Sunday, February 12, 2012

SAFARI YA BAGAMOYO....KUFUKUA HISTORIA YA MWANAMAKUKA

Kwa wiki mbili mfululizo kama ulifatilia kipindi changu cha leo tena utakuwa ulisikia nikitaja mara kwa mara jina la MWANAMAKUKA.Mwanamakuka ni nani?unajua nini kuhusu jina hili?Jumamosi nilifunga safari kwenda Bagamoyo mimi,Sakina Lyoka mama wa ng'aring'ari ambae ni mwenyeji wa huko.Producer wangu Domi,camera man Shagile na dereva Harun.
Ukifika Bagamoyo kuna shule inaitwa Mwanamakuka,ni shule ya msingi ambayo ilipewa jina hilo kama sehemu ya kumuenzi Mwanamakuka.




Shule hii inasemekana zamani wakati wa ukoloni iliitwa Aga Khan walikuwa wakisoma watoto wa kihindi tu hapo hakuna mswahili.Kwa sasa shule ni kubwa lakini wakati ule ilikuwa ndogo.

Eneo hili ndio eneo alilokuwa akiishi Mwanamakuka pia.

Nyuma ya shule kuna kaburi la Mwanamakuka ambako alizikwa yeye na mume wake.

Hapo niliposimama kwa nyuma hiyo kama nyumba ndio kwa ndani kuna kaburi la Mwanamakuka na mume wake.

Lakini je Mwanamakuka ni nani?

Ukiingia kwa ndani kaburi lake linaonekana hivi.

Muongoza watalii wa nje na ndani bwana Fadhili alinipa sifa iliyompa heshima kubwa Mwanamakuka.
SIFA

Mwanamakuka kwanza ni mwanamke wa kwanza kabisa MJASIRIAMALI katika historia yetu.Alikuwa mnyamwezi wa Tabora ailiyekuwa akisafiri kufanya biashara na wakoloni ambao wakati huo walikuwa waarabu.Mwanamakuka alikuwa akisafiri kutoka Tabora mpaka bagamoyo kibiashara.Na hii ilikuwa karne ya 18 leo tupo karne ya 21 ni miaka mingapi iliyopita?piga hesabu.
Ujasiriamali wa wakati huo ilikuwa ni mdadilishano wa mali ghafi,vyakula vya nafaka kama vile mahindi,mtama,uwele n.k


Pia vyungu,asali na chumvi.Waarabu walikuwa wakimpa vyombo na bidhaa za kauri.Kama ujuavyo wakati ule biashara zilikuwa za kubadilishana zaidi.Mama huyu sifa yake inayomuweka katika historia ni ujasiriamali.

WAJIHI WAKE


Hakuna picha za mwanamakuka ila wanasema alikuwa kipande cha mwanamke amepanda hewani.Mlimbwende mwenye weusi wa sungusungu wenye mg'aro mithili ya chungu ndio ulikuwa ukimpa chati wakati ule.
Alikuwa mcheshi mwenye cheko bashasha na mkarimu kwa watu.


Mwanamakuka aliolewa na Chifu Pazi,chifu wa kizaramo.Walikaa katika ndoa na mumewe lakini hawakubahatika kupata mtoto kurithi na kuendeleza jina..Alifariki mwaka 1793 na kuzikwa hapo bagamoyo katika nyumba aliyokuwa akiishi na mumewe pia Chifu pazi alifariki na kuzikwa hapo hapo.

Kwa kufatilia historia fupi tu ya Mwanamakuka naamini umeelewa.Leo hii katika karne ya 21 kuna wanawake wengi sana wajasiriamali.Tena katika wakati ambao fursa zipo za kumwaga ndio maana tunasikia safari za watu za china,dubai,thailand,Usa,Uk n.k leo hii watu wanasafiri kwa ndege wakati ule ilikuwa unatembea kutoka sehemu moja kwenda nyingine Mwanamakuka alifanya hivyo.

Je mwanamke mjasiriamali wa sasa unafata vipi nyayo za mwanamakuka??

Nikiwa hapo Bagamoyo pia niliendelea kuona historia nyingi tu.Moja wapo ni visima hivi ambavyo niliambiwa vilichimbwa toka karne ya 18.

Vilichimbwa na kutolewa msaada na mfanyabiashara kutoka west India Sewa Haji Paroo ambae anaonekana katika hicho kipicha.Naambiwa alikuwa akisaidia watu sana hasa ilipotokea vita ya panzi na nzige.Ni wakati ambao nzige walishambulia mashamba na kufanya watu kufa njaa kwa kukosa chakula.Hata hospitali ya taifa ya Muhimbili kuna wodi inaitwa Sewa Haji kama kumuenzi.

Visima hivi vipo 130 na zaidi hapo bagamoyo

Kama hiki naambiwa hakijawahi kukauka toka kichimbwe.

Na huyu ni muongoza watalii mwingine anaitwa Freedom Nyerere akinipa michapo ya kihistoria.

Tukisurvey katika pwani ya bagamoyo eneo ambalo ndio lilikuwa likitumika kibiashara na hasa kusafirisha watumwa.

Eneo hili la ufukwe ni safi sio kama za hapa Dar es salaam zilivyochafu


Nipo na Janet alinisindikiza na Sakina...nikaambiwa niiname nilingane nao maana nimewapita urefu loh!

Haruna,Domi,Janet,Shagile na Sakina.

Pia tukaenda kwa Profesa Samahani Kejeli.Huyu ni muongoza watalii(tourguide) wa kwanza kabisa katika historia.Kwa mujibu wake mwenyewe alikabidhiwa rasmi kazi hiyo na serekali ya mwalimu Nyerere mwaka 1977 katika eneo la bagamoyo.

