KUTOKA KATIKA WALL YA GODFREY LUGALABAMU....ANASEMA...
Huyu Dogo leo ka2chekesha sna ndan ya Daladala..nimemuhoj kwann Haendi shule badala yake anafanya bznes tym hii?chek alichojibu kwa kujiamini!"Mi jembe ww nkafanye nn class.kwanza unatakiwa unipongeze dogo kama mm nna ofisi alaf mm ndo Boss wkt kuna kubwa zima linaomba au kuiba..Kwa taarifa yako mm nasoma ELIMU YA MTAA.na sasa hvi niko form2 we cmpaka upelekwe na kuludishwa na basi ktoka shule ala...f getini utanipata ww?Biznes yangu hii inamwaka nauza nlianza kwny mifuko,sahani,cnia sahv kwny sanduku umu vnajaa na vnaisha..cha msingi nyie nlindeni life liendelee..Mi nayajua maisha cku ntakayo pata degree otea ntakuaje..aya nunua basi!?"..ckua na swali lingne zaidi ya kununua kikeki na abiria wengine wakanijoin huku wakicheka sanaaa..EM NIPE MTAZAMO WAKO MDAU JUU YA HILI NB:dogo hana wazazi wote!!
WACHANGIAJI NAO WAKASEMA
Sima Kazaura:OMG! sikulijua hilo!! ok! nimekusoma sasa maybe ndio maana anabehave hivyo alivyo..May his parents souls rest in eternal peace..Amen!!
Hemed Mollel :Inaonekana huyo dogo hana mfadhili wa kumpeleka shule! Isitoshe inaonekana anatoka katika jamii isiyojua umuhimu wa elimu, nikiwa na maana kuwa watu wake wa karibu wanaona sawa tu. Hebu fikiria kama ndivyo hivyo ni nani atakayemhurumia? Siku hadi siku mawazo yake yataendelea kudumaa. Labda atokee mtu wa karibu naye amhudumie na kumpeleka shule.
Abraham Kattaza :Huyu dogo mara nyingi hua nakutana nae maeneo ya ferry,akija kauli yake ya kwanza ni "nunua bagia maisha magumu" halafu utasikia" maisha ni kutafuta na sio kutafutana" amechangamka kupita maelezo na akija kwenye gari yako hata kama unasinzia lazima utaamka kwa sauti yake kali. All in all kila mtu ana njia yake ya maisha japo shule ndio njia inayoonekana kua bora zaidi kwa walio wengi.na wafanya biashara siku zote ndio watu wenye pesa kuliko hata watu walio maOfisnini,maadamu dogo anatambua hadi hatua alizopitia na anajivunia mafaninikio ya kukua kwa biashara yake usishangae nae siku moja akawa na viwanda vyake kama bakhressa.
Samwel SQ Willago: Mbona kuna jamaa miaka minne iliyopita alikua anatembeza tishet za kiume kwa mtaji wa 10000 mpk sasa ana maduka mawili ya kisasa ya nguo za kike...niamini mimi mitaa inashukurani sana ukiiheshimu na kuitumikia..kuliko miaka 40 kazini alafu miaka 10 mbele unarudi kwenye umaskini tena.....@all
Charles Chamberlain Nasikitika sana kwa hali kama hii ya kutokujitambua. Hakuna kujitambua,na hakuna akili nyingi,wala mafanikio ya baadae,Mtoto huyu hajitambui,hatambui anachopaswa kufanya kwa umri wake,hajui haki zake,sisi kama wazazi ni jukumu letu wote kupiga vita ajira kwa watoto na hata kujiajiri,tupigane kutetea haki zao kwa faida ya maisha yao ya baadae,hata kama mtoto mlengwa ni yatima.Hayo majibu aliyotoa ndio athari za kutokujitambua.Ni mawazo tu.
HAYA NI BAADHI TU KATIKA MAONI 76 YALIYOKUWEPO!

