JINSI YA KUTUMIA PAPAI KULAINISHA NYAMA KATIKA MAPISHI YA HARAKA.
Wapo wanaotumia tangawizi au ndimu kulainisha nyama au mbinu mbalimbali.Na pia wapo wanaotumia papai kwa kazi hiyo hiyo.
Nyama tunayoizungumzia hapa ni nyama ya ng'ombe ambayo unataka kuipika iive kwa haraka.Chukua papai lako bichi,menya na utoe zile mbegu kisha katakata vipande vidogo vidogo.Nyama yako utakuwa umeshaikatakata tayari umeiosha tayari kuichemsha.Weka kwenye sufuria na utie chumvi kidogo vile vipande vya papai bichi miminia kwa juu na uweke jikoni kwa ajili ya kuichemsha dk 10 nyingi nyama tayari imeiva lainiiiiiiii.Hapo unaweza kuunga rosti lako dada kwa namna unayopenda na familia ikajichana.
Sikiliza nyumbani kwetu leo katika leo tena kesho utaisikia hii.
Asante Dina nitajaribu weekend hii. Mi nilikuwa natumia tangawizi.
ReplyDeleteAsante mpendwa kwa kutuelimisha! Dunia hii imejaa mambo mengi ya kujifunza, tunashukuru ukiwa unatushirikisha ukijuacho mamii
ReplyDeletehata utomvu wa papai nimeona watu wanaweka ktk nyama ili kuilainisha (japo mie nauogopa utomvu) ila ni toni moja au mawili tu kwa kilo moja ya nyama vinginevyo ukizidisha utashangaa kukuta nyama imekuwa uji. na ndimu navyojua mie huwa hailainishi nyama ila inakata shombo. maana ndimu au limao hutumika kukata vitu vingi jamaniiiii
ReplyDeletemie kawaida natumia tangawizi na vitunguu saumu na binzari nyembaba (itangwe) hiyo ladha yake acha tu tamu unaweza kula ugali na hiyo nyama bila hata kuiiunga
DA J
Tangawizi pia naona ni nzuri. Sasa hayo mapapai yakiiva hyo nyama inakua na ladha ya aina gani?
ReplyDeleteColleta
mbona mie nimejaribu mara kadhaa na haijalainika,yani baada ya kuosha,nimekatakata,then nikaiweka jikon pamoja na vipande vya papai,Yale maji kukauka nyama bado ngumu,inabidi tena kuweka maji kama mara mbili ndo inaiva,nakosea wapi
ReplyDelete