Sunday, February 12, 2012

R.I.P WHITNEY HOUSTON

Sijui hata nieelezeeje,nikiwa kama mpenzi na shabiki wa whitney nimeguswa sana na kifo chake.Ni jumatano tu nimenunua DVD ya nyimbo zake za live pale rese garden.
Jana usiku niliporudi kutoka Bagamoyo nikawa naangalia na kufurahia DVD yangu
Tena nikawa nasifia kweli style yake ya nywele.Hata sikumaliza nikawa nasinzia nikazima tv,taa na kwenda zangu kulala.Alfajiri napata meseji kutoka kwa producer wangu Moonshine akinifahamisha juu ya kifo cha Whitney Houston.Duuh nikashangaa sana na leo siku nzima nimeshinda naangalia hiyo DVD.


Katika picha hii whitney akiwa na mama yake mzazi Cissy mwaka 1984 wakati ndio anaanza kuingia katika muziki akiwa ni binti tu wa miaka 21.Yeye na mama wake walikuwa wakiimba katika night club ndio akaja kuvumbuliwa na boss wa arista records.Alikuwa na sauti ya pekee ambayo mfano wake hauelezeki.


Kwa miaka mingi nimekuwa nikisikiliza nyimbo zake bila kuchoka kama the greatest love of all,i have nothing,i wanna know,i will always love you,my love is your love,when you believe,i learn from the best,try it on my own na nyingine kibao.


Kwa muda mrefu amekuwa akipambana kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya.Kifo chake inasemekana kimetokana na drug overdose japo haijathibitishwa bado.Aligunduliwa kuwa amefariki na bodygurd wake akiwa amezama bafuni kwenye bathtub .Whitney alikuwa katika hotel ya Beverly Hilton ambapo alikuwa anatakiwa kuperfom muda mchache baadae katika concert ya pre grammy bash.Alifariki jana jumamosi saa 3:30 pm saa za huko Marekani akiwa na miaka 48.Ukiacha muziki nilipenda sana filamu alizowahi kucheza waiting to exhale,the preacher's wife,the bodyguard pia kuna filamu yake mpya ya mwaka huu inaitwa sparkle bado sijaiona maana ndio imetoka.

Whitney ndio msanii aliyevunja record ya guiness book of record kwa kuwa msanii wa kike aliyewahi kupata tuzo nyingi kuliko wote.Mpaka mwaka 2010 alikuwa na jumla ya tuzo mbalimbali za muziki 415.

Kwenye maisha yake yote alijaaliwa kupata mtoto mmoja tu wa kike Bobby Christina.

Whitney na Michael Jackson walikuwa marafiki na walishafanya kazi kadhaa pamoja.Michael alikuwa King of Pop na yeye queen of pop.Wote ni ma Icon wa muziki na ambao hatunao duniani.

Whitney amewainfluence wa wasanii wengi sana wakubwa kwa wadogo.Miongoni mwao ni Celin Dion,Mariah Carey,Ton Braxton,Christina Aguilera,Nelly Furtado,Jessica Simpson,Kelly Clarkson,Britney Spears,Ciara,Jenipher Hudson,Lady Gaga,Brandy,Mary J,Leona Lewis,Beyonce,Alicia Keys na wengine wengi ambao wote wanafanya vizuri kimuziki.

Mwaka 2009 alitokea katika kipindi cha Oprah na kusema hadharani kuwa alikuwa akitumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu ila ameacha.

Picha hii alipigwa siku mbili kabla ya kifo chake ambapo alikuwa amelewa na aliparty ile mbaya.Na inasemekana usiku huo alikuwa na mood mbaya kweli alikuwa akigombana sana na watu.


R.I.P Whitney Elizabeth Houston

14 comments:

  1. Rip whitney houston u will be missed.sooo sad i will alwyz love u

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli kifo chake kinasikitisha. Pole kwa familia yake. Mungu amuweke mahali pema peponi Ameni!!!

    ReplyDelete
  3. ki ukweli dina namkubali sana huyu mm hasa katika move yake ya the bodyguard n wimbo wake wa i will always love u naupenda sana na huwa kamwe haunihisi hamu, mungu ailaze roho yake mahali pema peponi Amin.

    ReplyDelete
  4. R.I.P Whitney houston sina la kusema zaidi ila nimehuzunika sana.