Mi nakushauri Dina mfanye huyu kijana aweze kutoka, najua unaweza kama ukiaamua kwani kuna kijana ulishawahi kumpigia debe akatoka na shule akaenda na mahitaji yote akapata kutoka kwa wadau wako.Pse mtafute msaidie kupitia leo tena na blog yako, nahisi ana akili huyo mtoto na anajitambua shida aliyonayo ndo maana anakuwa mbunifu wa kuvutia wateja wa bihashara yake kuliko kwenda kuomba omba au kulelewa kwa watoto yatima. ukim intervew unaweza kujua kipaji alichonacho na namna gani ya kumsaidia.
ReplyDeleteHUYU DOGO MASKINI INAELEKEA AMEKATA TAMAA YA KUWEZA KUSOMA THAT WHAY ANAJIPA MOYO KIVYAKE VYAKE... NDIYO MAISHA YA BONGO SASA TUFANYAJE....
ReplyDeleteMbona hiyo daladala kama siyo ya bongo hivi?
ReplyDeleteMimi ndo Godfrey Rugalabamu nlie Post hyo info da Dina..kama vipi naomba uifanyie muendelezo ikiwezekana tukawa sehemu ya mabadiliko katika kusaidia hawa watoto pa1 nakuipa changamoto serikali.mimi nashukuru kwa kuichagua kushare na wanajamii ..Nimatumaini yangu haita ishia apa kama alivyoomba mdau aliyepita.
ReplyDeletewe nawe eti sio ya bongo ya wapi sasa tatizo mwapenda kuwaza negative tu
ReplyDeletehuyo mdau alopita kama nimemuelewa vizuri ni kama anajitoa katika kusaidia jamii ikiwemo huyo baby boy (yah ni baby coz kama angekuwa ktka familia bora angekuwa anapelekwa shule na dada au na school bus. kabla ya kutaka dina atoe support wewe mdau na mimi nikiwemo tumefanya nini? dina atafanya yote? kupost tu amefanya kitu kikubwa. tujufunze kujua wajibu wetu. mtoto hana wazazi lakini je hana ndugu hata mmoja wa kumpa elimu ya kujitambua na kumpeleka shule hata kwa kuchanga? kila mtu angekuwa anatimiza wajibu wake watoto kama hawa wangepungua mtaani kama sio kutokuwepo kabisa. unakuta mtoto hajarudi home hadi saa 2 usiku wazazi hawajali, kesho haendi shule hawajali, keshokutwa anaingia mtaani hawajali pia na ukimuuliza anasema sasa mie nifanye nini mtoto hasikii> please wazazi tujitahidi ni kazi ngumu lakin ni wajibu wetu. Da J (Mamy)
ReplyDeletenakuomba usibanie comment yangu kwani leo nimepata pa kuanzia, ni kweli kabisa dogo hajitambui na pia anajua kuwa anachokifanya sio sawa ila anajipa moyo kwa kauli anazozitoa ili kuhalalisha anachokifanya. dogo anahitaji msaada awezeshwe atoke huko alipo suala la ku win bila darasa tusilipe nafasi, wasiojitambua hapa nchini wako wengi wakiwemo baadhi ya watu wenye majina makubwa tu hapa nchini, niliwahi kumsikia mtnagazaji wa kipindi cha wanawake live akitetea hoja yake ya kuwin kimaisha bila kusoma kweli nilishtuka na nilipiga marufuku kipindi hicho kisiangaliwe kwani angeniharibia watoto ambao nakosa usingizi kuwatafuta ada halafu leo atoke mtu alikotoka na kutetea upuuzi, ni kweli kwangu ni upuuzi, mtu anajaribu mpaka kutoa mifano ya kina Bill Gate, je ni kina Bill Gate wangapi tunao hapa tanzania ni wazi kuwa kwa nchi zetu mifano kama hiyo ni adimu ingawa ipo lkn swala la elimu ni lazima lipewe kipa umbele. ushauri: nadhani dogo tunaweza kumtoa huko aliko lkn kwanza pate counseling ajitambue ajue haki zake kama mtotona wajibu na majukumu yake katika jamii.
ReplyDeleteUnajua sisi binadamu (Watanzania) huwa tuna hurka moja , yakuwa kila tunachokifanya sisi na kukiamini basi unataka kila mtu lazima akifanye hicho hicho sababu tu wewe umefanikiwa kufanya hivyo.
