Stoy hii ilianza kwenye leo tena kama ifuatavyo,kawaida katika kipindi changu huwa napenda sana kumshirikisha msikilizaji wangu mwanafamilia wa leo tena.Nikaomba kama kuna mwenye story anataka kutushirikisha apige simu tuongee nae.Kweli akapiga simu dada mmoja kutoka Tanga akasema yeye amekuwa akitembea na mume wa mtu katika mahusiano yao mkewe wa huyo jamaa akagundua.
Baada ya kugundua kwa muda mrefu wakawa wakitukanana matusi kwenye simu lakini baadae kumbe yule mke alipoibua hoja kwa mumewe muwe akamwambia ni kweli na anataka kumuoa huyo hawara.
Mwenye mke akaanza msako kumtafuta huyo dada,muda si mrefu akamjua na akamfata mpaka kwenye duka analouza.Kufika kule akamwambia mimi sina ugomvi na wewe na mume wangu ameniambia anataka kukuoa.Mimi kilichonileta hapa nataka tuwe kitu kimoja tuwe marafiki.
Basi kweli dada akakubali na mpaka natupigia simu wamekuwa mashost pika pakua,wanatembeleana,wanasindikizana mahali,wanatumiana meseji na kupigiana simu n.k
Sasa hili likatuacha na maswali ni kweli mke wa jamaa ana nia njema na hawara wa mumewe au la?Wakati tukijiuliza maswali kuna dada anaitwa Sharon akanitumia meseji akasema mwaka 1984 kuna mwanamke anaitwa Asha Mkwizu aliwahi kumuua hawara wa mumewe kwa ukaribu kama huo wa urafiki.Alimuua kinyama tena nyumbani kwake baada ya kumkaribisha kula na kunywa.Nikampigia simu akatupa kisa chenyewe kwa urefu ilivyokuwa.Na tukasisitiza kuwa watu wawe waangalifu na urafiki wa upande pinzani kumbuka huyo anampenda mumewe na haujui mangapi wanayapitia pamoja moyo wa mtu kichaka ni ngumu kujua anawaza nini.
Wakati tunaendelea kuna kaka akanitumia meseji akasema nijaribu kugoogle hiyo story ya kesi ilivyokwenda ipo nitaiona.Baada ya kugoogle kweli nikaiona kwenye mtandao wa jamii forums ikiwa imewekwa na mtu anayetumia jina la MTAMBUZI.Ni ndefu siwezi kuiweka yote ila naweka link yake uingie ukaisome huko.Huyo mama alihukumiwa kunyongwa wakati ule wa Nyerere lakini alipewa msamaha wakati wa Mzee Mwinyi 'ruksa'.Nasikia yupo hai na nimepewa direction alipo bado nafanya mchakato namna ya kukutana nae kama ikiwezakena.
INGIA HAPA KUISOMA
http://www.jamiiforums.com/mahusiano-mapenzi-urafiki/234276-asha-mkwizu-hauli-na-kesi-ya-kumuuwa-hawara-wa-mumewe-6.html#post3617175

dina asante na ukipata hilo hitimisho na muhusika itakuwa poa kweli manake kenye JF imeishia kahukumiwa kunyongwa
ReplyDeleteAiseh nimeisoma hii story inatia simanzi kwa kweli, huwezi amini kama kuna wanawake wa aina hii kama hujaona au kusikia bt namuomba huyo dada awe makini sana na huyo mke mwenza.. Imani yangu inaniambia hakuna mwenye huo moyo dunia ya leo
ReplyDeleteKeep your friends close but your Enemy Closer!!
ReplyDeleteHey dina.....nashukuru umeweka source ulipoitoa hii story maana nilishaanda makabrasha kuelekeza kwako kwa kuto sema source ni JF.......
DeleteDina leo kwenye kipindi ulimaanisha Steven Seagal ndiye huyo movie star wako?
