Thursday, October 9, 2014

ASANTENI KWA LIST YA CHAKULA CHA MTOTO.

Jamani nashukuru kwa msaada wa mawazo leo Zion amekula kitu tofauti.Amekula ndizi bukoba moja,kiazi kimoja,karoti na supu ya nyama ikasagwa.Amekula vizuri tu na akamaliza.

Ila papai kalichoka kweli,wakati dada yake anampa chakula alipoona kibakuli akaanza kulia na kufunga macho na mdomo akijua ni papai alipoona taste tofauti akaacha kulia.

Kuna mdau pia kaongelea position ya kukaa wakati mtoto akila.Sikujua hilo pia so ataanza kula akiwa wima kwenye baby walker yake.

Ntakuwa naweka topics za watoto au kama kuna mtu anataka kujua kitu or kushare jambo ambalo ungependa sisi kina mama wapya tujue pls niandikie kwa email dina_marios@yahoo.com

14 comments:

  1. King zion hawez kataa ndizi bukoba yeye senene lubisi anagonga tu #dam ya kihaya

    ReplyDelete
  2. Mnunulie high chair ni kiti kwaajili ya mtoto kuanzia 6 month mpaka 3 yrs,pia itakusaidia yeye kujifunza kila mwenyewe.

    ReplyDelete
  3. hata siku mmoja usimpe mtoto wako chakula bila kuonja na hilo pia wadada waambiwe maana kuna siku utampa chenye chumvi nyingi au chochote maziwa unaweza ukampa mabaya au ya moto sana ikawa tatizo so tujifunze kuonja tusije wapa watoto wetu vitu vibaya.

    ReplyDelete
  4. Asante wadau mlotangulia. Nina mtoto wa mwezi moomoja, napenda pia kujifunza toka Kwa akina mama wenzangu. Dina asante kutukutanisha.

    Namuunga mkono mdau namba mbili hapo kuhusu kumkalisha mtoto kwenye kiti kirefu ili aifikie meza ya chakula. Ni muhimu sana Kwa mtoto angalau mlo mmoja aungane na familia yote katika chakula. Ila tu ni Kwa Yule mtoto anaekaa vizuri. Usijali atachafua chafua mezani na sakafu ila atauwa amejifunza.

    Kuna baadhi ya watoto hawawezi kukaa mezani kula na familia walizoeshwa kukaa chini, ushauri wangu kama unameza ya chakula please join na watoto ni vizuri sana, hapo utaona mtoto jinsi anavyokula na utaweza kumrekebisha pale akoseapo.

    Jingine wazazi tuwafundishe wanetu angalau kutumia kijiko/uma wakati wa kula tangu wakiwa wadogo kwani ni vizuri sana wajue, huwezi jua mwanao ataenda wapi au ataalikwa wapi au nchi gani. Sehemu nyingine wasijemcheka akajisikia vibaya.

    Kila lakheri Dina na akina mama wote.

    Mama Silvia.

    ReplyDelete
  5. Mpaka raha !Ila jitahidi asipewe chakula kingi unajua mama Zion sio kina mama huwa unaona raha mtoto akila ila tunasahau wakati mwigine wanaliswa kuzid uwezo wa tumbo lao. Jitahid kama ni dada mpangie kiasi gani ampe ili aweze kuwa na nafasi ya kula tunda. maji ili apate choo vizuri .
    Vitamin zote ni muhimu
    .Akimlisha asimlaze sana mie nimezalia majuu huwa tunawaweka kwenye kiti chake anakula kwa raha zaid na tunawalisha kwa muongozo klinik

    mfano nilimnyonyesha ntoto nampa maziwa kila baada ya masaa 4 kio kila akilia mtoo kulia ndo kuongea kwake.
    .huyo anony wa juu nae katoa maelezo ya kiti ,
    Kingine hata akikataa kula nakuisitiza wewe na kina mama wenzangu asizibwe pua hata akikataa kunywa dawa asizibwe pua,

    Mtoto anahema kwa njia ya mdomo na pua zaid hana .
    shoga angu kamziba mtoto pua akimlazimishakula uji na ndo akamaliza uhai wa mtoto hapo Dar,
    .
    . Pls mpe dada kibakuli maalumu atumie kwa ajili wa mtoto,
    Mkimpa hata akitumia mda msilazimishe ale kwa haraka , nimeona hili nilipokuwa bongo .dada anamlazimisha mtoto kula awahi kazi basi anajikuta anajza chakula , wakati mtoto analia yy ndo anaweka chakula , Je kikipita ktk njia ya hewa pls tuzingatie sana . Watoto hawana uwezo wa kutuhadithia tuwe tunawasoma kwa macho .

