Tuesday, April 17, 2012

SAJUKI NA WASTARA KIPIMO CHA MAPENZI YA KWELI AMBAYO YANAKUMBWA NA DHORUBA NYINGI

Hawa ni waigizaji katika tasnia ya  maigizo na filamu hapa nchini.Walikutana katika filamu ya mboni yangu na kuwa wapenzi.Katika mapenzi yao walivalishana pete za uchumba na hatimae kupanga kufunga ndoa.Siku chache kabla ya ndoa yao walipata ajali na Wastara kuvunjika kabisa mguu.
Watu wakajiuliza kweli Sajuki atamuoa Wastara pamoja na kukatwa kabisa mguu?Baada ya wastara kupona jeraha ndoa yao ikafungwa dada akitembea kwa magongo.Baadae alifanikiwa kupata mguu wa bandia na sasa anatembelea mguu wa bandia.
Mitihani haikuishia hapo katika familia hii ambayo wamejaaliwa mtoto mwenye mwezi mmoja na siku kadhaa.Sasa hivi Sajuki anaumwa sana maradhi ambayo yalifanya mpaka apelekwe India kwa matibabu.Inasemekana ana uvimbe tumboni,alipopelekwa India ilishindikana kufanyiwa matibabu maana Sajui alikuwa dhoofu sana.Akarudishwa Tanzania ili afanye matibabu na kurudisha angalau nguvu kidogo ya kwenda kuanza matibabu ya huko India.Miezi miwili ijayo atalazimika kusafiri kwa ajili hiyo.Watanzania wameombwa kushirikiana na familia hii kufanikisha hili ikiwemo michango ya pesa.
Nimefikiria huyu ni mwanamke tena bado binti lakini yupo na wakati mgumu sana wa kuuguza huyu mume.Inasemekana Wastara ni yatima mumewe ndio roho yake.Hivyo nikachukua shauri la kumuita kesho kwenye leo tena tuzungumze atupe picha kamili watanzania na tuone tunamsaidiaje katika mtihani huu.Anasema ameshalia sanaaa katika maisha yake maana kila kukicha anapata mitihani.Mitihani tumeumbiwa binadamu lakini je tunasaidiana vipi katika hiyo mitihani?usikose kesho kusikiliza.

23 comments:

  1. YOTE NI MITIHANI YA MWENYEZI MUNGU NA KWA UWEZO WAKE ATAWAONDOLEWA...AMIIN.. HUWA NAWAPENDA SANA HII FAMILY..KWASASA SINA LAKUWASAIDIA ZAIDI YA KUWAOMBEA KHERI...TUPO PAMOJA..NAPIA TUTAOMBA NO YAKE KM ITATOKEA KUNAKITU NAWEZA MSAIDIA.

    ReplyDelete
  2. ki ukweli hawa wanandoa wana mitihani sana yani kabla hawajaona mpaka wanaona asee inatisha, ndo ile wanasema jamani ndoa nyingine nuksi ndo hizi duh non stop asee wanajuta, lkn ni mitihani ya mwenyezi mungu wamuombe sana maana yeye ndio muweza wa yote Inshallah Mwenyezi Mungu awafanyie wepesi

    ReplyDelete
    Replies
    1. wacha kiherehere wewe,alokuambia wanajuta nani,mbona unakuwa sio mstaarabu? nuksi ni wewe usojua nini cha kusema na wapi!!ahla!

      Delete
  3. kilio.........naamini mungu yupo.Watanzania tujumuike pamoja kutoa michango yetu ya hali na mali.Katika tasnia ya filamu,sijaona wasanii wanaojiheshim kama Dada Wastara na Brother Sajuki. Mungu anamaana na mapenzi makubwa kwa familia hii ndiyo maana amewabariki kiumbe. Ni jukumu letu tuwasaidie watu ambao pamoja na umaarufu walionao, bado wanasimama kama familia yenye maadili.....nasshindwa kuendelea kuand...

    ReplyDelete
  4. eti ndoa nyingine nuksi ndo hizi duh non stop wanajuuta,,,,,,watu wengine sjui wakoje jamani.

