Friday, March 30, 2012

HUWA UNAENDA UMBALI GANI KATIKA KUMUADHIBU MTOTO WAKO ANAPOKOSEA?

Hii imetokea nchini Cambodia.Baba amfunga mtoto wake kwenye mti  mtaani kwa  mnyororo na kufuli .Kisa  hakwenda shule badala yake alikuwa mtaani kwenye internet cafe anacheza video game.Mtoto huyo mwenye umri wa miaka 13 alifungwa hapo mtini ili watu wamuone wamcheke na akome tabia ya kutokwenda shule.Majirani walipiga simu polisi na baba yake kukamatwa kwa kosa la child abuse.

Hii haina tofauti na mzazi mwenye mtoto anaeshindwa kujizuia kutoa haja ndogo kitandani.Wapo wazazi wanaomdhalilisha mtoto kwa kumwanika hadharani watoto wenzake wamwimbie ''kikojozi,kakojoa na nguo kazitia moto''Wazazi wenye tabia hii mkome kabisa kwani hujui kwa kiasi gani unamdhalilisha mtoto wako na kumnyanyasa kisaikolojia.

7 comments:

  1. Leo umenena.watoto wengi wa kibongo huteswa kwa kuwa eti kakojoa kitandani,wakati si kosa lake kwani akikua maranyingi huacha. pia inampunguzia mtoto kutojiamini mbele ya watoto wenzie. naongezea kweli wazazi komeni acheni ushamba msaidieni mtoto. kaka s.

    ReplyDelete
  2. Inauma sana .Mzazi asie na busara humtembeza mwanae .Serekali yetu bado iko nyuma kwa maisha ya wananchi.wako mbele kwa maisha yao binafsi . Wakubwa wanamali za mabilion .wangechanga wawasaidie watoto wanaonyanyasika na Wangetakiwa wazazi kupewa adhabu wafanyapo mabaya kwa watoto.

    ReplyDelete
  3. UNAJUA DINA SASA HIVI WAZAZI WANAKAZI YA ZIADA KTK SWALA LA MALEZI DINA MPAKA MZAZI ANAAMUA KUTOA ADHABU HIYO C KM KAPENDA NIKWAMBA MTOTO NI MDOGO NAKILA ANAPOELEZWA KITU HASIKII MPAKA MZAZI ANAAMUA KUTOA ADHABU KALI HIVYO NA MBAYA...NI ANAONA MTOTO WAKE ANAPOELEKEA C PAZURI MFANO NILIWAHI KUKUTAN NA MAMA MMOJA POLISI KAMKWIDA BINTI YAKE WA MIAKA 19 ANAMLILIA RPC MWANAE APELEKWE MAGEREZA KULIKO ANAVYO MNIGINIZA ROHO ANASEMA ASIJE AKAMFANYA(YANI YEYE MAMA)MAISHA YAKE YAKAISHIA JELA UNADHANI MPAKA MZAZI ANAFIKIA KUSEMA HIVYO KASHAJITAHIDI KIASI GN HUYO MAMA ALIKUWA ANAJARIBU KUELEZWA MADHARA YA MAGEREZA LAKINI AKSEMA HAPANA KWANI MWANAE HAKUNA BAYA NA ZURI ASILO LIJUA. HUYO MAMA ANAKWAMBIA AMESHA MPELEKA AKAFANYIWE KANSELING LAKINI WAPI,KAMPELEKA KWENYE MAOMBI YA DINI MBALI MBALI LAKIN WAPI KUBE HUKO SHULE ANAGURUPU BAYA NA AKILI YAKE NI YA KUSHUKIWA NYUMBANI ALIKUWA ANAWAITA WASHAMBA HUYO MAMA HIYO SIKU ALIFANYA KUKUTANA NAE GHAFLA BINTI YAKE HATAKI KUKAA NYUMBANI BILA SABABU ANASEMA ANATAKA UHURU WAKE KWELI MTOTO UNAYEJUA UCHUNGU WAKE UMUACHIE UMRI(19)HUO ARUDI MUDA ANAOTAKA, ALALE NJE MZAZI WA WAWAPI ANAYEMTAKI MTOTO WAKE MAISH MAZURI AMUACHUE TU..WATOTO WAMEKUWA HAWANA UWOGA MTOTO ANARUDINYUMBANI MPOLE ANARUDI MUDA UNAOTAKIWA KUMBE MUDA WA SHULE ANAGURUPU BAYA ANAVUTA BANGI NA MACHAFU YOTE MZAZI HAJUI..(WAZAZI JAMANI NAWAO WAFANYAJE?)SIJASEMA WAADHIBIWE HIVYO VIBAYA BAYA...TUSAIDIANE MAWAZOO

    ReplyDelete
  4. nikweli mimi nilikuwa kikochozi sasa badala ya kukujenga kisaikolijia wanakutukana matokeo yake unajenga kiburi wakati kwakweli saayakukojoa husikii lolote au wakati mwingine unaota uko nje unakojoa kumbe sio

    ReplyDelete
  5. tatizo watoto wa siku hizi wanajua kuliko wengine na mambo ya mtandao haya utawaambia nn ukifundisha ni kama unarudia, unauonmba mungu tu akuongozee wa kwako aishi maisha mema, nothing else

    ReplyDelete
  6. He Dina! huyo wa Cambodia kapitiliza shoga! eehh!!

    ReplyDelete
  7. Jamani kumuadhibu mtoto mbele za watu ni kumkomaza wala si kumfunza,mimi nina mtoto ana miaka 10,uwa nikitaka kumuadhibu nafanya siri kubwa,hata baba yake sometimes hajui,namuita chumbani kwangu,namuadhibu kwa maneno tu,wala si kiboko,na uwa anaelewa na harudii,sipendi kumdhalilisha mwanangu,haitamtoka kichwani,mimi nilidhalilishwa sana na mama yangu,mpaka leo sijasahau,na uwa inanima sana,alinipeleka mpaka shuleni mwaka 87 nikiwa darasa la 2,sitasahau.MUNGU AMREHEMU MAMA YANGU HUKO ALIKO.

    ReplyDelete