Tuesday, October 7, 2014

MSAADA WA MAWAZO KWA CHAKULA CHA MTOTO KUANZIA MIEZI SITA

Nimekuwa nikipata mwaswali kutoka kwa wazazi wenye watoto wadogo ambao ndio uzao wa kwanza.Kuhusu chakula cha mtoto kianzia miezi sita mpaka nane,tisa.

Ndio nikaona niweke hapa ili tuweze kupata mawazo wote kwa pamoja maana hata mie nahitaji.Mwanangu sasa hivi ana miezi saba anaenda wa nane.Ukiacha maziwa ambayo anakunywa na kunyonya hivi ndio vyakula ambavyo nimekuwa nikimpa.

1.Uji wa mahindi ulochanganywa na maziwa na sukari kidogo.
2.kiazi kitamu nakichanganya na karoti nakichemsha pamoja kikiiva nakiweka maziwa kisa nakiblend kwenye blander.
3.Wali bokoboko naukatia humo karoti kisha naublend na maziwa.
4.ugali laini na mchuzi wa maharage yaliyopikwa na kitunguu tu bila nyanya.
5.ugali laini na mchuzi wa samaki
6.cerelac hasa usiku
7.Matunda kama papai
8.juice ya tikiti ilokamuliwa juice ya chungwa
9.juice ya chungwa
10.maji ya kunywa huwa nampa mara kwa mara kuna saa hataki kuna saa anayanywa.Maana ni ngumu kujua wakati gani ana kiu.
Hii ni list tu sio ratiba sasa tunaomba mawazo ya vyakule vingine.Ndizi sijaanza kumpa nilisikia huwa zinaleta gas kwa watoto.Na je ni muda gani aanze kunywa uji wa lishe?

56 comments:

  1. Uji wa lishe haushauriwi na wataalam sababu karanga huvunda na kuwa na sumu, bora dona uongezee maziwa. Mwanangu nampa na ndizi sija observe ishu ya gesi. All the best ktk kulea

    ReplyDelete
    Replies
    1. asante sana hata mie hili la karanga nimelisikia

      Delete
    2. Nakubalia na mtoa jibu hapo juu. karanga huwa zina vunda, not unless unasaga nakuitumia hapo hapo.

      Delete
  2. hi Dina, ndizi mpe za bukoba zile laini hazina gas unamchemshia kwenye soup ya kuku wa kienyeji ila nyama humpi uazisaga ndizi tu kwenye blender

    ReplyDelete
  3. kuanzi miezi sita anaruhusiwa kuanza kula chakula ikiwa na uji wa lishe ila kikubwa ni kuwa makini wakati wa kuandaa na uhivaji kawake pia kama utaweza naomba mtengenezee lishe ya dona ambaya mchanganyiko wake unakuwa na vitu hivi mahindi yasio kobolewa,soya iliyo chemshwa na kukaushwe vizuri,karanga zikaange vizuri,na mchele kidogo kisha unasaga pamoja na unaanika ule unga vizuri kisha chekecha na unakuwa tayari kutumia kwenye uji unaweza weka maziwa na vitu vingine utakavyo penda kuweka

    ReplyDelete
    Replies
    1. nashukuru sana lakini nilisikia hata kuna mtu amecomment pia humu.Kuwa karanga si nzuri inavunda na kuwa sumu unless usage na uji unywewe siku hiyo hiyo sio unga wa kukaa muda mrefu.

      Delete
  4. hongera sana Dina mtoto amekua na ana afya nzuri.

    ReplyDelete
  5. supu zaina zote samaki nyama, maharage mpe. mtori pia sawa, mbogamboga pia anahitajika kula unaweza kupiga mtori wako then karibu unaiva dumbukiza mbogamboga blend pamoja. la chemsha mbogamboga mpe supu yake.akikisha anakula nyama samaki, maini hata kama utablend pamoja na chakula chake pia sawa maana wakati huo yeye hawezi kutafuna

    ReplyDelete
  6. Boga la kuchemsha nachanganya na maziwa,mimi mtoto wangu ana miezi nane na wiki tatu,nampa maziwa ya ng'ombe ila yanatakiwa kuchemka vizuri,ndizi bukoba nachanganya na viazi mbatata na karoti na kitunguu,pia naweka broccoli au cauliflower alafu nasaga kwenye blander.
    Pia kwa upande wa tunda parachichi ni zuri unaweza kuchanganya na chungwa linamletea ladha nzuri.
    kwa upande wa uji nimeshaanza kumpa lishe ambayo ina mchanganyiko wa mahindi,mchele,ngano na ufuta.nikiwa naupika naweka maziwa,butter na peanut butter.
    Vyakula vingine ninavyompa ni kama alivyovitaja Dina.