    ReplyDelete
  5. Dina yaani kama huna imani thabit katika mapenzi hakika utaishia njiani.Me mwenyewe hapa ninavokwambia nina boyfrnd ambae naweza kusema sasa ni kama zaidi ya boyfrnd.Akiwa mdogo alichomwa sindano ya kuzuia polio vibaya akapooza mguu.So anavaa lichuma.Lakini maneno ya kejeli ninayopata toka kwa marafiki na ndugu acha2.Lakini ninachoshukuru mungu ananipenda sana na ananijali kuliko hata hao wenye maboyfrnd wazima wenye miguu yote.

    ReplyDelete
  6. kuna kitabu kinaitwa the secret mwambie wastara akitafute asome kitamsaidia sana

    ReplyDelete
  7. wengine hatuwezi kusikiliza kipindi chako tunakuwa tayari makazini, ungeweka namba za simu (Mpesa,tigopesa,airtelmanoy etc) ili tuweze kuchanga chochote tulicho nacho..maana watanzania tulivyo ni mabingwa wa kuchangia harusi na misiba kuliko msaada wa matibabu.Mungu awatangulie na awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu,pole wastara na sajuki.

    ReplyDelete
  8. hongera Dina kwa kuweka hii habari.binafsi sina malalamiko na Sajuki na familia yake.ni couple ya kistaarabu sana, na inauma sana kuona kwamba kwao mitihani haiishi.naimani ipo siku mitihani yote itakuwa historia.cha muhimu najua hii familia ni kipenzi cha watu wengi, na ninauhakika watu wengi sana wataitika wito wa kusaidia.njia rahisi sana ya kusaidia hata shilingi elfu moja ni kuweka namba zao za simu kwaajili yakuwatumia M-pesa,Tigo pesa,na Airtel money.dunia ni mzunguko, leo kwao kesho kwa mwingine,hakuna maana yakutoa mchango siku ya mazishi, au harusi, kama mtu unashindwa kumsaidia mtu akiwa katika ugonjwa.and thats what true love means right? weka namba zao Dina and lets help each other.LETS HELP SAJUKI'S FAMILY TODAY.Be Blessed All.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umenena vizuri, Dina weka namna ya kutuma hela hapa....weka namba zao za simu ili tuwasiliane nao kama tunataka kutuma hata kwa western union tufanye hvyo......

      Delete
  9. LEO MTU HUYU ANAUMWA KILA MMOJA ATAKUWA MZITO KUCHANGIA MATIBABU YAKE LKN KESHO AKIFA MUNGU AEPUSHIE MBALI WATAJITOA VIMBELEMBELE KIBAO KUCHANGIA MSIBA NA MASIFA KIBAO KUWA SAJUKI ALIKUWA VILE MARA ALIKUWA HIVI NA SARE ZITASHONWA PICHA ZITAPIGWA MIWANI NDIO USISEME NA PENGINE WENGINE WATAJITIA KUZIMIA KWA UNAFKI ILI MRADI WAONEKANE KAMA WALIVYOFANYA KWA MAREHEMU KANUMBA SIJUI BINAADAMU TUNAELEKEA WAPI SIKU HIZI?HATA IMANI YA DINI HATUNA KAZI KUIGA UPUUZI TU.

    ReplyDelete
  10. NAIMANI MUNGU ATAWASAIDIA PAMOJA NA MISAADA YA KIBINAADAMU MUHIMU NI KUMUOMBA MUNGU SANA KWENU YABIDI MJITOE MNO KWA MOLA WENU YEYE PEKEE NDIO MWENYE KUWEZESHA KILA KITU IBADA MSIISAHAU NDIO ITAWASAIDIA KILA LA KHERI KATIKA KUFAULU MITIHANI MNAYOPITIA

    ReplyDelete
  11. daah hawa wanandoa wanastahili pongezi kwanza ni atu walioshikamana sana na wenye moyo wa kupendana hawana maskendo tokea wapo pamoja wanastahili kwa kila tulichokua nacho tusaide mwenzetu kwakila hali aeze kupata tiba sijui kwa tulioko nje tunaweza kutuma kwa njia gani dina

