Monday, March 26, 2012

WAPO WATOTO WA MITAANI WAMEAMUA KUACHA FAMILIA ZAO NYUMBANI NA KUINGIA MTAANI...ZIPO SABABU NYINGI.

Ulisikiliza leo tena jana?katika hekaheka?juu ya mtoto Lulu ambae aliokotwa Mwananyamala kwa manjunju na kusema kuwa mama yake alimuacha hapo na kumwambia anaenda sokoni.Lulu ana miaka 8 na anasoma darasa la kwanza.Baada ya kuokotwa watu hao akiwemo Gea walijaribu sana kutaka kumpeleka kwao bila mafanikio.Tukasikia story yake na baadae mama yake mzazi kuja ofisini na mimi kumpeleka hewani studioni.Alisema Lulu ni kawaida yake kukimbia nyumbani nikamuuliza kwa nini akajibu ''ni mjeuri tu na pia huwa ni muongo muongo''niliuliza maswali ambayo mama kama mama alikuwa akieleza kuwa ni kawaida yake hata wakati wakiishi Moshi.Lulu kabla ya kuanza kuishi na mama yake alikuwa akiishi na bibi yake mwaka juzi mama yake akamchukua na kuanza kuishi nae hukohuko Moshi.Mwaka jana mwezi wa 12 wakahamia hapa Dar.Baada ya mimi kuona mama ameshampata mtoto nikamwambia Gea ampeleke mama amchukue mwanae huko kwa mjumbe.Na nikamwambia akifika huko aangalie kwa makini reaction ya mtoto akimuona mama yake.
Usiku nikampigia simu Gea kujua kulikoni akasema Lulu alipomuona mama yake alilia kama kafiwa.Akamwambia mjumbe hataki kurudi nyumbani anataki kubaki na mjumbe.
Nina maswali mengi kichwani kwa nini Lulu hataki kurudi kwao kwa baba na mama?Mtoto wa maiaka 8 wa kike bado ni mdogo sana kukimbia nyumbani.Kwa nini yupo radhi ahangaike mtaani kuliko kukaa nyumbani?
 Geana mjumbe wakakubaliana Lulu abaki kwa mjumbe.Nika mwabia na mama Lulu aje leo kwenye kipindi.Unajua kwa nini?Lulu wakati anaogeshwa juzi kwa mjumbe kuna kitu kiligundulika katika mwili wake.Sikiliza leo tena leo.

21 comments:

  1. Daaaah Mwenyezi Mungu atunusuru na watoto wetu.

    ReplyDelete
  2. Hey Dina! Tunaomba yale atakayoyaeleza Lulu kt leo tena tujulishwe hapa kwenye blog yako maana wengine muda wa hicho kipindi tupo maofisini hatuwezi kusikia. Nazungumzia huo ugunduzi katika mwili wake. Tafadhali tujulishe maana inavyoelekea mama yake Lulu alimfanyia kitu kibaya mtoto ndo maana hataki kurudi tena kwao.

    ReplyDelete
  3. N i kweli dada Dina, tunaomba kila kitakachoongelewa leo kwenye leo tena kuhusu huyo mama na mtoto wake utujulishe kwenye hii blog yako nzuri, maana wakati kipindi kinarushwa hewani kuanzia saa tatu mwajiri anakuwa naye anabana mbavu upande mwingine, kusikiliza inakuwa vigumu, haiwezekani kabisa. Wamama tuna kazi sana na hawa watoto wetu kama tusipoweza kuzuia hasira zetu na tunajisahau kwamba mwisho wa yote watoto wetu wanategemea sana kujifunza toka kwetu kwa kila tunalowafanyia, tunahitaji kutumia zaidi hekima na busara zetu katika kukabiliana na haya yote

    ReplyDelete
  4. Sawa mnawasaidia sana watoto kwa kuwaokoa kwenye makucha ya hao manyang'au, lakini mbona hatusikii chochote kuhusu hatua za kisheria zilizochukuliwa juu yao? Au TZ hakuna sheria za kulinda watoto? Mfano yule mama alimdefile mwanae yawezekana mpaka leo anadunda aendele kuwapedophile watoto wengine.

    ReplyDelete
  5. jamani wamama mbona tumekuwa na roho mbaya hivyo kweli,mimi bado sijabarikiwa mtoto lakin jamani napata masha uchungu ninaosika wamama wakiadithia kila mtu kwa style yake kweli ni uchungu au utamu mbona tuwe wakatili kwa wanetu,na hakika lazima ipo sababu kubwa tena kubwa huyo mtoto kukimbia nyumbani kwao na kumkataa mama yake,tena mama mzazi mbona bora angemkataa baba,lakin si mama jamani.jokinda

    ReplyDelete
  6. Dina machozi yananitoka, hata mimi nina mtoto mtundu sana tena sana yupo darasa la tatu bt huwa natafuta njia za kumpa adhabu siyo kumpiga kila siku, naweza kununua kitu kizuri ambacho najua anakipenda simpi basi mwenyewe tu anabadilika siyo kumpiga hadi atoke alama.

    Roho inaniuma sana na laiti ningekuwepo hapo naapa ningempa kipigo huyo mama na nipelekwe segerea. Amesahau uchungu wa labour huyo mwanamke jamani.

    Dina kiukweli huyo mama asipewe huyo mtoto na ikiwezekana tumuombe huyo mjumbe abaki na Lulu jamani hata wakaandikishe polisi.

    Roho inaniuma sana tena sana na tumbo la uzazi linaniuma.