    ReplyDelete
  7. kwa kuongezea unaweza kumpa boga unachanganya na gimbi kidogo unavichemsha then unblend pia ni chakula kizuri sana kwa mtt,ndizi za bukoba unachanganya na smaki sato au kuku wa kienyeji unablend pia supu ya samaki sato ni nzuri na inampa calcium nyingi mtt

    ReplyDelete
  8. parachichi wachanganya na ndizi mbivu na maziwa una blander maji unatia kidongo inakuwa nzito kama uji

    ReplyDelete
  9. dada dina hii mada imenigusa kuchangia mi mwanangu nampaga hivi kwa kuongezea
    Asubuhi;uji ambao huo uji ndani yake unakuwa na ufuta wataalamu wanasema ufuta unasaidia mtoto IQ simuwekeagi karanga so nikiupika namchanganyia na maziwa na blueband kidogo maana ukiweka nyingi so nzuri kwa mtoto mafuta.
    saa nne;anakula cerelack.
    mchana;anakula viazi ambavyo vimechemshwa siweki mafuta naweka carrot hoho kitunguu namiwekea na uyoga wataalamu pia wanasema inasaidia IQ
    saa tisa:juice machugwa au papai au parachichi na passion any matunda namtengenezeaga.
    saa kumi na moja;anakunywa maziwa ya lactojen
    usiku;ndizi zilizochanganywa na samaki samaki ni nzuri sana kwa mtoto inasaidia afya nzuri na IQ.
    alafu ka akichelewa kulala ikifika saa nne nampa celelack den kulala.

    huo ndo mlo ninaompaga mwanangu mtoto anashauriwa kila baada ya masaa manne ale.asante dada dina tuna share ideas inabidi u add samaki na uyoga kwa zion ni nzuri sana naweza kukutumia pic ya mwanangu he'z health and I believe h'z genius haaaaaaaa lol.

    ReplyDelete
    Replies
    1. nashukuru sana my dear nitumie picha kwa email dina_marios@yahoo.com

      Delete
    2. Mambo nimependa huo mpangilio yani kama wangu kabisa sasa mie nikawa naogopa kwamba namnyima maziwa muda mwingi na ana miezi saba sasa kwani wako anamiezi mingapi au nakosea plz nijuze

      Delete
  10. me nashauri mtori wa ndizi bukoba, butternut, gimbi, boga pia mzuri kwa mtoto pia unaweza kumpa na supu ya kichwa cha samaki ni nzuri mno, kwnye juice unaweza kumpa juice ya carrot, parachichi na nanasi ni nzuri pia
    pia kwenye mtori unaweza kumuwekea zukin,conrflower,etc

    ReplyDelete
    Replies
    1. shukrani sana kweli mwanangu alikuwa ana miss vitu vingi

      Delete
  11. 1. Kiazi mviringo kikubwa kimoja na kipande cha samaki hasa sato au sangara...unachemsha pamoja...chumvi kwa mbali sana yaani kidogo then vikiiva unachambua hakikisha hakuna mfupa kisha unablend...hakikisha huongezi maji ule mchuzi ndiyo inachanganyiwa kwenye rojo

    2. Asubuhi hakikisha anakunywa uji wa dona...uchemke sana uji usipochemka husababisha madhara kwa mtoto tuwakanye na house girls kuhusu hili wasiripue

