Monday, April 2, 2012

MWENYE KUJUA DAWA KIBOKO YA MBA TUNAOMBA MSAADA

mambo Dina ? hope ur okay. nahitaji msaada wako  nina tatizo kubwa sana kwa muda sasa nina kama ukoko kichwani mwangu yaani nimekuwa nikikwangua mba after every 2 days yanatoka miukoko hiyo balaa hila siwashwi kabisa. nywele zangu zimekuwa dhahifu mno sababu ya hii. naomba kama kuna yoyote anajua dawa ya hii anitumie jina nikaitafute maana naona nitabaki sina nywele.
Asante!

24 comments:

  1. wanasema sabuni ya unga inasaidia sina uhakika sana hilo jaribu kuulizia pia.
    Au kama vp dada zikate tu ,unaweza kupata matatizo baadaye.Mwisho jaribu shampoo kana unaweza kumudu gharama zake.

    ReplyDelete
  2. dawa ya mba ni Radiant NI MAFUTA YA KUPAKA KWENYE NGOZI YANATOKA UGANDA, JINSI YA KUTUMIA, UNAOSHA NYWELE ZAKO VIZURI, KISHA UNAPAKA KWENYE NGOZI HAYO MAFUTA, NA HATA JUU YA NYWELE UNAPAKA KISHA UNAZIKAUSHA KAMA HAZINA DAWA, KAMA ZINA DAWA NA UNATAKA KUSET, UNAPAKA KWENYE NGOZI NA JUU KWENYE NYWELE, KISHA UNAFUNGA ROLLERS, MAFUTA YATAKAUIKIA KWENYE NYWELE, NI MAFUTA MAZURI SANA SANA YAMENISAIDIA, NILIKUWA NA MBA UNASHUKA HADI USONI KWA MBELE, LAKINI SAA HIZI SIWASHWI, WALA SIJIKUNI, BEI NI SHS 5000 TZS TU, KOPO LAKE LINA PICHA YA MSICHANA MWEUSIIIII NA MAANDISHI YA MEUSI NA RANGI YA KIJANI NA GOLD, HATA KARIAKOO YAPO

    ReplyDelete
  3. Pole sana najua how u feel haswa kwetu kina dada ni kitu ambacho kinakosesha amani sana ikizingatiwa na nywele ni moja ya urembo wetu. japo c mtaalam sana ila ningekushauri usikimbilie kwenye mafuta tuu ila angalia kuanzia shampoo steemin na dawa unazotumia zinaweza zikawa ni tatizo coz unaweza kubadilisha mafuta kumbe tatizo lipo kwenye dawa au steemin au shampoo unayooshewa saluni. so angalia nanture (text) ya nywele yako kwanza then go for its product na kwakuwa wewe unataka kutibu kwanza. Na pia tafuta na ushauri kwa watu wa hair beauty tho wengi wao ni waongo kama watabiri so be careful unaweza ukawa para zaidi.

    ReplyDelete
  4. Pole sana mdau kwa kwa tatizo lako. Jaribu kutumia NIZORAL SHAMPOO. Huwa inauzwa kwenye maduka ya dawa (PHARMACIES) makubwa. Jaribu hiyo, inaweza kukusaidia.

    ReplyDelete
  5. soul mate ipo kwenye kopo la njano dada ni dawa na mafuta mazuri sana kwa nywele za mba. ukitumia mba zote kwisha....

    ReplyDelete
  6. Pole sana. Mba huwa ni dalili kuwa ngozi yako ni kavu, ngozi ikiwa na mafuta huwa hakuna Mba. Jaribu muda wote ngozi yako iwe na mafuta, sidhani kama aina ya mafuta ina-mater. kwa kuanzia unaweza hata kupaka ngozi yako mafuta mara 2 kwa siku

    ReplyDelete
  7. anonymous namba mbili nakubaliana nae mi pia nlikua nna mba mpaka ikawa kero kwangu maana mda wot nlikua ni kujikuna hata mbele za watu nlikua nashindwa kuvumilia ila toka nimetumia RADIANT mba kushney...kizuri kula na wenzio,LOVE U ALL...

    ReplyDelete
  8. Pole sana ,lakini kwa jinsi ulivyojieleza,unahitaji kuonana na daktari wa Ngozi kwanza, Kabla ya kupaka chochote, its a medical condition.

    ReplyDelete
  9. Hi da dina.. huyu dada wa mba kanigusa sana ni hivi.. kitu kikubwa kinacholeta mba ni kutoosha nywele, kubadilisha badilisha mafuta ya ngozi au kama ni mtumiaji wa chemical tofauti tofauti ni shida pia. sambamba na utumiaji wa nywele bandia. also kama ni mtu anayekwenda salon all the time kutengeza nywele ajitahidi kuwa na vifaa vyake bila kusahau kunywa maji ya kutosha. mara nyingine unakuta ni ngozi kuwa kavu sana au kama yuko kwenye medication inaweza kuwa sababu.
    thanks

    ReplyDelete
  10. Mambo,
    Kuna mafuta ya NYWELE yanaitwa RADIANT, ni mazuri sana na bei yake ni ya kawaida kabisa. Me nilikua na tatizo hilo lakini tangu nimeanza kuyatumia tatizo limeisha kabisa. Unaweza kuyapata kwa hadi sh 5,500/-, yajaribu!