ReplyDeleteMhh! hii habri ndefu sana, inatisha na kusikitisha mno
ReplyDeletekwa kweli kila mja ana MOYO hana jiwe. hvyo huyo dada asichezee na mali za watu. MUME AUMA SANA
Kwa dunia ya leo dina kweli hakuna mwenye moyo km huo ni ngumu sana jaman ila kwa miaka ya nyuma ilikuwa ni mambo ya kawaida tu coz mie mfano halisi ninao baba yangu mzazi alizaa na mwanamke mwingine ila mama yangu mie wala hakuwa na kinyongo na yule mke mwenzie ila ss huyo mke mwenza alikuwa tafrani mara anamtema mate lkn mama yangu mie dina huwezi amini akuwai kumtukana wala kumsonya so ikawa km bahati ile nyumba aliokuwa anaishi yule mama wa kambo alikuwa amepanga aunt yangu so tukawa tukitoka shule tunaenda huko kwa aunt na mama anatufuata jioni so tulikuwa tunapita nyumba kubwa ukumbini ndio huyo mama alipanga so aunt alikuwa anakaa chumba cha uani.So yule mama akaleta soda mara akaleta wali mama akasema kuleni so tulivyoondoka akatusindikiza so toka hapo akawa anakuja home yule mama wa kambo so mama akawa anampokea ila kwa siku ya kwanza baba alivyomuona pale home alishtuka sana ila mama akamwambia mie sina roho hiyo uliokuwa unanifikiria.Na baba alizaa na yule mama wa kambo na huwez amini dina yule mtoto kalelewa na mama na mpka ss ni baba mkubwa tu coz alizaliwa 1988,Mpaka ss ni kama ndugu coz yule mama wa kambo anaishi na mwanaume mwingine na baba na mama bado wapo pamoja.Wanasaidiana kwenye shughuli km harusi na hata misiba i mean mama yangu na yule mama wa kambo
ReplyDeleteHalima
Asante sana dada Dina kutuletea hiyo habari lakini tunamuomba huyo mama kama anataka uhai aachane kabisa urafiki na huyo mke wa huyo bwana wewe uliona wapi unamuibia mwanamke mwenzio halafu anakuomba ushoga nawe unakubali akatapishwe naona huyo mke wa jamaa kamlisha madawa!!! siyo bure.
ReplyDeleteDINA NIMEKUSIKILIZA KWA MAKINI INAONEKANA ASHA MKWIZU HAKUDHAMIRIA KUUWA KAMA ALIPOSEMA MWENYEWE JAPO NDIYO KASHA UWA NA MWENYEWE KUKURI YOOOTE SABABU MWANAUME, MUME INAUMA ALAFU ANAYEKUCHUKULIA TENA AKULETEE KEJELI ALAFU UWE NI MTU WA KUHAMAKI UNAWEZA FANYA LOLOTE KWA KWELI INASIKITISHA WANAWAKE TUWE MAKINI KWAKWELI HASWA UNAPOJIJUA NI MWIZI KULA KIMYA KIMYA LASIVYO YATAKUTOKEA KMA ASHA MKWIZU... JAMANI DINA NTAFURAHI KWELI KM UTAWEZA KUMPATA ASHA MKWIZU TUMSIKIE MAJUTO YAKE ANASEMAJE...JAPO KWA SASA ATAKUWA MTU MZIMA SANA.
ReplyDeleteDina hii story imenikumbusha mbali sana nilikuwa darasa la pili ila mimi niliwahi kumuona huyu mama dodoma gereza nilipokwenda kumuona aunty yangu Sara Simbaulanga sasa sijui kama alitoka au bado kwani Aunty Sara yeye ameisha toka kitambo
ReplyDeleteSamahani kama nitakukera. Nilikuwa nakuomba kama utapata wasaa utwekee/utupe maisha ya mama simba ulanga mara baada ya kutoka jela mpaka leo jinsi maisha yake yanavyoendelea kwani ni mtu muhimu katika jamii ya kitanzania(japokuwa wengine wataguna)
DeleteMH UYO DADA AWE MAKINI MI BIBI YANGU ALIUNGUZWA USO NA MKE MWENZAKE MKE MWENZA KABISAAA WA NDOA AMBAE ALIKUWA MDOGO BIBI YANGU ALIKUWA NDIO MKE WA KWANZA. LAKINI WIVU AKAVIZIA SIKU YAKE YAKUWASHA TAA KIJIJINI UKO BASI AKAENDA KUTAFUTA PETROLI ALIPOITOA ANAJUA YEYE AKAITIA KWENYE KOROBOI MASKINI BIBI YANGU ANAENDA KUWASHA MAANA ILIKUWA ZAMU YAKE WACHA KIKOROBOI KIMLIPUKIE AKAUNGUA SEHEMU YA USO NA SHINGO YOTE MPAKA ANAKUFA MAJUZI ANABONGE LA MKOVU UKE WENZA HUOOOOO. KWA HIYO DADA JIPANGE KAA NAE MBALI KABISA HATA MKIOLEWA USITAKE USHOGA NAE HABARI NZURI KILA MTUI AKAE KWAKE.
