Thursday, August 23, 2012

MAMBO VIPI WALE WENZANGU TULIO KATIKA MAPAMBANO YA KUPUNGUZA MWILI??

Habari za wakati huu ukisoma ujumbe wangu huu kwa ajili yako wewe uliye katika mapambano ya kupunguza mwili na kujijengea afya iliyobora.
Kwanza nawapongeza wote mliofatilia kwa kina ile diet niliyotoa wakati ule na napenda kufahamu mnaendeleaje??pls naomba basi mnipe matokeo???
Pili naomba radhi kwa wale ambao sikuweza kuwajibu nimeamua diet ile nitaiweka hapa ili iwe rahisi maana email zimenielemea sana.Hasa kwa wale ambao hawakuniandikia kwa muda muafaka.
Kubwa lililonileta....nina habari njema.Unakumbuka niliahidi kutoa nafasi ya kushiriki katika mazoezi na mimi gym ya AZURA?Haya ndio nimekuja kukupa hiyo nafasi.

VIGEZO NA MASHARTI.
1.Uwe tayari kushiriki nami katika hii safari ya kupunguza mwili,kuwa fit na mwenye afya.Nikisema uwe tayari nina maana hutaanza visingizio vya kutokuja mazoezini.
2.Pia uwe tayari kushare kila tutakachokifanya na wadau wengine wa blog,maana napenda tuonyeshe njia tunazopita hadi tukakapo pata matokeo mazuri.
3.Kwa nini unataka kupunguza uzito?unaitwa nani,unaishi wapi,una kilo ngapi kwa sasa?

AZURA watatupa trainers,dietitians atakaetupangia chakula cha kula kulingana na mwili wako.
AZURA fitness club wapo kawe baharini kabisa,ukiwa unaniandikia zingatia pia urahisi wa wewe kufika kila siku.

Kwa kuanza nitachagua watu wawili tu,Upo tayari?haya niandikie hapa hapa.

47 comments:

 1. Mr. Malangahe JosephAugust 23, 2012 at 5:06 AM

  Kwa nini unataka kupunguza uzito: Uzito wangu na kimo haviendani kabisa, natakiwa niwe na kilo 64 kulingana na kimo changu, unaitwa nani: Mr. Malangahe Joseph,unaishi wap: Nyegezi jijini Mwanza,una kilo ngapi kwa sasa: Nina kilo 84

  ReplyDelete
 2. Nashukuru kwa hii opportunity.

  Naitwa Angela naishi mbezi beach na nina kilo 75.Napenda kufanya mazoezi na nimeanza kufanya mazoezi kwa makini kutokea Februari mwaka huu lakini mwili wangu unazidi kuongezeka tu na sijui ni kwanini kwa hiyo nahofia nisije kuwa obese coz natry alomst everything but naincrease tu so natumain hii opportunity itanisaidie kurudia hali yangu ya kawaida especially tumbo. Naona pia itanisaidia kupata motivation nikipata watu wakishirikiana kwenye maswala haya.

  Kazi yangu tunawahi kutoka na sidhani kama mda wa kwenda gym ni tatizo na pia napita hiyo gym kwenda home na haitakuwa ngumu kufika pia.
  Natumai nitapewa hii chance.
  Angela.

  ReplyDelete
 3. Mmh! Dina, mbona kama nawe umeanza tena kunenepa? au hiyo picha ni siku nyingi?

  ReplyDelete
 4. dada niko tayari but wa mbali tunafanyaje maana mie nipo arusha jamani woinde shizz

  ReplyDelete
 5. OK.. BAHATI HIYO MLIYOPO BONGO C YA KUCHEZEA TENA MI BADO NAJIANDAA NA ILE DAYAT ULIYONITUMIA NIKIWA TAYARI NATAKUTUMIA MY PICTURE WAKATI NAANZA..THAN U MDADA

  ReplyDelete
 6. habari naitwa Oliver Samson naishi sinza nina kilo 98 natka kupungua ili niwe na afya njema maana kwa sasa nikitembea kidogo tu nimechoka. pia hata nikivaa nguo sipendezi . nikipata nafasi hii nitashukuru sana

  ReplyDelete
 7. Helo dina mi naitwa Janeth napenda kushirik nawe katika hilo zoez ingawa sina mwil mnene ila napenda kuwa fiti nina kilo 54 naishi kinondon.nakuahidi kushirik hilo zoez kikamilifu my dear!

  ReplyDelete
 8. Helo dina mambo vp? Naitwa Janeth naishi kinondoni mi si mnene nina kilo 54 but napenda kuweka mwil wngu fit kwa afya bora. Nakuahid ntashirik kikamilifu mazoez hayo!

