Tuesday, April 24, 2012

ZIWA SINGIDANI...

Tulipelekwa katika bwawa ambalo wenyewe wanaliita ziwa Singidani.Bwawa hili wenyeji wanasema huwa linakauka kila baada ya miaka kumi.Likikauka wenyeji huenda kuvuna chumvi wanajaza majumbani hawajui chumvi inatoka wapi.Maji yake ni ya chumvi kabisaaa.Ikifika mwaka wakumi likikauka hapo panakuwa njia na watu wanapita halafu baadae linajaa upya humo ndani kuna samaki pia watu wanavua.Hapo ndio beach yao watu huenda kupumzika na kubarizi maharusi kupiga picha pia.

7 comments:

  1. kiukweli nyie clouds fm mpo juu, sisi hapa Singida mda wote ni Clouds fm 89.8 wakati wote na ndiyo radio ambayo inpendwa na watu wa rika zote. Tunatamani muendelee kuwepo Singida na kuzidi kutupa burudani na elimu mda wote. Mimi binafsi mtu hawezi kunibadilisha kuipenda Clouds fm kwani mda wote kuanzia power breack fast mpaka kunachwea nipo nanyi kwenye 89.8 fm. Tunaomba pia mtujulishe mwakilishi wenu hapa Singida ni nani kwani tunapenda habari za Singida pia zijulikane mikoa mengine. Dina na team yako mko juu natamani nifike hapo mjini niwaone. Mimi Stanford Mkude wa Misuna Singida

    ReplyDelete
  2. leo tena iendelee kuwepo Singida dada Dina, jana niliwaona Singidani lakini sikuamini kama mlikuwa ni nyie lakini sasa nimeamini baada ya kuona picha zenu kwenye blog yako. Kiukweli nyio mko juu naipenda 89.8 fm

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana kwa kweli!!! kwa kweli kutoka nje ya Dar nako kuzuri!! Unabadili hata hali ya hewa, na kuona watu wengine wanaishije? Saafi sana! Haya twasubiri hayo ya Dodomia!!

    ReplyDelete
  4. Hongereni jamani huku ndo kwetu singida (bomani)

    ReplyDelete
  5. waoh... mlienjoy jamani ndo utali wa ndani huo big up clouds...

    ReplyDelete
  6. Hongera sana cloudsfm mnajua mnapata ya njia kwani mnakutana na mazingira na watu tofauti kuna mliyozoea na mambo mengine kwenu yatakuwa mapya na mtaweza kuishi popote duniani basi hiyo ndio elimu ya njia nawatakia safari njema mungu awaepushe na mabalaa ya njia, awanusuru na shari ya majini na watu, awarejeshe majumbani salama muweze kuungana familia zenu

    ReplyDelete
  7. Du dina umenikumbusha mbali Singidani mwe, nakumbuka miaka ya 93/94 niliishi huko, tena nyumba zilizopo karibu na ziwa hilo, nasikia sikuhizi imejengwa zinga la hoteli du, nitarudi siku moja kuwala samaki wa Singidani, ila pamoja na kuishi huko kwa miaka miwili sikuwahi kuisikia hiyo story ya kukauka kila baada ya miaka kumi au sijui kwa vile nilikuwa mdogo.

    ReplyDelete