ReplyDeleteInawezekana kabisa kuna ambao waliwatafutia waume zao mke mwenza,tana hii karibuni...na wanaishi kwa raha, ukionoda roho ya `umimi' inawezekana kabisa. Tujiuliza lipi bora kumuacha mume atembee nje, au kumleta mtu unayemuamini akaolewa mkawa mke mwenza.
ReplyDeleteKwa kweli penzi si la kugawanywa. If you real love someone kweli waweza kabisaaaaaa kukubali kushare na mwengine. Aisee mi siwezi; though Mungu aninusuru nsije kuua. Ila kama mwanamume na mimi nshamchoka ntamkaribisha tu huyo second wife ili nijipumzikie. To my reasoning hao wanaokubali uke wenza BILA vinyongo wanakuwa penzi lishachuja kwa waume zao. Ni kama wanatua zigo
ReplyDeleteEE jamani ni jana tu nilikuwa namsimlia rafiki yangu kisa cha Asha mkwizi,,,nikikumbuka siku hiyo huwa nasikia moyo kusisimka ingawa nilikuwa mdogo sana,,na watoto wa Asha mkwizi walikuwa karibu sana na sisi,,lakini baada ya mama yao kuuwa tulikuwa tunawakwepa kama ukoma maana tulijuwa na wao ni wauwaji kama mama yao.,,,Yaani hile harufu ya nyama ya kuchoma ilisambaa karibia nyumba zote hapo jirani,chumbani bafuni,lakini baada ya harufu hiyo nahisi tulikaa muda mpaka kuja kusikia mapolisi wamekuja na kusema hiyo sio nyama ni binadamu kachomwa moto,Sijasoma hiyo habari ndefu sana,,lakini,mbona sisi tulijuwa huyo mtumishi ndo aliyechimba shimo?,,kisha ndo akatumwa atoke hapo arudi baadae?,,Ee ni zamani hiki kisa huwa ni cha kutisha sana,,tangu siku zile huwa siamini mtu,mimi,,hata kama sio mke mwenza,kuna wengine anaweza kukuchukia bila sababu,,inatakiwa mtu ambae una wasi wasi nae uende na mtu mwingine wa kukusindikiza
ReplyDeleteEnzi hizo mtaa wa Lugalo Upanga ulitinga visa ,,,na ndo wakati huwo wahindi walikuwa wanagombe girlfr. sijui au mke wakauwana katika gari jiraji hapo hapo,,baada ya siku kuna aliyezaa mtoto akamtupa katika taka taka,,basi wasisakwa wasichana wote wakubwa wakubwa kujuwa aliyetupa mtoto ni nani?na hicho kisa cha huyo mke wa tajiri,,,Mr D aliyeuwawa na mdogo wake,,Na kuna wakati wezi walikuja kuiba gari basi wakamkuta dreva ndo kwanza kamtoa mtoto shule hapo Pwani Tours sikumbuki driva aliuwawa,na mtoto wa kike mdogo walivyofika mbele wakamshusha kwa kumrusha kakakimbia kurudi nyumbani kanalia.Yaani Upanga hasa mtaa wa Lugalo Mauwaji ilikuwa kama movie.Eti Dada zangu walivyokuwa wakichukuwa tax wakisema wanaenda Upanga Lugalo,,tax dreva anasema nitakushusha mwanzoni mwa mtaa,,ule mtaa siingii balaa
Mdau London
Tupe maujuzi mkuu,una gae gani sasa?
Deletedada dina upo0o juu km mawingu dah hongera sna !! Najickiaga raha sna kuckilza vipind vyko big up ma lovly sis huna mpinzni cloud
ReplyDeleteyaan wakati anahukumiwa mm nilikua na mwezi mmoja tangu kuzaliwa,nimeshtuka mno na hili mambo ya ukatili yameanza kale kumbe,Mungu atunusuru jaman,wanandoa na wapenzi tutulie jaman msongo wa mawazo wa kuharibika kwa mahusiano sababu ya hawara n mbaya though haijustify alichokifanya bi Asha.....kama movie jaman haa,Mungu atusaidie
ReplyDelete