Wednesday, April 18, 2012

LEO NIMEBAKI NA MAWAZO NA HUZUNI TU

Nakumbuka rafiki yangu Gerald Hando aliniambia Dina ukisikiliza sana matatizo ya watu unaweza ukaogopa maisha.Yaani leo nimealia na nimehuzunika sana nilipokutana na Wastara na kunipa hadithi nzima ya kinachomkabili sasa.Na mpaka naandika hapa bado namfikiria sana.Ni mwanamke aliyepitia mengi na anendelea kupitia mitihani mingi akiongea analia kiasi cha kunifanya hata mimi nilie.Kweli binadamu hatujafa hatujaumbika tumshukuru Mungu kwa kila jambo unaweza kudhani wewe una mitihani hapa duniani kumbe kuna aliyekuzidi.
Najua nilikuahidi kuwa nitaruka leo na Wastara live katika leo tena ila nilichofanya nimerekodi kipindi kizima ambacho kitaruka hivi karibuni.Huyu mwanamke anahitaji msaada sana wa mumewe kutibiwa mwezi ujao anatakiwa kusafiri kwenda India kwa hayo matibabu ambayo yanaweza kugharimu zaidi ya ml 25 hela ambayo hata robo yake hawana.Nitakuomba sana mtanzania ushirikiane nami na hii familia hata kama hatutafikia pesa yote angalau ifike nusu.Hapa nimeshaanza kufanya mazungumzo na watu kadhaa ninao wajue ili tuhamasishane kuchangia haya matibabu.Wasanii tunaowaona kwenye movie wakiendesha magari ya kifahari na majumba yale sio maisha yao halisi hata kidogo ni watu na shida zao.
Kuna ac namba nitaitoa pamoja na tigo pesa ili kwa unaeweza kuchangia kwa huko.

51 comments:

  1. kabla sijasikia hicho kipindi, leo naenda cheza bahati nasibu kwa ajili yake, Inshallah nikibahatika kuipata maana ni hela nyingi bac natoa yote,ama ukiona kimya mpenzi Dina ujuwe sijabahatika sema nitachangia kidogo nilichonacho.

    ReplyDelete
  2. bONGO mOVIE WACHANGIE JAMANI SIO WASUBIRI HADI MTU KAFA NDIO WAANZE KUONYESHA UFAHARI

    ReplyDelete
  3. Dada Dina kuna tulio nje ya nchi pliz naomba utoe na details za majina ambayo mtu anaweza akatuma western union fasta fasta tafadhali

    ReplyDelete
  4. dina twakuomba utuhadithie na sisi ambao muda huo tulikuwa job nasisi wengine japo tupo nje ya nchi tuweze kujifunza kutokata tamaa maana wastra kapitiamengi huyu dada mwenyezi atakusaida ishaalah..

    ReplyDelete
  5. kwa kweli sijasikiliza kipindi leo lakini kwa kwakusoma tu hapa nimejisikia vibaya sana kama msichana/dada/mama,nasubiria hiyo namba nichangie atleast kidogo nilichonacho. Inauma sana kwa kweli.

    ReplyDelete
  6. mh masikini wastara yani tangu ndoa yake hakuna amani hata kidogo du! ndivyo inavyosemakana kuwa ukiwa na mitihani mingi Mwenyezi Mungu anakupenda sana, Mungu atawaafu Inshallah

    ReplyDelete
  7. ni kweli binadamu hujafa hujaumbika,mimi ni mwepesi kulia dina yaani nishalia hapa kwenye meza yangu mpaka wananishangaa hata story sijaisikia laikn i feel the pain ya kuuguza alafu huna msaada wala fedha nilishapitia hayo maisha dina kila kukikucha unalia mchana unalia usiku unalia wala usingizi hupati,na bahati mbaya mgonjwa wangu alifariki.hivyo basi tujichange vilivyo tuokoe maisha ya huyo kaka na ikibidi turudishe tabasamu la mwanamke mwenzetu.pole kwa mgonjwa na mkewe pia.siku njema dina. its me jokinda

    ReplyDelete
  8. inshaallah mwenyez mungu atawapa wepesi kwani hakuna mtihani unaomshinda kwani anatoa yeye mtihani na hakika anatoa jibu la mtihani. inshaallah next week nitakachojaaliwa nitatuma. nasubiri hiyo namba ya tigo pesa.

