Tuesday, April 24, 2012

KESHO KATIKA LEO TENA KUTOKA DODOMA

Kesho katika leo tena tukiruka moja kwa moja kutoka Dodoma utasikiliza mazungumzo niliyoyafanya na Wastara.Kama nilivyoahidi kabla sijasafiri ni  kushirikiana na familia hii kuhakikisha tunakusanya pesa za kumsaidia mumewe Sajuki kuweza kwenda kutibiwa India Mwezi wa tano.

Nikekuwa nikifanya hivi kwa watu mbalimbali wenye uhitaji kupitia hapa kwenye blog na kipindi changu cha leo tena.Watanzania nachukua nafasi hii kukushirikisha kufanikisha hili.Mlioomba namba ya simu kwa ajili ya kuchangia sikuiweka makusudi maana Wastara aliibiwa pesa zote zilizokuwa zimechangwa huko.Nitatoa muongozo mzuri wa namna ya kuchangia au unaweza kuwasiliana na mimi kama utaguswa.Kutoa ni moyo kama hujaguswa naomba uache tu bila kumjunja moyo yule aliyeguswa na yupo radhi kuchangia.

1 comment:

  1. tunaomba muongozo kuwa ameibiwajee?ili kama ni fundisho na sisi wengine tujifunze.maana si ana namba ya siri,sasa ilikuwaje jaman.mimi ni miongoni mwa watu tulioguswa nilimchangia kupitia namba yake ya tigo,na bado nipo tayari kushirikiana na ww kumsaidia huyu dada wa watu.

    ReplyDelete