Saturday, February 25, 2012

MSHIRIKI WA TATU

Huyu ndio yule kama ulisikiliza kipindi barua yake ilikuwa ndefu kuliko zote.Anaitwa Tatu Mwenda Ngao mkazi wa Majohe.
Tulifika kwake ambako ni Gongo la mboto mbele kabla ya kufika Pugu.Akatupokea na kutupeleka nyumbani kwake.

Mgeni mie nikakaribishwa kiti

Tatu ujasiriamali wake aliuanza mwaka 1995 akitengeneza na kuuza tambi za dengu

Baadae visheti,mayai ya jumla na keki

Kabla hajaingizwa hasara haya majiko yalikuwa 7 ya kutengenezea keki.Alikuwa na uwezo wa kuuza keki mpaka 1,200 kwa siku.Baada ya kutapeliwa mara kadhaa mwisho biashara ikafa.Majiko manne akauza yamebaki hayo matatu ambayo hajui hata kama akianza biashara upya yatafanya kazi.

Nyumba hii ambayo alihamia haijaisha aliijenga kwa biashara hiyo ya keki,alihamia ikiwa chumba kimoja tu.Amekwama kuimalizia baada ya msingi wa biashara kufa.

Anatengeneza pia sabuni za maji za kufulia ana vitu vyote vya kutengenezea kanitajia hata sijavishika.

Dukani kwake kwa sasa panapompa hela za mahitaji ya kawaida

Biashara yake ya visheti pia anaendelea nayo

akiwa na watoto wake wawili,watatu alikuwa shule


Pia ni mwenyekiti wa vikundi 40 vya kina mama wajasiriamali kata hiyo ya majohe.

Akanipeleka kwenye kikundi chao cha akina mama ambacho yeye ni mwenyekiti

Pana mwendo kidogo kutoka nyumbani kwake.

Tukakuta kinamama wapo busy wanasindika karanga

wengine wanakaanga na kuzitoa maganda

Kikundi chao wapo kinamama 25



Karanga iliyosindikwa kabla ya kuwekwa kwenye chupa

Hivi ndivyo zinavyoonekana zikiwa kwenye chupa

Hazina kitu chochote ndani zaidi ya chumvi na zinaka bila kuharibikwa kwa miezi 6

Mzigoni

Picha na wakinamama

Tukamaliza na safari ya kurudi makwetu ikaanza



Kesho jumapili tutamalizia na washiriki wengine wawili wale walioingia hatua ya tano bora.Ukitaka kumpigia kura anayekuvutia kuwa anastahili andika neno MK acha nafasi kisha jina lake kwenda namba 15678.Na ni kwanjia ya simu.

12 comments:

  1. Mungu akubariki dadangu,this is so touching and inspiring..

    ReplyDelete
  2. Duu safi sana nakupongeza kwa kuwa na aidia mpya ya kuwasaidia wanawake waliyo wahi kuthubutu.. Naomba kura yangu iende kwa huyu mama aliyekuwa akipika keki akakwama.. ni mimi NIWA MBAGA

    ReplyDelete
  3. Mimi nipo nje ya nchi sijui nitawezaje kupiga kura, au tuambie tunafanyaje, lakini kwa kweli nimemzimikia Bi Tatu kwangu mimi ni mwanamke wa shoka, ameanguka lakini anaanza kusimamia magoti, she is a fighter.

    ReplyDelete
  4. Nimempenda huyu mama! Ananonekana ni BINTI MWANAMAKUKA kweli! Mjasiria mali wa kweli hakati tamaa.

    ReplyDelete
  5. hai dina mambo?u look so sex gal,luck is the man sleeping with u the whole nit

    ReplyDelete
  6. very interesting,wazo zuri idea nzuri,tumalizie na hao washirik wengine ili tupige kura

    ReplyDelete
  7. Kumbe ulifika meneo ya kwetu, ningelijua siku hiyo tungekutana, karibu tena

    ReplyDelete
  8. Nimependa sana hiyo idea ya kuwawezesha wanawake wajasiriliamali,keep it up mdada!

    ReplyDelete
  9. sure dina upo juuuuuuuuuuuu ...... ebwana mautunsu yako yako juuuuuuu mbaya..... just visit wwww. letehabaritz.blogspot.com tusheee mautundu au siyo pamoko sana

    ReplyDelete
  10. Dina hongera sana dada yangu kwa kazi unayoifanya wewe ni mfano wa kuigwa! God bless u!

    ReplyDelete
  11. mama wa keki yupo juu

    ReplyDelete