Wednesday, April 25, 2012

SINGIDA PIA TULIMTEMBELEA BIBI RAJABU

Tulimtembelea bibi Rajabu anaishi Singida karibu na ziwa Singidani.Ni bibi mcheshi sana anaongea na anastory huyo.Bibi taaluma yake ni mwalimu.Alikuwa mwalimu wa shule za msingi miaka ya 40 mpaka 70 akastaafu pia aliwahi kujiingiza katika siasa.Anasema katika taaluma yake ya ualimu aliwahi kumfundisha hata Bibi Titi kusoma na kuandika.

 Mimi napenda  sana picha,na picha zinatumikaje katika kupamba nyumba?Nilipenda sana mpangilio wa picha nyumbani kwa bibi Rajabu.Kila picha unayoona ina hadithi ya kusimulia.Bibi aliibahatika kuhishi na mumewe wa ndoa kwa muda mrefu kabla mungu hajamchukua.Ukiangalia picha hapo unaona mpaka waliposherehekea miaka 50 ya ndoa.Nilimuuliza bibi kwa miaka hiyo mzee walikutana vipi.Akajibu kuwa alimchumbia wala hakuwa akimfahamu.Anasema enzi zao ulikuwa unachumbiwa bwana uwe unamjua humjui umempenda hukumpenda posa ikija wazazi wameridhia unaolewa tu.Ila anashukuru yeye mume wake walipokutana tu wakaridhiana.
Bibi amejaaliwa watoto 10 ila mmoja mwenyezi Mungu alishamuita mbele ya haki.Watoto wake wote wamesoma mtoto mwenye elimu ndogo ana degree tu wengine wote wamevuka hapo kwa degree kadhaa masters kadhaa n.k.Hapo nyumbani anakaa na mtoto wake wa mwisho ambae kabla baba hajafariki alimwambia akae nyumbani kumuangalia mama yake.Hivyo anakaa hapo na mkewe wengine wote wameolewa ama kuoa wako kwenye miji yao.
Ni mambo mengi tuliongea na bibi kama ulisikiliza leo tena jana ulimsikia.

6 comments:

  1. habari dada! nakupongeza sana kwa kazi nzuri usifanyazo kuelimisha jamii na kusaidia wa2 wenye matatizo sio siri mi ni miongoni mwa watu wanaukupenda! unanifanya nifungue blog yako kila siku. hongera sana dada!

    ReplyDelete
  2. Nimependa sana utaratibu na ustaarabu wa Bibi Rajabu.Walimu wa sasa hawana utaratibu hata wa kutunza kumbukumbu za maisha yao.Huu ni utaratibu mzuri sana ingawa wakati mwingine unakuumiza kwa kukumbuka maumivu na misalaba ya dunia.

    Big Ups Bibi Rajabu.

    ReplyDelete
  3. dada dina sio 'mastars' ni masters rekebisha kwenye para ya tatu utoka mwisho.
    unafanya kazi nzuri na unaimudu, hongera sana!

    ReplyDelete
  4. DINA DOGO LANGU MIMI BILA KUFUNGUA BLOG YAKO SIKU INAKUWA NGUMU HALAFU MBAYA MUNGU AKUJAALIE KWA KAZI UNAYOIFANYA !MSHUKURU MUNGU KWA KARAMA ALIYOKUPA.

    ReplyDelete
  5. Hongera sana Dina yani navyo kipenda kipindi chako mpaka basi hongera sana Big up to bibi Rajabu ni mfano hai uliobakia Tz am so proud of her and the whole crew of Clouds Fm ur da best.
    it's me zay wa MTIBWA

    ReplyDelete
  6. m so happy and proud of bibi rajabu, which happens to be my real grandmother(my dads mom)....so happy i have her in my lyf and dat shes a living example!! thank u dina for her paying her dat pleasant vist....MUCHLOVE

    ReplyDelete