Wednesday, January 18, 2012

TAARIFA ZAIDI KUHUSU WOMEN IN BALANCE---KITCHEN PARTY GALA

SIKU ZIMEKWISHA SANA NA JUMAMOSI YA TAREHE 28 JANUARY INAKARIBIA KWA ILE KITCHEN PARTY GALA.WADADA NA WANAWAKE KUANZIA MIAKA 18 NA KUENDELEA TUNAKUTANA NA KUJADILI CHANGAMOTO MBALIMBALI ZINAZOTUKABILI KATIKA MAISHA/ MAHUSIANO/NDOA.KUNA MENGI YA KUJIFUNZA NA KUKUMBUSHANA.


KIINGILIO NI TSH 30,000 KWA MTU MMOJA NA KAMA UNAHITAJI MEZA WEWE NA WATU WAKO WA KARIBU NI TSH 300,000(meza ya watu 10)
MUDA KUANZIA SAA 8 MCHANA MPAKA SAA 2 USIKU(Jamani kina mama mzingatie muda)

CHAKULA NA VINYWAJI VITATOLEWA

AUNTY SADAKA



MAMA VICTOR


BI CHAU

NA WENGINE KUONGEZEKA PAMOJA NA BURUDANI.

KUFANYIKA KATIKA UKUMBI WA DUNKEN HOUSE UPO MIKOCHENI KWA WARIOBA BARABARANI KABISA KARIBU NA MBALAMWEZI BEACH.NI UKUMBI MPYA NA WAKISASA.


TICKET ZITAANZA KUPATIKANA WIKI IJAYO KWA

MAWASILIANO 0787 583132 NA 0789333537

20 comments:

  1. Itakua sa ngapi?au mpaka tiket zianze kupatikana ndo mda utajulikana?

    ReplyDelete
  2. hongera dear, but ushauri hao watu kumi weka punguzo ili watu wakusanyane kuja kumi kumi utatengeneza pesa nyingi. kila la kheri.

    Kokusima

    ReplyDelete
  3. si ya kukosa hii, tiketi zitapatikana wapi??

    ReplyDelete
  4. AT LAST IMEFIKA thanks ngoja tusubiri ticket na kuomba uzima S.

    ReplyDelete
  5. Dah thanx nilikua ninaisubiria kwa hamu ila sasa nina harusi ya kaka yangu siku hiyohiyo ninaomba kujua ni saa ngapi mpendwa

    ReplyDelete
  6. Duh na Bi Chau atakuwepo sipati picha itakavokuwa yani I can't wait loh!

    ReplyDelete
  7. kwa nini kila kitu wamama tu?kwa nini na wababa nao wasihusishwe pia?nao wajifunze vilevile.

    ReplyDelete
  8. Nimeipenda sana hii Dina nifanye nipate tiketi mapema kipenzi big up sana always nakukubali

    ReplyDelete
  9. Theme ni nini bi dada, au twavaa tu chochote?

    ReplyDelete
  10. dina hakuna meza ya watu watano? as a group tungependa hiyo kama ipo

    ReplyDelete
  11. kama utaona muhimu na wewe itundike kwenye blog yako. mdau.

    http://bukobawadau.blogspot.com/2012/01/wadau-kama-mlivyoomba-turudie-hii-video.html

    ReplyDelete
  12. Mambo Dina, Yaani this time hatutaki kukosa ila mama mbona una namba za mtandao mmoja tu. hauna tigo line?? pili naona kama maelezo hayajitoshelezi hivi na matangazo mamii mbona kidogo wapo wanaotaka ila hawajui maana si wote watumiaji wa mtandao hapo cloud wakusupport hata kwa tangazo mamii maana unafanya kitu cha maana siku hizi ndoa ngumu jamani na wezi wa waume wengi sana.
    kheri inshallah mungu atakuwa nasi.

    ReplyDelete
  13. we dina kama kazi ya blog imekushinda acha kuupdate hadi ukose kazi, unatuboa sa na kila tukifungua hamna ishu, kama uko busy acha kublogua unatupotezea mda

    ReplyDelete
  14. hongera kwa kufanikisha maandalizi dina. nitashiriki mungu akinipa uzima.

    ReplyDelete
  15. katika utafiti wangu usio rasmi,nimegundua asilimia karibia 60 ya wanawake wanaowafunda wenzao mambo ya ndoa na namna ya kuishi na mwanume wao wameshaachika au hawajawahi kuolewa rasmi ni wahangaikaji tu wa mjini,we chunguza utaniambia

    ReplyDelete
  16. Mdau uliesema asilimia 60,wahangaikaji tu wa mjini ina maana gani?uwa awana ajira au?sijakuelewa hapo.

    ReplyDelete
  17. Dina wewe mwenyewe hujaolewa sasa sijui unataka kutufunda nini,au hela zutu tu unataka kula,kwanza umeiga Idea ya Joyce Kiria sema yako ndo hivyo unajifanya unaelimisha na kutaka kusaidia wanawake huna lolote

    ReplyDelete
  18. KWELI KUSOMA KUELEWA KUKESHA MBWEMBWE KWANI HUJASOMA WAZUNGUMZAJI WA SIKU HIYO NI KINA NANI MPAKA UMSEME DINA WA WATU???WATU WIVU TU!!!DINA YEYE KAANDAA TU NA WAHUSIKA NI WOTE WALIOOLEWA NA WASIIOLEWA NYOOOOOOOOO
    KWANZA HUYO JOYCE ANALIPI LA KUIGWA HALAFU HUWA NACHEKA SANA NIKIPITA MITANDAONI ANAVYOPIGIWA DEBE JAMANI YA UKWELI INAJULIKANA.TENA UKOME KUMLINGANISHA DINA WETU NA JOYCE.TENA JOYCE ALISHASEMA MARA KADHAA KAZI ALIJIFUNZIA CLOUDS WALIMU WAKE DINA NA SOPHIA KESI SASA WEWE ONGEA USIYOYAJUA KALAGABAHO

    ReplyDelete
  19. Just ushauri tuu! please uwe unaweka recent updates zinatokea kwenye jamii hasa matukio muhimu yanayojiri nchini.

    ReplyDelete