Jana najua nilikuacha njia panda kwa wewe ambae hukusikiliza heka heka za leo juu ya mtoto Lulu.
1.Juzi wakati Lulu amelala nyumbani kwa mjumbe aliogeshwa na kukutwa mwili umejaa makovu ya fimbo na vipigo.
2.Akamwambia mjumbe nyumbani akikosea anapigwa sana na baba.
3.Lulu alipomuona mama yake alilia kwa uchungu sana na kugoma kurudi nyumbani wala kumsogelea mama yake.
4.Wananchi wenye hasira nusura wampige mama mtu.Na baba alipoitwa akasema hawezi kwenda kwani yupo kazini.Hapo ikumbukwe Lulu amepotea kwao toka tarehe 23.Hivi mzazi uitwa kwa suala la mwanao utagoma kwenda kisa kazi?labda.
5.Usiku baba yake alienda kwa mjumbe kumuomba Lulu arudi nyumbani lakini hakufanikiwa mtoto alikataa katakata.
Mwisho wa siku Lulu alibaki kwa mjumbe.
Mimi binafsi,Gea pamoja na ushauri kutoka kwa msikilizaji tukaona Lulu abaki kwa mjumbe kwanza.Mpaka wazazi wake watakapo kuwa tayari kuwa wawazi kushirikiana na sisi kujua chanzo cha matatizo ya Lulu.Kwa haraka haraka Lulu amekosa upendo na wazazi wake kuelewa hisia zake.Embu nikuulize mdau wewe mtoto wako wa miaka 8 pamoja na utundu wake ana makovu kwa kiasi kinachozungumzwa cha Lulu?
Itambulike kuwa sisi ni chombo cha habari na burudani tunapotoa habari hizi vile vyama vya kutetea haki za watoto,NGOs mbalimbali,wizara ya wanawake jinsia na watoto mjitokeze kushirikiana nasi katika hili.Haya matukio ni mengi na hatuwezi sisi kuyatatua tunajaribu kwa uwezo wetu.
Tunashukuru jana kuna NGO inaitwa WILDAF ilikuja hapa ofisini na kuamua kufanya kazi na sisi na kufatilia suala la mtoto Lulu.Wakijitokeza watu kama hivi sisi tunaendelea na kazi yetu ya kuwaeleza nini kinaendelea katika maisha yetu ya kila siku na wao wanachukua jukumu la kutatua.
mm sielewi dina tunasema watoto wa ss wanautovu wa nidhamu, wameharibika, lkn ukichunguza kiundani wazazi ndio suluu, mm binafsi nasema kama huwezi kuzaa ni bora uache kuliko kuzaa mtoto unamtesa utafikiri wa kambo, hebu angalia yule mm aliyemfanyia vibaya wanae kumuingiza plastic sajary yani mm hata sielwi watu sasa wanaroho mbaya kupitiliza.
ReplyDeleteHATA KAMA NI WA KAMBO HAKUNA MTOTO ANAYESTAHILI KUTESWA,WANA HAKI YAKUPENDWA NA WAZAZI NA HATA JAMII HAPO NDIPO TUTAJENGA TAIFA LA KESHO
Deletemasisikitiko yangu mimi ni kwa serikali, yani kuanzia hile story ya mama kumsaga mwanawe na hii ya lulu, lakini sijasikia hata siku moja ustawi wa jamii imeingilia kati, mijitu hipo offisini inakula kodi zetu, wakati issue zote hizi walitakiwa wazibebe kijuu, tuna safari ndefu sana watanzania, unampeleka mtoto polisi, wao wanasema nenda nae nyumbani maana wao pa kumuweka hawana, serikali ivunje tu hii takataka inayoitwa ustawi wa jamii, nina hasira sana kwa kweli, watoto wanaranda randa mitaani, wengine hawaendi shule, wengine wanafanya biashara, serikali hipo na hicho chombo cha kushughulika na hayo yote kipo, mwisho wa mwezi wanavuta mishaara, ni kichefu chefu, mamigari mikubwa lakini wafanyalo hakuna, halafu jitu linarudi nyumbani linapretend limechoka kweli ni nini alichofanya zaidi ya kupulizwa na kiyoyozi, moyo wangu unaniuma sana, kila mtu akiwajibika ipasavyo kwenye kazi yake, i swear mambo kama haya yatakuwepo,lakini si mengi kama yalivyo sasa, sorry kwa kuandika sana nina hasira kweli na watendaji wasiotenda kazi zao.