  ReplyDelete
 9. Katika utakao wachagua usimsahau shoga yako gea msaada unaazia nyumbani kwanza

  ReplyDelete
 10. Hellow Dinah,nataka nipunguze mwili kwa ajili ya afya yangu maana nimekuwa mzito kuliko height yangu.Naitwa Sophy, Naishi Tabata, nina kilo 80 kwa sasa nitafurahi kama nitakuwa mmoja wa wawashiriki na wewe katika hayo mazoezi.

  Thankx in advance

  ReplyDelete
 11. habari Dina.....
  mi naitwa Atuganile,naishi kijitonyama
  nna kilo 97 saivi na nina miaka 26 tu,mi ni mfupi kwa hiyo kitaalamu nimeambiwa nnatakiwa nipunguze uzito mpaka at least kilo 60..pia nataka nikivaa nguo nipendeze maana mwili nlionao saiv hata sijioni napendeza..
  please naomba niwe mmoja wa utakaowachagua please

  ReplyDelete
 12. Mpendwa Dina,ni muhimu sana kupunguza mwili kwa mazoezi,nashukuru kuwa kuna wataalamu watakaotoa ushauri wa `lishe' kwani wengine tunakosea, mtu ukitoka kwenye zoezi, unaendea kiti moto, kibobori, nyama choma, nk, maana hapo utakuwa kama vile una mwaga maji kwa kopo, halafu unaongeza kwa ndoo.

  ReplyDelete
 13. Naitwa Faith, nakaa sinza nafanya kazi mjini, nina kg 115, nataka nipungue maana nimenenepa sana na nimejaribu kupungua kwa muda mrefu nimeshindwa. Naomba niwe mmoja wa utakaowachagua

  ReplyDelete
 14. Hi Dina! nashukuru sana kwa habari hii nzuri.je naweza pata tena nami hii diet?

  ReplyDelete
 15. Mpedwa Dina naitwa Lucy,nina kilo 84 nataka kupunguza mwili kwani ni hatari kwa afya kuwa na uzito mkubwa, napenda niwe na kilo 75. Naomba niwe mmoja kati ya utakao anza nao. Ahsante kwa kutushirikisha

  ReplyDelete
 16. hi D, MIE NAPENDA KUPUNGUA SANA NA NINGEPENDA KUSHIRIKI NA WEWE KATIKA HILO ZOEZI LAKO LKN NAFANYAKA KZ POSTA KUTOKA OFSN SAA 11 NAISHI MWENGE NAFIKA LATE HM BY SAA 2 JE UTANISAIDIAJE ? NILIKUWA NA KILO 92 SASA HIVI SILI MCHANA NAJINYIMA NIMEPUNGUA NA KILO 88 NATAKA KUPUNGUA TENA HASWA MIKONO NA TUMBO NDIO TATIZO LANGU ILA MIE MREFU KAMA WEWE YAANI KAMA VILE TUNALINGA MWILI.

  EVE

  ReplyDelete
 17. Habari Dinna me nisaidie me naitaji kuongezeka nifanyeje sipendi wembamba angalau niongezeke kidogo umri wangu na uzito ni tofauti what can i do

  ReplyDelete
 18. Naitwa salma naishi Kigamboni ninakilo 70.9 na ni mfupi na ni mfupi natakiwa kupunguza uzito nilionao. Kwahiyo ninataka nifanye mazoezi angalu niwe na kila 60 au 65

  ReplyDelete
 19. mi naitwa grace. nina kilo 72, nataka niwe na kilo 60. napenda hasa kupungua tumbo maana baada ya kujifungua ndipo uzito ulipoanza ghafla. tafadhali naomba hiyo chance maana sijawahi kupata chance kama hiyo.email yangu ni mmandag@yahoo.com

  ReplyDelete
 20. Me nilianza vzr diet na ww na nikawa naenda gym hapa karibu na home nikaloose 5 kg toka tume anza ila week iliyopita nimejigundua nimeconsive so nguvu zimeniishia itbidi nifanye diet ndogo sio kiasi kile na mazoez kiasi kwakuwa sasa am expecting will be back nikijifungua ila nilikuwa naendela vzr sana hadi nilifurahi ila ndo hvo tena mtoto naye muhimu kila la kheri

  ReplyDelete
 21. Hellow,am Hellen Stephen,25yrs old,am weight is 67,staying at sinza kijiweni.The reasons want to loss weight is that,first,want to be healther and fit,becouse gt heart problem n fell to control my body weight gv alot difficult in breathing smtime.Second,want to be free when am with ma frnds bcs smtime i do feel inferior towards them,lastly,want to be proud of my body cs realy smtime i do hate my body especial my berry.Thank u hope u will consider me cs am ready to do anything for my body.be blessed.