    ReplyDelete
  9. Hayo matatizo anayo yapata ni kamba za mauti na shida za kuzimu nampa polesana ushauri wangu ni aende kwenye maombi EFATHA mwenge nimeona wengi waliokua na matatizo mengi kuliko yakwake wakifunguliwa na kupona kabisa asijiulize maswali mengi kwasababu naelewa ktk shida hiyo amefanya mengi nauhakika YESU atamsaidia

    ReplyDelete
  10. pole sana dada na familia yako,kila jaribu lina mlango wa kutokea.dina tunaisubiri hiyo tigopesa tuchangie

    ReplyDelete
  11. pole sana dada nimesoma tu nimelia imenisikitisha sana, toa namba tumchangie pia hao bongo move wamchangie.

    ReplyDelete
  12. pole sana wastara, nampendaga sana huyu dada ametulia na anajua nini maana ya maisha, ni mshabiki wake mkubwa mno huwa napenda kusoma habari zake, mimi mwenyewe niliangalia kipindi cha take one kilichorushwa wiki chache zilizopita kwa kweli nilishindwa kuzuia machozi kutoka baada ya kumuona wastara anaelezea maisha yake na especially pale alipo ulizwa ni kitu gani kinachomfurahisha duniani, yaani aliongea kwa hisia kutoka moyoni kwamba yeye bila mume wake sajuki hawezi kua na furaha tena maishani, kweli huyu kaka anahitaji msaada , wapendwa tumsaidie kwa kila hali ili mwanamke mwenzetu arudishe furaha yake, dina plz toa hiyo namba ya tigo pesa nitachangia chochote nitakacho barikiwa

    ReplyDelete
  13. maisha ni mapambano na majaribu ya kila aina unaweza ukataka kujiua!lkn kwa nini ujiue wakti mungu alikuumba hapa duniani ili upambane na kuyashinda majaribu kuwazomea waliosema ushindwe kwa kusema unaweza!naimn hy ni mapito tu ya wastara na ipo siku mungu atamjaalia na kila kitu kitakaa sawa bila kusahau maombi na kufunga pole sana dada yngu pole sna nami sijasikia stor nzima ila nimeuzunk kwani ananikumbsha mbali!

    ReplyDelete
  14. inshaallah tutashirikiana nao kwa hali na mali kulingana na uwezo tulionao.

    ReplyDelete
  15. mtawekaje picha za mapozi kuomba msaada?

    ReplyDelete
    Replies
    1. hiyo picha ilipigwa zamqni acha ushamba kama unachangia changia tu

      Delete
    2. if ur not willing to contribute just shut ur mouth,poz or no pose wat we are after is the contribution,wacha uswahili,ila watu kama wewe hawakosekanagi!!! eeew!

      Delete
    3. kama una nia ya kuchangia changia, hutaki kaa kimya, imewekwa picha ya wastara, enzi za furaha, sasa ulitaka aweke picha gani hapo? yote kwa yote, nia ni kuleta ujumbe kwa wenye moyo wa huruma wasaidie. watu kama nyinyi kutwa kukosoa hata msaada wenyewe hamuwezi kutoa au mkitoa ni matangazo hadi mtaa wa kumi. hebu wwachie wanaojua utu.

      Delete
    4. WE ANONYMOUS 19,2012 01:47 TUTOKEE HAPA KWA HIYO ULITAKA IWEKWE PICHA ANALIA MPAKA MAKAMS YANATOKA AU??? WATANZANIA TUJIFUNZE BUSARA BANA INA MAANA WW KILICHOELEZEWA HAPO HAKIJAKUINGIA HATA BADALA YAKE UMEONA PICHA TU MFYUUUUUUUUUUUUU!!!
      WASTARA MPENZ MUNGU YU MWEMA NA KILA ALIFANYALO ANA MAKUSUDIO YAKE,, MUAMIN ANAWEZA KWA KILA JAMBO NAAMIN MUNGU ATAMPONYA MUMEO NA ATAREJEA HALI YAKE VIZUR,,, NAIOMBEA NDOA YAKO IDUMU MILELE AMEEEN