ReplyDeleteDina..hongera sana mdogo wangu kwa kazi unazozifanya Mungu atakulipa..Mimi naona hawa wazazi na wauwaji kabisa.tena mabarazuli...sioni haja ya wao kupewa huyo mtoto..mkichunguza nna uhakika mtakuta kuwa pengine baba ni wa kambo jamani..au huyu si mama yake..looh dunia kweli imekwisha..huyo mtoto apewe msaada jamani hata akirudi huko hawezi kuwa na amani kabisa.
ReplyDeleteHi! Dina na wote hapo Clouds. Big up sana kwa kweli mnajitahidi lakini fanyeni kazi Mungu atawalipa kwa jinsi aijuayo. Mimi ni mzazi nimeguswa na hili na ninawapongeza kwa kweli. Mimi nadhani kuna haja ya kuliombea Taifa letu. Hainiingii akilini kama kweli mtoto uliyembeba miezi tisa tumboni ukapata uchungu siku ya kujifungua ukamfanyia ukatili wa jinsi hii. Siko hapa kuwajudge hao wazazi maybe they have a reason behind it lakini bado sipati picha
ReplyDeleteDUNI HII JAMANI EWE MWENEYEZI MUNGU TUSAMEHE WAJAWAKO NA UTUPELEKE KWENYE NJIA SAHIHI MAANA SIJUI DUNI INAELEKEA WAPI
ReplyDeleteUnajua Dina, mkiwa mnatoa habari kama hii ya Lulu mnatakiwa muwe mnaendelea kufuatilia kama kuna hatua zimechukuliwa au la kisha mnaripoti tena kwenye media yenu, hivyo ndivyo vyombo vikubwa vya media vinavyofanya. Wanakomaa na hiyo ishu mpaka wanafika nayo mwisho na hii inawafanya wahusika kutake action kwa sababu wanajua vyombo vya habari viko mgongoni mwao. Ndio maana kuna investigattive reporting, very risk lakini mnafanya kwa manufaa ya watoto. Msione watu wanakimbilia kutoa taarifa kwenu badala ya polisi au kwenye NGO zinazojifanya zinatetea haki za binadamu, hao wako kwa maslahi yao, kwa kesi kama hizo hakuna hela ya mzungu/project fund wala allowance huwezi kuwaona wakijitokeza hata kutoa msaada wa kisheria cause it is not their intrest wewe waambie mambo ya siasa na maandamano watajitokeza ka nyuki.