ReplyDeleteSijui kama nitakuwa nakosea ama la. Watanzania itabidi tubadili tamaduni na mtazamo wa maisha kwa ujumla. Sababu inayonifanya niseme hivyo ni kuwa, kama utaangalia kwa Tanzania tunavyofahamu sisi ukiwa na elimu basi utafanikiwa kimaisha. Tumekuwa wasahaulifu wa kuwa ukiwa na malengo, nia, juhudi na maarifa utafanikiwa (Ujasiliamali). Elimu inaweza kuwa ni formal au informal na ukafanikiwa.
Huyu dogo kwa maelezo yake mafupi tu ni intellegent sana sababu kwa alichosema ni pure entrepreneurial consciousness mind (Survival of the Fittest). I am so sad when someone said that education is the only way to come through......
We are very naive to use education as the only way to a success. I have an opportunity to read so many books about wealthy individuals in this world. You will be suprised how little formally educated.
Nitakupa mfano wa Richard Branson, Virgin group owner. Jamaa hana elimu kutisha, ni elimu ya msingi tu ya kusoma na kuandika. Aliaacha shule na kuanza kufanya biashara akiwa na miaka 15 tu. Na kuna wakati biashara yake ilivyokuwa inakuwa akaona sababu hana elimu ya kutosha ya biashara ngoja awape watu waliosoma ili waiendeshe biashara yake. Tabiri nini kilichotokea? biashara ikaanza kuyumba ikabidi airudishe kwenye umiliki wake mwenyewe na ona ilipo Virgin sasa.
Huyu dogo what he need is support from good wishers and not to distract from his vision.
I would like to meet this boy one day. He is an inspirational to me. Keep going young man I will even add few bobs in your venture to support your vision.
Kuna siku nilikutana hapa ughaibuni na mzee mmoja ni Mtanzania. Amekaa hapa kwa muda wa miezi sita tu alikuja kutembelea familia yake. Katika mazungumzo yetu nikawa namuelezea nachofanya hapa kwa sasa na kielimu nilipofikia na malengo yangu ya baadae. Katika yale mazungumzo yote kuna hili neno alisema na sitalisahau maishani mwangu. " Katika nchi hizi elimu si lazima uende shule tu. Kwa niliyojifunza kwenye kipindi hiki kifupi hapa kitaleta madiliko makubwa kwenye maisha yangu mafupi yaliyobaki hapa duniani. Ule msemo wa Tembea uone hapa ndiyo umedhihilika". Huyu mzee amesoma na ameshika nyadhifa mbalimbali serikalini ila hakuwahi kukaa nje ya nchi kwa muda mrefu kama huo. Hii ni informal education.
Mdau ughaibuni
Buckinghamshire, Virgin Island.
Dogo anahitaji msaada mkubwa sana, majibu aliyoyatoa ni kweli ya mtu aliyekata tamaa, Je, ktk nchi hii ni nani mwenye wajibu wa kumrudisha kwenye mstari hapo inaonyesha familia iliyobaki wameshindwa au ndo wanaochangia hilo, Je serikali haina kitengo kinachoweza kuingilia kati kumpatia msaada wa kisaikolojia, arudi shule na uhakika wake wa kula na kulala usingizi bila ya nightmares za kuwa kesho atakula nini?!
ReplyDeletemdau wa buckinghamshire safi kabisa unajua watu na hasa watz wao wanafikiri kusoma mavitabu basi ndio kufanikiwa wakati mafanikio ni kutenda zaidi kuliko kusomasoma makaratasi,zamani miaka ya 60 mpaka 85 kulikuwa na mzee mmoja yeye alikuwa anauza ugolo basi watu wanamshangaa akasomesha watoto wake mpaka chuo kikuu watu wanashangaatu sasa nilichotaka kukisema watanzania wanatabia ya kukatishana tamaa sasa huyo dogo yuko kazini na lugha ya biashara anayo watu ee mara shule mara sijuinini.... wakati mtu yuko kwenye pratical yenyewe...