      Delete
  16. Kwanza nianze kwa kuwapa pole wote walioguswa na tatizo hili. Pili namuomba Mungu awaondoshee maradhi hawa wenzetu wanaoumwa.
    Nianze hivi:Katika maisha yenye kuleta usawa katika jamii,kuna kitu tunaita "precedence". Maana yake ni,kama una-simpathize na tatizo la mtu fulani katika extent fulani,je,ikitokea tukio linalofanana na hilo kwa mtu mwingine,tuta-simpathize katika kiwango hichohicho? Wandugu point ninayotaka kubainisha sio kutaka hawa watu wasisaidiwe,la hasha,ni kutaka kuleta uwiano usio na upendeleo katika maisha yetu ya kila siku. Najua ni ngumu kukubali au kuelewa,lakini nataka kusema kitu kimoja,leo tunanadi tatizo la hawa wasanii kuwa wasaidiwe,lakini mimi na wewe tujiulize kitu kimoja,hawa ndio watu pekee wenye tatizo kubwa kiasi hichi mpaka kutaka kuuzia mamilioni ya watanzania huruma hata kama hawaitaji kununua huruma hii! How many orphans,dissabled who cant even talk,infants, do we have in our homes,who doesnt even know where to address their problems,their daily meal,life is at stake?
    BTW,tujiulize kitu kimoja,huyu Sajuki kabla ya kuumwa,aliishi maisha gani?We must also educate our celebrities how to balance their life between show off and real life.!We must educate them how to plan their life of tommorrow which is in fact the real life! Kuitwa msanii sio kuishi maisha ya kisanii for life,kuna mambo mengine nje ya sanaa kama kwenda shule,biashara yoyote,kulima shamba,n.k. Mi na wewe tunawajua watu wanaopigika na kazi ngumu huko mitaani,uonevu dhidi yao hauishi,na bado huumwa maradhi makubwa tena kuliko haya aliyonayo huyu msanii,na wanasubiri kufa kwa kuwa wanajua there is no alternative for them,rather than to die hard! Dina kama huamini haya ninayosema,go to poor families,villages,it is easy to se this. Yawezekana huwa unajua tu yale matatizo unayokutana nayo redioni,kuna matatizo zaidi ya hayo. Hawa wasanii wanapokuwa kwenye peak,huwa hawaamini kama kuna ups and downs kwenye maisha,ndio maana wanaishi maisha ya anasa,ku-overspend,kutaka kujionyesha maisha wanayo-practise luningani ndio maisha yao halisi,wakati future yao ni utata mtupu. Wajifunze kuwekeza kwenye maisha nje ya usanii,vinginevyo wataishia kutaka huruma ya watu kuwasaidia wakati wameshachezea maisha,na kuna watanzania wenye kuitajia misaada kuliko hata wao! Rai yangu,aliyeguswa na tatizo la hawa wasanii achangie,lakini twende zaidi ya hapo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. we fala hebu kalale mbele huko,,km huwezi kusaidia kakumbatie mkeo mlalane,,,umeniharibia mood yangu,,kutoa ni moyo na si utajir na hao wa mitaan na vijijin pia waje waseme pia watasaidiwa..mwehu weeeeeeeeee

      Delete
  17. Mimi pia nitajitahidi kutoa kidogo nilichonacho, Anony 01:47am ni nini unatafuta? umeombwa msaada na sio kuangalia ni pic gani imewekwa! au ulitaka wakuwekee pic ya dada wastara analia ndio ujue kuwa ana shida??? kutoa ni moyo dada sio utajiri, binafsi sijafurahishwa na hiyo comment yako.

    ReplyDelete
  18. INASIKITISHA SANA POLE SAJUKI. PAMOJA NA KUTIBIWA NA DAWA ZA HOSPITALI APELEKWE PIA KWENYE MAKANISA AKAOMBEWE. AWEKE UDINI PEMBENI MUNGU NI MMOJA NA MAOMBI YANANGUVU KWA IMANI ATAPONA INSHALLAH.