    Dida mpende anaye kulelea mtoto kuliko hata unavyojipenda wewe au mzazi mwenzio amini atampenda mwanao kama wake ataata maelekezo yako,
    Mungu awabariki wanawake wenzangu wote

    ReplyDelete
  6. ni kweli watoto wakati mwingine anataka uhuru sana wakati whakua kula unapombana bana sana inamnyima raha ya Chakula .

    ReplyDelete
  7. Kijiko ktk picha ni kikubwa sana so jitahidi kutumia kijiko kidogo au cha saizi ya kati.Pia jitahidi kubadilisha vyombo vya kumlishia chakula ili asivikariri

    ReplyDelete
  8. Dina kijiko cha mtoto sio kwani huyu ndo anaanza/kuota meno, nakumbuka uliwahi post kuhusu matumizi ya visu kukata matunda kuwa unatumia plastik. Vipi yeye chakula hutumii vyombo vya mfupa?

    ReplyDelete
  9. Mimi ninamtoto ana 2.8 now na ameanza shule last month amekuwa mvivu kula sana Tanya ameanza shule sasa mwanzo nilikuwa natumia nguvu sana kumpa chakula kwamba lazima ale akitoka shule ndio akalale type hataki kulaanataka kulala tu tena analia sana sana akawa aneloose. Sana nikaanza kuumia maana mtoto. Amepungua nikaamua tu let me change niende nae anavyotaka keeling nmeona changes ikabidi nihakikishe fridge haikosi city vidogo vidogo kwaajili yake ili atakapokihitaji kisijekuwa jalopies so nahakikisha mayai soseji samaki maziwa havikosekani so akiamka unamuuliza installs nini anasema unamtengenezea haraka anakula anaenjoy bila kusahau Marina na nmeona matokeo mazuri afya pia imerudi

    ReplyDelete
  10. Mimi mwanangu ana umri wa mwaka mmoja na miezi kumi (1.10) na menu yake ni wali bokoboko na kichwa cha samaki kilichochemshwa na kuwekewa nyanya moja,kitunguu nusu,karoti nusu,maharage machanga kama pc 4,na hoho robo samaki anachemka muda mrefu then unamtolea soup ya samaki na then kichwa unakichambua unachanganya na bokoboko ya wali unasonga kdg,viazi vitamu,viazi chips,ndizi ngombe,na spaghetti hivyo hivyo kwa kichwa cha samaki sato or sangara daily.

    ReplyDelete
  11. Kwa upande wa matunda kila siku nahakikisha nampatia chungwa moja na tunda tofauti kila siku kwa mf papai,embe,parachichi,apple,karoti naigrate then nakamua kama tui la nazi hii pia inasaidia kama mtoto ana minyoo,Ndizi kisukari naponda ponda nachanganya na maziwa fresh ya uvuguvugu nampa,matunda yote nayapondaponda isipokuwa embe na apple naya blend kwenye blenda.

    ReplyDelete
  12. Hongera kwa kuamua kuitwa mamma Dina maana kuna watu hawataki uzee wanahisi watakua wamechoka. Sasa mbona mimi naona baadhi ya wadau wanaongelea malezi ya familia bora tu vipi wale wenye maisha duni wawawekeje watoto wanapokula? Hivi kumpeleka mtoto wa 2.8 shule kwangu naona ni kukwepa majukumu kama mama. Tusifike hatua mtoto akawa ni wa dada wa kazi na mwl huko shule, mimi naishi kijijini maisha duni sasa hii uma na kisu mmh!! Sio ajifunze kula kwa adabu mambo ya visu akikutana nayo atajifunza kwani atakua na akili, tuwafunze watoto maisha bora ya kiafrika kama tulivyolelewa sisi

    ReplyDelete
  13. Habari.

    nilishachangia apo juu ila pia niwakubushe sio kila siku kwenye uji tunawaweka watoto karanga badala yake tuwe tunawawekea na Almonds ni nzuri mno kwa mtot na kwa mtoto aliye na meno unaweza mpa akatafuna zinapatikana shoppers, pia tukumbuke kwawekea Bitruits kwenye juice maana nayo ni Anti Cancer.

    kila la heri katika malezi..... na mungu atulindie watoto wetu

    by

    nyabo

    ReplyDelete
  14. asanten akina mama wenzangu kwa mada nzuri..mi mwanangu ana miezi 6 na wiki mbili lakin hatak kula kila chakula ninachomuandalia hakipendi.nifanyeje?

    ReplyDelete