Tuesday, March 27, 2012

WADAU NASHUKURU MUNGU DHAMIRA YANGU INAENDELEA KUFANIKIWA

Nakumbuka zoezi hili nililianza mwaka jana mwezi wa nane la kupunguza manyama uzembe na uzito.Wakati huo nilikuwa na stress hatari baada ya kujaribu kila kitu ili kupunguza mwili bila mafanikio.Uzito wangu ulifikia 96 kgs unajua kwa sasa nimefikisha ngapi baada ya kupunguza kadhaa??ntakwambia.
Nilikuwa sipendi mazoezi kabisa ila sasa yamekuwa sehemu ya maisha yangu ya kila siku.Wapo niliowainspire na wao wanafanya mazoezi nakuanza kuangalia muonekano wa miili yao na afya zao.
Pamoja na mazoezi nafanya diet ya wiki mbili mbili kila mwezi ninayoandaliwa na Edgepoint.
Hawa kila siku wananiletea chakula cha diet kuanzia breakfast mpaka dinner.Popote nilipo wanaleta iwe nyumbani au ofisini.Wakati mwingi tunashindwa kufanya diet kwasababu ya muda wa kuandaa chakula hatuna wao wanakurahisishia hilo.
Wanakuletea katika kifurushi kinachofanana hivi.Mimi wananiletea bure lakini wewe watakutoza unahitaji?kama unahitaji piga 0715808038 kwa maelekezo zaidi.Nina miezi miwili sasa nafanya na inanisaidia.Diet yao ni wingi wa matunda,mboga mboga na protine inayotokana na nyama ya ng'ombe,samaki,kuku na mayai bila kusahau maji ya kutosha angalau lita 2.
MAZOEZI hayaepukiki hapa,ni lazima ufanye mazoezi kwa matokeo mazuri angalau kwa dk 30.
Nilipofikia tumbo na mikono ndio bado nasota navyo kwingine kote sina mashaka.
Kwa muda mrefu kina dada,kaka,mama mmekuwa mkiniuliza nafanya nini kupunguza mwili.Ukweli ni kwamba sio kazi rahisi kupunguza mwili kubwa ni NIA ya dhati na uwe umeamua kweli maana unaweza kuishia njiani.
Hivyo basi nimeamua kuanzisha club ya mazoezi.Kivipi?kwa nini?unashiriki vipi?ntakufahamisha hapahapa endelea kutembelea.

*thanks dada Anna wa powerful 4 slimming kwa zawadi ya gauni.Umeona nimelitupia nilikwambia utaniona nikiweka kwa blog.Ulijuaje kama nimeshafika size hiyo?asante my dear.

44 comments:

  1. ss unaonekana u msichana dina maana ulikuwa unaanza kuonekana mmama utafikiri una watoto 3 kip it up

    ReplyDelete
  2. Wow umependeza sana dina...naomba uniambie mazoezi gani ni kwa ajili ya mikono nataka nifanye pia..mwili wangu upo gado kwa ajili ya zoezi pia ila mikono bado cjaridhika..plz

    ReplyDelete
  3. Heeee!!! Dina nimekutamanije jamani, mimi si mnene sana ila najichukia hili tumbo baada ya kuzaa tu imekuwa balaa nashinda na njaa lakini wapi, nakunywa maji lita 4 kwa siku ofisini 2 na nyumbani 2 shida yangu tumbo tu, lina niharibia shepu hatari

    ReplyDelete
  4. DINA KWAKWELI NAKUPONGEZA KWANI UMEPUNGUA HASWA NA KUPENDEZA MI MWENYEWE HAPA NA SOTA KUJIPUNGUZA MAANA UNENE NOMA NA KUJIPUNGUZA PIA NI SHUGHULI NZITO UMEPENDEZA SANA MALIZIA KITUMBO.LOVE U MUCH

    ReplyDelete
  5. Waooo, umejitahidi dada yangu hongera sana.

    ReplyDelete
  6. jaman dina umependeza sana...mi iko penda ivo viatu sana....

    ReplyDelete
  7. umependeza sana dina

    ReplyDelete
  8. HONGERA SANA DINA, NAOMBA UWEKE PICHA YA BEFORE NA AFTER ILI KUTUTIA MOYO SISI TUNAOANZA. OTHERWISE, UMEFUNIKA.