ReplyDeletehuyo dogo yupo kazini nyie fanyeni nae mchezo,ni shombo sha dora icho.....
ReplyDeletesasa huyo muuza ugolo alisomeshea nini watoto wake mpaka chuo kikuu wakati elimu sio muhimu si angewarithisha biashara ya ugolo na wao waendeleze urithi? na wewe uliytoa mifano ya kina Richard Bronson uliweza vp hata kusoma hivyo vitabu na na ukatoa mifano wakati hata elimu ya awali huna, na uzungu mwingi ulioutumia ni dhahiri wewe ni msomi hata kama secondary kinachozungumziwa hapa ni kuwa huyu dogo hana elimu ya awali je na tumuache aendelee na biashara yake, wako kina bakhresa wametoka lkn mbona wameajiri wasomi kusimamia biashara zao na ni wazi kama nagebaki yeye kama yeye bila wasomi tena expert sidhani kama Bakhresa angefika hapo, katika nchi zetu elimu bado ni ufunguo pekee. na ikitokea mifano kama uliyoitoa hapo basi ujue ni wizi wa mali ya umma, ufisadi na ujambazi ndio mtu anafanikiwa. sisi bado dunia ya watu tusiige.
ReplyDeleteNaweza kukubaliana na wewe na bila kutokukubaliana. Mfano wa Bakhresa uko sawa kabisa haujakosea. Lakini ulitakiwa ujiulize maswali kwanza kabla ya kutoa mfano wa Bakhresa? Je kama angeshurutishwa au kusukumwa na watu aache alichokuwa anakifanya ili aende shule unadhani angefika alipo sasa? Je wale waliosoma wangewezaje kuajiliwa na Bakhresa kama angeacha alichokuwa anafanya na kwenda kutafuta elimu ya darasani?
DeleteMtazamo/muono wa Bakhresa kibiashara umewezesha watu kupata ajira na analipa serikali kodi. Hivyo anasaidia uchumi wa Tanzania kwa namna fulani. Na hilo ni jambo zuri la kushukuriwa na kuigwa.
Pili nakuja kwenye "uzungu mwingi" hapa ndugu yangu mbona unaonyesha udhaifu. Lugha inahusiana nini na kuelimika au kuwa msomi? Unajuaje labda nimekulia ughaibuni na nina elimu ya kusoma na kaundika tu. Sikujua kama bado tuko dhama zile zile za anayeongea Kingereza amesoma???
Tatu, kama umesoma sentesi yangu vizuri usingejaanzisha haya yote. Nimesema si kuwa na elimu peke yake ndiyo utafanikiwa kimaisha. Nilikuwa nina maana yakuwa kama unataka kusoma nenda kasome kama huyu kijana anataka kufanya biashara basi anahitaji msaada ili afikie malengo yake. lakini mkianza shule! shule! shule! mnakuwa hamtendei haki.
Juhudi na maarifa ndizo zimenifanya nijue ninachokiongea na siyo elimu yangu ya msingi niliyokuwa nayo. Lugha ya Kingereza niliyotumia imetokana na mazingira yaliyonizunguka na wala siyo usomi bandugu. Kwani kusoma vitabu mpaka uwe msomi??? Nasoma vitabu kuongeza upeo wangu, kujua yanayojili na yaliyopita.
Kuna wangapi wamemaliza vyuo vikuu hawajui hata kutengeneza sentensi si Kiswahili wala Kingereza? La mwisho ningependa kukuuliza mbona wale walioajiliwa na Bakhresa hawana mafanikio kama aliyokuwa nayo mwajili wao? Kwanini kama wanavipawa na utashi wa biashara wasianzishe za kwao?
Najua unachotaka kujibu kuwa hawana mtaji. Je Bakhresa alikuwa na alipoanza biashara yake? Je nini kinaanza kabla ya chenzake IDEA au MTAJI? Na kama IDEA kwanini wasianze kama alivyoanza Bakhresa? Kama mtaji mbona Bakhresa ameanza bila mtaji?