    ReplyDelete
  19. Mungu wa Ibrahimu na Isaka na Yakobo ambaye ni Mungu ninayemwamini akuponye maumivu/uvimbe ulioko tumboni ukanyauke kwa Jina la Yesu. Dina Naomba Uprint comment hii umpe Wastara akampe Mumewe...Naamini akiisoma kwa imani atapona.

    ReplyDelete
  20. pole sana wastara hayo ni majaribu tu na yatapita,mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu tupo pamoja

    ReplyDelete
  21. We anonym wa pili ukitaka kutoa toa na kulia kushoto kusijue Mil 25 sio mchezo ,Tunachotakiwa tushirikiane kwani tunajua story kamili ya Stara na mguu wake mmoja .Tutoe tulichonacho

    ReplyDelete
  22. Katika maisha kuna mengi,furaha, huzuni na mitihani ya Mwenyezi Mungu,Tunapopata furaha tumkumbuke na kumshukuru,tukiwa na huzuni tumuombe atufariji,tukiwa na mitihani tumuombe atupe ushindi katika mitihani hiyo kwakuwa ni yeye pekee ndiye ajuae hatma yetu,sisi kama binaadamu tunatakiwa kushirikiana na kuona tunamsadiaje mwenzetu kwa chochote tunachoweza kila mtu kwa nafasi yake.Inshaallah Mwenyezi Mungu amsaidie sana,amtie nguvu na ampe imaani katika wakati huu mgumu.Nakupenda sana Wastara Inshaallah tuko pamoja.

    ReplyDelete
  23. Kweli ni muhimu kuchangia,kuliko kusubiri mtu afe ndio wanajazana watu kibao,...

    ReplyDelete
  24. sidhani kama picha hii ni ya sasa.

    ReplyDelete
  25. mimi hata sijaelewa chochote hapa,natamani kujua ni kitu gani kilichomsibu huyu dada ili nami nimsaidie mchango wangu wa fedha na mawazo.i guess its something very serious, i wanna hear it

    ReplyDelete
  26. mwenyez mungu atakusaidia, endelea kuwa na subira kwan subira ni ibada, yataisha , tutamchangia tu na kwa uwezo wa mungu maradhi yatamuondokea mume wake na yeye atapata faraja ya ndoa cku moja.

    ReplyDelete
  27. kachukue picha global uweke hapo ya sajuki mwenyewe alivyosasa. yaani anasikitisha sana na kuhuzunisha. ondoa hiyo ya mkewe haionyeshi kama anataka msaada. ni wazo tu Dina.

    ReplyDelete
  28. kachukue picha global uweke hapo ya sajuki mwenyewe alivyosasa. yaani anasikitisha sana na kuhuzunisha. ondoa hiyo ya mkewe haionyeshi kama anataka msaada. ni wazo tu Dina.

    ReplyDelete
  29. dinah hongera kwa moyo unaouonyesha wa kuwasaidia watu kupitia kipindi chako. kwakweli sijackiliza hiyo story lkn moyo umeniuma wastara ni mfano wa kuigwa kwasisi wanawake kwajinsi alivyomvumilivu. Mungu azidi kumtia nguvu na kila jaribu lina mlango wa kutokea.

    ReplyDelete
  30. pole wastara, pole sajuki, mungu awape subira. unapopatwa na matatizo.unatakiwa uwe na subira. na kumuomba mungu usimamizi wake.wastara mdogo wangu mitihani ni sehemu ya maisha, unatakiwa uwe na nguvu na subira. mdogo wangu wastara mkumbuke mungu muombe mungu ulipo kosea. ki ukweli niliumia roho nilipo ona tumbo lako la mimba ukilianika kwenye magazeti. ilichofanya kiungwana si kizuri mbele za mungu. mwili wako ni pambo kwa mumeo sio macho ya watu. vitu vingine vina mchukiza mungu. usirudie tena mpendwa mdogo wangu wastara. mungu atamjaalia mumeo atapata nafuu na tunakuombea akupe nguvu na afya njema. na ampe afya njema sajuki

    ReplyDelete
  31. inaonekana wewe hata utu huna na ni zaidi ya mnyama wewe?yaani mumgu akisema ubadilike utageuka kuwa mnyama. kwani picha inahusu nini na matatizo yaliyopo, au ulikuwa unataka awekwe akiwa mchafu ndo ataonekana ana shida.wewe kama unataka kumsaidia saidia tu acha maneno machafu.