    ReplyDelete
  12. ETI NDOA NYINGINE NUKSI..HIVI WEWE HAPO JUU UNAABUDU MASHETANI AU MUNGU?.....UKISEMA NUKSI UNAMAANISHA NINI?..KWA IMANI YA DINI YA KIISLAM MUNGU ANAPOKUPA MITIHANI KAMA HIYO NA UNAPOMKUMBUKA NAKUHSUKURU NA KUMUOMBA MSAADA BASI UNAFUTIWA DHAMBI ZAKO....MUNGU ANAJUA ANACHOKIFANYA KATIKA HIYO FAMILIA...NA ANAJUA ALICHOKIPANGA...KILICHOBAKIA NIKUWASAIDIA KATIKA HALI NA MALI NA KUWAOMBEA DUA MUNGU AWAPE NGUVU NA APONE HAYO MARADHI YAKE WAISHI KWA AMANI NA FURAHA ZAIDI...TUKO PAMOJA NAO INSHALLAH KAMA KUNA CHOCHOTE TUTATOA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwanza alomwambia kuwa wanajuta nani,jini mkubwa yeye,kama anakosa ustaarabu in public hasa kwa mambo mazito kama haya basi sijui in private akoje,shame on u up there!!!

      Delete
  13. pole wastara na Sajuki Mungu awatie nguvu wasomaji wa blog hii tujitoe kuokoa maisha ya mpendwa wetu

    ReplyDelete
  14. kwa kweli binadamu hatujakamilika mimi ni shabiki mkubwa wa Sajuki niliumia sana siku niliyomuona akiongea sikuamini km ni yeye kweli nilishika kichwa nikapiga kelele ndugu yetu anaumwa tena anaumwa sana tufanye maombi ya kila hali ili alwah amuondolee huu mzigo wa maradhi naamini hatima ya mardhi yake iko kwa alwah, tuko pamoja familia yote ya sajuki na mkewe mungu alishasema kiumbe yoyote asiyekubali mitihani yake siye mja wake

    ReplyDelete
  15. WASTARA MDOGO WANGU USILIE HII NI MITIHANI YA MUNGU UWE MSTAAMILIVU KWA HAYA YOTE OMBA SALI SWALA ZA USIKU NAAMINI ALWAH YUPO PMOJA NA WEWE UTAUSHINDA HUU MTIHANI ULIOUPATA

    ReplyDelete
  16. Hongera Dina kwa kutuhabalisha!Wastara na Sajuki ni familia ambayo ina maadili mema na tunaweza kujifunza vitu vyingi kutoka kwao, toka mwanzo wa uchumba wao na mpaka hapa walipo, Katika ulimwengu huu kuna majaribu na mtihani mingi, Mungu aliuumba hivyo vyote ili kupima subra,na uvumilivu wetu ili kukubalina na vyote hivyo atuna budi kukabiliana navyo. Tuko pamoja nao katika wakat huu mgumu kwa Wastara na kumuombea pia ili Mungu aweze kumvusha katika wakat huu mgumu.

    ReplyDelete
  17. Dada Dina sisi mimi ni kazi wa mkoani sina uwezo wa kwenda kumuona brother Sajuki na Dada Wastara, lakini tunaweza tukafanya kitu kama wadau wa Blog yako. Angalia uwezekano wa kutupa njia na sisi watu wa mikoani tushiriki katika kutoa michango yetu ya kifedha japo ni kidogo lakin nahisi itasaidia.Dada Dina tufanye sasa....wakati ni huu...Dada Wastara kuwa na subra kama aliyokuwanayo Brother Sajuki, tupo pamoja kwa sala,dua na maombi.Dada Dina fanyia kazi ombi langu na kama lipo nifahamishwe

    ReplyDelete
  18. jaman mumsamehe huyo alileta habar za kichwa naona amedisconnect ubongo sasa anatumia kamas kufikiri

    ReplyDelete
  19. jaman polen xna Sajuki na Wastara, Mungu ana makusudi yake msivunjike moyo mwendelee kumshukuru kwa kila jambo. tunakuombea bro. Mungu atakuponya soon!

    ReplyDelete
  20. pole sana dada kwa mitihani unayopitia uwe mvumilivu MUNGU WETU ni mwaminifu atamponya na kumrudisha katika hali ya kawaida

    ReplyDelete