Nilisema nitakwambia kwa nini wimbo huu unaitwa MBONI YANGU.Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.Thanks kwa coordinator Ruge Mutahaba & Dina Marios
Director Mwasiti Almasi
Producer Tuddy Thomas














dah!pole sana sajuki MUNGU atakuhafu.ila nimejifunza jambo moja kuwa movies za kibongo hazilipi,utaigiza picha kibao bt stil umaskin uko palepale,wasanii jipangeni.wanafunzi somen msikimbie shule kisa kuigiza movies,mtaishia kupata umaarufu2,somen mjiwekee strong economic base.watanzania tujitokeze kwa wingi kumchangia juma kilowoko
ReplyDeletehongera dina,mungu atamponya sajuki,leo mko offline kwaiyo nimepitwa sana na huo mpango wa kuchangisha,bt well done.
ReplyDeleteDina Unastahili kupewa Hata tuzo kwa kazi unayoifanya kwa jamii, hii kweli inatia moyo na siku nying nakukubali sana..anyway waTz tujitokeze kwa wingi katika kuchangia matibabu ya mwenzetu mtanzania mwenzetu Sajuki, plz plz huku kwetu nitawahamasisha wenzangu tutoe tulichonacho. Dina na wasanii wote mliojitolea kutengeneza wimbo huo bila kuwasahau waheshimiwa Mungu Awabariki sana...na Watanzania wote mtakao changia na wale ambao hawatachangia inawezekana wakawa hawana ila kwa namna moja wakawa wanachangia kwa maombi yao...Mungu Awabariki.
ReplyDeletehuyu sio ananyonywa na jini subiani kweli?
ReplyDeletejini subiani kapewa na baba yako!!!!? au wewe ndo mchawi wake??? mwana*****u wewe!! loh watu wanaongea ya maana wewe unaleta pumba. shetaani wewe ushindwe. dina bwana comment nyengine usiweke zinatia kichefuchefu. watz tuwe na moyo huyu kichaa asitubadili mawazo
DeleteAnonymous wa saa 05:41 am sidhani km anonymous wa saa 03:20 am km kasema vibaya kwasababu hayo mambo ya majini yapo na yanatesa wanadamu kwel naisi umemuelewa vibaya na kila mtu ana imani yake,yeye anaamini majini wewe na yule mnaamini microscope ya Mzungu so tuache kuchambana pasipo sababu jamani.
DeleteDinah mie nashauri msanii Sajuki aende kwenye maombi Nigeria kwa Prophet TB Joshua wa SCOAN (Synagogue church of all Nations) Watu wengi wamekuwa na matatizo kama hayo ya uvimbe na mengine zaidi na wamepona kutokana na maombi ya Prophet huyo TB Joshua. Ukitaka kushuhudia angalia TV Emmanuel
ReplyDeleteWEWE huyu T.B unamjua vizuri? kwanza anatumia nguvu za giza au unataka Sajuki akafie huko? maadam Madaktari walishajua tatizo lake, changa pesa acha uswahili.
DeleteHuyo TB.Joshua ni mwongo kufuatana Na wafanyakazi wake waliofichua Siri. Tumchangie Sajuki. Mungu atupe moyo wakuchangia Na amponye ndugu yetu, nilipoona mboni yangu niliwaza ni Sajuki tu, Kwani ile movie ilinisisimua sana.
DeleteHata mimi nilikuwa natafuta namba ya Wastara nimwambie kuhusu hili la kwenda kwa Prophet Joshua Nigeria...Najua ni waislamu ila wangejitahidi pia wapate hata anointing water tu kama watashindwa kwenda Nigeria...hayo maji yatamsaidia wakati akisubiri kwenda India kwa matibabu. Pia aangalie emannuel tv wakati wa maombi ya kuombea viewers all over the world basi ashike screen. Please Dina mshauri na hili pia wakati anasubiri kwenda kwenye matibabu.
Deletemmmh kina ray wako wapi JB Cheni n.k mbona hatuwaoni
ReplyDeletewanasubiri afe wawe kimbelembele kubeba jeneza na kupiga picha kuweka kwenye mtandao
DeleteJaman dada Dina....huo uvimbe wa sajuki ni wa aina gani mpaka aende India..???mbona hapa KCMC watu wenye matatizo kama hayo wanafanyiwa operation na wanapona.....wats up wid him...???au ts something else mi sijaelewa....Jaman Sajuki.......
ReplyDeleteSidhani kama madaktari walioshauri apelekwe India ni wajinga hawajui kama KCMC kuna hayo matibabu.Na mtu haanzi tu kujipeleka India madaktari wakishindwa ndio wanashauri mtu apelekwa wapi kwa matibabu zaidi ili kuokoa maisha yake.
