaka sasa amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani baba yake alipofariki miaka mitatu iliyopita alimuachia jukumu la kuwalea wadogo zake.Anasema hajatoka katika familia bora toka anaenda Afrika kusini miaka 8 iliyopita ilikuwa kama zali maana maisha yalikuwa magumu.Baba alikuwa amepata stroke anaumwa uchumi umeyumba hivyo alitakiwa kusimama kupambana na maisha maana yeye ni mtoto wa kwanza.Baba alipofariki alihakikisha anachokipata kinasaidia familia yake kwanza amesomesha wadogo zake wapo chuo sasa na anamtunza mama.Ndio maana alikuwa kimyaa bila kujishughulisha sana na mambo mengi ya kijamii au kuinua wengine katika upande huo wa modeling.Sasa amekuja rasmi maana malengo yake ameshatimiza hilo la FAMILIA yake kwanza.
Ukiacha modeling anapenda na ana kipaji cha kuimba.Bado hajaolewa na wala hana mtoto anasema muda ukifika atatufahamisha kwani bado anajipanga zaidi kimaisha.Tuliongea mengi sana ila haya ni kwa uchache.

20 comments:

  1. Hongera mamie kwa kupendeza! Ukweli umejaaliwa, shepu yako, shingo yako, rangi yako. Yaani nakupendaga!

    ReplyDelete
  2. love u happie,u are myrole model katika urembo

    ReplyDelete
  3. katika ma misss wote Tanzania huyu dada nampenda sana,ila kuna fununu etiii ni hawala wa rais mstaafu mkapa.

    ReplyDelete
  4. Kiukwel da dina happy ni mfano mzur wa kuigwa c kila cku skendo ziczo na maana mi ni hayo 2u mamy

    ReplyDelete
  5. rangi yake bana c ya kitoto.

    ReplyDelete
  6. jamani dina mimi ni model but vitu vingi vinanikwamisha kiasi kwamba nahisi fan yangu inapotea. unaweza kunisaidia nionane nae ili anipe ushauri na chance, hata nikipata mdhamini itakua vizuri.

    ReplyDelete
  7. jamani! mbona mnapenda kuongea mambo yasio wahusu? kama hawara yake ww ulikua unatakaje?

    ReplyDelete
  8. jamani da dina,huyo upande wa pili wa maisha anajisahau.mpaka leo hajaolewa na hana hata mtoto!!!akumbuke umri unasonga (usiku unabisha hodi)ooooh

    ReplyDelete
  9. nakwambia iyo ngozi c mchezo nyurtiiiiiiiiiiiiiiiiiiii co za kina mwafulani mabaka yamikorogo tehe tehe

    ReplyDelete
  10. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  11. Hongera Millen kwa kukumbuka wengine, nafikiri umepata "wake up call" ulivyokuwa mgonjwa, mpaka umekumbuka na wengine, maana wengi tu wanashida na wanasaidia kote kote kwenye familia na kwenye jamii, kwani huwezi kukamilisha kote kote lazima shida za familia zipo tu kama sio nduguyo basi cousin atahitaji msaada wako. Anyway hujachelewa bado!

    ReplyDelete
  12. Mambo Dina, Mimi namtakia kila la kheli katika fani yake ili aweze kuwasaida wadoga zake pamoja na mama yake
    Kaza buti mtu wangu mungu atakusaida.

    ReplyDelete
  13. sor da dina naomba nikukosoe,labda ulimckia vbaya da happy aka millen ila ukwel ni kwamba millen c mtoto wa kwanza kwao yy n wa pili wa kwanza anaitwa ''GRACE''.
    ila apart 4rm dat millen anajitahid sn ktk professional yake,lv u millen n kip t up dearest!!!

    ReplyDelete
  14. Dah....mtoto shoo!rangi ya jogoo,ntapata wpi kama huyu. Inbox me

    ReplyDelete
  15. Mtoto shoo!rangi ya jogoo mfano wa kuigwa,jamn ntapata wpi rngi adimu hi inbox me. Bobsule@gmail.com

    ReplyDelete
  16. Mtoto shoo!rangi ya jogoo mfano wa kuigwa,jamn ntapata wpi rngi adimu hi inbox me. Bobsule@gmail.com

    ReplyDelete
  17. Mtoto shoo!rangi ya jogoo mfano wa kuigwa,jamn ntapata wpi rngi adimu hi inbox me. Bobsule@gmail.com

    ReplyDelete
  18. kama sikosei kuna kipindi nilisikia amechumbiwa tena kwa pete ya almasi ya gharama sana, viliishia wapi?

    ReplyDelete
  19. sasa ukisikia kioo cha jamii ndio hawa akina Millen, ni mfano wa kuingwa hp mamiss wote wangekuwa na tabia kama yake fani hii isingechukuliwa vibaya kama ilivyo kwa sasa

    ReplyDelete