Tuesday, April 10, 2012

SABABU ZA KIFO CHA KANUMBA ZATAJWA,BAADA YA JOPO LA MADAKTARI MUHIMBILI KUFANYIA UCHUNGUZU MWILI WAKE

MSANII nyota wa filamu nchini, Steven Kanumba amefariki dunia kutokana na tatizo la mtikisiko wa ubongo linalojulikana kitalaamu kama Brain Concussion, taarifa za kitabibu zimeeleza.

Taarifa hizo za ndani, zilizopatikana jana baada ya jopo la madaktari bingwa watano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu huyo, zimeeleza kuwa tatizo hilo linaweza kumfanya mtu apoteze maisha mara moja au baada ya siku kadhaa. Mmoja wa madaktari hao ambaye aliomba jina lake lisitajwe alisema waligundua tatizo hilo baada ya kumfanyia uchunguzi huo kwa zaidi ya saa mbili.
“Tulianza kuufanyia uchunguzi mwili wa marehemu kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 6:45 mchana na tukagundua kuwa marehemu alifariki kutokana na mtikisiko wa ubongo kwa kitaalamu, Brain Concussion,” alisema daktari huyo. Alisema Kanumba alipata mtikisiko wa ubongo ambao husababisha kufeli kwa mfumo wa upumuaji (cardio-respiratory failure) “Kilichomuua hasa ni mtikisiko wa ubongo, ambao endapo unatokea katika sehemu ya nyuma ya ubongo (cerebrum), huua kwa haraka” alisema daktari huyo na kuongeza kuwa mtikisiko wa ubongo wa nyuma, husababisha matatizo ya mfumo wa upumuaji na hilo limeonekana katika mwili wake.
“Baada ya ubongo wake kutikiswa kwa nguvu, mfumo wa upumuaji ulifeli na ndiyo maana tumekuta kucha za Kanumba zikiwa na rangi ya bluu, huku mapafu yake yakiwa yamevilia damu na kubadilika kuwa kama maini, hizo ndizo dalili za kufeli kwa mfumo wa upumuaji.”
“Mtu aliyepata mtikisiko wa ubongo huweza kutokwa na mapovu mdomoni na hukoroma kabla ya kukata roho na ndivyo ilivyokuwa kwa Kanumba kabla hajafariki.”
Daktari mwingine aliyeshiriki katika uchunguzi huo ambaye pia aliomba jina lake lisitajwe alisema ubongo wa mwigizaji huyo ulikuwa umevimba na kushuka karibu na uti wa mgongo na hivyo kuathiri mfumo wa upumuaji.
Alisema sehemu ya maini na majimaji ya machoni ya marehemu, vimepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini endapo kuna sumu au kitu kingine katika mwili huo.


19 comments:

 1. That is possible and let us abide to that. I believe and will still believe what you is written above.

  The only remaining things for us is to pray so that God rest his soul in eternal peace, amount of people and prayers being made signify who was Kanumba. He was loved by many people and will always be The Great.

  Rest In Peace Steven Kanumba "Mwanadamu, aliyezaliwa na mwanamke, Ana maisha mafupi na yenye kujaa msukosuko. Amechanuka kama ua na kukatiliwa mbali, Naye hukimbia kama kivuli wala haendelei kuwako." Ayubu 14:1-22

  Mr. Anacleto Cirilo Pereira Jr.,
  Dar es Salaam.

  ReplyDelete
 2. DINA .. MIE HAPA BADO NASISITIZA SANA KWA WASANII WOTE NA WATU MAARUFU KIJAMII WAJIFUNZE CHOCHOTE KUTOKANA NA MSIBA WA KANUMBA, KWA KWELI KASHFA NYINGI TUNAZOZISIKIA JUU YAO (SIO WOTE BALI WENGI WAO) HAZIENDANI KABISA NA HESHIMA WANAOPEWA.

  KANUMBA KAZIKWA KWA HESHIMA ZOTE ZA KISEREKALI NA KIJAMII YAANI HAPO IMEKASORO BENDELA TU KURUSHWA NUSU MLINGOTI KWA SABABU ZA KISIASA.

  JAMANI MPAKA KOVA KUPIGIA SALUTI MAITI JAMBO AMBALO ASINGELIFANYA KWA KANUMBA HAI NA KAMA ANGEFANYA UNAJUA NINI KINGIENDELEA?

  HATA MIE SIJUI.

  ReplyDelete
  Replies
  1. Maiti yeyote hupigiwa salute na mwanajeshi anapokuwa na uniform,coz marehemu kijeshi hupewa cheo kinaitwa most senior!hata ww ukifa na Akitokea mwanajeshi akahudhuria mazishi yko na uniform lzm akupigie salute.mkuu hujapitia JKT?