    ReplyDelete
  9. hongera dina wetu, the thing is una moyo wa kushare na wenzio no one can take that from you huo ni upendo kila nikiingia humu unatushirikisha vitu vizuri tu be blessed my dear. Umependeza sana na unaonekana kufurahia mwili wako.hiyo club ya mazoezi naitaka sana i hope itakuwa nafuu kuliko zilizopo ila usitupige picha wengine tupo shy kutokea mitandaoni

    ReplyDelete
  10. lakini naona pia unapromoti sana biashara zenu.

    ReplyDelete
  11. Dina umependeza sana sana,yani kama mtoto vile,unafanya mazoezi ya aina gani? nami natamani nipungue,nimeanza zoezi hilo mwezi unaisha sasa ila nimefanikiwa akupunguza kilo 4 tu, naomba tips zaidi

    ReplyDelete
  12. dina ukitaka kupungua mikono na tumbo kwenye mikono beba vyuma uzito wa kawaida na kufanya pushups kwa wingi na tumbo unaitaji situps kwa wingi sana ukigogle utapata mbinu za kupunguza tumbo na mikono.bila hivyo utabaki na manyama nyama tu inabidi ufanye hivyo kukuaza manyama ya tumboni na mikononi kila la heri

    ReplyDelete
  13. oooh my Dina Marios,u luk gorgi for sure yaani the look is slplendid sweetheart,ntakutafuta aisee ili nianzishe na mimi mchakato with ur company!xoxo!!

    ReplyDelete
  14. nimeona kweli tumbona mkono bado ila kdg kdg tutafika umepiga hatua sn sn sn ukilinganisha na zamani

    ReplyDelete
  15. dah u have inspired me alot! i weigh 107kg na hapa cna mtoto yan naonekana kama am38 kumbe ndookwanza 32!ntajitahd mazoez

    ReplyDelete
  16. Hongera sana mamii luking gud hop ata wewe mwentewe wajisikia mwepesi sasa kip it up the gud work hapo cha kukazana ni tumbo na mikopo.

    ReplyDelete
  17. dina mwenzio nilikuaga sipendi kukuona ulivokua asee..ila kwa mabadiliko haya,hakyannan umekua mreeeeembo sn...saiv angalau unaendana na umri wako ss..malizia tumbo ma dia...ila hayo mazoezi ya mikono uwa yakoje?

    ReplyDelete
  18. hongera dina umependeza sansana ten years yonger mama

    ReplyDelete
  19. You looking good my dear, umefanya kazi nzuri sana! lakini tumbo lako siyo kubwa kiasi hicho maanake vinginevyo hapo ulipokaa mkanda usingeonekana kabisa

    ReplyDelete
  20. Umependezaaa, keep it up, hata mimi siku hizi mazoezi ni sehemu ya maisha yangu, baada ya kumaliza kuzaa nilikuwa na kg 95, huwezi amini sasa nina kg 77 siku hizi nayaheshimu mazoezi kama nini bora nikose hela ya kununulia nguo lakini nipate hela ya kwenda GYM

    ReplyDelete
  21. Hongera, you look gud na ninajua its not easy. Looking forward to joining your club, so please keep us informed. Stay blessed n keep up the gud work.

    ReplyDelete
  22. Hongera sana Dina, yaani umenispare big time, nadhani mazoezi na hiyo diet ndiyo inasaidia sana, hizo slimming dozi siyo kihivyo. Keep it up, Ukiweza, achana na red meat, kazana na vegetable na white meat only

    ReplyDelete
  23. dina mimi sion mnene kivile ila mikono ndio naweza sema minene sasa inaniboa sana. tafuta basi zoezi la mikono. hongera umepungua sana

    ReplyDelete
  24. Hongera,umejitahidi, na umependeza tuambie kuhusu club ya mazoezi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hongera sana Din!! umependeza sana, mpaka nami umenitia hamasa ya kufanya mazoezi. Siyo tu kupunguza mwili hata kwa afya mazoezi ni mazuri sana!! hongera sana ma dear!