Hii ilikuwa mida ya saa tisa njaa inauma hatari,tukapata ugali na kuku na matembele.

Kwa ufadhili wa mama mdogo wake Sakina,kitu cha kuku wa kienyeji wa kuchoma kakolea ndimu na pilipili.Matembele ninavyoyapenda na hivi sikuwa nimekula ugali siku nyingi sipati la kusema.

Chakula hicho tulikibeba mpaka kwa Profesa Samahani Kejeli,akatupisha tule kwanza ili tukae sawa.

Baada ya mlo tukaendelea na maongezi.Akatuletea vitabu kadhaa vya kihistoria na hasa ya hapo bagamoyo.

Picha inayopatikana katika vitabu hivyo...mtumwa akiwakokota wenye nazo wakati huo ndio hao wakoloni.

Anasema kabla hajakabidhiwa rasmi hii kazi alifanya kazi kwa karibu sana na Dr.Leakey aliegundua mtu wa kale Olduvai goarg.Walikuwa marafiki na walikuwa wakifanya hiyo kazi pamoja japo yeye alikuwa kijana kidogo.Wakati Dr.Leakey ameenda Olduvai yeye alikuwa ameenda kuchimbua magofu ya Tongoni Tanga.

Ameishia darasa la nane lakini amepewa uprofesa kwa heshima ya mchango wake katika kutunza hostoria na kuelezea historia.

Kwa sababu alikaa sana hapo kaole bila kuwa na watu akaanzisha utaratibu wa kusign katika daftari lake mfumo unaotumiwa na matourguide wengi kwa sasa.




Ana vitabu vingi sana alivyobandika bussiness card za watu mbali mbali wa nje na ndani ya nchi.




Kiufupi safari yetu iliishia hapa lakini kubwa usikose kufatilia leo tena kuanzia jumatatu hasa kwa mwanamke mjasiriamali.Mwanamke mjasiriamali mbunifu na mtendaji lakini bado kuna vikwazo vinavyokufanya ushindwe kufikia malengo.

SHUKRANI

Sakina Lyoka mkuu wa msafara

Dereva wetu Haruna

Cameraman Shagile

Producer Domminic na ma friend Janet.

11 comments:

  1. Hongera sana Dina! nimefurahia story nzima ya Bagamoyo. Yaani nilivyokuwa naisoma, nikahisi kama nami nilikuwa Bagamoyo. Asante kwa kutujuza.

    ReplyDelete
  2. Hongera sana, yani Mungu akubariki kwa kutujuza na kutufungua macho mabinti na wanawake kwa ujumla. Mimi ni mdau wa mambo ya utalii namshukuru Mungu nina BA(Bachelor degree ya Utalii/Torism na elimu ya Utamaduni wa binadamu/Cultural Anthropology),nimefurahi kujua nisivyovijua.Kila la Kheri katika ujenzi wa Taifa.

    ReplyDelete
  3. Hallow Dinna asanteni sana kwa kutufufulia historia kidogo ya Bagamoyo maana ni wengi huwa hatuendi kuangalia mambo ya histiria live....umenikumbusha tukiwa A-level KIBOSHO girls trip ya Bagamoyo...tulipomuona PROFESA SAMAHANI KEJELI...tulicheka mpaka...ASANTE SANA SANA.

    ReplyDelete
  4. asante saana dina..mimi mwenyewe nimezaliwa bagamoyo na nimesoma hiyo shule ya mwanamakuka bagamoyo...yaani nilivyoiona hii story nimeifatilia kwa uzuuuri..asanteni sana, bagamoyo oyeeeeeeee..dina oyeee..luv u all

    ReplyDelete
  5. Asante sana Dina, yaani hicho kisima, nilichukua maji yake nikayaweka katika chupa. Huwezi amani yamekaa karibu mwaka hayajafanya mwani, hayanuki, zaidi yalikuwa kama yanapungua kwa mbaliiii. Mungu mkubwa jamani.

    ReplyDelete
  6. Nimefurahi sana kwa history ya Mwanamakuka, first nilikuwa nasikiliza Leo tena ya clauds FM. ndo nikaamua nifwatilie kwenye mtandao, Nimefurahi sana ukichukulia kuwa mimi ni mdau ktk tourism, Iam professional Degree holder in Tourism. But one thing, Dada zangu mlivyovaa mnatutega na mmewatega wengi Bagamoyo. Mngevaa mavazi ya kujisetiri zaidi yanayoendana na watu wa kule na wala si kuiga USASA. Aksante!!

    ReplyDelete
  7. Niaje dada Dina kiukweli we ni bonge la feminist mie nakukubali sana na unapenda maendeleo kwa kuwajali wanawake, kitu unachokifanya ni kizuri sana na kwa upande wangu umenipa historia mpya ya mwanamakoka niliyokuwa siijui mwenzangu, ol the best dada.
    big up sanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  8. Excellent, Keep up.

    ReplyDelete
  9. Hongera sana Dina! Yaani story ina mvuto sana nimefurahia sana. sijawahi kwenda Bagamoyo napatamani kama nini.

    ReplyDelete
  10. Hongereni sana kwa kwenda bagamoyo kwa kupata historia ya Mwanamakuka, mimi mwenyewe nimesoma shule hiyo lakini sikuwahi kujua historia ya jina hilo leo nimefahamu nashukuru sana kwa kuongeza knowledge kwangu.

    ReplyDelete