   Delete
 3. RIP.lakini hiyo brain concussion.si inasabishwa na kusukumwa au kupigwa na kitu au kuanguka.ina maana kuna kitu kilitokea na kusababisha hivyo.na mwenye kujua ukweli ni lulu.at the end end,i feel sorry for the girl,her life won't be the same

  ReplyDelete
  Replies
  1. For sure Lulu's life wont be the same. whether found Gilty or not gilty... feel sorry or the young girl!!

   Delete
 4. we nae habari zako haziko update mbona upo nyuma nyuma hebu tembelea blog za watu wengine uone walivyoweka manews na picha kibao about bro steve mi unaniudhi

  ReplyDelete
  Replies
  1. Wats wrong with you,she is posting wat she is sure of ,she doesnt need to go thrw other blogs to gather material to post,sorry to say ur among those who goes to any direction that the wind blows,kama wameweka nenewez na picha kama unavyosema,hizo ni findinings zao,comeon!!!

   Delete
 5. Kanumba was under alcohol influence before his death... that is the key.

  ReplyDelete
 6. Amekwenda kwenye maisha ya milele! Na hataamka tena aliyotenda ndio yatakayomsaidia pamoja na dua zetu. Lakini Dina kuna kitu mi kinanikera sana sijui na bongo tuu au na kwingineko! Watanzania tuna penda kuhukumu jambo kabla hatujalifanyia uchunguzi, mitaani Huku ukimwambia mtu unaumwa atakusaili kama daktari na kukuambia kunywa dawa fulani. Basi mi nachooka sasa hili la lulu yamezuka utafikiri walikuwepo na ndio ulikuwa usiku wamelala ingekuwa mchana?

  ReplyDelete
  Replies
  1. Umenigusa ndugu yangu, tumwondolee hukumu kuchafka kwa Lulu ni magazeti ya udaku ili yauze, juzi nimemmsikia Wema akihojiwa na cloudsTv lakini walipo post wakaongeza chimvi na hawataki kutaja jina la chanzo kwa vile mi waongo.

   Tumpe mapumziko Lulu Mungu aliyekuwepo Siku hiyo anayajua yote tuache unafiki utadhani sisi wasafi. Wengine kwa umri wa Lulu hawawezi hesabu idadi ya mabwana wao na saa nyingine walikuwa wakilala na waume za watu je wangewafia? Tuache unafiki wabongo mtu awapo kwenye Hali Kama hii c kumhukumu kwani hili laweza mtokea mtu yeyote

   Delete
 7. Maji yakishamwagika hayazoleki kazi anayo lulu ya kujitetea maskini Ndio maana Jana kafichwa alivyopelekwa mahakamani wananchi hawakujua kinachoendelea pasingetosha mahakamani.

  ReplyDelete
 8. R.I.P Kanumba!
  Pole Lulu, mwalimu wako alikufundisha uigizaji, ukafunzu, akakufundisha mapenzi,ukafunzu sasa siamini kama wewe umemlipa kifo!

  ReplyDelete
 9. Hatuna haja ya kuhukumu kwa kuwa tuna amini sheria itafuata mkondo wake!
  Ila mkumbuke walikuwa wote saa saba usiku tena chumbani,leo kafa Kanumba mnasema hayo,Je angekufa Lulu ungetoa hukumu hiyo? Think before you act.

  ReplyDelete
 10. R.I.P Jembe letu Kanumba!
  Mimi nasikitika kwa kuwa tumempoteza actor mahiri sana ktk tasinia ya Bongo movie!
  Upande wa pili Wasanii mjifunze, Jembe lilikuwa linatembea na Mtoto.Sasa sijui huo ndio ukioo cha Jamii!
  Kwa namna yeyoye ile Lulu alikuwa ni mtoto sana kwa K.

  ReplyDelete
 11. Lulu let the Almight God be with u, in this matter!I believe you know the reality on what happened to Jembe K.but your too young to face such charges.

  R.I.P Kanumba!

  ReplyDelete
 12. Najaribu kumfikilia MZAZI wa Lulu, sipat picha atakuwa anajutia sana kumruhusu mtoto aingie kwenye uigizaji!

  Mmemfundisha uigizaji mpaka mapenzi, ona sasa!

  ReplyDelete
 13. Jaman dinna natamani kujua utaratibu wa diet yako masikini umependeza sasa ndo utakuwa msomali khaswaa.mungu akubariki sana mpendwa.

  ReplyDelete
 14. SALMONELLA neisseriaApril 16, 2012 at 4:00 PM

  i can conclude by saying that despites of its strongest the lion might be killed by a monkey.
  go in peace the lion of film kanumba the great

  ReplyDelete
 15. wah what aa lose!!! we loose the man of the game who can play its part !!!!

  ReplyDelete