Kuna wakati NYAYO za miguu HUWA kavuu.Unaweza kufanya yafuatayo ili kuondokana na hali hiyo.Kwa kawaida ngozi ya kwenye nyayo huwa ni kavu ukilinganisha na ngozi ya maeneo mengine mwilini.
Vitu vinavyosababisha ukavu mpaka kupasuka nyayo ni
1.Kutembea sana peku
2.ukali wa jua na miguu unaikanyaga chini
3.Kuogea sabuni ambazo hazina moinsture
4.tatizo la kisukari na thyroid
5.kuogea maji ya moto kupitiliza kila siku
6.matatizo ya ngozi eczema ambayo hupelekea ngozi kuwa kavuu
Unatibu vipi ukavu wa nyayo?kuna watu ambao tayari wana asili ya ngozi kavu hivyo ni lazima wafanye kazi ya ziada kulainisha miguu.
1.Ukimaliza kuoga tu unahakikisha unapaka nyayo zako mafuta au lotion zenye moinsture.Usipake lotion zenye kemikali au alcohol huzidisha ukavu wa miguu.Paka hata mafuta ya watoto ambayo hayana kabisa kemikali.
2.Pia unaweza kuloweka miguu yako kwenye maji yenye juice ya limao,juice ya limao husaidia kuondoa zile dead skin
3.Paka miguu yako mchanganyiko wa kijiko kimoja cha olive oil na matone kadhaa ya limao.Changanya vyema kisha paka kwenye nyayo ili kuipa moinstrure yaani unyevu unyevu.
4.Unaweza kutengeneza scrub yenye mchanganyiko wa unga wa mchele,olive oil,veniger na asali.Unazifanyia scrub nyayo zako na huo mchanganyiko.
5.Ukishasafisha na kufuta miguu yako paka vegetable oil...mafuta kama hayo ya olive na mafuta natural kabisa ya nazi.
Haya ni mafuta ya nazi natengeneza MIMI mwenyewe kiasili kabisaa yatakufaa kwa miguu na nyayo zilizo kavu.Ukivutiwa na wewe huwezi kutengeneza mwenyewe tuwasiliane.Tayari nimewauzia wengi tu kwa ajili ya kupaka watoto wao na hata watu wazima wanaopenda mafuta ya nazi.
Ukiyapaka kabla hujaenda kulala vaa socks ndio ulale.Fanya hivi kila siku.
6.Kabla ya kulala Chukua mafuta ya vaseline ujazo wa kijiko kidogo cha chai na kamulia limao zima kisha koroga vyema huo mchanganyiko kisha paka kwenye nyayo zako.Fanya hivi ukiwa umenawa miguu na umeifuta vizuri imekauka ndio unapaka.Vaa socks zako ndio upande kitandani kulala.
****kumbuka ni muhimu kumuona daktari hasa kama una hali mbaya kwa ushauri na matibabu zaidi.Na pia kama hali hiyo inatokana na magonjwa niliyoyataja hapo juu.
asnte kwa utaalamu dear
ReplyDeleteThanks for the tips. Hasa sie wa mikoa yenye upepo mbaya na baridi miguu wakati mwingine huitamani
ReplyDeleteDada Dina hayo mafuta ya nazi tunayapataje sisi wa mikoani, na unauza sh.ngapi?
ReplyDeleteumenisaidiaje manake nyayo zangu huwa zinanikata stuimu kuzaa sandals, guu nnalo lkn nikiangalia unyayo nakosakujiamini
ReplyDeleteAsante dada Dina kwa tips nzur
ReplyDeletehii nimeshaijaribu sana lakini kulala na socks ni mtihani sana kW hapa dar. Yaani unackia joto hadi moyoni!!
ReplyDeleteTunashukuru kwa hizi tips pia mimi nilikuwa na nyayo kavu sana kuna product moja ya Oriflame inaitwa Feet Lotion imenisaidia sana na kumaliza tatizo la ukavu wa miguu napaka wakati wa usiku then navaa soksi nalala sasa hivi nyayo zangu ni kama za mtoto lol....
ReplyDeleteSasa nitamlaza vipi mume na mifuta miguuni! Au ndio kusubiri alalee? Nikisema nipake kwanza yoote yataishia everywhere!
ReplyDeleteKWANI SIUNAVAA SOKSI? NA HATA HUYO MUME PIA UNATAKIWA UMSAFISHE MIGUU NA UMPAKE MAFUTA HAYO NYOTE MUWE NG'ARING'ARI MIMI NAPAKA MAFUTA YA VASELINE YENYE BLUE SEAL MGUU LAINI KAMA WA MTOTO ILA NITAONGEZEA NA UJUZI WA DADA DINNAH.
ReplyDeletetumia glycerine uwe unavaa viatu
ReplyDelete