    3. Hakikisha chakula chochote unachompikia usiweke sukari kwa wingi, chumvi au mafuta

    4.Akifikisha mwaka wengi huwa wavivu kula hakikisha unamtayarishia mboga mboga kwa wingi wangu nilikuwa nampa majani ya maboga na bamia yaani unakuwa mlenda wanapenda sana watoto ila mara mbili au moja kwa wiki....pia mboga zake ziive vizuri ila zisipoteze ukijani

    Mengine Dinah kamaliza

    ReplyDelete
  12. mimi nilishamaliza kulea mwanangu wa mwisho ana miaka 5!! Nimependa kushare nanyi kuhusu samaki ukichemsha supu tumia kichwa cha samaki ndo umtengenezee supu, kichwa cha samaki ni kizuri sana kwa mtoto anayekua,vingine vingi mlivyoshare viko poa.

    ReplyDelete
  13. JE UNATAKIWA KUMPA MTOTO CHAKULA KILA BAADA YA MUDA GANI KWA MTOTO ANAYEANZA KULA

    ReplyDelete
  14. Asanteni na mimi nimejifunza hapa .
    Mtoto wangu anafikisha miezi 9 mwisho wa mwezi ; vyakula vyake ni
    Mtori wa ndizi uganda nablend na kipande cha nyama ya kuku, au samaki , au beef
    Wali boko boko nablend na karoti
    Mtori na njegere na karoti
    Brocoli, zuchini , kiazi na karoti
    Butternut , karoti na kipande cha nyama
    Nyama ya kusaga nablend na mboga mboga
    Viazi vitamu na karoti nablend na maziwa
    Samaki nachemsha na mboga mboga nablend
    Juice ya parachichi na chungwa
    Ndizi mbivu nablend na embe na maziwa
    Papai na embe
    Juice ya tikiti
    Uji nampa dona ..namuwekea na maziwa na siagi kwa mbali
    Uji mwingine nimetengeneza leo naanza kumpa nimechanganya ufuta, ulezi, mahindi ya bisi ,ngano isiyokobolewa, na brown rice.
    Sijatumia karanga kwa sababu wanasema sio nzuri kwa mtoto badala yake ndo ufuta.
    NB : ukitengeneza huo uji zidisha mchele na mahindi.
    Mama malkia

    ReplyDelete
  15. note:celac sio nzuri kwa watoto inapoteza hamu ya kula, celac ni tamu ukija kumpa uji wa dona hatakuelewa,pia unga wa lishe sio mzuri kwani huo mchangako kila kitu kina boiling point tofauti,yani mchele utawahi kuiva zaidi ya unga wa maindi,au mtama utaungua wakati mahindi bado hayajaiva,ni bora umpe mahindi tu na maziwa,mchele tu na maziwa,.

    ReplyDelete
  16. Mtoto inatakiwa ale kila baada ya masaa mawili tafadhali.Asubuhi saa mbili uji,saa nne supu/maziwa,saa sita juisi,saa saba chakula,saa tisa tunda la kuponda/maziwa,kumi na moja cerelac, ikifika kumi na mbili na nusu supu/maziwa, saa mbili kamili chakula, kabla ya kulala akichelewa mpe cerelac. ukitaka cerelac unaweza korogea na maziwa.Juisi ya chungwa si nzuri kwa watoto chini ya mwaka,inaleta gas sana,mtoto anawezashindwa kula vizuri vyakula vingine sababu hiyo.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau kwa mtoto wa miezi sita hapo ni kum-overfeed. Ndio maana wamama tunalalamika watoto hawali kumbe tunawazidishia kipimo cha chakula. Kumbuka kuwa bado hawako active kwahiyo wakila chakula kinakaa tumboni muda mrefu. Kifupi mtoto wa miezi sita chakula chake kikuu ni maziwa ya mama/kopo. Juice labda mara moja kwa siku, na vi-mbogamboga kidogo vilivyosagwa mfano: karoti, njegere, mchivha, kiazi kitamu. Nia ni kuanza kumzoesha ladha mbalimbali lakini isiwe ndio chakula kikuu.