DeleteDina tuwekee sehemu ya LIKE ktk comments kwani nimependa sana majibu yako,ninge like mara 100.
DeleteINSHAALAH KHERI MUNGU ATAUWEZA KILA MMOJA WAPO...... INANIUMA IMENIKUTA WAKATI SINA UWEZO WA KUMSAIIDA LAKIN INSHAALAH KHERI IPOSIKU NAMI NTAWEZA KUWATAFUTA NA KUJITOLEYA JAPO KWA KIDOGO.
ReplyDeleteHuyu nae anonym 4 mmh .Utapona Sajuki Kuwa karibu na Alwah watanzania tujitokeze kwa wing .Hata sh. 10 yako yaweza kuwa mchango mkubwa kwake.
ReplyDeleteMwenyezi Mungu akuzidishie Dina.
ReplyDeleteyaani mpaka chozi lanitoka kwa upendo mnaouonyesha.Mwenyezi Mungu mwingi wa wa Rehema awabariki na kumponya mwenzetu. ushirikiano huu ni Adhimu.
ReplyDeletedina nalia kwny ofisi ya serikali, sio namlilia sajuki alivyokonda la hasha nalia kwa ajili yako dina, una moyo wa ajabu sana wewe, sidhani kama bila wewe hata komedy jana wangeomba michango kwa waheshimiwa, hakukuwa na nguvu yoyote kuhusu kumsaidia huyu kaka jamani nakuombea kila la kheri mpenzi. nampa pole sana sajuki kwani kuugua co kufa na nisehemu ya mitihani ya mwenyezi mungu. NAKUPENDA SANA DINA!
ReplyDeleteKwa kweli Dina sikutegemea kumuona Sajuki hivi alivyo yaani roho inaniuma sana lakini yote ni mipango ya mungu nasi tunaendelea kumuombea kwa mola.Nawe mungu akuzidishie kutokana na moyo unaoonyesha kwa jamii.
ReplyDeleteMUNGU akubariki dada Dina kila uamkapo na ulalapo maana mambo uwafanyiayo watu hakika yanampendeza MWENYEZI MUNGU
ReplyDeleteDina, M/Mungu azidi kukujaalia na moyo wako wa huruma, inshaalah! Umeletwa duniani kwa sababu, na sababu zenyewe ndo hizo. Longo live Dina
ReplyDeletePole sana Sajuki,watanzania tufanye jitahada Wastara asipoteze mboni yake 'Sajuki'.Hongera sana Dina na nyote mnaofanya jitihada kwenye kuhamasisha uchangiaji huu wa matibabu ya Sajuki.Dina kuna kipindi Sajuki aliwahi kwenda India,ila madoc walishindwa kumfanyia op kwa sababu ya hali ya udhaifu aliyonayo na aliambiwa arudi nyumbani ili apate kugain kidogo,je!kuna sababu zozote za ongezeko ili la gharama za matibabu?
ReplyDeleteTimu iliyoshiriki kwenye wimbo huo ni watu wazito sana,na ni matumaini yangu kama wangefanya maamuzi magumu 12Mil isingewashinda,japo natumaini walitoa chochote na si kutia sauti tu.
Kwenye msiba wa Kanumba takribani 72Mil zilitumika,japo mpaka leo kuna zengwe kwamba kulikuwa na fedha zaidi ambazo kamati inashutumiwa kuzitafuna.Muungano wa wasanii uko wapi?juhudi zilizotumika kuchangisha kwenye msiba wa Kanumba kwanini hazifanywi kwenye ili la Sajuki?kwa mujibu wa Dina nadhani salio ni 12Mil tu,au mnasubiri afe mchangishe mara 3 yake?
Dina na wadau wote,bila kumung'unya maneno nachelea kusema wasanii wa bongo movie ni wanafiki wakubwa,wanajiita mamilionea lkn kwenye ili wanashindwa kusaidiana,au labda wanaangali nani kafikwa na dhahama.Sote tunakumbuka Mzee Kipara alipoanza kuumwa mpaka umauti ulipomkuta.,maskini Kanumba aliemsaidia nae ametangulia mbele ya haki.
Mwisho namuombea kila la heri Sajuki,Mungu atakuafu Insha'Allah
Nakuunga mkono Manyuva, yani wasanii wa bongo movie hawana lolote ingekuwa pati ungewaona na ma makeup yao na walivyovaa uchi, kusaidiana kwenye matatizo hawaonekani. Kujidai tu kuishi maisha ya ufahari ya kulazimisha. Kwasababu hili swala la kuchangisha lilitakiwa lianzie kwao. matokeo yake watu wengine Kabisa wamelianzisha. Yani hata watu wa bongo flavour wamewashinda...wamejitoa ipasavyo yani mpaka nimewakubali i see....keep it up Dina and your team!! May almighty God bless you all always!!!!