    ReplyDelete
  11. Mafuta ya nywele vaida yanasaidia sana kuondoa mba. Yako kwenye chupa ya kijani yanatengenezwa zimbabwe...pia yanaondoa mvi. huku uswekeni kwetu yanauzwa sh. 3500 last time i checked...mjini Dar yaweza kuwa cheaper. all the best

    ReplyDelete
  12. hata mimi nilishawahi kupata tatizo hilo nikaenda kwa dr wa ngozi akaniambia nitumie zenoral shampoo na dawa inaitwa elocom na niitumie kila siku for a week,kila siku unaosha na hiyo shampoo na unapaka hiyo dawa na ikanisaidia

    ReplyDelete
  13. HEY LADY POLE KWA TATIZO LA MBA NIMETUMIA MAFUTA FLANI YA MKOROGO YAPO MWANZA,WANACHANGANYA MIDUDE KIBAO LAKINI SIJUI NI NINI EXCTLY BT WHAT I KNOW YANAITWA MKOROGO, BEI NI 1500 TU ,KAMA UTAITAJI NAMBIE

    ReplyDelete
  14. Dada tumia hivi 2:
    1. mafuta ya mgando yanaitwa SULFUR 8. Kopo lake ni njano.
    2. shampoo inaitwa HEAD & SHOULDERS ITCHY SCALP DANDRUFF SHAMPOO.
    Dada utashangaa mba wote utaisha mara moja na utarudi hapa kushukuru.

    ReplyDelete
  15. sister mimi nilikuwa na tatizo kama hilo,nimetumia dawa nyingi sana bila mafanikio,kuna dawa niliipata phamarcy moja hiko magomeni kwa fundikira,hiyo dawa inaitwa NEO MEDLOL,inauzwa sh-20000,amini usiamini sister nimepaka mara 2 tu,tatizo kwisha,mi naiishi UK,nimeonana na doctor wangu mara nyingi,lakini sikupata mafanikio,siku 1,nilikuwa TZ,kama bahati nikaingia hiyo phamarcy,wakanishauri nitumie hiyo dawa,kwa kweli nashukuru sana

    ReplyDelete
  16. radian ni kiboko ya mba, mimi nilikuwa kama wewe yani hata nioshe nyewele leo kesho mba zimejaa. natumia radiant nina mwezi sasa tangu nimeanza kutumia mba umekimbia na siwashwi tena. nilinunua sh. 6000/= kwa sababu nililetewa ofisini, labda ukienda dukani mwenyewe unaweza kupata kwa 5,000/=

    ReplyDelete
  17. RADIANT NI KIBOKO...KUNA YANAYOUZWA ADI KWA SH..4OOO DA DINA..ATA UKISUKA RASTA UNAPAKA KWENYE NGOZI BEFORE HUJASUKA...HAKUNA KUWASWHA WALA NN..PIA YANAJAZA NYWELE....tuombe tu Mungu wasituletee fake

    ReplyDelete
  18. Hi

    Pole kwa tatizo la mba ila radiant hayo mafuta ni mazuri sana pia yanajaza nywele na zinakuwa nyeusi na wanauza elfu tatu tu k,koo ila kwa maduka ya yetu ya uswahilin kutakuwa zaidi ya hapo na product zao ni nzuri sana kuna sabuni pia za kutoa mabaka so km wataka kujua zaidi mie naona bora uende k,koo km upo hapa dar wapo mtaa wa JANGWANI opposite yake wanapaki magari ya mbezi-kimara-k,koo

    Halima Juma

    ReplyDelete
  19. hata sulphur 8 kama utapata shampoo na mafuta yake ni dawa nzuri ya mba ingawa iko bei kidogo

    ReplyDelete
  20. Tumia mafuta ya Radiant kutoka Uganda na zitaisha

    ReplyDelete
  21. Paka tube moja hivi inaitwa VIRGIN hiyyo ni kiboko.Pia uwe unaosha nywele na kukausha kila mara angalau kwa wiki mara moja.

    ReplyDelete
  22. TUMIA SULPHARE 8 KOPO LA NJANO NI MAFUTA KABISA PAKA KWENYE NJOZI! DAKIKA MI NILIKUWA NA UKOKO KNW NGOZI NYEUPEEEEE.

    ReplyDelete
  23. Jaman mi naomba mnisaidie natafuta maduka yanayouza dawa zaa kuongeza makalio kwa mkoa wa dar es salaam na morogoro na pia bei zake naomben msaada wenu jaman nisaidieni

    ReplyDelete