      Delete
  25. i love you sana, you look mwa! hebu anzisha hiyo gym yako uone itakavyofula wateja, tena anzisha ya ukweli katikati ya mji wapenzi wako waweze kufika kirahisi. Tafuta mtaji mkubwa ili upate vifaa vya kisasa ili kuwa impress wateja wako. kama utashindwa kukopa benki due to colateral basi tafuta watu wenye hela zao ambao hawana idea ya hiyo venture kisha fanya nao perternership utaniambia matokeo. niliwahi kuona taharifa ya habari ya kenya CITIZEN live at 9 kama miezi 6 ilopita walikuwa wakiwashindanisha wadada/wamama wanene kipindi kilikuwa kinaitwa slim possible, wanawalipia gym kila wiki wanaenda kupima kilo zao live aliyepungua uzito mdogo anatoka kwenye mashindano ilikuwa nzuri sana walipungua sana uzito. ukishafungua gym yako unaweza kuanzisha kipindi chako kwenye clouds Tv na ukashindanisha wadadana wamama kila wiki wakawa wanakuja kupima uzito live utasaidia wengi na gym yako itajaa

    ReplyDelete
  26. Congrats Dina! Umependeza sana na uko juu my dear. Luv u:-)

    ReplyDelete
  27. hope utatapata wa kukuoa sasa,bse at that time,na na naaaa

    ReplyDelete
  28. Yaani Dina miye nitakuwa wa kwanza katika club, nimejufungua mtoto wa pili kawaida, sasa nimenenepa na tumbo mwe, ingawa nimelifunga lakini wapi, nataka kurudi fresh jameni.

    ReplyDelete
  29. Mh mwili mkubwa noma pole na hongera sio rahisi aisee , umejitahidi sana , nikikumbuka ulivyokuwa umejiachia, nilikuwa nachukia utadhani ni mimi , yani cpendi mwanamke asiyejali shape yake ,

    ReplyDelete
  30. Dina usichelewe basi kuianzisha hiyo club bana na sie tupungue maana tunatisha wengine hapa.

    ReplyDelete
  31. Hongera sana, nlikuambia mpaka ufikie kama hiyo picha ya profile hapo juu, Mi nahitaji sana kuondoa Abdomen stomach..nakachukia kwelikweli haka katumbo ka chini..hata nikivaa nguo za usiku sipendezi...haya cnt wait to join ur club..creative as usual..keep it rolling dear...

    ReplyDelete
  32. hello Dina, kiukweli kbs nakufurahia mno kukuona ukiwa umepungua na umependeza sana kuliko ulivyokuwa mnene, kamwe usije ruhusu ile hali tena, ilikufanya uonekane mzee kbs, keep it up

    ReplyDelete
  33. Hongera mamii kupungua kunataka moyo Nami nilifanya diet nkapunguza mi kg kibao sasa nimerudi tena kufikia summer nifikie malengo yangu bado mikono na tumbo vyanitesa. Hongera mamii.

    ReplyDelete
  34. Dina una pozi zuri la picha lakini kamera yako aitoi picha vizuri.i mean the quality.Nimeipenda sana picha ya pili lakini ina ukungu hata sura yako inaonekana kwa shida.wadao wako wamesha complain about the quality of your pictures but you havent done anything about it. it is time now to work on feedback for improvement.Let us know if you have no budget for it for this month/year wadao wako twaweza kuichangia thru tigo au M pesa, we love you, we love your blog and pse take it positive.

    ReplyDelete
  35. Hongera sana Dina umependeza jamani looh!!! nimekutamani sana,
    mi ni kibinge inabidi niige mfano wako

    ReplyDelete
  36. Umepenzeza! hongera sana

    ReplyDelete
  37. Hongera sana kwa kupunguza mwili coz coz mazoezi $ Diet yanahitaji moyo my dear. Umependeza sana mamito na hilo gauni limekutoa kweli,endelea na mazoezi

    Lizbeth

    ReplyDelete
  38. mamy hongera me nataka ya tumbo na minyama ya pembeni advise please naona umeelekea kuzuri

    ReplyDelete
  39. jaman dina umependeza sana, mie nnakilo 90, nnaonekana kama mmama wakati co, umenitia moyo sasa naanza kwa kasi mazoezi na diet.

    ReplyDelete
  40. naomba utuwekee picha ya ulivyokuwa bonge ili niamini

    ReplyDelete
  41. dah umepeneza mi naitaji sana kupungua sasa naomba nipatie list ya mlo kuanzia asubui hadi usiku ili nianze diet coz i dont kno wat kind of food i should eat to maitain plz dina do so by da way i am very interestin in u sisy!

    ReplyDelete
  42. Quite an inspiration. Waitng for the details of the health club

    ReplyDelete