Unapoweza kuwa unajiuliza maswali magumu wewe mwenyewe utagundua ya kuwa:MALENGO,JUHUDI, MAARIFA na NIA ndiyo mafanikio ndugu yangu.
Nimeaamua kuacha Kingereza ili nisionekane msomi sana.
Mdau ughaibuni
Buckinghamshire, Virgin Island
mdau naona unajichanganya kwani shule ni mpaka uende darasani? ninavhyojua dogo kama akilazimishwa kwenda shule kama hana interest itakua ni kazi bure, na ndio maana basi tukawa hata na shule za ufundi stadi n.k ambapo ungefahamu kuwa pamoja na idea alizonazo dogo bado anahitaji muongozo ambao kwangu mimi naona ni elimu, inawezekana kabisa huko uliko hayo uliyoyasema yanawezekana, Vp hapa kwetu wakati hata haki yako ya msingi inabidi uinunue, nina imani ukiwa na upeo wa elimu utaitetea.tukirudi swala la Bakresa umesema alianza bila mtaji sasa hilo sijui linawezekana vipi ningefurahi sana kupata darsa kutoka kwaoe kwani inaelekea unauhakika na unachokisema ukweli mimi nina ndoto, Idea nguvu na maarifa lkn nakwamishwa na vitu vingi la msingi ikiwa ni mtaji.tukirudi kwenye sualal la lugha kuwa kipimo cha elimu kwangu hilo halina nafasi kwani kuna vijana kule zanzibar wanafanya kazai kama Tour guides wanaongea kiingereza, kitalino na kifaransa utadhani wamezaliwa huko. na hawakusoma ila huwa najiuliza je wangejendeleza si wangefanya kibiashara zaidi kuliko kuridhika na kipato cha siku hiyo tu. mdau mimi sijui ila kwangu nasimamia usemi wangu bado elimu naipa nafasi lkn pia niko tayari kujifunza kutoka kwako.
ReplyDeleteNashukuru kwa kuchukua muda wako kujibu hoja zangu. Ila hapa naona tutakesha bila kuelewana. Naona nitumie ujumbe wako kama muongozo wa kujibunhoja zako na kama ifuatavyo: Ila samahani kwa kutumia herufi kubwa ili kuweza kutenganisha uliyochangia wewe na ya kwangu mimi.
Deletemdau naona unajichanganya kwani shule ni mpaka uende darasani? HAPA SIJAKUELEWA UMEULIZA NINI KAMA UTASOMA MICHANGO YANGU TANGU KUANZIA KULE JUU NTAONA NIMESEMA SHULE INAWEZA KUWA YA DARASANI AU YA MTAA.
ninavhyojua dogo kama akilazimishwa kwenda shule kama hana interest itakua ni kazi bure, na ndio maana basi tukawa hata na shule za ufundi stadi n.k
YEYE HII SHULE YA UFUNDI STADI ITAMSAIDIA NINI WAKATI MWENYEWE KWENYE MAELEZO YAKE ANATAKA KUFANYA BIASHARA YAKE IKUWE.
ambapo ungefahamu kuwa pamoja na idea alizonazo dogo bado anahitaji muongozo ambao kwangu mimi naona ni elimu, inawezekana kabisa huko uliko hayo uliyoyasema yanawezekana, Vp hapa kwetu wakati hata haki yako ya msingi inabidi uinunue, nina imani ukiwa na upeo wa elimu utaitetea.NDIYO MAANA NILISEMA MWANZO HUYU DOGO ANATAKA MSAADA KUTOKA KWA WAPENDA MEMA NA SI VINGINE.
tukirudi swala la Bakresa umesema alianza bila mtaji sasa hilo sijui linawezekana vipi ningefurahi sana kupata darsa kutoka kwaoe kwani inaelekea unauhakika na unachokisema KWENYE MCHANGO WANGU MIMI SIJASEMA BAKHRESA AMEANZISHA BIASHARA BILA MTAJI. ILA NIMEULIZA SWALI HIVI; JE BAKHRESA ALIKUWA NA MTAJI ALIPOANZISHA BIASHARA YAKE? SASA ULITAKIWA WEWE NDIYO UKAFANYE UCHUNGUZI WAKO UJUE ALIANZA VIPI BIASHARA KABLA YA MIMI KUKUPA JIBU LA SWALI NILILOULIZA.