      Delete
  17. Boga ni nzuri sana..ila jamani karanga hapana dona is the best kwa kweli..pia papai waweza changanya na ndizi au parachichi..juice ya carot pia nzuri usafi uwe 100% ni bora mama kutengeneza peke yako na sio msichana wa kazi hizi juice

    ReplyDelete
  18. Mtoto anakula naada ya masaa 3

    ReplyDelete
  19. Dina nashukuru sana kwa mada hii nintoto anamiezi 11 hataki kula naombeni msaada wa mawazo.

    ReplyDelete
  20. Dina maziwa weka kwenye uji na umpe anywe tu pendelea kuweka supu kwenye chakula,pia lishe mpa ila weka maind ngano ulez na ufuta inatosha kabisa,pia tambi changanya carot hoho na main af saga inakua nzur sana

    ReplyDelete
  21. Af nilisahau dina achana na macerelac mavyakula ya kopo sio mazur pia kwa umri alionao zion kama unaweza pata mtu mwenye ngombe ambae unamwamin mpe ya ngombe achana na makopo sio mazur basi tu tunatumia but now anaweza kunywa na kama hayamzuru poa kabisa,pia jitaid sambil awe amekula il usiku apate kunyonya vzr maana wamama weng mchana hatupo hom watoto hawapat kunyonya vzr so uck ndo wanapata kunyonya

    ReplyDelete
    Replies
    1. Maziwa ya ng'ombe mpaka mtoto afikishe mwaka mmoja. Maziwa ya mama ndio the best, ila pia kuongezea na ya kopo sio mbaya kama nyonyo pekee haitoshi. Chakula kikuu cha mtoto chini ya mwaka mmoja ni maziwa, hivyo vingine vinatakiwa viwe kiasi kidogo sana.

      Delete
  22. Pia mtoto anatakiwa ale akiwa amekaa mwenyewe chini au kwenye kiti cha kulia cha watoto(high chair) au unampakata ila usimbane na mikono, ukimbana ndio mana watoto wanalia na kukataa kula coz wanaona kubanwa. Ila ni vizuri kuanza na chakula kimoja kimoja ili kuona kama kitamdhuru mana ukimchanganyia moja kwa moja na kimpa tatizo hutojua ni chakula gani. Pia usimpe chakula kingi mtoto chini ya mwaka mmoja mpe mara mbili tu, kama asubuhi uji jioni msosi sana maziwa ya mama kwa sie tunaonyonyesha na maji.

    ReplyDelete
  23. Ila mmetaja vyakula vingi sana mtoto anatakiwa apate wanga protin mbogamboga matunda vyakula vingine mnakuwa mnawaova doz watoto badala ya kuwa na IQ kubwa anashuka hata mim sipendekezi macerelac na maziwa mtoto chini ya miaka miwili mkazanie maziwa yako mama mimi ni hodari wa kunyonyesha kuliko lishe kwa mtoto mchanga na mwanangu wa kwanza darasani ni wakwanza tu nahis na wapili atafuata nyayo maziwa ya mama ni bora zaidi ila mama inabidi ule sana madocta wanashauri hivyo vyakula ni ziada tu maziwa ya mama ndo mpango mzima ndo maana wamasai watoto wao wananyonyaga tu miaka mitatu bila kupewa chochote

    ReplyDelete
  24. ongeza mboga za majani. chemsha tu then mpe ile supu yake esp mchicha, majani ya maboga, mnafu..weka kachumvi kwa mbaali kuongeza ladha. you can also blend with cucumber.....very good for cell development.

    ReplyDelete
  25. ahsanten wamama,mnatusaidia wamama wa mtoto wa kwanza,mbarikiwe sana barikiwa dada Dina

    ReplyDelete
  26. Nimeipenda sana mim mtoto wangu ndo anaanza kula kweli nimepata pakuanzia mana nlikuwa cjuh chochote

    ReplyDelete
  27. Dina kweli wewe una maono na mungu akuzidishie maisha.mimi sina mtt mdogo ila mdogo wangu ana mtt wa mwakammoja na miezi miwili suddenly amekataa kula kila kitu , nilipoona hii topic nikamwambia alog kwenye blog hii halafu asome comments za watu. akafanya hivyo .jana nimeongea naye nikamuuliza kambadilishia mtt chakula ? akasema yes jana alimpikia kiazi akachanganya na ndizi akaweka carrot na maziwa hajawahi kupikia hivyo , yaani nasikia mtt alikula mpka wakahisi atavimbiwa. walimpa na juice ya tikiti hajawahi kupewa hiyo alikunywa ila kidogo. mama mtu alifurahi sana maana alikuwa analalamika mtt anapungua hataki kula.amenunua note book na comments za diet zote walizotoa watu humu ndani ameandika .nashukuru sana kwa msaada.

