Monday, February 27, 2012

JUMAPILI TUKAIKAMILISHA KWA KUWATEMBELEA MSHIRIKI NAMBA NNE NA TATO W\A SHINDANO LA MWANAMAKUKA.

Mida ya saa saba hivi mchana tulikuwa tayari nyumbani kwa mama mjane wa watoto wa tatu Bi Joyce Mabula.
Tulimkuta akikaanga samaki biashara yake kubwa na inayomfanya mkono uende kinywani.Wateja nao walifika kujinunulia samaki,watamu haoooooooo sikubaki nyuma kuwaonja.

Bi Joyce anaishi magomeni na bibi yake ambae anaonekana kwa mbali akimsaidia kukaanga samaki.

Anachohitaji ni pesa ya kukuza mtaji na kuweza kuajiri mtu wa kumsaidia kukaanga samaki maana tayari moshi ushaanza kumsumbua na mgongo.

Kama unahisi mama yetu hapa Joyce Mabula anastahili kushinda mpigie kura kwa simu yako ya mkononi.Andika neno MK cha nafasi na andika jina lake kwenda 15678 umwezeshe.

Hapa ndio nyumbani ndani anapoishi na wanawe watatu,wawili wamemaliza kidato cha nne na wa mwisho ndio yupo darasa la saba.

Watoto nao wakiona mgeni kaingia mtaani kwao hawasiti kukukaribisha..
Picha na watoto ,wenyewe walikuwa wanaitana nyieeeeeeeeee njooni tuuze sura huku hahahahaha.

Safari yetu ikaendelea mpaka Mabwe Pande mpaka nyumbani kwa Bi Mwanne Msekalile.Mama mjasiriamali wa watoto 6. Ni mfugaji,anatengeneza batiki na vikapu kwa vitu asilia vinavyotuzunguka.

Kuku,bata na njiwa

Nyumba waliojenga na mumewe baada ya kupewa kiwanja na mama waliyekuwa wakimlindia nyumba.

Akatuonyesha mazingira ya nyumbani kwake.Yeye alianza kuunza genge wakati huo na mumewe nae akiwa muuza genge.Kuna mama alikuwa amejenga nyumba ila hajahamia akawa akitafuta watu wakuishi kumlindia ndio wao wakapata bahati hiyo.Wakaishi hapo kwa miaka kadhaa baadae huyo mama akawa anaihitaji nyumba yake.Lakini kwa upendo wa huyo mama akamwambia asijali atampa kiwanja na wakijitahidi wanaweza kujenga kidogo kidogo.Kweli huyo mama akawapa kiwanja na miaka michache baadae wakajenga nyumba kwa kushirikiana na mumewe.

Hivi ni vitu mbalimbali anavyotengeneza vya urembo majumbani hasa vikapu vya kuhifadhia maua.





Nikapewa hilo dude nikawekee urembo .Bi Mwanne ni mcheshi sana na mzungumzaji mzuri.Anasema amedumu kwenye ndoa yake na mumewe kwa miaka 30 sasa nikamuuliza siri nini?akasema UWAZI,UAMINIFU,USHIRIKIANO NA UVUMILIVU ndio vimewafikisha hapo.

Mpaka hapo zoezi la kuwatembelea kinamama hawa likawa limekamilika.Muwezeshe Bi Mwanne Msekalile kwa kuandika neno MK acha nafasi na kisha jina lake kwenda namba 15678.
Tukakaribishwa chakula cha mchana

Baada ya chakula tukaanza safari ya kurejea kwetu.

Katika kuzunguka kukutana na hawa wakinamama nimegundua sifa kubwa ya mjasiriamali wa kweli ni mawasiliano.Wengi ni waongeaji,wacheshi,wakarimu,wanajua kujieleza na unaona kabisa ushupavu wao ukiacha changamoto zinazowazunguka.Hizi ndio sifa alizokuwa nazo Mwanamakuka.

8 comments:

  1. JAMANI DINA HII PROJECT NIMEIPENDA IMENIPA CHANGA MOTO YA KUTOKATA TAMAA MAAN HEBU ANGALIA MAISHA YA HAWA WENZETU TENA NA WANA WATOTO LAKIN HAWKATI TAMAA MASKINI NINGEKUWA NA UWEZO NINGEWASAIDIA WOOTE LAKINI MUNGU YUPO PAMOJA NAO..MAAN MI KITU KIDOGO NAKATAGA TAMAA NA KUANZA KIJIFUNGIA NDANI KULIA KUMBE KUNA BAKUBWA KULIKO YANGU..ISHAALAH WOTE MOLA ATATUPA WEPESI...

    ReplyDelete
  2. JAMANI DINA HII PROJECT NIMEIPENDA IMENIPA CHANGA MOTO YA KUTOKATA TAMAA MAAN HEBU ANGALIA MAISHA YA HAWA WENZETU TENA NA WANA WATOTO LAKIN HAWKATI TAMAA MASKINI NINGEKUWA NA UWEZO NINGEWASAIDIA WOOTE LAKINI MUNGU YUPO PAMOJA NAO..MAAN MI KITU KIDOGO NAKATAGA TAMAA NA KUANZA KIJIFUNGIA NDANI KULIA KUMBE KUNA BAKUBWA KULIKO YANGU..ISHAALAH WOTE MOLA ATATUPA WEPESI...

    ReplyDelete
  3. daaaaaaaaaaaah.

    kwa kweili dada Dina umepungua sanaaa yaaani its hard to belive kama ungepungua kiasi hicho.Bigup

    regards,

    Godfriend

    ReplyDelete
  4. hi dina,
    hongera kupaungua na hongera kwa yote ufanyayo.nauliza KITCHEN PARTY GALA ni lini tena

    ReplyDelete
  5. acha uvivu ku up date hata mduara wa jana kah.

    ReplyDelete
  6. huyo wa dagaaa awezeshwe, kwanza nimezitamanijee

    ReplyDelete
  7. Dina hongera na kazi. Navitaka hivyo vikapi contacts plz!

    ReplyDelete
  8. HONGERA SANA DINA KWA HII PROJECT NZURI..BI MWANNE MSEKALILE NI MJASIRIAMALI WA KWELI NINAPENDA UBUNIFU WAKE KWA KWELI. KWANI UJASIRIAMALI UNAENDANA NA UBUNIFU AMBAO UTAKUPA SOKO.NAMTAKIA KILA LA HERI..

    ReplyDelete