    ReplyDelete
  5. SOOO SAD, Inauma sana, sauti yake tamu isiyoisha hamu kumsikiliza. R.I.P WHITNEY

    ReplyDelete
  6. Mama Jos' said,

    Kwa kweli mdogo wangu dina sina cha kuaongea zaidi kwa mwanamama huyu. Nyimbo zake zilikuwa zinamtoa nyoka pangoni, hata nikiwa sipo katika mudi nikisikia nyimbo zake I have nothing, I will always loving you nilikuwa nafarijika sana.
    Mugu aiweke roho yake mahali peama peponi Amin!!!!

    ReplyDelete
  7. Dina muongo acha kupotosha Whitney ni Queen wa R&B na sio Pop.Madona ndio queen wa Pop usiwe mvivu wa kusoma na kujifunza zaidi maelezo mengi ulioandika sio sahihi.Alale mahali pema peponi.

    ReplyDelete
  8. Siwezi kubishana na wewe ila kwa taarifa yako Whitney hajawahi kuwa queen wa RNB coz sio aina ya muziki aliokuwa akiiimba.Whitney anatambulika kama queen of pop kubali kataaa huo ndio ukweli.Kama ni msomaji mzuri hutabishana na hilo.Kwa kukusaidia hata katika link hii ingia usome kwa kirefu.
    http://www.dailymail.co.uk/news/article-2100018/Whitney-Houston-dead-2012-Fallen-star-ravaged-drugs--life-pictures.html

    ReplyDelete
  9. mimi nikisikiliza wimbo wake wa Trt it on my own....huwa nasikia raha sana na huwa najiamini kuliko kiasi

    ReplyDelete
  10. Kwa upeo wako wa unamuweka Whitney wapi au kwavile mwandishi wa uingereza kaandika hivyo basi kwao ni sahihi.Acha mambo ya copy and paste mawazo ya watu.Michael mpaka kufa kwake alijulikana kama king wa pop,unakumbuka ni miaka mingapi Whitney alitoa single na haikufanya vizuri na apoanza tour mashabiki walimkataa na kumzomea kinyume na Michael Jackson ambae kweli ni King wa pop.Kwa hiyo Whitney hajamfikia bado Madona.Sio uwezi kubishana ila utumie upeo wa kufikiri na kujifunza sio usome tu na copy.Education is SEXY.

    ReplyDelete
  11. halafu aliyegundua kuwa amefariki ni hair designer wake ambaye yeye pamoja na stylist wake na bodyguards wawili walikuwa kwenye hiyo room wakisubiri wampambe akaperform na wote walishangaa baada ya kuona saa nzima imepita bado Whitney akiwa bafuni ndipo hair designer wake ambaye ni mwanamke alipoenda kumgongea, akaona kimya akafungua mlango na kumkuta kichwa kikiwa kwenye maji na miguu juu ndipo aliposcream na one of the bodyguard akakimbilia huko na kumtoa akiwa unconsious na baadae kugundua kuwa ameshafariki!! source TMZ NA MTO(Media Take Out)

    ReplyDelete
  12. Kuhusu kugundua kufa kwake kwani wewe ulikuwepo??UMESOMA KATIKA vyombo vya habari kama nilivyosoma mimi.Na vyombo vya habari kila kimoja kinaweza kuelezea story kwa namna tofauti lakini kikawa ni kile kile.Kama ambavyo wewe umesoma na mimi nimesoma pia hivyo hivyo maana wote hatukuwa marekani!
    Na kama unabisha kuhusu yeye kuitwa queen wa Pop ni sawa maana sijakulazimisha kukubaliana na hilo ila mimi natambua kuwa alikuwa akipewa hiyo title na Madonna pia the same.

    ReplyDelete
  13. wabongo kwa ubishi wa kipumbavu sasa nimeamini wa Tz wengi akili fupi,mnavyobishana hapa ova mshindi anapewa milions of money,we Dina amini unavyoamini na mdau amini unavyoamini full stop.
    Kubwa I like the way dina ulivyoileta hii story,vyombo vingi vya hapa kwetu wali copy n paste tuu ila dina kidogo maelezo yako yamewafungua wengi yani yapo in details safi mama kazi nzuri.

    ReplyDelete
  14. Kwa zaidi ya miezi 6 sikuwahi kusikiliza nyimbo za whitney lakini jioni ya kifo chake nilisikiliza album yake moja ambayo nilikua naipenda sana yenye baadhi ya nyimbo kama "THE GREATES LOVE OF ALL" na "HEART BREAK HOTEL". TO MY SUPRISE USIKU HUO NDIO KIFO CHAKE KILIPOTOKEA.....

    ReplyDelete