Monday, April 16, 2012

KATIKA AZIMIO HILO LA APRIL TEAM LEO TENA TULIINGIA

Gerald na Babra walimaliza muda wao na kutukaribisha sisi.
Moja kwa moja tukisikika kutoka viwanja vya mnazi mmoja mimi na Gea Habib.
Clouds fm kwa mwaka huu 2012 itakuwa ikitutoa studio mahali ambapo tumekuwa tukifanyia vipindi mpaka mtaani nje ya studio .
Millard Ayo akikusanya habari kumi za azimio la april....AA.
Wanafamilia wa clouds walifika mnazi mmoja kutoa maoni yao na kuzungumza nasi.
Gea akiongea na wadau.
Tulikuwa na live band ambapo tuliperfoam na Isha Mashauzihapa sijapata picha yake ila ntaziweka.
Baada ya kumaliza kipindi tulipita kuongea na mashabiki wetu.
Katika azimio hili la April pia msimu mpya wa vipindi wa clouds fm yafuatayo yatafanyika.
1.Kuanzia sasa leo tena itaanza saa nne mpaka saa saba mchana.
2.Dula kibajaji atatoka ameshapiga story sana na kutakuwa na MCHINA
2.Nyumbani kwetu leo kina mama/dada kutoka manyumbani mtakuwa mkitupa maujanja ya huko nyumbani.
3.Kila ijumaa kutakuwa na KAPU LA MAMA lina nini?sikiliza leo tena.
4.Kila wiki kutakuwa a BESENI,lina nini sikiliza leo tena.
5.Kwa muda mrefu umesikiliza hekaheka unajua nini kinaendelea katika maisha ya wale uliowasikia kwa miaka mitatu,miwili iliyopita?inakuja BAADA YA HEKAHEKA.
6.Safari ya leo tena kwena MOROGORO,DODOMA NA SINGIDA.
7.Tuzo za dada bora wa kazi za nyumbani.
Kwa mengi zaidi sikiliza leo tena ya clouds fm kwa maoni tuandikie email leotena@cloudsfm.co

11 comments:

  1. Kama kawaida yenu,so creative, mko juu!
    Big up sana!

    ReplyDelete
  2. Dina hiyo jump suit wala hata sikusomi yaani husomeki kabisaa. tisheti na jeans ungependeza zaidi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unemwambia Dina Kuwa T shirt na jeans angependeza so asibadilishe? Yaani avae t shirt na jeans siku zote ? Wee unauako bwana kasomeka sana kwanza hakuja kuonyesha mavazi alikua kazini Asa wee uliyoyaona hayo yako, na mtu huwezi pendeza sk zote,,, Aii,,

      Delete
  3. dada dina nakupenda sana.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli mmefanya mabadiliko makubwa! Hingereni kwa kutusidishia burudani! Kwa mtazamo wangu mabadiliko mliofanya katika kipindi cha leo tena binafsi sijaridhika nayo, kusema ukweli siipendi tena kama zamani, hamna kinachonivuta kusikiliza sana sana ni matangazo kwa wingiiii! Jaribuni kuangalia ni vitu gani vilikua vinawavutia wasikilizaji mviboreshe na sio kuvitoa hewani mfano heka heka nadhani mmesema inakuja kivingine au muda ndio mmebadilisha? Pia mngembadilisha Aunt Sadaka mkakaribisha wataalamu wengine wenye uelewa katika fani hiyo najua inaweza kuwa challenge but work on that kumsikiliza mtu mmoja kila siku you don't gain much and I am sure she is not an expert kwa kila topic mnayochagua kuiongelea, jaribuni kutafuta wataalamu wengine.

    Keep the good work!

    Shauna

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shauna nimekupata...mbona hekaheka zipo?ila tumebadili muda tu.Pia sadaka tupo nae kwa sababu mlengwa wetu zaidi ni mwananchi wa kawaida ambae anahitaji sana elimu hiyo.Pengine wewe huitaji kwa sababu upo na exposure ya kutosha labda unajua hayo mambo tofauti na yule mama au dada wa vingunguti huko au yombohuo ni mfano.Ila tuna vitu vingine ambavyo tunaviintroduce taratibu tayari tuna daktari wa wanawake na wataalamu wengine watakuwa introduced baadae.

      Delete
    2. Ahsante Dina kwa kutumia muda wako kunielewesha. Nafurahi sana kuona kwamba unajali maoni ya wadau na unayafanyia kazi, Nimefurahi sana. Big up! Keep on shining, sky is the limit!

      Best,

      Shauna

      Delete
  5. kweli ukisikiliza kila mtu utachanganyikiwa mi eti nimeipenda hiyo jumpsuit kiukweli sikutanii na naona umependeza

    ReplyDelete
  6. Big up sana whole team.

    ReplyDelete
  7. Hi Dinna, sasa mbona mnapunguza muda wa kipindi cha LEO TENA.
    Wakati mnaanza saa tatu muda ulikuwa hautoshi sasa mnaanza saa nne mbona kuna vitu tutakuwa tunakosa. Kama msikilizaji mzuri wa kipindi chako sijafurahi hata kdg.

    ReplyDelete
  8. luv u.dinaaaaa ur just a hero. much love from sweden

    ReplyDelete