    ReplyDelete
  28. Dunia ya sasa kila kitu ni sumu!!! Karanga ni sumu....mbona hata maziwa ya ng'ombe hayaruhusiwi kumpa mtoto wa binadamu kuyatumia? Mana wanasema kuwa ni magumu kuwa digested...so which is which?
    Wazazi wetu ndo walitulea kwa hizo karanga na ndo tumekua na akili za kumwaga lols. Any ways maisha ni kujifunza mana kila siku research zinatuletea ufahamu mpya.

    But kwa ishu ya sumu wallah unaeza ukaacha kula maana hata hao samaki wamesha kula mercury wakiwa majini nazo zina sumu, mboga mboga ndo usiseme mana sinamwagiliwa dawa bila kufuata ushauri wa wataalamu saa ingine zinamwaigiliwa dawa leo kesho zipo sokoni sasa hizo si ni sumu pia?
    AKILI ZA KUAMBIWA.......CHANGANYA NA ZA KWAKO lols

    ReplyDelete
  29. Dada Dina asante kwa hii topic kwa wanaolea kama nimi nimefaidi sana. Mimi mwanangu amekataa kunyonya akiwa na miezi 7 sasa yuko mwezi wa 8 ila ni majanga make hata kula anasumbua mpaka ameloose weight. Mbarikiwe wamama.

    ReplyDelete
  30. http://www.babycentre.co.uk/a9144/solids-by-age-at-six-months

    ReplyDelete
  31. Msiwape watoto wadogo nyama nyekundu, inahitaji nguvu nyingi kusagika. Imagine watu wazima wanakatazwa nyama nyekundu nyie mmekazana humu nyama ya kusaga, nyama ya kusaga ya nini jamani?

    Wapeni jamii ya kunde na maharage zaidi, kama vile choroko, hizi unaweza kuziloweka kisha ukaziotesha kama unaona kazi nunua zilizooteshwa supermarket. Choroko zina protein na iron ya kutosha.

    Weka dengu, au dal, ina protein ya kutosha na ziko dal za aina nyingi tu, moon dal etc, nenda Shoppers section ya hivyo vitu utapata kila kitu mpaka unga wa uwele ambao nao una protein ya kutosha.

    Usiweke blueband kwenye chakula cha mtoto marufuku, weka natural fat kama parachichi ina faida kubwa na haina additives.

    Kama mtoto uzito wake unapungua, kuna nazi weka tui la kwanza la nazi kwenye chakula chake badala ya maziwa. Kwa sababu nazu ni chakula bora sana na dawa pia, ina anti fungal, anti viral and anti bacteria.

    Mpake mtoto mafuta ya nazi badala ya kuhangaika na mafuta fake yasio na benefit yoyote.

    Pendelea kummassage mtoto ukishamuogesha, hii inamfanya arelax na akuwe vizuri.

    Ni mimi bibi wa watoto wote.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante bibi kwa ushauri wako nimeupenda sana.

      Delete
  32. Mdau 10:26 nazi pia si nzuri sana kwa chakula zina kiwango kikubwa cha chorestrol wataalamu wanashauri isitumiwe kila mara. Hapa duniani vitu vingi vina madhara jamani ukivifuatilia basi hutakula ahahahahaha

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aliyekwambia nazi ina cholestrol ni nani? Macelebrity wanakunywa mafuta ya nazi kila siku for healthy and good skin. Hebu nenda kagoogle benefits of coconut, au tafuta nature cures not medicines. Huwa nawatibu watoto wenye utapiamlo kwa kutumia smoothie ya tui la nazi na ndizi mbivu. Mafuta ya nazi yana anti bacteria, antifungal na antivirul.