ukweli mimi nina ndoto, Idea nguvu na maarifa lkn nakwamishwa na vitu vingi la msingi ikiwa ni mtaji.tukirudi kwenye sualal la lugha kuwa kipimo cha elimu kwangu hilo halina nafasi kwani kuna vijana kule zanzibar wanafanya kazai kama Tour guides wanaongea kiingereza, kitalino na kifaransa utadhani wamezaliwa huko.KAMA HUO NDIYO MUONO WAKO ILIKUWAJE UKASEMA KUWA "NA UZUNGU MWINGI ULIOTUMIA DHAHIRI WEWE NI MSOMI"
na hawakusoma ila huwa najiuliza je wangejendeleza si wangefanya kibiashara zaidi kuliko kuridhika na kipato cha siku hiyo tu. mdau mimi sijui ila kwangu nasimamia usemi wangu bado elimu naipa nafasi lkn pia niko tayari kujifunza kutoka kwako. NAKUBALIANA NA WEWE KUIPA ELIMU NAFASI LAKINI SIYO NJIA PEKEE YA WEWE KUFANIKIWA KIMAISHA. HII INATOKANA NA MATAKWA YA MTU TU. KUNA WENGINE HAWATI KUWA NA UWEZO KIFEDHA ILA WAWE NA UWEZO WA UFAHAMU MAMBO MABLIMBALI. HUYU DOGO YEYE ANATAKA KUENDELEZA BIASHARA YAKE IFIKE ANAPOTAKA YEYE SABABU ALISEMA HIVI "HAPA NIKO FORM TWO JE NIKIFIKA CHUO KIKUU NA KUHITIMU" SASA HAYA MANENO INAONYESHA HUYU DOGO ANA MALENGO YAKE. SIYO MPAKA AKWAMBIE NATAKA NIWE KAMA MENGI AU BAKHRESA NINI MWENYEWE UNATAKIWA KUUMIZA KICHWA ILI UPATE KUJUA.
LA MWISHO NDUGU YANGU KAMA UNAKWAMISHWA NA VITU VINGI KWENYE IDEA YAKO BASI MAARIFA HUNA NA SAMAHANI KUSEMA HIVYO SABABU HUO NDIO UKWELI WENYEWE.
KAMA NIKO MBAGALA NA NATAKA KWENDA KARIAKOO NITATUMIA JUHUDI NA MAARIFA KUFIKA KARIAKOO HATA KAMA NAULI SINA. NITATEMBEA, NITAKIMBIA, NITAOMBA NAULI AU RIFTI ILI MRADI NIFIKE KARIAKOO SABABU NIMEDHAMILIA.
AHSANTE NA SAMAHANI KWA KUTUMIA HERUFI KUBWA, PIA KAMA KUNA LILIOKUUDHI NAOMBA UNISAMEHE NDUGU YANGU WALA SIJAKUSUDIA.
KAMA UNAONA KUNA KITU NAWEZA KUKUSAIDIA WALA USISITE KUNIULIZA. MIMI HUWA UKINIULIZA SWALI NINAKUWA NAFURAHA YA KUKUPA MBINU ZA KUJIBU SWALI BADALA YA KUKUPA JIBU. SIKU NYINGINE NITAKUELEZA NINA MAANA GANI.
Mdau Ughaibuni
Buckinghamshire, Virgin Island
kituo kikubwa chake ni pale ferri.kiukweli isku ya kwanza kumuona niliona huruma sana nikiwa na mimi ni mzazii.lakini nilikuja kujua mtoto huyu mazingira anayotoka si mazurii..maana analugha chafuu, yaani(matusi)kwa mfano siku 1 alikuja ktk gari yetu akanikuta nikiwa nasubiria boti nimesinzia...aliongea vitu vibaya sanaa.huku akimwambia mr etii nauza gongo..mnunulie alewe vizurii,binafsi nimetokea kumchukia.mitusi yake...
ReplyDelete