ReplyDeletenchi yetu imeoza kwenye swala la kushuhulikia watoto.basi angalau tuige mambo mazuri,nchi za wenzetu,huyo mama asingepewa tena huyo mtoto,na angelelewa na familia nyengine ambayo serikali inawalipa{foster care}katika kazi ninayofanya,mtoto ukimuona na makovu,unaripoti,social services.au mtoto ukimpeleka hospitali,nesi au dokta akiona makovu makovu kama ya kupigwa,anaiarifu,social services.kwa kweli wenzetu wanajitahidi.huwa najiuliza,wale watoto wanaozurura mitaani,jamani hakuna sehemu husika ya kuwasaidia hao watoto?radio zenu zinawasaidia wengi,maybe sehemu husika wataona aibu
ReplyDeleteasante Dina kwa habari hii na updates yake kiukweli mimi nimeumia sana coz nina mtoto wa kike mtundu namchapa lakini c kwa kiasi hicho chA KUMLETEA MAKOVU MWILINI,na kumchapa kidogo ni kama njia mojawapo ya kumfundisha kuwa asifanye kitu flani mfano asitukane unaweza kumchapa kidogo ili siku nyingine asirudie maana anajua akirudia atachapwa, kwakweli kwa story ya huyu mtoto lulu nimeumia sana imeniuma mno utadhani ni mtoto wangu yaani hapa ninavyoongea natokwa na machozi kwanini huyo mama amtese mwanae wa kumzaa?nikijiuliza je anajua uchungu unaumaje?au mtoto si wake?hapana bado nina maswali na majibu sipati,ningekuwa hakimu ningehakikisha mama kama huyu anafungwa maisha,jamani natamani kujua kila kitakachokuwa kinaendelea juu ya mtoto lulu,Mungu ampoze majeraha na machungu anayopitia malaika wake,pole lulu!asante Dina na Gea Mungu awabariki nanyie pia!
ReplyDeleteIt’s so so sad,tanzania tuko mbali sana tena nyuma sana if it was in a well developed country huyo mtoto angedakwa fasta sana na wampekele in a good children’s home mpaka wazazi watakapo kuwa proven they are ready to take care of the kid, but hare watoto wana kaa kwa wajumbe,hiyo sio kazi yao!!!! ustawi wa jamii wanafanya nini?wats their work???? Or do they want us in the streets to demonstrate that we need to see them on their feet’s??what the heck is happening mean in this year 2012 bado watu hawajui how to handle such things ,Tanzania sio maskini ila wengi hawataki kujaribu,hawataki kuthubutu,not confident at all, do you want the whites to do everything for us even thinking?? we are blessed with a big land so much enough to biuld a good I mean perfect children’s home, and so much more that we need but then what, nothing is happening!!! Counseling centers,mtu anapelekwa baada ya hekaheka,jamani kweli hivi mpaka lini? hivi vitu sio vya wazungu tuu we need them too! Na NGO hazipewi sapot na government otherwise they would be up their shining and on the lookout of all this that is happening
ReplyDeleteDina hongera sana mi pia mtoto wangu ni mtundu alikuwa akitoroka shule na nyumbani pia lakini nilikuwa sili silali hadi nimuone naongea nae anakuwa kama kanielewa lakini atarudia tena na hiyo hali inaendelea lakini kama mama sijachoka kuomba na kuongea nae na pia nashafanya appointment ya kumpeleka kwa mwanasaikolojia (Dina ana mkono wake hapo) namsubiri arudi likizo shule japo nishapata taarifa mbaya kutoka shule juzi tu. mbaya zaidi mie ni single parent, nilishawahi kumpeleka upande wa baba yake nione labda mie kanizoea sana ndo sababu anafanya visa, lakini nilimfata baada ya kupigwa kipigo cha mbwa mwizi na baba yake mkubwa (ngumi na mateke) na kufukuzwa huko na kuambiwa akionekana eneo hilo la familia ya baba yake watamuua, akifa hawatakuja, wakifa wao asiende. kipigo kilikuwa kikubwa sana alirudi kachakaa ninazo picha zake za makovu yake hayo. inauma lakini mie ndio mama na rafiki yake nitapigana hadi mwisho na mungu naamini anasikia dua zangu ipo siku atatulia na asome vizuri kwani amejaaliwa akili ila utundu wake umezidi kupita kiasi, na kadiri anavyokuwa hofu kwangu inaongezeka sijui atakuwaje baadae, eeh mungu nijaalie na unusuru vizazi vyetu na taifa letu. Kulea mmmh! Da J
ReplyDelete.......mtoto mdogo hivyo anachukia wazazi kiasi hicho....there is something fish is going on.keep digging.
ReplyDelete