    Mama Abdul - Morogoro

    ReplyDelete
  7. nimeumia nafsi saaaana pole Lulu. najifikiria mimi kama mzazi mtt wangu alie kilio cha kufa mtu tena mbele ya watu nahisi kupata maumivu makali.wazazi tunapaswa kuonya na kurekebisha watt wetu na si kuwaumiza mwili na hisia zao.

    ReplyDelete
  8. Dina, nilikuwa nasikiliza leo tena nikiwa ofisini mara kipindi kikakatika ghafla nilikuwa na hamu ya kujua hatma ya Lulu kwani matangazo ya clouds yalikatika wakati Lulu analia jamani nilipatwa na huzuni sana jamani mpaka sasa Arusha hamsikiki, pia clouds TV hakuna sauti kabisa sijui kuna tatizo gani?

    Mdau Arusha

    ReplyDelete
  9. Dina pendwa me leo cja ckiliza leo tena nilikua nimetingwa na kazi mbaya. Nakuomba kwa isani yako 2wekee kilicho tokea baada ya Lulu kukutanishwa na mama yake!! nakuomba sana sana.

    ReplyDelete
  10. Jamani nasikia tumbo lakuhara kabisa maana kila nikisikia hivi vitu nawawaza wanangu japo naishi nao. Hivi ni nini lakini?
    yule mtoto mwingine kesi yake imeishia wapi? jamani dina uwe unatuwekea online maana naona siku nyingi kweli huja update clip za heka heka wengine tuko mbali hatuwezi kusikiliza redio tunapata na kujifunza huku kwenye mitandao.

    ReplyDelete
  11. NIONAVYO MIMI TAABU YA MAISHA PEKE YAKE HAIMFANYI MTOTO AKIMBIE NYUMBANI KWA SABABU NI WACHACHE TU WANAOISHI BILA TAABUU YA MAISHA, LKN TAABU HII IKIAMBATANA NA MATESO YA MZAZI NA KUKOSA MAPENZI YA KWELI TOKA KWA WAZAZI NDICHO KINACHOMFANYA MTOTO AKIMBIE NA KUGOMA KURUDI NYUMBANI.

    ReplyDelete
  12. Roho imeniuma mpaka machozi yamenitoka hata sielewi sisis viumbe nini kimetufika mpaka vizazi vyetu tulovibeba tumboni kwa raha na taabu vitushinde .Mungu msaidie Lulu apate penye faraja.Dina elimisheni kupiga sio kulea

    ReplyDelete
  13. hapo lazima baba atakuwa namchezea mtoto tuuu fyuuuuuuuuuuuuu yan nitamkata ktu mbupu ake dah kwa mwanangu shiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  14. dina nimesikiliza kipindi cha leo huyo mtoto kuna kitu anafanyiwa na hao wazazi wake na si ajabu huyo baba sio baba yake ni mume tu wa mama yake na atakua anamtesa arudishwe kwa bibi ake na pia mngepata mawasiliano ya kwa bibi ingekua vizuri maana anaweza asifikishwe hata moshi

    ReplyDelete
  15. Nimeisikiliza leo iliuka inasikitisha sana,huyu mama cjui kama alizaa kwa uchungu,yaani mtoto hamtaki mamake anataka abaki kwa mjumbe.Watoto ni zawadi toka kwa mungu na tuwapende bac,hata kama mtoto ni mtundu huwezi kumuadhibu vile,mtoto amechapwa mpaka amebaki na alam mwilimi,INAUMIZA SANA,nleteeni LULU mimi nimlee..........

    ReplyDelete
  16. Mhhhhhhhhhhhhh!
    sijajua ni kitu gani kilichogundulika ila mwili wangu wote umenyong'onya.
    Mana nakumbuka yale yale ya yule ya mtoto wa Kigogo alivyokuwa akifanyiwa vibaya na mamaYE.

    DUNIA HADAA WALIMWENGU............................

    Kisensi

    ReplyDelete
  17. dina uwe una upload vipimdi tusikilize tunakosa uhondo wa leo tena

    ReplyDelete
  18. Jamani yani kesi kama hizo zipo nyingi sana na ukija kufuatilia mzazi hamtendi vizuri mtoto. Unajua wao ni watoto lakini wanajua baya na zuri pia. Fuatilia vizuri kuna kitu kisicho sawa hapo, na kwa wakati huo tafuteni sehemu salama ya kumuhifadhi huyo mtoto hadi utakapojua ukweli.
    Hongera kwa kazi nzuri ya kufichua na kuweka wazi matukio kama hayaaa.Mimi katika kituo changu cha watoto Guardian Angel nina watoto wenye kesi kama hii na tunaendelea kufanyia uchunguzi

    ReplyDelete
  19. Wifi Dina, unaweza kutuwekea link ya vipindi vya leo tena? wengine hatuwezi kusikiliza live wakati wa kipindi kwa sababu ya time zone. Tuwekee kwenye play list yako tutafarijika sana.

    ReplyDelete
  20. jamani dina naomba tujulishe kwenye blog yako.nipo uk,huwa nasikiliza leo tena on line,ila leo kilinipita na kesho nitakuwa busy,sitokuwa na nafasi kusikiliza.aah dunia hii,wee acha tu,lazima kutakuwa na kitu kwa huyo mtoto.maisha ya nyumbani maisha mtoto anaonekana muongo,ila nchi za wenzetu,mtoto huchunguzwa,mpaka ukweli ukajulikana.nilipenda sana dina ulivyomuelezea gea,huna mtoto ila ilikuwa ni kama mtu mwenye experience na kama umesomea fani ya saikolojia

    ReplyDelete
  21. mungu atusaidie n na watotowetu. na tuombe sana

    ReplyDelete