DeleteJaman nampa pole sana sajuki na mkewe wastara...yan sina cha kufanya zaidi ya kumuombea kwa mungu....
ReplyDeletelakini dina hili jambo tuwe tunafanya kwa watu wote maana watanzania wapo wengi wenye hayo matatizo na hawana uwezo wa kufanya chochote..na sio kwa mtu maarufu tu.
ahsante
Kweli nimeamini sisi ni maua unaweza kung'aa na na kunyauka kwa mda mfupi lakini nimeshtuka zaidi nilipoiona hiyo picha ya Sajuki alivobadilika.
ReplyDeleteNaamini Mungu ni mwema na kila tulifanyalo kwa ajili ya Sajuki linamaanisha maombi kwa mwenyezi Mungu. Mungu amtupi mja wake.
Ubarikiwe Dian na Couds fm kwa ujumla kwa kuijali jamii yetu.
Mungu amsaidie apone na wote mnaojitoa kwa ajili yake mbarikiwe muongezewe mnapotoa
ReplyDeletewewe anon wa may3,2012;05;41 asante kwa kunitu*****..i mimi hilo nimelisema kwa kulijua ila ndohivyo nisiseme mengi pamoja madk wamemwambie aende huko India bado mimi ninatumai hata hapa anawezaakatibiwa maana madaktari wetu wakati mwingine wanafanya makusudi kama hujawafatilia kwa umakini au ukajitia katika namna yakuwa nao karibu.mfano mimi ninayeandika hapa kulikuwa na jamaa mmoja anumwa disk za mgongo tulikuwa tunaumwa wote na mimi basi yeye kwa pesa zake akakimbilia India basikwenda kule wakamfanyia operation ya neururol sugery mpaka akapararise mwili wote mimi nikamwendea dk mmoja anaitwa PROF.KAHAMBA akanifanyia hapahapa ugonjwa huohuo nikapona kwahiyo hapa wataalamu wapo ilawatu wengi wanapenda kukimbilia India.pamoja na hivyo mimi ninamuombea sajuki afanikiwe na apatiwe matibabu sahihi awezekupona
ReplyDeleteunajaribu kusema nini? bado sijakuelewa kabisa!
DeleteHATA MIMI NIMEKU...... NGOJA DINA AIPUBLISH UTAONA,WEWE KM UNAAMINI MAMBO YA KINA SUBIANI NI WEWE,KILA MTU NA IMANI YAKE USITULETEE HAPA,BORA UNGESEMA KUNA PROF KAHAMBA KULIKO KUNYONYWA NA SUBIANI,AU WE MWENZETU ULIKUWA UNANYONYWA NA SUBIANI NDO MANA UNA UZOEFU?UNAROPOKA TUU WAKATI WATU WANAHANGAIKA KUMSAIDIA MTZ MWENZETU APONE,HILOOOOOO
Deletewatu wazima mnaongea km watoto ebu acheni mnaker a sasa hasa nyie wawili hapa juu yangu naweza sema mna tabia mbaya mwenyewe anajieleza kwa upole mnaleta nyodo mnapinga mambo ya majini wakat mnashinda kwa waganga kila siku non-sense kabisa.
DeleteHongera sana Dina na pamoja na uongozi mzima wa Clouds Entertainment kwa harambee kubwa mliyoifanya ya kumchangia SAJUKI. Hakika mungu atawalipa mema. Naamini ya kudra zake ALLAH sajuki atapona na kurejea katika hali yake ya kawaida na kuendlea na shuhuli zake za kila siku kwani kuugua si kufa na tuko pamoja katika maombi kuhakikisha unarudi kama siku zote. Ama kweli hujafa hujaumbika. Naomba unipe maelekezo juu ya kudowload wimbo wa mboni yangu kupitia namba 0752348766. Be blessed
ReplyDeletePole sana kaka,Hakuna jambo linaloshindikana kwa mungu nenda kanisa la Siloam pale maeneo ya mwenge atapona haijalishi tatizo linamda gani lazima utapona tu mtangulize mungu kwa kila kitu
ReplyDeletekaka tunakuombea kwa mungu ili hali yako iludi kamazani mahana watanzania wote kwa ujumla twakuombea ww ili upone A meni..
ReplyDeleteEe mwenyeenzi Mungu, Mungu wa rehema uliyekaa mahali patakatifu msaidie mja wako Sajuki, muonee huruma Wastara, watie nguvu wote wanaoshughulika na matibabu yake. waongezee wote wanaojitoa. wasamehe wote wanaonena mabaya juu yake.Hatuna msaada mwingine pasipo wewe.AMEN.