      Wenzenu huko duniani wanatumia maziwa ya nazi kwa chai kama healthy option umecrem wapi nazi inaleta cholestrol?

      Delete
    2. Ndio nazi inachoresrol kwani macelebrity ndo wanaguide tule nini ebo!!
      Cha msingi kila kitu kina mdhara hata kama ni kizuri.

      Delete
  33. Mimi mtoto wangu ana mwaka sasa hivi na miezi miwili, uji nnaompa una KARANGA nakaanga vzuri tu, soya, mahindi yale ya njano ya bisi, ngano, ulezi na mchele vyote navitayarisha vizuri tu, hata kama wanasema ss hv karanga zina sumu, jamani sie tumekua na hizo lishe za makaranga, na mwanangu sitaacha kumpa karanga ndivyo nilivyoelekezwa na walionilea mm
    Kingine nimeona wengi hamjaongelea KIINI CHA YAI namchanganyia na uji mara 3 kwa wiki ndo nampa.
    Na sio kila siku mtoto anakula uji jamani anachoka asbh uji asbh uji...mbadilishie badilishie.
    Vingine anavyokula mwanangu
    -Mtori wa samaki au kuku wa kienyeji
    -wali bokoboko na apple na maziwa
    nasaga kwa pamoja
    -ugali wa dona laini na mchuzii
    -dengu
    -veggies namuwekeaga kwenye vyakula
    njegere
    -machungwa ndo anayapenda sana naona
    -samaki kua makini na ambao hawana
    mercury nyingi
    -oat meal
    -makaroni ukipata mazuri unamchanganyia na njegere carrots kitunguu
    -boga la maziwa
    Anakua vizuri tu nashukuru Mungu kwa lishe nnaompa alhamdullilah hata akiumwaga hapungui kg nyingi na hajawahi shuka graph ya kwenye kadi alhamdullilah.
    NB; simpi hivyo kwa siku moja hapana, na zingatia mafuta na chumvi havifai kwa under 1yr, ukitaka kilainishi cha uji atleast TANBOND.

    ReplyDelete
  34. Nilisahau...Ili kupata mboga zisizo na madawa nimepanda mchicha kwaaajili ya mtoto na pia ndo anaoupenda sana, na majani ya maboga...asanteni

    ReplyDelete
  35. Jamani nnavyoandika kila baada ya masaa mawili mtoto ale sio kweli jamani...kha hapumziki kulala huyo mtoto, atleast matatu au manne maana watoto wanalala sana wengine kama wangu kwakua anakula vzr anashiba hakataagi chakula alhamdullilah na siri kubwa yangu ni kumchezeshea ratiba tu hazoei chakula kimoja...yes pia i second mdau aliesema samaki kichwa bwana upate jibichwa la sato utapenda, muwekee na ndizi, kiazi, kabichi, kitunguu, hoho na carrot akitoka hapo huo usingizi wake balaaaa....malezi mema jamani.

    ReplyDelete
  36. DINa ubarikiwe sana na mwenyexi mungu hakuna mambo yanayotusumbie sisi wageni first mothrI kama hay a nakuona ni mkomboxi wetu kwa kweli

    ReplyDelete
  37. Hi Dina. Mimi mwanangu huwa najitahidi kwa wiki ale samaki mara tano. samaki ni wazuri sana. unaweza ikampa n'a ugali, wali au ndizi. mimi huwa simpi viazi sababu huwa vinamsababishia gesi. Pia jitahidi kila siku iwe unampa matunda ya aina tofauti.

    ReplyDelete
  38. hi dina, mmetaja vyote mmesahau green beans mnamuwekea kwenye mitori na milo yote

    ReplyDelete
  39. Aisee,mmetusaidia sana,asante mtoa mada

    ReplyDelete
  40. Hi dina nimefurahi kuona jinsi gain wamam tunapenda name kupeana ushauri. Mimi pia ni mama mwenye motto wa kwanza nimeona comment kuhusu samaki mwanangu nikimpa supu ya samaki Leo kesho anaamka anavipele mwilini. Nifanyeje maana samaki ni nzuri kwa mtoo

    ReplyDelete