Saturday, February 25, 2012

JUMAMOSI YA LEO KATIKA KUWATEMBELEA WALIOINGIA TANO BORA YA SHINDANO LA NYAYO ZA MWANAMAKUKA

Nilikuwa mimi,Godliver akiwakilisha U.W.F mbao ndio tunashirikiana nao katika kumwezesha mwanamke mjasiriamali aliejaribu kujikomboa lakini akakwama kwa sababu ya changamoto mbalimbali.Sharti la kwanza lazima uwe ulijaribu ukashindwa na sio uwe una idea lakini hujawahi kuifanyia kazi. Cameraman P.Diddy kutoka clouds tv na dereva wetu juma tukaanza safari ya kukatiza maeneo kadhaa hapa jijini Dar es Salaam.
Tukaanzia Mwenge anapoishi Sikudhan Daud mwenye umri wa miaka 29.Hapo anapoishi ni nyumbani kwa mama yake mdogo.

Mimi,Sikudhani na Godliver


Baada ya hapo tukaja kinondoni palipokuwa eneo lake la biashara.Sikudhani hufanya kazi ya promotion katika bar mbalimbali.Mwaka 2009 alishiriki katika shindano la malkia wa Ngwasuma na kushika nafasi ya tatu.Pesa aliyopewa 900,000 ndio aliitumia kama mtaji wa kufungua pub.



Pub ambayo mwaka jana alilazimika kuifunga baada ya ndugu yake kusepa na pesa za mauzo na bia zilizokuwepo kuziuza katika maduka ya jumla.

Wakati anauza hivyo vitu Sikudhani alikuwa safarini Mwanza katika kazi zake za promotion.Kurudi akakuta pub imefungwa yapo makreti matupu.


Shunguli ikaishia hapo licha ya kujaribu sana kurudi upya


Anachotaka sikudhani ni kuwezeshwa mtaji wa kurejea upya biashara yake.Kama unaona anastahili kuwezeshwa kwa heshima ya Mwanamakuka chukua simu yako andika neno MK acha nafasi jina lake kwenda namba 15678.


Baada ya kutoka Kinondoni safari ikawa kuelekea Ukonga mpaka nyumbani kwa dada Nasra Said.


Kufika akaniambia japo nakusikia sikujui nikiona picha yako kwenye gazeti nikijumlisha nahisi kama tunafahamiana.


Nasra yeye katika ujasiriamali wake mwaka 2009 alibahatika kuwa supplier katika supermartket za PATCO.Alikuwa akipeleka vitu kama vile visheti,ubuyu,senene,vileja na farfar.


Hizi ndio farfar nimezionja leo kwa mara ya kwanza


Mwaka 2010 tajiri wa supermarket 4 za PATCO alitaifiishwa na bank iliyokuwa ikimdai.Yeye alikuwa akisubiri malipo ya biashara aliyopeleka bahati mbaya hakuweza kulipwa maana ilikuwa nje ya uwezo tena.Biashara ikaishia hapo msingi wote umeenda hana hata pakuanzia.Akauza baadhi ya vitu vyake vya ndani akapanga hapo chumba kimoja.


Akaanza biashara kidogokidogo lakini mpaka sasa hajaweza kurudi tena msingi mdogo amejaribu saccoss mbalimbali anakuta masharti magumu.


Nasra na Godliver


Kama unaona tumuwezeshe Nasra kupitia simu yako ya mkononi andika neno MK acha nafasi kisha jina lake kwenda namba 15678.

Kama unakumbuka nilishakuletea historia ya Mwanamakuka,mwanamama wa kinyamwezi mjasiriamali wa kwanza katika pwani ya Afrika Mashariki.Aliishi karne ya 18 ambae alikuwa akisafiri katika misafara ya kibiashara wakati huo ilikuwa ya mbadilishano.Akibeba vyungu,asali,pembe za ndovu,mtama,mahindi,uwele,chumvi,samaki wakavu n.k



Biashara yake alikuwa akiifanya pia na wakoloni ambao wakati huo walikuwa waarabu.Kuelekea siku ya wanawake duniani tunataka kinamama wajasiriamali wa sasa wa karne ya 21 wamjue huyu na wafuate nyayo zake.Na pia kuchukua fursa ya kuwashika mkono wale waliokwama ndio maana kuna hili shindano la NYAYO ZA MWANAMAKUKA.Mshindi atazawadiwa siku ya wanawake duniani 8th march pamoja na mshindi wa pili na wa tatu.

No comments:

Post a Comment