  ReplyDelete
 22. hello Dina,pole na kazi
  mi ni mmoja kati ya wale wa diet ile ya mwanzo,maendeleo ni mazuri nashukuru,natamani ningepata nafasi hii ya sasa lakini ndio hivyo nadhani ni kwa ajili ya watu wa dar waliokaribu,nitakutumia picha zangu nilipofikia.Asante sana.

  ReplyDelete
 23. hapo chacha, kumbe me hata nisipoomba manake nimeona kuna wahitaji zaidi yangu.

  ReplyDelete
 24. naitwa mary nina kilo 85 natakakupunguza kwaajil umri wangu hauendan na umbo langu pia hata kimo changu pia nipo teyar da dina maana nilikuwa nataka nipunguzmwil

  ReplyDelete
 25. hi dada dina naitwa mary nakaa mabibo nataka kupungua kwaajili umri wangu haundan na mwili wangu na sababu za kiafya zaid nipo teyar tena kwa moyo mmoja nina kilo 82 nitashukuru kama utanichagua

  ReplyDelete
 26. Naitwa Emma Kahere naishi sinza madukani,kwa sasa nina kilo 89.kinachonifanya nihitaji kupungua ni kwasababu uzito unanifanya nishindwe hata kuinama na cwez kufanya hata kazi za msingi na mwil unanifanya nionekane kama mmama wakat mi nina miaka 24 tu;‎؛vile vile ni vizur kiafya kufanya mazoezi؛‎;na ninazid kumuomba Mungu ili nipate hii nafasi kwan utakuwa umenisaidia sana Dina.

  ReplyDelete
 27. DUH YANI MM NINA KILO 108 NANINATAKIWA KUA NA KILO 64 KUTOKANA NA KIMO CHANGU,NI HATARI KWAKWELI SIJUI HATA PAKUANZIA.........MSAADA TUTANI

  ReplyDelete
 28. NAITWA EGGY NINAKILO 75 NAPENDA KUWA NAKILO 62 KUTOKANA NA UREFU WANGU. NAISHI AIRPORT ILAKUJA GYM HAKUNA TABU NITAFIKA2. HOFU NINAKIMO CHUO SASA SIJUI MAZOEZI YANAANZA LINI UNGETUMA MUDA TUNGEJUA VIZURI JINSI YA KUJIPANGA MAMY

  ReplyDelete
 29. Dina, mi naungana na huyo mwenzangu hapo juu anayetafut kuongez uzito niko underweigh na siumwi wala nini, tusaidie na sie diet

  ReplyDelete
 30. na mimi jamani tupe tips sie wa mikoani

  ReplyDelete
 31. Hi Dina naomba uweke tena hiyo diet manake ya kwanza ilinipia. Asante

  ReplyDelete
 32. Hi Dina naitwa Rahuwiya na kg 130 nimejaribu sana kupungua lakini end of the day bado nipo hapo hapo natamani nipinguze japo nifike 90 kwa afya yangu maana maisha ni mafupi sana tunapokwenda pabaya ningependa uniweke kwa list yako plse.

  ReplyDelete
 33. mambo da dina mimi Magreth. uzito wangu ni 62 napenda sana kufanya diet ila sijapata mtu wa kunielezea, mm ni mkazi wa dar es salaam kimara
  naomba rudia tena ....
  Asante kazi njema

  ReplyDelete
 34. mambo da dina mimi Magreth. uzito wangu ni 62 napenda sana kufanya diet ila sijapata mtu wa kunielezea, mm ni mkazi wa dar es salaam kimara
  naomba rudia tena ....
  Asante kazi njema

  ReplyDelete
 35. Hey dina mambo,am harrieth, uzito wangu ni kg 95, napenda sana kupungua nimejaribu kufanya mazoezi nakatishwa tamaa pale rafiki wanaposema sita pungua mie ni mbantu, waafrica hatupungui hii sijaipenda napingana nao kila siku, pili ni afya nzuri naitafuta kuepusha maradhi maana nilishapata problem ya kuvimba miguu sometimes inatokea, siwez tembea na viatu virefu mda mrefu nachoka na miguu inauma uzito umezidi na mie mpz wa viatu virefu, ningependa nijiunge nione km kweli naweza pungua nakuwa fit, asnte ubarikiwe

  ReplyDelete
 36. Mi naona utoe kipaumbele kwa wale obese, maana hata mtu uwe mrefu vipi kilo kuanzia 90 ni hatari

  ReplyDelete
 37. Kuna watu vibone jamani; mi hata nilipokuwa na ujauzito sikuwahi fikia kilo 80...sasa mtu ana kilo 90 mwingine 130. Kuweni na nia hakuna mwili unaogoma kupungua kama kweli nia unayo. Kuleni kwa kiasi otherwise hata ukijinyima kula kabisa haitasaidia endapo hiyo milo miwili unayokula ni funga kazi.