ReplyDeleteOrodha yote hiyo ya waimba nyimbo ya nini kama siyo kumdhalilisha tu, kwanini nyinyi wenyewe msimchangie kwanza. Mnamdhalilisha tena sanaaaaaaaaaaaaaaaaa.
ReplyDeleteMnapofananisha mchango wa matibabu ya Sajuki na msiba wa Kanumba, mnasikitisha, Kanumba keshatangulia mbele ya haki, kinachotakiwa ni kuhamasishana tuweze okoa maisha ya mwenzetu,sio mada zilizokwisha pita.
ReplyDeletetunaomba up-dates dada dina kuhusu matibabu ya sajuki wengine hatujasikiliza redio leo.nachukua nafasi hii kukupongeza kwa juhudi zako.mungu atakubariki kwa moyo wako!!!
ReplyDeletePole sana Juma Kilowoko, Mungu atakusaidia utapona ili uendelee na shughuli zako za kila siku, Pole nawe Wastara, yote ni mitihani ya duniani, ila Mumeo atapona tu, Mungu mkubwa.
ReplyDeleteJAMANI NIMEUONA NA KUUSIKIA HIYO NYIMBO YA MBONI YANGU DUU IMENITOA MACHOZI DINA INAHUZUNISHA SANA JAMANI DAAAA NIMENDA SANA ALIPOINGIA AFANDE SELE,FIDQ, NA CHID BEZZ SIJU SABABU NAPENDA HIPOP.. WENGINE PIA NAWAPONGEZA SANA KWA WALIVYO WAKILISHA. LAKINI DINA SIJAAELEWA ALA HUO WIMBO INAKUWAJE? TUFAHAMISHE TAFADHALI..HONGERA SANA NA WEWE..
ReplyDeletekwanza natoa shukrani kwako Dina kwa moyo wako wa upendo mwenyezi mungu akuongezee, vile vile natoa pole kwa kijana mwenzetu Sajuki mungu yu pamojanae ataponya, mi nilpoiona hii picha machozi yalinitoka ila tupo pamoja nitatuma kidogo nilichnacho ili kiweze kusaidia matibabu yake.
ReplyDeletepole sana Dina kwa kazi uliyonayo,mwenyezi mungu akuzidishie kwani uumekuwa mstari wa mbele ktk mamba ya kijamii, vile vile napenda kumpa pole ndugu yangu Sajuki kwa matatizo ya kiafya mungu yu pamoja nae, tuko pamoja ktk maombi na kwa kila hali.
ReplyDeleteMUNGU NI MUAMINIFU NA AHADI ZAKE ZINA DUMU MILELE,MUNGU ALIMRUHUSU SAJUKI KUJA HAPA DUNIANI COZ HE HAD GOOD PLANS FOR HIM AND SO THE PLANS ARE STILL THERE! KWENYE BIBLIA IPO SEHEM INASEMA''I HAVE GOOD PLANS FOR YOUR LIVE,I HAVE PLANED FOR GOOD AND NOT FOR EVIL'' NINA AMINI HIVYO.God kindly give Sajuki more nd more faith and the healing from up above as i believe in you and so does he. Av never meet sajuki but i have a strong inner feeling for him and the family,ur all in my prayers!!
ReplyDeletepole sana wastara mana hilo ni jaribu lako, amini Mungu atakushndia ktk yote uyafanyayo! pole saaaa....! bt majaribu ni mtaji.
ReplyDeletepole sana wastara Mungu ni wa wote hivyo atakuona tu wala usjal mpendwa wngu mwamini mnyaz MUNGU atakusaidia
ReplyDeleteNi vizuri kama pesa ya matibabu imepatikana kwa njia hii..lakini natoa kero yangu kuhusu wasanii wa bongo movie kupenda starehe na kujikweza kwenye party ilhal mwenzao anaumwa hata kuchangia laki hakuna!!Blog moja nimeona eti msanii anajitapa kavaa nguo ya Dola elfu mbili!!inaleta kwel maana?kichefuchefu zaid yuko nyumba ya kupanga..jamani tusipende maisha yasiyokuwa yetu
ReplyDeleteEe mwenyez Mungu wa rehema wabariki wote walomchangia sajuki na waliohamasisha wananchi katka hil.Kweli hujafa hujaumbika, nktazama hyo picha inanitia uchungu saana.Mungu amtie nguvu Wastara hasa ktka kpind kigumu hiki.Ee mungu uliempitisha dada huyu ktk magumu ya nyuma msaidie,familia yake bado inamuhitaji.
ReplyDelete