    ReplyDelete
  32. Pole sana my dear, But remember God is able; kimbilia kwa YESU nina hakika utapata uponyaji na kurudisha furaha katika familia yako.

    ReplyDelete
  33. hua siishi kulia kila nitaposikia matatizo ya wastara akyamungu sikatai nina mitihani rkn yke inaniumiza kwa kweli,cna kitu ila inshaalah nipo nao ktk dua zangu m mungu atawaafu siku moja,MARIAM

    ReplyDelete
  34. hua nalia kila nisomapo matatizo ya wastara& sajuki,akymungu sikatai ata mm nina mitihani rkn yao inaumiza sn,sina cha kuwapa rkn inshaalah nipo nao pamoja ktk sala zangu zoote inshaala m mungu atawaondolea yoote,dina m mungu akujaalie watu wakusikie ktk michango.

    ReplyDelete
  35. Jamani Dinna mbona hujatuwekea hayo mahojiano uliyofanya na wastara? leo nimemuona Sajuki kwenye gazeti kweli anatia huruma sana. Anahitaji msaada wetu wote (watanzania)pia na maombi yetu.

    ReplyDelete
  36. naamini kuwa atapata pesa mana Mungu yupo kwa ajili yetu naomba mungu anijalie angalau niweze kuwatolea wenye matatizo

    ReplyDelete
  37. HUJAFA HUJAUMBIKA MUMY.

    ReplyDelete
  38. kwan umeambiwa hiyo picha ndo kapiga jana????ovyoooooo

    ReplyDelete
  39. kuna mjitu mingine bhana cjui hata ikoje we hiyo picha sasa imekukera nin?? rohi mbaya na kuweka mdole mwekundu kwenye kila jambo ndo style ya maisha yako mfyuuuuuuu kama nakuona na mtambi wako wa minyoo na mitege kama banio ulivoshupaa ku comment upupu,, shwaiiiin

    ReplyDelete
  40. pole sana wastara Mungu akiniwezesha ntachangia maana hata mie nmemwona sajuki nikahuzunika saana utadhan namjua in person!lakni pia msipuuze swala la maombi kipindi hiki mnachosubr kwenda kwenye matibabu maana hata huko makanisan mtapata marafiki wapya na faraja!udini muweke pemben,uzima kwanza!get well soon

    ReplyDelete
  41. Ni bora kumchangia mwenzetu ili tuokoe maisha yake kuliko kusubiria mtu afe ndiyo tuje tuchange hela kwa ilivyopita kwa msanii aliyetutoka hivi majuzi

    ReplyDelete
  42. Pole sana wastara amini ya kwamba hyo ni mitihan ya dunia na kwa n guvu za Mungu utaishinda tu

    ReplyDelete
  43. Pole sana sajuki inshallah mwenyezi Mungu atakujaalia na utapona sisi tunakuombea.

    ReplyDelete
  44. Pole sna Wastara,Mungu yu mwema atakukirimia hakuna linaloshindikana kwa Mungu naamini yote ni m,apito yatakwisha
    tu.

    ReplyDelete
  45. jamani mmeshaambiwa ugonjwa unahitaji upasuaji mmekazana maombi maombi mungu wa Isaka na Yakobo Mungu ni wa wote kinachotakiwa ni michango na mtu arudi India kwa matibabu aache kwenda kwenye upasuaji aende kwenye maombi dua zitaendelea huku mtu awe ameshaanza tiba.

    ReplyDelete
  46. Pole sana mpendwa M/Mungu atafanya wepesi kwani kwa wanaadamu jambo kubwa kwa Allah (s.w.t)ni jambo dogo sana kwani akisema kuwa lina kuwa hakuna mwenye kupinga Inshallah kwa uwezo wa Jalali atapona.

    ReplyDelete