  Na alowadanganya ku skip lunch kunapunguza mwili nani???? Kama ingekuwa hivyo basi ndugu zetu Waislamu wangepungua wakati wa mwezi mtukufu.

  ReplyDelete
 38. Hi Dina, mimi naitwa margaret, mimi ni mama mtu mzima, ni obese tayari nina kg 100, niko kwenye program yako ya mboga mboga na juice lakini naona nampugua kidogo sana. Naomba ni join group la kwanza la kwenda gym kupunguza mwili ili niwe na afya jema. tayari mimi ua na tembea asubhi km 30. asante

  ReplyDelete
 39. Hi Dinna,

  Naitwa Vanessa, nina kilo 92.. nina miaka 25.. Naishi dar es salaam na ningependa kukujoin..

  ReplyDelete
 40. mambo dina.naitwa mama iness nakilo 124 naomba kupatiwa nafasi hii kwani kilo nilizonazo haziendani ma kimo changu isitoshe nikiwa tuko campany tunafanya mazoezi inatia moyo sana kufanya mazoezi na hivi umesema kila kitu unakiweka kwenye blog haitakua busara unipatie nafasi hii alafu nianze sababu za kutokufika.hivyo naomba kupatiwa nafasi hii nipungue angalau niwe na afya nzuri maana huwa nasikiaga moyo unakwenda mbio na nikitembea kidogo navimba miguu na kuchoka sana.pia mume wangu na wifi zangu wananisema kweli mm ni mnene sana na wanadiriki kumsema mume wangu ameoa mtu mzima wakati mm namiaka 28 na mume wangu 32 kiukweli inaniuma sana lakini ndo sipungui nafanyaga mazoezi nafika sehemu naacha mana nakuaga peke yangu.

  ReplyDelete
 41. tunaomba tu utuwekee diet humu na aina ya mazoezi maana naona kuna wenye matatizo zaidi yetu me nina 72kgs nataka by dec 31st niwe na 55-60kgs tu so i need to cut like 4kgs every month from this september...

  ReplyDelete
 42. Hello Dina,
  Mimi Naitwa Magreth ni mkazi wa makongojuu nina miaka 24, hapo awali nilikuwa na kilo 112, kwanzia mwezi wa nne nilipima na kugundua kuwa cholesterol level ipo alarming nikaanza kubadili lifestyle yangu haswa kwa upande wa chakula na maji. nimefanikiwa kupungua kwa sasa na kilo 97, nahitaji kuongeza swala la kufanya mazoezi ili niimarishe afya yangu yote kwa ujumla. Nipo tayari kujitoa kufanya mazoezi.

  ReplyDelete
 43. Hi DM
  Kwanza kabisa naomba ujue niko tayari kabisa kupungua na nakuahidi sitakua na visingizio vyovyote.Pili nitakua tayari ku-share kila kitu tunachofanya kwenye blog yako na kukabiliana na challenges bila ya kukata tamaa as kushare vitu katika blogs kila mtu ana uhuru wa ku-comment kitu anafikiri;Freedom of speech.Sababu ya mimi kutaka kupungua ni kujiepusha na magonjwa yanayonyemelea watu wenye uzito mkubwa ikiwemo ugonjwa wa moyo,shinikizo la damu na kisukari,ukizingatia baba yangu ni diabetic so nina possibility kubwa ya kupata ugonjwa huo kama sitachukua hatua za haraka.Mbali na hilo i really want to stay young and fabulous.Naitwa Neema,naishi sinza na uzito wangu ni kilo 120!Looking foward to getting this special opportunity as i've tried so many times to loose wait and failed

  ReplyDelete
  Replies
  1. Hey

   Dada Dina kwa kweli am tired of waiting those list of diet to be displayed. Umekaa kimya mno kiasi cha kukatisha tamaa. kwa muda huo uliokaa kimya unajua ungeserve watu wangapi katika hili tatizo. Umesema unafanya mazoezi na kufuata ratiba za diet ulizopewa at the same time unasema mlo wako wa kila siku siku hizi ni mchemsho wa kuku, u cant be serious, hiyo michemsho ni miongozi mwa vitu vinavyowafanya watu wagain sana wait. Waulize wataalamu on this watakuambia. Take care and all the best

   Delete
 44. Hallo dd Dina mm naitwa Renatha naishi kimara. mm pia nina tatizo la uzito mkubwa, nina kilo 105 na nina umri wa miaka 25. nimejaribu njia nyingi lakini bila mafanikio.lkn naamini nikipata mtu wa kushirikiana nae nitapata matokeo mazuri, naomba unichague mm dada Dina ninahitaji msaada maana afya yangu naona ipo hatarini!! lov u!  ReplyDelete
 45. Vp dada mim npmtayar ila bdo cjapma uzto pl je vp kuhusu malpo

  ReplyDelete